INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Thursday, July 5, 2012

MWIGIZAJI WA FILAMU JENNIFER KYAKA (ODAMA) KUHUDHURIA KATIKA KULETA FURAHA KWA WATOTO WA KIJIJI CHA SOS DAR ES SALAAM PAMOJA NA MKE WA RAISI MAMA SALMA KIKWETE.

Mke wa rais Mama Salma Kikwete alijiunga na wafanyakazi wa kiwanda cha Sadolin Paint (ambacho ndicho kilichozindua rangi bora ulimwenguni ya DULUX hapa Tanzania), pamoja na wanajamii wote, wageni waheshimiwa, maofisa wa serikalini, waalikwa wakijumuika na watoto wa kijiji cha SOS
Lengo kubwa lilikuwa ni kupaka rangi za kung’ara na kubadilisha hali ya rangi iliyokuwa ukungu na chafu.. Watoto hawakuishia kupaka rangi ya kuta bali walipaka na sura zao. Kulikuwa na DJ na watoto walipata muda wa kuimba nyimbo zao.
Mama Salma Kikwete alishirikiana katika shufghuli nzima ya upakaji rangi, kupanda mti wa kumbukumbu na kuwashukuru waandaji.
Mkurugenzi wa DULUX, Dr. Alex Lengeju alimshukuru Mama Salma Kikwete na muwakilishi mwigizaji wa filamu Tanzania, Jennifer Kyaka (Odama) kwa kazi nzima walioifanya na watoto wa kijiji cha SOS
Kituo cha chekechea cha kijiji cha SOS ndicho kilichobahatika kuwa cha kwanza kupata huduma hii.

NB: DULUX ni rangi murua ya Akzonobel na inapatikana katika nchi nyingi kama 26 na mabara kama Ulaya, Amerika Kaskazini, Latini Amerika, Asia na Afrika. Makao makuu yako Slough Uingereza
Madhumuni ya kampuni hii ni kubadilisha mazingira machafukwa rangi za kung’ara.
Kitu pia kupanga kwa pamoja furaha na huzuni katika kufanya utofauti katika maisha ya watoto.
Odama: akielekea Kijiji cha SOS
Leo ni leo rafiki yangu, Mama Salma Kikwete na Odama LIVE kijijini kwetu...Mbona tunabahati!!!!.
Hivi ni vyeti tunakupa mheshimiwa Nagu
Tulia nikupendezeshe, utapata zawadi kwa wageni wetu hapa kijijini
Mwana naomba utulie kabla ya kuanza kupaka rangi ukutani ngoja tuanze na nyinyi kwa usoni kama mfano.

Mwanangu lazima ufike mbali, Baba yako JK aliaanza hivi hivi..Kazana
Wall Painting ikiendelea na mama Salma Kikwete
 Mheshimiwa Nagu akichekelea ucheshi wa Odama


Nashukuruni sana DULUX kwa zawadi yenu 

STEVE NYERERE AKABIDHI FILAMU YAKE YA MWL NYERERE KWA MAMA MARIA NYERERE

Mwigizaji wa filamu nchini Stive Mangele 'Stive Nyerere jana alikuwa anakabidhi filamu yake ya Mwalimu Nyerere kwa  Mama Maria Nyerere ikiwa kama shukrani zake, baada ya mama huyo kumsaidia katika kukamilisha filamu hiyo ambayo aliifanyia Butiama. Stive alisema kwamba kumpa filamu hiyo ni kuweka kumbukumbu kwamba, anathamini msaada na mchango wake  katika filamu hiyo na hana kikubwa cha kumpa wala cha kumfanyia zaidi.

Mama Maria Nyerere akionyesha filamu hizo alizokabidhiwa na Steve Nyerere
 
Amesema Mama Maria Nyerere alimsaidia sana katika kumuonyesha vitu gani mwalimu alikuwa akifanya, na vitu gani mwalimu alikuwa akivipenda, na sehemu ambazo mwalimu alipenda kukaa baada ya kazi zake. Pia ametoa shukrani kwa wasanii wenzake ambapo walijitahidi katika hali moja au nyingine kuhakikisha filamu hiyo ili ikamilika.

Wednesday, July 4, 2012

WATUNZI WASIO NA UBUNIFU WANASHUSHA THAMANI YA FILAMU ZETU – AUNTY EZEKIEL…!!


MSANII nguli katika tasnia ya filamu bongo, Aunty Ezekiel, ameuambia mtandao wa DarTalk, kuwa anaamini kukua au kuporomoka kwa tasnia hiyo kutatokakana na watunzi wenyewe pale wanapokuwa wanatoa stori zinazofanana bila kutumia ubunifu.

Mkali huyo alidai kuwa zipo baadhi ya filamu ambazo hakutaka kuzitaja majina ambazo zinafafa, na ndizo zinazoweza kuwafanya mashabiki pamoja na wadau kushindwa kuzitofautisha pindi zinapokuwa sokoni.

“Kufanana kwa filamu kunasababisha hata zinapokuwa sokoni watu washindwe kuzinunua kitu ambacho hata maisha ya wasanii yawe magumu kwani kazi zao huwa zinafanya vibaya sokoni,” Alisema Aunty.

YUKUTI KUNIDHULUMU-NICE (MWIGIZAJI FILAMU)



MWANDISHI wa muswada wa Swahiliwood, Ali Yakuti ameshutumiwa kwa kumdhulumu mwigizaji wa filamu za Bongo, Godliver Godian Nice malipo yatokanayo na ushiriki wa filamu ya 'Who Is The Looser'.

Filamu hiyo iliandaliwa na mwandishi huyo na kwenda kurekodiwa huko Kibaha. Msanii huyo amedai: "Naamini karibu washiriki wote wa filamu ya Yakuti wamelipwa, lakini kwangu imekuwa shida, ukimpigia simu hapokei, lakini jambo la pili baya zaidi linalonifanya roho iume zaidi ni jinsi nilivyojitoa katika filamu hiyo.

"Yaani nilizimika hata kufanya kazi nyingine tofauti na ile ya kuigiza, najiuliza kwanini hataki kunilipa fedha ambayo ni jasho langu?"

Nice amesema kuwa wakati filamu hiyo ikirekodiwa hakukuwa na mtu wa mapambo (Make Up) kazi ambayo aliifanya kwa ajili ya kuifanya filamu hiyo iwe bora.

Anasema kuna wakati Yakuti alimpigia simu akimtaka kurudia vipande vya filamu hiyo, jambo ambalo hata yeye lilimshangaza.

"Nikamkumbushia fedha zangu, akasema atanipa na pia tukapanga siku ya kurudia vipande hivyo, lakini siku ilipofika Yakuti hakupokea simu yangu," alisema.

Unajua mimi niliacha kazi kwa ajili ya kurekodi kazi yake kwa sababu pamoja na kusomea fani nyingine lakini napenda sana kuigiza, nimekaa Kibaha zaidi ya wiki halafu mtu bila huruma anakudhulumu jasho lako hakupi hata senti tano! Inauma sana,anasisitiza Nice.

Mwanaspoti ilimtafuta Ali Yakuti kwa njia ya simu lakini simu yake iliita tu na baada ya muda haikupatikana tena.