INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Thursday, August 9, 2012

MWIGIZAJI WA BONGO MOVIE, ROSE THOMAS AFARIKI DUNIA

Marehemu Rose Thomas alikuwa mwigizaji wa filamu za Kitanzania (Bongo Movie) kwa kipindi kirefu sana. Kuna baadhi ya filamu ambazo amecheza na wasanii wengine kama Jennifer Kyaka (Odama). Filamu hizo ni Roleen, Rude, House Maid, na pia Chocolate ambayo haijaingia sokoni. Marehemu Rose alikuwa anahusika na maswala ya "make up" wakati wa maandalizi ya kutengeneza filamu.

Marehemu alikuwa anasumbuliwa na tumbo kwa muda mrefu mapaka mauti ilipomkuta siku ya Jumamosi 5 Agosti 2012 katika hospitali ya Muhimbili Dar es Salaam Tanzania. Marehemu ameacha mtoto mmoja Loveness mwnye umri wa miaka 11.

Mbali na uigizaji Marehemu Rose Thomas alikuwa akifanya kazi  Salon.

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI

Rose Thomas enzi za uhai wake

Ndugu na jamaa wakiwa Muhimbbili mochwari






 Kutoka kulia ni Jacquiline Wolper, Odama na Roda wakiwa katika mawazo wakati wa kusubiria mwili wa marehemu mochwari Muhimbili
 Ndugu na jamaa wakisubiriya mwili wa marehemu Rose Thomas
Mdogo wa marehemu, Happy Thomas (aliyekaa) akiwa katika majonzi
 Dada wa marehemu, Pilly (katikati) akipelekwa mahali pa kupumzika wakati akisubiri mwili wa marehemu.
 Wasanii wa Bongo Movie kutoka kushoto ni Slim, Yusuph Mlela wakisubilia mwili wa marehemu.
 Jeneza la Marehemu Rose Thomas, nyumbani kwa Baba yake mkubwa Mabibo-DSM tayari kwa kuagwa
 Kutoka kulia wa pili ni msanii wa Bongo Movie, Recho Haule, akimkumbuka rafiki yake kwa majonzi makubwa.
 Mchungaji akitoa neno la mwisho Mabibo Dar es Salaam
 Katikati ni msanii wa Bongo Movie, Jennifer Kyaka-Odama akishuhudia mwili wa rafiki yake mpenzi Rose Thomas wakati wa kuuaga.
 Kutoka kulia ni Odama, Roda na Mainda (Wasanii wa Bongo Movie)

 Roda akiwa katika masikitiko wakati wa kumuaga rafiki yake.

 Pumzika kwa amani mwanangu, tulikupenda ila Mungu amekupenda zaidi.
 Mdogo wa Marehemu Happy akiwa ameshikiliwa baada ya kuaga mwili wa dada yake mpendwa.
 Msanii wa Bongo Movie, Odama akishindwa kutembea baada ya miguu yake kufa ganzi kutokana na uchungu aliokuwa nao kwa kupotelewa na rafiki yake mpenzi ambaye amecheza naye filamu mbalimbali.
 Odama akitoa machozi na kutoamini kuwa kweli rafiki yake hatamuona tena dunia.
 Msanii wa Bongo Movie, Hashim Kambi akimshikilia Odama baada ya kuaga mwili wa rafiki yake mpenzi Rose Thomas.
 Marehemu Rose Thomas akiwa katika nyumba yake ya milele.

 Rafiki yake na marehemu mama Bryan akitoa heshima zake za mwisho kabla ya mazishi kufanyika..

 Mwili wa marehemu Rose Thomas ukipelekwa katika nyumba yake ya kupumzika milele.





 Mama mzazi wa marehemu Roda Thomas katikati akimlilia mwanae Roda Thomas

Mdogo wake marehemu, Happy akiweka shahada katika kaburi la dada yake.

Odama akiweka shahada kama ishara ya upendo na kumuaga rafiki yake mpendwa marehemu Rose Thomas


 Mtoto wa marehemu, Loveness akiliweka shahada katika nyumba ya mama yake kama ishara ya upendo na kuagana.





SINTAH AMJIBU AGNESS MASOGANGE JUU YA USAMABAZAJI WA MKANDA WA X WA MASOGANGE

Mwigizaji  mwenye  mbwembwe nyingi  kutoka ndani ya  tasnia ya filamu Bongo Christina Manongi 'Sintah' amemtaka  video queen wa Bongo Agness Gerald Masogange   kufunga bakuli lake (kunyamza kimya) na kuacha  kumapakazia meneno machafu kwenye vyombo vya  habari.

Akizungumza na mwandishi wetu  mapema leo Sintah amesema kuwa amesikitishwa  sana na kitendo cha  Agness kumtaja yeye (Sintah) kuwa ndiye anahusika na kuisambaza kwenye mitandao video  inayomuonyesha Agness akiwa mtupu huku pia akionekana kufanaya  matendo kadhaa ya kingono.

"Nimemsikia na isitoshe kuna watu wengi wameniambia juu ya hilo la kunitukana na kunitaja redioni kuwa nahusika, mimi  sijui lolote awaulize marafiki zake  ambao mimi naamini ndiyo wanahusika kuzisambaza kwani hata kwenye BBM yangu ni wao ndiyo walinitumia namuomba afunge bakuli  lake la siivyo nitazitoa zaidi kwani ninazo pati wani mpaka 3 na zote nimetumiwa na marafiki zake ambao yeye anacheka nao lakini hajui kama ni ma-sn***ch" alisema Sintah

Akiendelea zaidi Sintah amefunguka kuwa  kamwe hajui lolote kuhusu kamera anayoisma Agnes, kwani binafasi hajawahi kukutana naye  na  alimjua  kupitia   nyimbo za wasanii wa Bongo Fleva kwa kuwa msichana huyo anapenda kuuza sura  na zaidi hajui hata  anapokaa.

MPOKI AMCHANA COP, "NENDA KWANZA FIELD"




Kwenye YOU HEARD ya XXL ya Clouds Fm, Soudy Brown amempigia simu Mpoki kumuuliza kuhusiana na story iliyoandikwa na gazeti la Ijumaa Wikienda kuhusiana na Masanja Mkandamizaji mwishoni mwa wiki iliyopita kudaiwa kutandikwa makofi hadharani na polisi baada ya kuingilia msafara wa gari lililokuwa limebeba fedha.

Katika mahojiano hayo Mpoki amemwambia Gossip Cop kuwa hana taarifa zozote kuwa Masanja amelazwa kutokana na kichapo hicho na kummshauri kuwa aende kwanza field ili ajifunze uandishi wa habari kwakuwa hauwezi.

Mpoki amejinadi kuwa yupo kwenye game kwa miaka 12 hivyo hayumbishwi na kitu.

Habari hiyo iliandikwa:

MCHEKESHAJI wa Orijino Komedi, Emmanuel Mgaya ‘Masanja’, mwishoni mwa wiki iliyopita anadaiwa kutandikwa makofi hadharani na polisi baada ya kuingilia msafara wa gari lililokuwa limebeba fedha.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, tukio hilo lilitokea kwenye njiapanda ya Chalinze mkoani Pwani ambapo msanii huyo alikuwa akitokea Dar kuelekea Tanga huku akiendesha gari kwa kasi ya ajabu.

Chanzo hicho cha Ijumaa Wikenda kinachopiga kambi maeneo hayo kilieleza kuwa jamaa huyo alikutwa na kasheshe hilo baada ya ‘kuliovateki’ gari hilo lililokuwa likisindikizwa na polisi ambapo pamoja na kuzuiwa na wajeda hao, Masanja alijitoa fahamu na kujifanya kichwa ngumu.

Kilisema: “Baada ya ‘kuwaovateki’ wale polisi, ndipo nao (askari) wakamkimbiza hadi wakamkamata na alipotaka kuleta ‘mbovumbovu’ za kujifanya staa kama wale wenzake waliopoteza umaarufu na mvuto, ndipo akala mbata zake safi na soo likahamia kwenye Kituo cha Polisi cha Chalinze Njiapanda na kumshikilia kwa muda kisha kumuachia baada ya mahojiano.”
Ili kupata mzani wa habari hiyo, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Masanja ambaye alikiri kutokea kwa tukio hilo na kudai kukamatwa na askari kutokana na makosa ya barabarani kwake ni suala la kawaida huku akikanusha kupewa kibano.

WEMA AFUNGUKA KUWA YEYE NA DIAMOND NI KAMA RIHANNA NA CHRIS BROWN


 
Wema Sepetu.
http://blog.greatlakesmix.com/wp-content/uploads/2012/03/diamond.jpg
Nasibu ‘Diamond’ Abdul.

BAADA ya kubainika kuwa mastaa wa Bongo, Wema Sepetu na Nasibu ‘Diamond’ Abdul wamerudisha uhusiano wao, Wema ameibuka na kuufananisha uhusiano huo na mastaa wa majuu, Chris Brown na Rihanna.
Wema alisema hayo hivi karibuni katika mahojiano yake na Mtandao wa Dar Talk ambapo aliunadi uhusiano wao na kueleza namna unavyofanana na mastaa hao wa mtoni.
“...yaani utadhani Rihanna na Chris Brown vile haya matukio maana juzi nilikuwa Kigoma, nikasikia Rihanna naye ameonekana sehemu na Chris,” alisomeka Wema.

JACK WA MAISHA PLUS ADONDOKA CHOONI

STAA aliyezalishwa na Maisha Plus Season 2, Jacqueline Dustan (pichani) ambaye hivi sasa anajaribu bahati yake kwenye sinema alipatwa na balaa baada ya kudondoka chooni.
Katika tukio hilo lililojiri hivi karibuni, jijini Dar es Salaam, Jack aliumia goti na kukimbizwa katika Hospitali ya Micco iliyopo Mwananyamala kwa matibabu.
“Siyo mara ya kwanza kuanguka chooni, jambo linalonipa wasiwasi maana nasikia ni ishara mbaya. Namshukuru Mungu kwa sababu bado napumua lakini maumivu hayajaisha, mguu unauma sana,” alisema Jack.

Wednesday, August 8, 2012

KAMPUNI YA STEPS YASHIRIKIANA NA WASANII KUWAKAMATA WEZI WA KAZI ZAO


MSANII MOHAMED NICE 'MTUNISI' AKIZUNGUMZA JINSI WALIVYOKAMATA MZIGO FEKI WA KAZI ZA WASANII MBALIMBALI KWA KUSHIRIKIANA NA KAMPUNI YA STEPS ENTATAINMET YA JIJINI DAR ES SALAAM INAYOSAMBAZA KAZI ZA WASANII NCHINI
MTUHUMIWA WA KURUDUFU KAZI ZA WASANII AKIWA CHINI YA ULINZI BAADA YA KUKAMATWA
MSANII MOHAMED 'NICE' AKILIA KWA UCHUNGU BAADA YA KUKUTA KAZI ZAO ZILIZOKUWA ZIKIUZWA KATIKA MOJA YA DUKA MTAA WA MAGILA NA LIKOMA LEO
Msanii wa filamu nchini Mohamed Nice 'Mtunisi' kushoto na Jacob Stevin 'JB' wakiwa katika duka ambalo lilikuwa linauza kazi zao ambazo ni feki ambapo walikamatwa kwa kushirikiana na Kampuni ya usambazaji ya Steps Entantainment ya jijini Dar es salaam
Moja ya gari lililokuwa limejaa kazi za wasanii mbalimbali nchini zinazouzwa kiholera baada ya kurudufu kinyume na sheria na kukosesha wasanii mapato mazuri.
Baadhi ya watu wakiwa wamezagaa kushudia ukamatwaji wa kazi za wasanii mtaa wa Magili na Likoma Dar es salaam leo.
Baadhi ya wasanii pamoja na askari polisi wakiwa wamelizingira duka lililokuwa linauza kazi feki za wasanii
Gari lenye namba za T 608 BWD lililokamatwa na kazi mbalimbali za wasanii zikiwemo zinazosambazwa na Kampuni ya Steps ya jijini Dar es salaam linalofanya kazi na wasanii hao
BAADHI YA KAZI FEKI ZA WASANII ZILIZOKAMATWA LEO
MSANII MOHAMED NICE 'MTUNISI'  KUSHOTO AKITOA MAELEZO MBALIMBALI KWA MAOFISA USALAMA WALIOFIKA KATIKA UKAMATAJI WA KAZI FEKI ZA WASANII

BAADHI YA WANANCHI WAKISHUDIA TUKIO HILO
MSANII KAPTEN RADO AKIKAGUA KAZI ZAKE MPYA AMBAPO KAZI YAKE MPYA IJULIKANAYO KAMA 'HATIHANI' ILIYOINGIA MTAANI LEO ILIKUWA IMESHA CHAKACHULIWA NA KUINGIZWA SOKONI 
MSANII WA MZIKI WA TAARABU,MZEE YUSUFU KUSHOTO AKIANGALIA MOJA YA KAZI YAKE ILIYOKUWA FEKI ZILIZOKAMATWA NA WASANII WENYEWE KWA KUSHIRIKIANA NA KAMPUNI YA STEPS ENTANTAINMENT YA JIJINI DAR ES SALAAM.
WASANII MZEE YUSUFU KUSHOTO NA MOHAMED NICE WAKIWA KATIKA DUKA LILILOKAMATWA KWA KUUZA KAZI FEKI ZA WASANII MSAKO HUO ULIWASHIRIKISHA KAMPUNI YA STEPS ENTATAINMENT PAMOJA NA WASANII WENYEWE.
BAADHI YA MIZIGO YA DVD MPYA KABISA ZILIZO FEKI ZIKIWA ZIMEKAMATWA LEO.

KAMPUNI ya Steps Entatainment ya jijini Dar es salaam inayosambaza kazi za wasanii kwa kushirikiana na wasanii wamekamata kazi mbalimbali za wasanii hawo zinazorudifiwa kinyume na taratibu na kutofaidika kwa wasanii wanaotoa kazi hizo

Msemaji wa Kampuni ya Steps  Kambarage Ignatios amesema kuwa ukamataji huo si wa zimamoto watahakikisha wanashilikiana na wasanii wenyewe kukamata kazi zao mana wasanii wengi wanadai kuwa kazi zao zinatoka sana kumbe zinachakachuliwa na kuwapa faida watu ambao wanakaa tu na kusubili kazi za wasanii ameiomba serekali kuchukua atua kali ili iwe fundisho kwa watu wanaorudufu na kunyonya kazi za wasanii hawo


Na mmoja ya wasanii waliojitokeza katika kamatakamata hiyo iliyofanyika makutano ya mtaa wa Magila na Likoma Kariakoo, Msanii Mohamedi Nice 'Mtunisi' amesema watu hawa wana akili za ziada kwani katika kava ya mbele wanaweka stika yetu halali na dvd ndio inakuwa imechakachuliwa akiangua kilio na kusema wasanii  wakifa wanakufa masikini kumbe ni watu wachache ndio wamekuwa wakinufaika na kazi zao bila kushiriki chochote


Baadhi ya wasanii walioshiliki katika kamata kamata hiyo ni pamoja na Jacobo Stevin 'JB' Mzee Yusuph wa kundi la Taarabu la Jahazi Simoni Mwapagata (
Rado) Mussa Msuba wa iliyokuwa Segere Orginal Seles Mapunda ,Mohamed Nice 'Mtunisi' na wengine wengi wasanii hawo wameungana pamoja kwa ajili ya kutetea kazi zao ili zisirudufiwe kiolela na kuiomba serekali  kupitisha sheria kali kwa mtu anaekamatwa na kazi kama hizo zilizokamatwa

Friday, August 3, 2012

NDIKUMANA:'SIJAWAI VUNJA NDOA YANGU



Irene Pancras Uwoya ‘Mama Krish’ akiwa  na mumewe Hamad Ndikumana ‘Kataut’.
Na Imelda Mtema
MUME wa Irene Pancras Uwoya ‘Mama Krish’, Hamad Ndikumana ‘Kataut’ ambaye kwa sasa anasakata kabumbu kwenye Timu ya Rayon Sports ya nchini kwao Rwanda, kwa mara ya kwanza ameizungumzia ndoa yake iliyoingia gogoro mwaka jana akisema kuwa hajawahi kuivunja ndoa yake.
Akizungumza kwa njia ya simu akiwa Rwanda, Ndikumana maarufu Bongo kwa jina la Ndiku alisema kuwa kumekuwa na maneno mengi kuhusu ndoa yake kuvunjika lakini alithibitisha kuwa hajawahi kusema lolote kwani hakukuwa na jambo kama hilo.
“Nilijua na ninajua watu wengi waliongea na wanaongea kuhusu ndoa yangu kuvunjika lakini ndoa inavunjikaje kama wahusika wenyewe hawajasema kama imevunjika?”
Mwanasoka huyo aliendelea kutiririka kuwa kama alifunga ndoa yake kanisani basi ni lazima kanisa lingejua kuwa imevunjika kwa maana lazima angeenda kusema.
0 comments

DUDE ADAIWA KUMTAPELI MWIMBA INJILI


STAA wa muvi Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ (pichani) amekwaa skendo ya kutapeli ngawira za Kibongo kiasi cha shilingi milioni 4 kutoka kwa mdau mmoja wa sinema, Felix Ilomo.
Kwa mujibu wa Ilomo ambaye ni mwimbaji wa nyimbo za Injili na mkazi wa Keko jijini Dar, alimkabidhi Dude kiasi hicho cha fedha ili amsimamie kushuti wimbo wake akimuamini yeye ni mzoefu katika masuala ya video.
“Nilimwamini Dude atanisaidia, nikamkabidhi shilingi milioni 4 ambazo alisema zinahitajika ili niweze kurekodi wimbo wangu wa Kwa Neema Yako Yesu. Fedha hizo nilimpa toka mwanzoni mwa mwaka huu lakini kila kukicha sioni video wala nini, alidai tungeshuti katikati ya Januari, nikimuuliza ananipiga kiswahili hadi leo. Nimechoka lazima nimchukulie hatua za kisheria,” alisema Ilomo.
Dude alipotafutwa kwa njia ya simu na kusomewa mashitaka, alisema: “Siwezi kumtapeli bwana, nashindwa kuelewa kwa nini anakosa imani wakati nimeshamwambia asubiri jamaa arudi tutarekodi.”

Thursday, August 2, 2012

FACEBOOK KUMCHAFUA SHILOLE


Zuwena Mohammed ‘Shilole’.

STAA wa filamu anayetamba katika anga la muziki wa mwambao, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ amechafuliwa vibaya na mtu ambaye anatumia jina lake kupitia mtandao wa Kijamii wa Facebook kwa njia ya kujipatia fedha isivyo halali,
Akizungumza hivi karibuni, Shilole alisema kuwa kuna mtu amekuwa akitumia jina lake kwenye mtandao huo na kuwaomba marafiki zake wamtumie fedha kwa kuwa mwanaye ni mgonjwa wakati si kweli.
“Jamani huyu mtu ni Shilole feki, tena ananidhalilisha sana kwa kuonesha kuwa nina matatizo wakati si kweli, kama ningekuwa na matatizo ningetumia magazeti na mitandao ingefuata baadaye,” alisema Shilole.
Staa huyo anayetamba na muziki wa mduara alisema kuwa aligundua hila hiyo baada ya kukutana na mtu barabarani na kumpa pole kwa kuuguza mtoto wake na kama alipata michango aliyoiomba kupitia Facebook.
“Natoa taadhari kwa mashabiki wangu wasikubali kumchangia mtu huyo kwani ni tapeli anayetumia jina langu kujipatia kipato, siku nikiwa na matatizo watayajua kupitia magazeti,” alisema.

NANA: NIMEROGWA


Pichani ni pozi tofauti za Nana alivyo kwa sasa.


MSANII wa siku nyingi wa Kundi la sanaa la maonesho la Kaole, Tausi Chuwa‘Nana’ameibuka hivi karibuni na kudai kuwa, amefanyiwa mambo ya kilozi na watu wanaotaka kumdhurumu nyumba yake,

Nana amesema kuwa, amejenga nyumba yake maeneo ya Kiwalani, jijini Dar lakini kuna watu wenye tamaa wanaotaka kummaliza kishirikina ili waweze kuichukua nyumba hiyo ambayo ameijenga kwa jasho lake.
“Kwa kweli ninaamini kuwa nimerogwa lakini sitapenda kuwataja wahusika walionifanyia hivyo kwa sasa, kwani hata nikiwataja hakuna anayeweza kuamini kama wanaweza kunifanyia ubaya ili nisiweze kuwa na mbele wala nyuma katika maisha yangu.
“Ndugu zangu wamenipeleka kwa waganga wakidhani miye ni kichaaa wakati si kweli, miye siyo kichaa ingawaje ninakiri kurogwa ili kuvurugiwa mambo yangu bado nina akili timamu najua kila ninachokifanya,” alisema.
Pia, msanii huyo amelalamikia kitendo cha kufungiwa ndani kwa wiki nzima ili asiweze kutoka na kuweza kufanya mambo yake ya kutafuta haki zake ili aweze kuishi na mwanaye nyumbani kwake hapo.
“Nafungiwa na ndugu zangu hata siku tatu au wiki ili nisitoke nje kwa kuaminika kuwa nimerukwa na akili kitendo ambacho sikipendi katika maisha yangu,” alisema kwa hasira Nana.

WAKATI MUMEWE AKISOTA JELA,JACK PATRICK AVUA PETE YA NDOA


Jacqueline Patrick ‘Jack’.

NDOA ya mwanamitindo Jacqueline Patrick ‘Jack’ na mumewe Abdulatifu Fundikira a.k.a Tiff ipo hatarini kuvunjika na habari kutoka jikoni ni kwamba, sasa Jack amevua pete ya ndoa na kubaki na ile ya uchumba.
Jack amefanya kitendo hicho, wakati mumewe akila msoto nyuma ya nondo katika Gereza la Keko, Dar akisubiri kesi yake ya madai ya kujihusisha na biashara haramu ya madawa ya kulevya inayoendelea katika Mahakama ya Kisutu jijini.
Mwandishi wetu alimnasa mwanamitindo huyo mrembo, juzikati, jijini Dar es Salaam, akijivinjari bila pete ya ndoa, ndipo alipomuuliza na kumpa majibu ya kushangaza kama siyo ya kushtusha.
SIKIA SABABU ZAKE
“Najua wengi wanaweza kunishangaa wakiniona sina pete yangu ya ndoa, lakini nataka kusema kwamba nipo sahihi na ninajua ninachokifanya. Kwa sasa ni kama sina ndoa au ndoa ipo nusu nusu.
“Siyo makosa nikisema kuwa, naona kama niko mguu ndani mguu nje. Hiyo ndiyo sababu kubwa iliyonifanya niamue kuvua pete yangu ya ndoa,” alisema Jack na kuongeza:
“Unajua mume wangu yupo kwenye matatizo sasa hivi (gerezani) na sijui nini cha kufanya. Kifupi nipo katika wakati mgumu sana, ndiyo maana nimefikia uamuzi wa kuondoa pete kidoleni mwangu.
“Nahisi kama inazidi kuniongezea machungu moyoni mwangu. Sioni faida ya kuivaa kabisa. Afadhali nibaki na hii ya uchumba.”
PEKUPEKU MITAANI

Chanzo chetu makini, kwa sharti la kutotajwa jina lake, kilitupenyezea habari kwamba, tangu Tiff apelekwe mahabusu katika Gereza la Keko, uhusiano kati ya wawili hao umelegalega.
“Kwanza Jack hajaenda kumuona mumewe hata siku moja...unajua hawa bwana, ugomvi wao haukuanza juzi, ni kabla jamaa yake hajapata matatizo. Sidhani kama kuna ndoa tena pale...na hivi mumewe yupo sero ndiyo kabisa,” kilipasha chanzo chetu.
Kikaongeza: “Jaribuni kufuatilia zaidi, lakini wale kuendelea tena, sidhani kama itawezekana kwa hali waliyofikia.”
SAUTI YA FUNDIKIRA KUTOKA KEKO
Tulifunga safari hadi katika Gereza la Keko, Dar kwa lengo la kumtembelea Abdulatifu ikiwa ni pamoja na kufuatilia habari hii.
Huyu hapa anazungumza: “Mke wangu hajafanya kitu kizuri. Inaniuma sana kusikia kwamba amevua pete ya ndoa. Jambo hilo linaninyima amani sana. Mimi kupata matatizo siyo sababu ya msingi ya yeye kuvua pete. Kwa kweli imeniuma sana.”

Wednesday, August 1, 2012

LULU APENYEZEWA CHAKULA CHENYE SUMU GEREZANI


LINGINE limeibuka! Kuna madai kwamba chakula kinachosadikiwa kuwa na sumu kilipenyezwa kwenye Gereza la Segerea, Dar es Salaam, mlengwa wa kukila alikuwa Elizabeth Michael ‘Lulu’,

Kwa mujibu wa chanzo chetu, kijana kutoka Mwanza anayekadiriwa kuwa na miaka 18-20 anatajwa kuhusika na ubebaji wa chakula hicho ambacho hadi sasa haijajulikana nani amesimama nyuma ya zoezi hilo.

HABARI KAMILI

Habari zinasema kuwa siku chache zilizopita kijana huyo akiwa na mfuko wa rambo wenye chakula hicho alifika gerezani hapo na kufanya ujanja wa kuingia ili kumpa chakula Lulu.

“Huyu kijana alipofika hapa alitumia ujanja wake akaingia ndani kwa lengo la kumpa chakula Lulu akijifanya ametumwa na familia,” kilisema chanzo cha ndani.

Inadaiwa kabla hajafika kwenye eneo la kukutana na Lulu, maafande walio macho muda wote huku wakizingatia maadili ya kazi, walimnasa kijana na kumbana kwa maswali ambapo alishindwa kujibu na kuingia mitini.

“Kabla hajamfikia Lulu yule kijana alidakwa na maafande wa pale Segerea, akapigwa maswali, lakini baadaye akaingia mitini. Nadhani alijua kiwewaka. Hapo ndipo alipotiliwa shaka kuwa huenda chakula chake hakikuwa na usalama ndani yake na huenda kilikuwa na sumu,” kilisema chanzo hicho.

KINGEANGAMIZA WENGI

Kwa mujibu wa habari za ndani kutoka jeshi la magareza, raia anapotumikia kifungo kuna watu wake watatu tu, wenye picha za vipande (passport size) ndiyo wanaoruhusiwa kumpelekea chakula.

Sheria ya magereza inafafanua kwamba kabla mfungwa hajakula chakula alichopelekewa, mpelekaji anatakiwa kuwa mtu wa kwanza kukionja ili kuondoa shaka kama kitakuwa na kitu kibaya kwa hiyo kijana huyo angetakuwa kula kabla ya Lulu.

“Unajua yule kijana kama kweli alitumwa kumwingizia Lulu chakula chenye sumu, basi aliingizwa mkenge, maana kabla ya kumpa Lulu ale, angetakiwa kula yeye kwanza, sasa si angekufa!

“Mbaya zaidi, chakula hicho kingeendelea kutoa madhara kwa wengine maana kuna wafungwa huwa wanasaidiana chakula. Kwa hiyo unaweza kuona ni jinsi gani chakula kile kama kilikuwa na sumu kingeleta madhara makubwa,” kiliongeza chanzo.

NDUGU WAPONGEZA

Jumamosi (juzi) gazeti hili lilimsaka mama Lulu (Lucresia Karugila) kwa kupitia simu yake ya mkononi, hakupatikana lakini ndugu mmoja wa Lulu ambaye aliomba hifadhi ya jina alisema ndugu wamewapongeza maafande wa magereza ya Segerea kwa sababu walimudu vyema kumdhibiti kijana huyo.

Hata hivyo, ndugu huyo alisema hakuna ushahidi wa moja kwa moja kama kweli chakula hicho kilikuwa na sumu kwani wapo wanaoamini kuwa, kijana huyo ni shabiki mkubwa wa Lulu kwa hiyo aliamini kumpelekea chakula ni sehemu ya kutoa hisia za mapenzi yake.

KWA NINI KIWE NA SUMU?

Ndugu huyo aliendelea kudai kuwa sumu ilidhaniwa kuwepo kwa sababu toka Lulu ashikiliwe na vyombo vya sheria kwa madai ya kujua chochote kuhusu kifo cha Steven Kanumba, amekuwa akipewa ulinzi mkali kwa sababu ya mitazamo ya baadhi ya watu kwamba staa huyo ndiye aliyemuua Kanumba.

JESHI LA MAGEREZA LINASEMAJE?

Baada ya kupata taarifa hizo, Julai 24, mwaka huu waandishi wetu walifika Makao Makuu ya Jeshi la Magereza Tanzania, jijini Dar na kuzungumza na msemaji wa jeshi hilo, Omary Mtinga kwa lengo la kutaka kujua anasemaje kuhusu madai hayo.

Hata hivyo, msemaji huyo alisema jeshi lake halina taarifa hizo lakini akaomba apewe muda ili aweze kuzifuatilia.

Julai 28, mwaka huu, paparazi wetu alimpigia simu msemaji huyo na kumkumbushia kuhusu ahadi yake, lakini akasema yuko safarini nje ya jiji la Dar na alitarajia kurudi wiki inayoanzia leo.

Lakini kwa msisitizo mkubwa Afande mtinga alisema aliwatuma vijana wake wa makao makuu kufanya upelelezi mkali gerezani Segerea, kwa hiyo akirudi atapata jibu na kuyaweka wazi.

Akaongeza: “Lakini kama ni kweli ni kosa kubwa, mtu hawezi kupita bila utaratibu. Kila mfungwa ana utaratibu wa watu watatu kumpelekea chakula gerezani. Hata huyo (Lulu) ana watu maalum watatu wakiongozwa na mama yake mzazi ndiyo wanaoruhiswa kumpelekea chakula.”

MZEE SMALL BADO HALI MBAYA,APATWA NA UGONJWA WA KUPOOZA

HUJAFA, hujaumbika! Hali ya staa wa vichekesho na filamu Bongo, Said Mohamed Ngamba ‘Mzee Small’ bado hairidhishi tangu mwezi Mei, mwaka huu alipopatwa na ugonjwa wa kupooza ghafla nyumbani kwake Tabata-Kimanga jijini Dar es Salaam,
Mzee Small alipatwa na ugonjwa huo wakati akitokea mkoani Mwanza alipokwenda kufanya kampeni ya kupinga mauaji ya albino, safari ambayo aliambatana na mkongwe mwenzie kwenye sanaa, Bi Chau.
TUJIUNGE NA MKEWE
Akizungumza tulipofika nyumbani kwake kumjulia hali, mke wa staa huyo, Fatuma Said alisema siku mumewe alipopata matatizo alifika salama na kuanza shughuli zake za kila siku lakini kesho yake, ghafla alishtuka kumuona mumewe ametokewa na hali hiyo (kupooza) ghafla.
Alisema kuwa mara baada ya kufikishwa kwenye Hospitali ya Amana, Dar, madaktari walimcheki na kugundua alipatwa na stroke (kupooza) ndipo matibabu yakaanza.
BADO HALI TETE
Akizungumzia afya yake, Mzee Small alisema: “Kwa kweli nilitakiwa kurudi hospitali kwa ajili ya kuchekiwa upya na kufanyiwa mazoezi tangu Julai 5, mwaka huu lakini kwa kuwa sikuwa na fedha sikuweza kwenda hivyo bado hali ni mbaya na naomba Watanzania wanisaidie.”
KUTOKA KWA MHARIRI
Kwa kutambua kuwa Mzee Small kwa sasa anashindwa kuendelea na kazi zake kutokana na ugonjwa huo, ni wazi kuwa anahitaji msaada wa kuweza kujikimu kwa matibabu.
Kama unagushwa kumsaidia Mzee Small, basi tuma chochote ulichonacho kwa njia ya M-Pesa kwa namba yake ambayo ni 0754 647265.

THEA AANZA UPYA BAADA YA KUMPOTEZA MWANAE

BAADA  ya mwigizaji Salome Ndumbagwe Mesayo ‘Thea’ kupata matatizo ya kupoteza kichanga chake juzikati, hivi ameanza upya kazi zake za uigizaji wa filamu.
Akizungumza na na Ijumaa Wikienda wikiendi iliyopita jijini Dar, Thea alisema kuwa anamshukuru Mungu kwa kile kilichomtokea kwani yeye si wa kwanza kupatwa na matatizo hayo na sasa ameamua kurudi tena kwenye gemu.
Thea alisema kuwa ameamua kujichimbia kambini kwenye Hoteli ya Lamada iliyopo Ilala, Dar kwa ajili ya kupoteza mawazo na kuanza kufanya shughuli zake kama ilivyokuwa mwanzo.
Mwanadada huyo ambaye ni mke wa ndoa wa mwigizaji Michael Sangu ‘Mike’ alisema hapendi kuongelea kilichomtokea kwani anaamini siku ikifika Mungu atampa mtoto mwingine.