INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Thursday, October 18, 2012

MATONYA AKIRI KUWA BONGO MOVIE WANAIGIZA HADI KWENYE MAPENZI


Inadaiwa kuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya Matonya aka Tonya Boy,alifungiwa ndani kimapenzi na mmoja ya wasanii wa bongo movie na kulizwa shilingi za kitanzania milioni 6, sasa ameamua kuweka wazi kuwa wanawake wa tasnia hiyo ni michosho kwani wanapemnda hela na wanaleta maigizo hadi kwenye mapenzi.

MATONYA,alidai kuwa kuna mmoja wa mademu wazuri wanaovuma kwenye tasnia bongo movie ndiye aliyefanya mchezo huo mchafu kwani alijifanya anampenda sana kumbe alikuwa anamuigizia na alikuwa na ishu yake.

Alidai baada ya tukio hilo kutokeo demu huyo hakumuona tena na alikuja kusikia yupo mkoani kitu ambacho kilimfanya aishiwe nguvu kwani hakuamini kilichotokea na hapo ndipo alipoamini kuwa mademu wa tasnia hiyo ni wapigaji na ukiwaonesha kwako utajuta.

“Bongo movie hakuna demu yani hata bure siwataki tena yani wanaleta maigizo hadi kwenye mapenzi dah kweli hii tasnia ina laana na inahitaji kuombewa kwani wasanii wake wanatamaa ya hela na wanamapepo ya ngono yani wakimuona mwanaume ana hela basi mate yanawatoka, hata wa bure siwataki tena,”
alidai.

Hata hivyo alipoulizwa jina la msanii huyo wa filamu alishindwa kumtaja kwa madai kuwa hata kama aliiba kiasi hicho cha pesa lakini kwa upande wake hana bifu naye ingawa hatamani hata kumuona.

ODAMA SASA AINGIA KIKAZI ZAAIDI




MWANADADA nguli katika tasnia ya filamu Swahiliwood, Jenifer Kyaka Odama ameingia katika kundi la akina dada wajasiriamali baada ya kuamua kufungua kampuni yake ya utengenezaji wa filamu kwa ajili ya utayarishaji wa filamu zake.

Kwa sasa hali ya ushindani ni kubwa sana kwa hiyo kama huna kampuni kwa ajili ya utayarishaji wa filamu zako utasumbuka hata kuharibu kazi yako.

Unapotumia kampuni ya nje unakutana na changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na kucheleweshewa kazi zako lakini pia unakosa usimamizi wa kazi hiyo, unaweza kupoteza muda kwani unapompatia kazi mtendaji hata kama ana kazi nyingi hasemi, hali ambayo huharibu ratiba kwa kucheleweshewa kazi hata kuharibiwa, anasema Odama.

Odama analia na wale wahariri wasio waaminifu kwani wao huwa ni sababu ya filamu kuchelewa au kuharibika, jambo ambalo linawakabili wasanii wengi kupoteza muda wa kutoa filamu zao kwa wakati.

Msanii huyo ni kati ya wasanii waliopo katika tasnia ya filamu kwa muda mrefu sasa na ameigiza filamu 36.

Kati ya filamu hizo, filamu 9 ameshiriki akiwa kama mtayarishaji. Ameigiza filamu kama All About Love, Odama, Shumileta, Rude na filamu nyingine nyingi.



Chanzo : Mwanaspoti
Written by Sports | February 21, 2012 | 0
Imechukuliwa kutoka katika tovuti hii: http://www.dullonet.com/sports/2012/02/21/odama-sasa-aingia-kikazi-zaidi/

WASANII LINDENI FARAGHA ZENU


Hivi karibuni kumeibuka mtindo wa wasanii wa kike na hata wa kiume kupata shutuma za aina mbali mbali ambazo nyingi kati ya hizo ziko kwenye mrengo wa maisha ya mtu ya ndani ambayo mara nyingi yanatakiwa kubaki kwa mtu mwenyewe.

Hapa tunamaanisha masuala yote yanayohusu faragha ya ndani kama masuala ya ndani ya kimahusiano, maadili, staha, utu na heshima ya mwili wa mtu au watu. Kwa bahati mbaya tangu masuala haya yameanza kuibuka hayapungui, bali yanazidi kuongezeka.

Kwa asilimia kubwa upande wa faragha ya matendo yanayohusiana na mahusiano na faragha ya viungo vya wahusika ndio vimekuwa ajenda kubwa katika vyombo vya habari. Matukio hayo yamekuwa si haba kujadiliwa katika mitandao ya kijamii pamoja na kurasa za magazeti mbali mbali karibu kila mwezi.

Tumeanza na maelezo hayo ili kujaribu kujadili yale yatokanayo na aina hii ya fedheha au kadhia ambayo imeonekana kwamba Watanzania wameanza kuichukia. Tutaanza na tukio la Diamond ambaye yeye alifanya kile kisichotarajiwa kwa kuonyesha nguo zake za ndani katika jukwaa la shoo ya Fiesta Dar-Es-Salaam kama ishara ya kuonyesha usafi wake.
Hapa cha kujiuliza je katika matendo yote ambayo Diamond angeweza kuyafanya ili kuiaminisha jamii juu ya usafi wake, hili la kuonyesha nguo za ndani ndio lilikuwa lenye umuhimu mkubwa kiasi cha kuamua kufanya hivyo? Je hakukuwa na aina nyingine ya kubainisha hilo?

Jambo lingine ambalo linakera zaidi ni namna wasanii wa kiume ambavyo wanapenda kuning’iza suruali ama kaptura zao (mlegezo). Wasanii hao wengi wao ni wale wa muziki wa kizazi kipya wamekuwa na tabia ambayo imekuwa inalalamikiwa sana ya kuvaa Jeans aina ya suruali na Kaptura chini ya makalio.

Narudi kwa dada zangu ambao wao ndio wanaonekana wahanga wakubwa wa matukio ya namna hii. Hatumaanishi kwamba tunataka kuwananga ama kuwasimanga, la hasha bali tunalotaka kushauri ni namna wasanii iwe wa muziki, filamu ama sanaa ambayo kwa namna moja ama nyingine inawafanya kuwa karibu na jamii.

Ni aibu kubwa kwa msanii kufanya jambo ambalo kwa maudhui yake kama hatakuwa na uwezo wa kulizuia lisidhuru heshima na haiba yake katika siku za usoni akaliruhusu lifanyike. Hapa tunamaanisha kwa mfano matumizi ya picha kwa kutumia aina yoyote ya camera iwe ya picha mgando ama zenye motion.

Ukiangalia kwa ndani mambo mengi ya namna hii hutokana na mazoea ambapo mtu huanza pole pole kwa kujipiga picha kisha akaziangalia mwenyewe. Baada ya hapo atapiga picha na kisha kuziangalia na wenzake mara nyingi huwa ni wale walioshibana wa jinsia moja.

Kisha tabia hiyo huanza kuenea kwenda kwa wapenzi wo. Hapa ndipo tatizo kubwa hutokea.
Shughuli ya faragha huanza kupungua kadiri siku zinavyokwenda ambapo mtu na rafiki zake huanza kuonyeshana picha hizo ambapo mpenzi wa kiume naye huanza kuwaonyesha maswahiba zake wa karibu na kisha kwa kutegemea uimara ama hatua ya uhusiano uliopo kati ya wahusika hao wote basi athari hujitokeza pale uhusiano huo baina ya watu hao utakapoharibika.
Upande mmoja wapo katika hali ya kukomoa ama kulipa kisasi huamua kuzisambaza kwa jamii kwa sababu anajua madhara ambayo yatamkuta mlengwa. Ushahidi wa hili lipo kwenye picha za mwanadada ambaye alishiriki video ya Masogange, Agnes.

Hatutaki kuingia kwa undani kuhusiana na suala hilo ila matokeo yake wote mnayajua.
Mwingine ambaye yamemkuta maswahibu ya namna hii ni pamoja na msanii wa muvi za kibongo Rayuu ambaye yeye kwa utashi wake ambao ni ngumu kuuelewa aliweka picha zake zikionyesha tattoo zilizoenea katika maeneo mbalimbali katika sehemu kubwa zaidi ya mwili wake, kitendo kilichoamsha majibizano makali kati yake na mdau mwingine wa tasnia ya filamu Sintah ambaye alihisi wao kama kina dada wamedhalilishwa na msichana mwenzao.

Pili uvaaji wa dada zetu ndio kichocheo kikubwa cha matatizo haya.Haiwezekani kwa akili ya kawaida tu mtu kuvaa nguo fupi isiyositiri faragha kwa asilimia 90 katika tafrija, sherehe ama shoo ya kijamii na kutegemea kwamba hali itakuwa shwari. Wema na Aunt Ezekiel ni mashuhuda wazuri katika hili.

Hatuna uhakika kama Aunt wakati analitolea utetezi suala hili alilifikiria kwa umakini wa hali ya juu na kusema waandishi wa habari wamekuwa wanawavizia chini ya jukwaa ili wawapige picha zitakazo onyshesha nguo za ndani.
Tunatambua kazi ya kueleimisha ama kuikosoa jamii ni ngumu lakini tunapenda kusema kwa hili itabidi dada zetu wabadilike kwani hawana ma jeans au nguo ndefu itakayofunika ugoko na kuondoa kadhia hiyo. Je ni lazima msanii avae nguo fupi sana kila wakati anapokuwa katika tafrija ya aina yeyote ile, ikiwemo na kwenye ku act?
Tunafikiri kama sio picha zile zilizowaonyesha Wema na Aunt Ezekiel namna ile, basi Jukwaa la fiesta jijini Dar-Es-Salaam lingekuwa na viroja kwani siku ile wengi wa wasanii walikuwa na tahadhari ya hali ya juu na kuamua kuvaa tofauti na hisia zao huwa zinavyowatuma.

Tulimwona jinsi Shilole alivyokuwa mwangalifu na hata ilimbidi kuvaa nguo ambayo ilimkwepesha na dhahama za picha chafu. Yeye pamoja na madensa wake walibadili aina ya nguo ambazo mara nyingi hutumia kwenye shoo zake.
Shilole akiwa jukwaani kwenye Fiesta Dar
Wasanii wanatakiwa watambue maana ya kudumisha uhusiano mzuri na jamii, usio na mikwaruzano ya ki itikadi, hisia, jinsia, dini, kabila wala fikra. Ingekuwa katika nchi nyingine tUnafikiri wasanii kama Diamond, Aunt Ezekiel na Wema sepetu wangepoteza nafasi zao za kibalozi kama wangekuwa nayo kama alivyo Diamond na ubalozi wa utalii.

Tunakumbushia tu…..Faragha ni kitu muhimu katika kulinda utu, kudumisha heshima na kustawisha maadili katika jamii.

Source: Vituko vya Mtaa

BURUDANI: KABURI LA KANUMBA LAJENGWA UPYA




Muonekano mpya wa kaburi la Steven Kanumba

 Kaburi la aliyekuwa msanii maarufu wa filamu Tanzania, Steven  Charles Kanumba limeanza kujengwa upya ikiwa ni baada ya wasanii wenzake kushushuliwa kuhusiana na muonekano wake ulivyokuwa.
Marehemu Steven Kanumba 'The great' enzi za uhai wake.

Hatua ya kulijenga upya kaburi hilo imechukuliwa na Mama yake mzazi, Flora Mtegoa na kampuni ya Steps kutokana na mauzo ya  kazi zake mbalimbali za filamu, hivyo  wameona ni vyema wakalijenga upya kwani lilikuwa ni gumzo kwa watu mbalimbali waliokuwa wakihoji hadhi ya kaburi hilo na umaarufu wa marehemu Kanumba.
Akizungumza na paparazi wetu, Mama Kanumba alisema kauli za kaburi  hilo kujengwa upya zilikuwa kama wimbo wa taifa  lakini  kuna mambo alikuwa akiyamalizia, hivyo kwa sasa ameshalijenga vizuri tofauti na lilivyokuwa mwanzo.
Mama mzazi wa marfehemu Steven Kanumba amesema kuwa Kaburi la Kanumba limejengwa upya japokuwa baba yake alisema hakuna haja ya kulijenga tena lakini lakini bado ana uchungu na mwanae japokuwa amemuacha huku bado anampenda na ataendelea kumkumbuka, kwa kushirikiana na kampuni ya Steps waumelijengea vizuri.
 Hivi karibuni wasanii mbalimbali wa filamu Bongo walilitembelea kaburi hilo na kupatwa na uchungu lakini walishushuliwa na mwenzao na kwa kuwaambia kuwa wamelisusa kaburi hilo.
 Imeonekana kuwa kaburi hilo halikuwa na hadhi ikilinganishwa  na umaarufu aliokuwa nao Kanumba, hakustahili kulala  kwenye kaburi lile, hivyo kuwataka kuchangishana fedha ili lijengwe vizuri lakini hakuna aliyeunga mkono badala yake waliishia kupeana manenoyasiyofaa

TANZANIA ENTERTAINMENT NEWS: SHILOLE ANENA KUHUSU KUONYESHA NYETI MAJUKWAANI



Kufuatia wasanii wengi nchini Tanzania hususani wa Bongo Movies na wale wa Bongo Fleva kuvaa nusu uchi wanapokuwa katika majukwaa kwa ajili ya Burudani imedaiwa kuwa ni tabia ya msanii binafsi na sio wote kama ambavyo wengi wanafikiri.
Akizungumza na JAIZMELALEO Mwigizaji wa Bongo Movies na Bongo Fleva, Zuwena Mohammed "Shilole" amesema licha ya BASATA kutamka na kuwataka wasanii waache tabia hiyo, kwa upande wake analiona kama ni suala la mtu binafsi kwani sio wote wanaopenda kufanya hivyo wanapokuwa majukwaani.
Itakumbukwa katika siku za hivi karibuni kumeshuhudiwa wasanii Wema Sepetu na Aunt Ezekiel wakiomba msamaha kwa wadau wa Bongo Movies kutokana na kuonyesha nyeti zao jukwaa.
You might a

Monday, October 15, 2012

NEY WA MITEGO AWASHAMBULIA UPYA BONGO MOVIE


 
BAADA ya ngoma yake ya ‘Nasema Nao’, kuleta misusuko kibao ndani ya tasnia ya filamu bongo kiasi cha kutishiwa maisha sasa msanii Ney Wa Mitego ameamua kutoa majibu kwa watu waliodhani kuwa hatoweza kuendelea kuwapa ukweli wao wasanii wa bongo movie, ambapo sasa pini lake jipya la ‘Wamenichokoza’, ni zaidi ya ‘Nasema Nao’ kwani ujumbe wake mzito.

Msanii huyo ameweza kufikisha ujumbe kwa wasanii wa bongo movie hasa wanawake ambao wanaishi kwa kutengemea wanaume, huku wakisahau kuwa wao ni kioo cha jamii wanatakiwa kuishi maisha ambayo ni mfano kwa wengine.

Akizungumza msanii huyo alisema kuwa ngoma hiyo kimewajibu wale wote waliodhani kuwa hatoweza kuleta mashambulizi mengine, kwani baada ya ngoma yake ya ‘Nasema Nao’ alipokea simu nyingi za vitisho kutoka kwa watu mbalimbali.

Msanii huyo alidai kuwa kufanya kwake muziki hakumanishi kwamba anatafuta bifu na mtu, kwani anafanya kwa lengo la kuburudisha na kufundisha jamii hivyo kila kitu ambacho anakuwa anakiimba ni mawazo yake lakini anachukizwa na watu wanaomtishia maisha, kamwe hawatoweza kumziba mdomo.

“Hakuna mtu anayeweza kuniziba mdomo na ndiyo maana kazi zangu zinakuwa na ukweli siku zote, na ndani ya ngoma hii mpya utaona vitu vilivyochambuliwa na kufanyiwa uchunguzi wa kina, mbona watajuta mwaka huu,” alisema Ney.

WEMA SEPETU VS AUNT EZEKIEL'WEMA SEPETU NA AUNT EZEKIEL WAAMUA KUOMBA RADHI KUTOKA NA PICHA CHAFU WALIZOPIGA WAKATI WA FIESTA



Wema

Waigizaji wa filamu nchini Wema Sepetu na Aunt Ezekiel wamewaomba radhi watanzania kwa picha zao mbaya walizopigwa kwenye show za Fiesta.

Wasanii hao wamezungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa habari maelezo jijini Dar es Salaam kwaajili ya kuomba radhi kwa kupigwa picha hizo za nusu utupu walizopigwa kwenye show hizo.


Wakiongena waandishi wa habari Aunty Ezekiel amesema ameumizwa na kitendo hicho kwakuwa wao kama wanawake katika jamii, wana wazazi, ndugu jamaa, marafiki pamoja na mashabiki wao wanaowapenda na kuwaheshimu.


Ezekiel

Hivi karibu Aunty Ezekiel alijitetea na kunukuliwa kwenye chanzo kimoja akisema, “Ni kweli nilikuwa ninacheza katika Jukwaa (Stage) na nilikuwa nimekunywa, lakini sikuwa nimedhamiria kukaa uchi bali ni mbinu za wapiga picha ambao walitumia njia ya kuamua kunidhalilisha kwa kunipiga picha wakiwa chini ya Jukwaa (Stage) ili wapate kuuza magazeti yao, hata ukiangalia picha zenyewe zimepigwa kiujanja sana.”

Waigizaji hao waliongozana na katibu Mkuu wa shirikisho la filamu Tanzania, TAFF, Wilson Makubi.


WOLPER AKANUSHA KUURUDIA UKRISTO BAADA YA KUACHIKA

 
               Jacqueline Wolper.

MSANII wa filamu ambaye alisilimu, Jacqueline Wolper amesema licha ya kwamba ameachana na mchumba wake Ramadhani Mtoro ‘Dallas’ atabaki kuwa Muislam hadi mwisho wa maisha yake.
Wolper ambaye sasa anafahamika kwa jina la Ilham alisema, ni kweli alibadili dini baada ya kuchumbiwa na Dallas lakini atakuwa anamchezea Mungu kama ataamua kurudi kwenye Ukristo baada ya uchumba kuvunjika.
“Mimi nitabaki kuwa Muislam hadi kifo, siwezi kurudi kwenye Ukristo kwani nilikuwa nikiupenda Uislam.
Akitokea mwanaume Muislam akataka kunioa niko tayari na hata akija Mkristo pia ila nitaendelea kuwa Muislam,” alisema Wolper.
Wolper alibadili dini siku chache zilizopita baada ya kuingia kwenye uhusiano na Dallas lakini hivi karibuni kulikuwa na madai kwamba amerudi kwenye Ukristo, jambo ambalo amelikanusha.

SHILOLE AKANA KUTOKA KIMAPENZI NA OMMY DIMPOZ



INASEMEKANA kuwa kimwana anayetesa kwenye filamu na muziki Shilole na Ommy Dimpoz, wapo katika mahusiano ya chini chini na hawataki kuyaweka wazi kwa kuogopa midomo ya watu.

Chanzo kilicho karibu na msanii
Shilole kilitoa fununu ya ishu hiyo kwa kudai kuwa wasanii hao mara nyingi wamekuwa wakikutana nyakati za usiku na awali kabisa walikuwa kama marafiki lakini kadri siku zilivyokuwa zinasonga mbele ukaribu wao uliongezeka na kuanzisha mahusiano.

Chanzo hichokilidai kuwa hakuna mtu anayejua wasanii hao kama wana mahusiano, kwani wanafanya siri kwa kuogopa vyombo vya habari na hata wanapotaka kuonana huwa wanatumia usafiri wa kukodi kwa sababu tayari magari yao yanajulikana.


“Ishu ambayo mimi naijua ndiyo hiyo kwa sababu ukaribu wao umekuwa mkubwa na sijui kama wanaweza kusema si wapenzi, kuna sehemu tata ambazo nimewahi kuwakuta na wakaniambia nisitoe ishu hiyo kwa mtu yeyote,”
kilidai chanzo hicho.

Hata hivyo chanzo hicho kilienda mbali zaidi na kudai kuwa zipo tabia ambazo mara nyingi Shilole amekuwa akizifanya, kama za kutoka usiku lakini sasa hana ishu hizo na inadaiwa kuwa Dimpoz ndiyo aliyemshauri na kumsihi atuliye na kama wanataka kutoka basi lazima wawe wote.


Mwandishi wa habari hii
, alimtafuta Shilole ili kuzungumza naye, na alipopatikana alidai kuwa yupo Morogoro kikazi lakini kuhusu kutoka na Dimpoz alikana kwa madai wao ni marafiki na huwa wanakutana kwenye kazi tu.

Aliongeza kuwa yeye anatoka na msanii mwingine kabisa ambaye mara zote watu wamekuwa wakimuona nae.


“Sina mahusiano ya kimapenzi na Dimpoz na huyo mtu anayetaka kuzungumzia ishu ambayo haipo anamatatizo yake, Dimpoz ni rafiki yangu sana tena kwa sababu ni msanii mwenzangu na hakuna kikubwa ambacho kinaendelea kati yetu,”
alisema Shilole.

SNURA AKIRI KUTAMANI NDOA

Snura Mushi akiwa ameweka pozi


MWIGIZAJI wa filamu za Kibongo ambaye pia ni msanii wa Bongo Fleva, Snura Mushi amefunguka kuwa anatamani ndoa kuliko kitu kingine chochote, japokuwa bado hajapata mwanaume anayemfaa,
Akichonga na safu hii, Snura alitiririka kuwa amekuwa akimwomba Mungu usiku na mchana ampatie mume mwema atakayekuwa na mapenzi ya dhati, mwenye heshima na mcha Mungu lakini wapi!
“Namuomba Mungu anipe mume mwema na hivi sasa nafanya kazi kwa bidii kwani ndiyo mkombozi wangu, najua siku ikifika Mungu atanipa mume mwema,” alisema Snura.

BABA MZAZI WA DIAMOND ATOA SABABU ZA WEMA KUWA MKWE WAKE

BABA mzazi wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Abdul Juma amefunguka juu ya mrembo anayetaka aolewe na mwanaye huyo.
Akizungumza na paparazi wetu jijini Dar, Septemba 27, mwaka huu, Mzee Abdul, mkazi wa Magomeni Kagera, Dar alisema awali alimtaka Diamond aoe msichana asiye maarufu na alimtambulisha kwake, lakini msanii huyo      akachomoa.
Akasema baada ya Diamond kuchomoa, mwaka jana alimpeleka Wema nyumbani kwake na kumwambia ndiye chaguo lake.
“Niliwahi kumwonesha Diamond msichana wa kumuoa, lakini akampotezea, mwaka jana akaja na Wema akidai ndiye chaguo lake.
“Hata hivyo, baadaye nikasoma kwenye magazeti ameachana na Wema, sasa yupo na Jokate, mara nikasikia amerudiana na Wema, mara amepata mwingine Kenya, lakini mimi nasema, Diamond muoe Wema, ndiye mwanamke anayekufaa mwanangu,” alisema mzee huyo.
Akasema kigezo anachotumia kumkubali Wema ni kimoja tu, nacho ni hiki, msikie:
“Hata kama ana machafu yake, lakini Wema ni mwanamke muwazi, hafichi mapenzi, wengine wanaficha, wanakuwa na Diamond, lakini wakiulizwa na waandishi wanajibu ni uzushi. Sasa huu usiri kusema kweli si mzuri, kuna kitu kinafichwa katikati.”
Mwezi Agosti mwaka huu, mama mzazi wa Diamond naye alitoa tamko lenye mtazamo wake wa mrembo anayestahili kuolewa na mwanaye.
Mama huyo, Sanura Kasim ‘Sandra’, mkazi wa Sinza Mori, jijini Dar alisema si Wema (Sepetu) wala Jokate (Mwegelo) anayestahili kuolewa na mwanaye.

SHILOLE NA SAJENTI WAKWIDANA CHOONI!


WASANII wa filamu za Kibongo, Zuwena Muhammed ‘Shilole’ na Husna Idd ‘Sajent’ hivi karibuni walizinguana na kufikia hatua ya kukwidana katika choo kilichopo ndani ya viwanja vya Leaders Club jijini Dar.
Chanzo chetu kilichokuwa katika eneo la tukio kilidai kuwa, kisa cha wawili hao kukwidana kilianzia kwenye kikao cha kuchagua uongozi mpya wa Bongo Movies.

Zuwena Muhammed ‘Shilole’.
“Katika kikao hicho, walianza kujadili mwenendo wa wasanii ambapo ilifika wakati Shilole na Sajenti walitofautiana, Shilole alipokwenda chooni, Sajenti alimfuata na huko ndiko kuliibuka timbwili,” kilidai chanzo hicho.
Katika kujua ukweli wa tukio hilo, Ijumaa Wikienda liliwatafuta wahusika ambapo Shilole alipopatikana alisema: “Zile zilikuwa ni tofauti za kawaida tu kama mnavyoweza kutofautiana nyie kazini, kwa sasa tuko sawa.”

Husna Idd

BABY MADAHA AKANUSHA JUU YA KIFO CHA MAMA YAKE MZAZI

SIKU chache baada ya kuenea kwa taarifa kuwa mkali wa ngoma ya Amour ambaye pia anafanya vyema kwenye filamu za Kibongo, Baby Madaha, ameondokewa na mama yake mzazi, staa huyo amefunguka na kuweka mambo sawa kuwa aliyekufa siyo mama yake mzazi kama watu walivyosikia bali ni mama yake mdogo aitwaye Maimuna.
Akichonga na Over The Weekend, Baby Madaha alisema mama yake mzazi yupo hai na hana tatizo lolote la kiafya hivyo watu wasielewe tofauti na kwamba mama yake mdogo ndiye aliyekuwa anaumwa kwa kipindi kirefu kabla ya kukutwa na mauti usiku wa Oktoba 9, mwaka huu na kusafirishwa hadi Musoma kwa mazishi.
“Nawashukuru watu wote walioguswa na kilichotokea lakini naomba kueleza kuwa aliyetutoka siyo mama mzazi kama ilivyoelezwa awali bali ni mdogo wake, mama yangu bado yupo hai na anaendelea na shughuli zake kama kawaida,” alisema Baby Madaha.

Thursday, October 11, 2012

DUDE ALIZWA NA HAUSIGELI

                                    Kulwa Kikumba ‘Dude’.

KIDUME kwenye Bongo Movies, Kulwa Kikumba ‘Dude’ amefanyiwa kitu mbaya na hausigeli baada ya kumtelekeza mtoto wa staa huyo na kumliza vitu vya ndani kisha kutokomea kusikojulikana.
Huku Dude akiwa shooting, Bongowood imeinyaka kuwa, juzikati msaidizi huyo wa ndani  alimwacha mtoto na ‘kuchikichia’ na fedha Sh. laki moja na nusu na vitu vingine vya waifu wa jamaa kama hereni, vipodozi na pafyumu, jambo ambalo jamaa huyo alithibitisha kumtokea.

MONALISA AGEUKIA UJASILIMIA MALI

                               Yvonne-Cheryl Ngatikwa ‘Monalisa’.
STAA wa filamu za Kibongo, Yvonne-Cheryl Ngatikwa ‘Monalisa’, baada ya kujikita kwenye filamu kwa muda mrefu, sasa amegeukia ujasiriamali ambapo amefungua duka la nguo la kisasa ‘boutique’ maeneo ya Kinondoni Meridian, Dar.
 Mona aliiambia Bongowood: “Unajua mimi nina familia, nina mahitaji mbalimbali hivyo siwezi kutegemea filamu tu ambazo napata fedha kwa kuwekeza fedha nyingi, nimeona nijaribu na biashara hii ili nipate kipato  halali.”

UWOYA AKIMBILIA NCHINI USWIZI

 
Irene Uwoya.

TAARIFA zilizotua kwenye meza ya Bongowood zinadai kuwa, Irene Uwoya amekimbilia nchini Uswisi ambako amekwenda kucheki mchongo wa kucheza muvi akitokea pande za Msumbiji alikokwenda akiongozana na mwigizaji Juma Chikoka baada ya kupata shavu la kutengeneza matangazo ya biashara.
Baada ya kunyaka mchongo huo, Bongowood ilimsaka Chikoka ambaye alikiri Uwoya kutimkia Uswisi kwa dili la kucheza filamu.

MSANII WA BONGO MOVIE 'RAYUU' AMAMUA KUCHORA TATOO KATIKA MAKALIO




MSANII ndani ya tasnia ya filamu na tamthilia za kibongo Rayuu amezidi kujichora tattoo kwenye mwili wake ambapo sasa aamua kuchora kiunoni na sehemu nyingine nyeti.

Mtandao huu baada ya kusikia taarifa hizo kutoka kwa rafiki yake kipenzi kuwa msanii huyo amezidi kujichafua mwili kwa kujichora ndipo ulipoamua kumtafuta ili kupata ukweli wa ishu hiyo na alipopatikana alifunguka kuwa ni kweli lakini zote alizochora hazina ubaya wowote.

Rayuu alisema kuwa amechora michoro hiyo sehemu nyingi za mwili wake kuanzia kiunoni, shingoni, kwenye maziwa, makalio na mapaja na alidai kuwa anajisikia furaha kuwa na tattoo hizo kwani hajafanya kwa kushawishiwa na mtu.

Alidai kuwa hata hivyo kati ya michoro hiyo aliouweka kiunoni unasomeka jina lake la ‘Rayuu’ na mengine ni ya aina mbalimbali, “tattoo nazipenda sana lakini kati ya zote hii ya kiunoni naipenda kuliko zote ingawa aliyenichora aliikosea kidogo,” alisema.

MESEJI ZA MAPENZI ZA WAZIRI ZANASWA ZIKIWA NJIANI KWENDA KWA LULU MICHAEL


Meseji zenye maneno ya kimahaba za kumshawishi kimapenzi staa wa filam za kibongo Lulu Michael kutoka kwa waziri wa wizara moja nyeti serikalini zimezagaa mitaani....

Kwa sasa Lulu  yupo nyuma ya nondo katika gereza la segerea akikabiliwa na kesi ya mauaji ya Steven Kanumba....

Inaelezwa kuwa mawasiliano ya wawili hao yalianza miezi kadhaa kabla ya Lulu kukutwa na msaala huo....

Vyanzo vyetu vya habari vinaeleza kuwa meseji hizo zimetoka kwa aliyekuwa waziri wa wizara moja nyeti serikalini kabla ya Rais kikwete hajavunja baraza hilo.....

Waziri huyo ni mbunge kutoka katika jimbo moja lililopo katika mkoa wenye maji mengi na uoto wa asili ya kijani kibichi ingawa hakuna bahari......

Katika meseji hizo zilizosambazwa kwa kasi, mojawapo imeandikwa hivi:
"Wewe ni mtoto mdogo lakini nakupenda sana.Ukinikubalia tukutane Nairobi ili nikupe raha za maisha"

Baada ya kuzinasa meseji hizo, mwandishi wetu alimtafuta rafiki wa karibu wa Lulu ili kujua kama ni kweli alinasika na Waziri huyo.....

"Ni kweli Lulu alikwenda Nairobi kukutana na waziri huyo ila kilichofanyika huko siwezi kukisema".....Alieleza rafiki huyo

WOLPER AMFANYIA UMAFIA ALIYEKUA MCHUMBA WAKE DALLAS

SIKU chache baada ya kutangaza kummwaga aliyekuwa mpenzi wake Ramadhani Mtoro ‘Dallas’, muigizaji Jacqueline Wolper amemfanyia umafia mchumba wake huyo wa zamani kwa kuliuza gari aina ya BMW X6 lenye namba za usajili T 574 BXF analodaiwa kuhongwa naye.

 Akizungumza na mwandishi wa habari hii juzikati, mtoa habari wetu ambaye yuko ndani ya TRA inayolishikilia gari hilo kufuatia utata wa ununuzi wake alisema, licha ya kuwa gari hilo liko mikononi mwao lakini si mali ya Wolper tena kwani tayari ameshamalizana na kigogo mmoja anayeshughulikia kulikomboa.  
“Kiukweli kwa sasa hatudili tena na Wolper kwani ameshakuja hapa na mtu ambaye amemtambulisha kuwa amemuuzia, kwa hiyo masuala yote atakuwa akishughulikia mteja wake huyo na si yeye,” kilidai chanzo hicho.

Baada ya kuzipata habari hizo, mwandishi wetu alimtafuta Wolper ambapo alikiri kuliuza gari hilo na kueleza kuwa, kwa sasa anamiliki gari aina ya Toyota IST wakati akijipanga upya.

“Ni kweli sina yoyote kwa sasa zaidi ya hii niliyoinunua hivi majuzi tu na kama umesikia kuwa hata ile BMW nimeiuza, huyo aliyekwambia hajakosea,” alisema Wolper.

BAADA YA KUACHIKA,WOLPER AUKATAA UISLAM


HABARI zilizolifikia muda mfupi kabla ya kwenda kiwandani zinadai kuwa sura ya mauzo kwenye filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper Masawe aliyebadili jina na kupewa la Kiislam la Ilham, ameukacha Uislam baada ya kushindwa kukamilisha vigezo vya kuingia na kutambulika katika dini hiyo.
 Sheikh Jafaar Mohamed Fota ambaye ni Imamu Msaidizi wa Msikiti wa Magomeni Kichangani ‘TIC’  aliyesimamia zoezi la kumsilimisha Wolper, hivi karibuni alisema kuwa staa huyo tangu afikie uamuzi huo, hakurudi kukamilisha hatua za kuufikia Uislam wa kweli.
Ukamilisho aliotakiwa kuufikia Wolper kwa mujibu wa Fota ni pamoja na kuhudhuria darasa la jioni kwa siku kadhaa mfululizo, kupeleka picha tatu kwa ajili ya kuweka kumbukumbu zake vizuri, mambo ambayo bidada huyo anadaiwa kushindwa kuyafanya.
 Akifafanua matumizi ya picha hizo, imamu huyo alisema, moja ingetumika mahakamani kula kiapo cha kubadili jina, nyingine ni kwa ajili ya rekodi za Bakwata na msikitini.
 “Cha kushangaza sasa imefika miezi mitano, sijawahi kumuona Wolper hapa,wala kusikia amefika msikiti wa wanawake kuswali, kanuni za kubadili dini hajazikamilisha, hilo ni tatizo,” alisema Fota.
Imamu huyo aliongeza kuwa, uongozi wa msikiti huo ambao ndiyo unaohusika na uamuzi wake wa kubadili dini, utamuita Wolper na kumshauri akamilishe taratibu lengo likiwa ni kumsaidia.
Kwa upande wake Wolper alipohojiwa  kuhusiana na kutotimiza taratibu za Dini ya Kiislam aliyotangaza kujiunga nayo alisema: “Taratibu gani? Nimekamilisha kila kitu, mara nyingi tu nawasiliana na imamu mkuu wa msikiti huo (hakumtaja jina) ambaye kwa sasa yuko nje ya nchi.”
Awali staa huyo aliutangazia umma kuwa anaukacha Ukristo na kujiunga na Uislam kwa kile kilichodaiwa ni kufuata dini ya mchumba wake, Abdallah  Mtoro ‘Dallas’ ambaye siku za hivi karibuni ametangaza kuuvunja uchumba wao.