INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Thursday, June 14, 2012

TUZO ZA FILAMU KUANZA MWEZI UJAO
 
Na Mwandishi Wetu

TUZO za kwanza kabisa za waigizaji wa filamu zimepangwa kufanyika mwezi ujao. Mratibu wa tuzo hizo kutoka kampuni ya Bantu Film Award, Stuart Kambona, alisema kuwa hatua ya kuanzisha tuzo hizo inatokana na muitikio wa soko la filamu za Tanzania kwa hivi sasa tofauti na awali.

Alisema kuwa Watanzania wengi walikuwa wanapenda zaidi filamu za kigeni na kuzipuuza filam za wasanii wa Kibongo wa hapa nyumbani.

Alisema kuwa kutokana na mapinduzi yaliyofanywa na wasanii wa fani hiyo, filamu za Tanzania kwa sasa zina soko la hali ya juu na imtokana na tabia ya watanzania kubadili mwelekeo. Alisema kuwa ili kuhakikisha Tanzania inafikia hatua ya Hollywood, wameamua kutoa tuzo kwa wasanii waliofanya vizuri na kuifikisha fani hiyo katika hatua ya sasa.

“Tunaamini kuwa kupitia tuzo hizi, waigizaji au wasanii wa filamu watatengeneza filamu zenye ubora wa hali ya juu ili kuweza kutwaa tuzo na soko kwa ujumla, tunaamini tutafikia lengo letu japo tumebakisha muda mfupi mpaka tuzo zenyewe kufanyika,” alisema Kambona.

Alisema kuwa kwa kuanzia watashindanisha filamu zote za Tanzania ambazo kwa sasa zipo sokoni ili kutoa fursa kwa kila msanii wa fani hiyo kushindana. Jumla ya tuzo 28 zitashindaniwa kwa mwaka huu.

Baadhi ya tuzo hizo ni Filamu Bora, Muongozaji Bora, Muigizani Bora mkuu wa Kiume, Muigizaji Bora Mkuu wa Kike, Msaidizi Bora Mkuu msaidizi wa kike na wa kiume, msanii chipukizi bora, filamu ya asili, Mpiga picha bora, Best Sound Track, Best Make-Up artist, Best Costume Designer, Best Documentary, Best Visual effect, best Film editor, best script na Tuzo ya Heshima.

Tuzo nyingine ni Outstanding Pioneer, Best Comedian, Best Cover Design, Best producer, Best Distributor, Best Action Movie, Best African Film outside Tanzania, Best Ligting, Best Sound na Best Story.

Muigizaji nyota wa kike nchini, Irene Uwoya aliwapongeza waandaaji hao kwa kuanzisha tuzo hizo ambazo alisema zitawapa changamoto kwao kuandaa filamu za ushindani.

Alishukuru kampuni ya Bantu kwa kuanzisha tuzo hizo ambazo anaamini zitawafanya kuandaa filamu zenye ubora wa hali ya juu.

"Tuzo hizi zitatufanya tufanye kazi nzuri zaidi ili kuingia katika ushindani, natoa wito kwa waigizaji wenzangu kufanya kazi kwa umakini ili kuleta msisimko na ushindani zaidi," alisema Uwoya.

Muigizaji Mkongwe, Jacob Steven (JB) alisema kuwa anaamini tuzo hizo zitawafikisha pale ambao wao wamekusudia na vile vile kuibua vipaji vingine katika tasnia hiyo.

JB alisema kuwa tuzo hizo zitawafanya mashabiki wao kujua undani wa fani yao kwa kuwajua watunzi bora, wapiga picha bora na wengineo.

MCHEZA FILAMU NA MWIMBAJI WA BONGO FLAVA DOGO JANJA AKIRUDISHWA KWA ARUSHA

Wakati mwingi Dogo Janja alikua akiongea na simu kuwaaga watu huku akiwa na furaha ya kuondoka Dar es salaam alikoishi kwa tabu, anafurahi kurudi nyumbani Arusha.

Washikaji nachomoka



Kwaheri Bono karibu Arusha
.

Dogo Janja akiagana na kaka yake mwenye T shirt ya bluu yenye mistari.

Nitawamisi kwenye majukwaa ya Bongo machizi wangu
.

Poa mwana tutaonanana Arusha
.

Kweli natimua..sijiamini
.

Kweli hii ni ticket ya kwenda Arusha?  Du kila jambo linamwisho wake
.
Bye bye.

MABADILIKO KATIKA TASNIA YA FILAMU YANAHITAJIKA SANA


MTAYARISHAJI wa filamu za Swahiliwood, Chrissent Mhenga Uncle Chriss, amesema kuwa tasnia ya filamu inahitaji mabadiliko makubwa ili ilete tija na maslahi kwa watayarishaji na wasanii husika.
Ukweli haupingiki kuwa wasanii wote hapa Tanzania wametoka katika kundi la Kaole ambalo mimi nilikuwa Mkurugenzi wake," anasema.

"Niliweza kuwajenga na wameweza kuliteka soko la tasnia ya filamu hivi sasa, lakini kuna jambo moja tu ambalo naliona ni tatizo. Hadithi hazishiki watu kwa muda mrefu tofauti na awali nilipokuwa nikiandikia wasanii hawa katika kundi la Kaole."

Hivyo amewasisitizia wasanii kujitahidi kujifunza vitu vya kitaaluma akisema filamu nyingi za siku hizi zimekuwa zikikosa uhalisi kwa kukosa taarifa kwa wahusika kuhusiana na jambo linachezwa katika filamu.
FIILAMU YA "HOUSE MAID" KUWA SOKONI SI MUDA MREFU KUANZIA SASA.
Jenifer Kyaka amesema filamu yake mpya ya "House Maid" itakuwa sokoni si muda mrefu kuanzia dakika hii, kwahiyo wapenzi wa filamu zake waanze kukusanya pesa kidokidogo ili siku ya kutoka hiyo filamu uwe wa kwanza kuiona. Utajifunza mengi kwa kupitia filamu hii ya "House Maid"

Wataarifu na jamaa zako ambao hawajabahatika kupata habari hizi kwa njia ya mitanda

Wednesday, June 13, 2012

KWELI FILAMU ZINALIPA--WEMA SEPETU ANATISHA NA MJENGO WA MILIONI 400.

























PICHA: MVUTO KWANZA BLOG.

Tuesday, June 12, 2012

JIPATIE FILAMU YA "HOUSE MAID"

Wadau wa Jeniffer Kyaka (Odama), nimekuandalia filmau mpya yenye kufundisha, kuadibisha na kuelimisha. Kaa mkao wa kuipokea ili uweze kujifunza na kuburudika. 

Tutawatangazia siku ambayo filamu itakuwa sokoni kwa kupitia mtandao huu wa ODAMA au mtandao wa RUMAAFRICA (www.rumaafrica.blogspot.com) na mitandao mbalimbali.

Filamu hii inaandaliwa na kampuni yangu ya J-FILM 4 LIFE kwa viwango vya hali ya juu sana.

Mimi nikutakie siku njema mdau wangu na zidi kuni-support kwa kazi zangu hasa za filamu.
Ahsanteni






Monday, June 11, 2012

ODAMA NDANI YA HOT MIX-EAST AFRICA
Msanii wa filamu Tanzania Jeniffer Kyaka a.k.a ODAMA wiki iliyopita alifanyiwa mahojiano na EATV kuhusiana na filamu yake mpya ya RUDE inayofanya vizuri sokoni kwa sasa. Mbali na hivyo alielezea maisha yake kwa ujumla na jinsi alivyofaidika na kazi ya filamu.
 
Kutoka kushoto ni mtangazaji wa Hot Mix, Anna Mbanjo, akifuatiwa na msanii wa filamu, Jeniffer Kyaka (Odama) na Fatna Ramole wa Hot Mix wakiwa katika studio za EATV
 
 Jennifer Kyaka mbali na uingizaji pia ni Mkurugenzi wa kampuni yake ya J-FILM 4 LIFE iliyoko Biafra Kinondoni Dar es Salaam. Aliongeza kwa kusema mbali na kucheza filamu za watu wengine na pia ametengeneza filamu katika kampuni yake ya J-FILM 4 LIFE kama The Avenger, Life 2 Life, All About Love, Loreen, RUDE na filamu mpya nyingine ambayo inakuja karibuni inayoenda kwa jina la HOUSE MAID .
 Odama akiwa katika pozi baada ya kufanya interview

Odama alimaliza kwa kuwashukuru wapenzi wake wanaom-support kwa kununua filamu zake, na hasa wanaotembelea blogu yake ( www.odama1.blogspot.com) ambayo imekuwa gumzo kubwa kwa kukusanya matukio ya wasanii wa filamu Tanzania na nje ya nchi.
 Wakitokelezea ndani ya EATV



 


.......PRINCESS GETRUDE ATOA MESEJI NZITO KWA WASANII....
 


PICHA JUU NA NI PRINCESS GETRUDE

Msanii chipikizi nchini (ambaye pia ni hot model wa blog hii) anayejulikana kwa jina la Princess Getrude amefunguka na kusema kwamba, wasanii ni muhimu sana katika ukuaji wa tasnia ya filamu nchini na kwahiyo kuwaomba wasanii wote kutokwenda kinyume na destruti yetu ya Kitanzania. Akichonga na blog hii msanii huyu ambaye kwa muda wote alioneka kuwa mpole na mwenye hekima, alisema kuwa kazi ya sanaa ni kazi kama kazi nyingine.

"Sisi wasanii ni kama wafanya kazi wengine, kwahiyo tunahitaji kuheshimiwa pia" aliongeza msanii huyo. hata hivyo aliongeza kuwa pamoja na heshima ambayo tunastahili kuipata kutoka kwenye jamii lakini pia na sisi kama wasanii tunatakiwa kujiheshimu na kufanya matendo mema mbele ya watanzania wengine na yanayokubaliwa na Watanzania.....

Msanii huyu ambaye muda si mrefu utaanza kumuona kwenye luninga kwenye tamthiliya moja ambayo hakuwa tayari kuitaja kwa sasa. Aliongeza kuwa pia yuko mbioni kuandaa filamu yake ambayo anaamini kwa itakimbiza sana mtaani.
WEMA SEPETU AONYESHA KIOTA CHAKE KILIVYO KILALI....KWELI FILAMU NI DILI
Wema akiwa na Zamaradi kutoka Clouds TV


 Wema akiwa na James mtu ambaye ametengeneza style yote ya nyuma ya Wema.

 
Gari yake ya kwanza ilikuwa hii
Gari ya pili ya wema
Wema Sepetu anaishi  maeneo ya Kijitonyama\
picha kwa hisani ya dj choka blog