INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Thursday, December 6, 2012

SHILOLE AANGUA KILIO UKUMBINI......

MSANII wa filamu na Muziki wa kizazi kipya Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, usiku wa kuamkia Desemba 3, mwaka huu aliangua kilio mbele ya umati baada ya kukumbushwa misiba ya wasanii wenzake, Hussein Ramadhan Mkieti ‘Sharo Milionea’ na Steven Charles Kanumba.


Zuwena Mohamed ‘Shilole’ akiangua kilio baada ya kuwakumbuka wasanii wenzake Kanumba na Sharo. Tukio hilo lilitokea kwenye sherehe ya kutimiza miaka 13 ya Clouds FM, iliyofanyikia Club Bilicanas, Posta jijini Dar es Salaa.
Kilio cha Shilole kilisababishwa na Mtangazaji wa Clouds FM, Adam Mchomvu baada ya kutoa fursa ya kuwakumbuka wasanii maarufu waliotangulia mbele ya haki.


...Shilole akiwa na simanzi baada ya kuwakumbuka wasanii hao. Akiwa jukwaani Mchomvu aliwaomba mashabiki waliojazana ukumbini humo kunyanyua mikono juu na waliokuwa na simu aliwataka wazinyanyue juu huku wakiwa wameziwasha ili zitoe mwanga.
Mtangazaji huyo alianza kuyataja majina ya mastaa waliofariki mmoja baada ya mwingine, huku watu kibao wakionesha simanzi zao.


...Kilio kikiendelea. Alianza kulitaja jina la Steven Kanumba kisha Sharo Milionea, akifuatiwa na marehemu Complex, Vivian na wengine kibao, ndipo Shilole aliposhindwa kuvumilia na kuangua kilio kama mtoto kutokana na uchungu wa kuwapoteza wasanii hao.
Msanii huyo alianza kubembelezwa na wenzake aliokuwa amekaa nao karibu na baadaye kutulia.


Marehemu Hussein Ramadhan Mkieti 'Sharo Milionea'.

Marehemu Steven Kanumba.
 
Source: Vituko vya mtaa!

Tuesday, December 4, 2012

BONGO MOVIE NA SAFARI YA IRINGA....!!!!

Hivi karibuni Bongo Movie tulivamia Mkoa wa Iringa kwa ajili ya kucheza mechi na Waandishi wa habari wa Iringa kwa madhumuni ya kumchangia ndugu yetu mpendwa Juma Kilowoko( SAJUKI) ili haweze kwenda kwenye matibabu yake ya mwisho Nchini India, kwa kifupi tulifanikiwa kwa kiasi chake si kikubwa wala kidogo lakini Mungu ndio muweza kila jambo tuna mpango wa kwenda mikoa mingine kwa ajili ya kufanya kitu hicho embu twende tukaone mambo yalivyokuwa.....
Sajuki na mkewe Wastara.....
Interview E Born Redio kwa ajili ya mtanange huo wa kukatana na shoka...
The Greatest & I.........

The Greatest akiongea machache......
Jennifer Kyaka(Odama).....
 Richie na Recho wakiongea juu ya ujio wa Bongo Movie Iringa....
Cloud...
 
Kitale....
 
Tino....
 
Me, Rachel Haule & Flora Mvungi........

Mtanange ukaanza wadau, hawa ndio vijana wa Bongo Movie wakipasha misuli.....
First Eleven ya Bongo Movie Unit iliyo mwaga cheche zake Mkoani Iringa....
Benchi la ufundi likiwa makini kufuatilia mchezo unavyokwenda..........

Chuchu Hans msanii toka Bongo Movie......
Me, Yusuf Mlele(middle) & Rachel.....
 Kitale.......

Half Time The Greatest akitafakari jambo....

Kocha Mkuu Bongo Movie Unit Single Mtambalike (Richie) akiongea machache wakati wa Half Time...

Mzee Yusuph naye akitoa yake machache aliyeyaona kipindi cha kwanza.....

Mawazo ya Kocha Mkuu yaliweza kufanya mabadiliko uwanjani tukapata bao la kwanza......

Wadada wa Bongo Movie wakishangilia ushindi.....

Mpaka mwisho wa mchezo Bongo Movie 2 na waandishi wa habri 2 hivyo ndivyo mambo yalivyokuwa wadau wa blog hii..

Saturday, December 1, 2012

R.I.P JOHN STEPHANO


Mwaka huu 2012 umekuwa ni mwaka mbaya kwa wasanii wa tasnia tofauti. Maana tumepata misiba mingi kwa wakati mmoja lakini hatupaswi kulalamika maana kazi ya Mungu haina makosa, Msanii aliyekuwa akichipukia kwa kasi ndugu yetu mpendwa wetu Bwana John Stephano alipofariki kwa matatizo ya tumbo Mungu ailaze roho ya maremu pema peponi.
Tino akisaini katika kitabu cha kumbukumbu..
Baba wa marehemu Mzee Stephano.
 Msanii Chiki Mchoma akielezea machache.....
Ratiba za kuwaga mwili wa marehemu zikiendelea.

Michael Sangu akitoa heshima zake za mwisho.
Mwili wa marehemu!
Watu walikuwa wengi sana..
Gari lililobeba mwili wa marehemu..

Odama katika majonzi....
Batuli katika majonzi..
Wasanii wakimpeleka mwenzao kwenye makazi yake ya kudumu.
Tukielekea makaburini.
Baadhi ya viongozi wa bongo movie unit wakijadili jambo.
Cloud.
Baba wa marehemu akiwasili..
Mwili marehemu ukitolewa kwenye gari nakupelekwa kwenye sehemu iliyoandaliwa
Hii ndi nyumba ya marehemu..
Tukiuingiza mwili marehemu kwenye kaburi
Ni huzuni kubwa sana unapondokewa na mtu uliyekuwa naye karibu.
Padre akimuombea marehemu..
Baba mzazi wa marehemu akiweka udongo..
Majonzi..
Huruma
Nape Mnauye akiweka udongo wa mwisho kwa marehemu
Saimon Mwakifamba Rais wa wasanii Tanzania nzima naye akiweka udongo wa mwisho.

255 ART CLINIC!!!!