DAR ES SALAAM: Zikiwa zimepita siku chache tangu staa wa filamu, Wastara Juma kufunga ndoa na Mbunge wa Jimbo la Donge, Zanzibar, Sadifa Juma aliyekuwa mpenzi wake, Bond Suleiman nusu afe, Risasi Mchanganyiko lina mkanda kamili.
Wakizungumza na gazeti hili, ndugu wa karibu wa kijana huyo ambaye pia ni muigizaji (jina linahifadhiwa) alisema siku moja kabla ya ndoa ya Wastara, Bond alitaka kujiua kwa kunywa sumu, lakini kaka yake aliyeingia chumbani kwake ghafla, akamuwahi kabla hajaibugia.














