Usiku wa jana Mastaa Wema Sepetu na Idris Sultan walidhibitisha kwa mara ya kwanza kwenye kipindi cha Ala Za Roho na mtangazaji Diva Loveness kuwa na uhusiano wa kimapenzi na kwamba wana tarajia kupata mtoto wao wa kwanza.
‘’Unajua kuna kipindi nilikuwa siamini nikawa namtuma mdogo wangu akaninunulie ‘pregnancy test’nyingi ili niwe na’test’ kila siku,nilikuwa natakiwa kwenda kufanya ‘process’ ya kusafisha kizazi,nikamwambia daktari wangu kuwa natakiwa kusafisha kizazi ila nikamwambi kuwa nime’miss’ period zangu,akaniambia kabla sijasafisha kizazi nipime kwanza kama nina ujauzito,’’Wema.