INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Tuesday, July 24, 2012

FILAMU YA SIKU YA MWISHO KUTOKA WIKI HII-666

Source: Ruma Africa & Papa Sam

(Kuhusiana na habari zingine kuhusiana na hii filamu tembelea www.rumaafrica.blogspot.com na www.samsasali.blogspot.com. Tunatakuwa tunakuletea kinachoendelea)

Ile Filamu ambayo inasubiriwa kwa hamu kubwa hususani Jamii Ya Kikristo Ya Siku za Mwisho inakamilika wiki hii na Kabla ya Kuingia Sokoni Mapema Mwezi Ujao.
 
Katika Filamu hiyo ya kibongo ambayo Papaa Ze Blogger amecheza kama Apostle P Nizo, ambaye ni Mtume na Nabii mwenye Kanisa lenye Ishara na Miujiza mingi na Baraka kadha wa Kadha pasipo waumini wa Kanisa hilo kutambua kuwa Apostle Nizo ana "Source Of Power" isiyotoka Juu.
 
Filamu hiyo yenye maudhui ya Kuwakumbusha Wakristo kuhusu Siku Za Mwisho na Kurudi Kwa Yesu Kristo imesheheni Vipaji Lukuki Vya Wakristo Katika kufikisha Ujumbe kwa Jamii.

Hapa ndipo Wanapokuwa kwenye Ibada Zao Wakisali ...Its a Nice Scene

Kushoto kabisa ni Papaa Ze Blogger akicheza Kama Apostle ndani ya Scene hiyo akiwa amevaa tofauti na wengine sababu na nafasi yake katika Impact katika Jamii

Hapa Apostle Nizo Akiwa anafatilia Ibada kwa Unakini Mkubwa ndani ya Chumba Cha Siri

Hapa Papaa Ze Blogger akiecheza Kama Apostle P, akidaka "power'
Apostle P Nizo akiwa na Kisu tayari kwa Ibada Ya Sadaka....Its very interesting Scene

ANGALIA MATUKIO MENGINE KWA KUBOFYA HAPO CHINI

Wakuu Katika Katika Kujipanga Kimkakati Mara baada ya Ibada ya Chumba Cha Siri

Kulia ni Papaa Ze Blogger ambaye amecheza kama Anointed Apostle, Katikati ni Pastor Alex, ambaye amecheza kama Mfanyabiashara mkubwa ambaye pia ni Mzee wa Kanisa Wa Apostle Nizo, na Kushoto Ni Mwanadada amecheza kama Mwanaharakati wa Haki za Wanawake na Mjasiriamali ambaye yuko connected na "chumba cha siri'

Laurence akiwa mwenzake ambaye wamecheza kama Askari wanaokagua magari kama yana sticker ya 666 maana hutaweza nunua mafuta wala kuendesha gari kama haijagongwa 666.

Hawa Watu Watatu wametisha Sana katika Scene hii ya "Chumba Cha Siri" Mpaka Pastor Kaduma Mtunzi wa Filamu hiyo, na Director Wa Filamu hiyo Mr. Mtitu Wakapiga picha na Jamaa

Scene hii Jamaa akiwa ameandaa Part nyumbani kwake ambapo amealika ndugu jamaa na marafiki,

PICHA ZINGINE BOFYA HAPO CHINI PALIPOANDIKWA "Read More"

Monday, July 23, 2012

JENNIFER KYAKA (ODAMA) - NAWASHUKURU WOTE KWA MCHANGO WENU KUHUSIANA NA KIFO CHA MAMA YANGU MDOGO

Nawashukuru wote mliofika katika hospitali ya Ocean Road siku ya Jumapili kwaajili ya kumuaga mama yangu mdogo, aliyefariki siku ya Ijumaa katika hospitali ya Ocean Road - Dar es Salaam. Ninawashukuru sana tena sana, mmefanyika baraka kwangu na kunifariji sana katika kipindi hicho kigumu. Nimetambua kuwa kumbe nina ndugu na marafiki wanaonipenda katika ulimwengu huu.

Mungu wangu na awarudishie mara dufu kwa mchango wenu na muda wenu mlioupoteza kwa kuja kumuaga mama yangu mdogo, Ocean Road hospital. Pia nawashukuru wale wote waliopiga simu zao kunifariji na kunitia moyo. Wengine mlifika nyumbani kwangu kunifariji na kunipa mawazo ya jinsi gani mama yangu atasafirishwa kwenda Shinyanga kwaajili ya mazishi.

Jennifer Kyaka (Odama)

Ndugu zangu nawashukuru sana kwa wema wenu na upendo wenu mliouonyesha kwa mama yangu akiwa amelazwa pale  hospitalini. Nimeona huduma zenu, mmekuwa bega kwa bega kuhakikisha mama yangu anapewa yale mahitaji yaliyokuwa yanahitajika.

Nawashukuru madaktari wa hospitali ya Ocean Road kwa juhudi zenu. Mmetumia elimu yenu na ujuzi wenu kuhakikisha mama yangu mdogo anapona, lakini haikuwezekana kutokana na Mungu kumpenda zaidi.

Nawashukuru Watanzania wote kwa maombi yenu. Sina cha kuwalipa, ila Mungu wangu atawalipa. 
Ahsanteni sana na Mungu bariki familia zenu na kazi ya mikono yenu

AMENI

PASTOR MYAMBA WA BONGO MOVIE AFUNGUKA KATIKA KITUO CHA PRAISE POWER RADIO

Haya yalikuwa mazungumzo kati ya mtangazaji wa Praise Power, James Temu ambaye na yeye ni mwigizaji wa filamu za Kitanzana na Pastor Myamba Supar Star wa Bongo Movie .

James Temu (Uncle Jimmy) alisema:-

Kupitia kipindi cha Rise & Shine ni nacho fanya mimi na Swahiba yangu Erick Martin kuanzia Saa 6:00 adi Saa 10:00 asubuhi, Pastor Myamba Supar Star wa Bongo Movie amesema Filamu zote anazo fanya kupitia Kampuni yake zina asilimia 80% za kuwawaleta watu kwa Yesu.

Amefunguka zaidi na kusema huu ni mwaka wake kuakikisha analiteka soko la filamu nakulipeleka sehemu nyingine ya watu kufahamu umuhimu wakuijua siri iliyo kwenye Wokovu.


Uncle Jimmy na Myamba kwenye One end 2 Praise Power Fm

Pastor Myamba ambae alichelewa kufika katika kipindi siku ya ijumaa kutokana na foleni za hapa Bongo amesema Filamu yake mpya ya {GOD"S KINGDOM} aliyofanya na Kampuni yake ya Born Again Films Production. Ni Filamu inayoonyesha kazi ya Kristo katika kuwaleta watu kwake, Ni filamu iliyokuwa na upako wa ajabu kwa maana baadhi ya sehemu walizokuwa wakifanya shooting ilibidi kusimamisha ili Roho mtakatifu afanye kazi yake.

NUKUU-"Uncle Filamu hii nilimuona Mungu akiwaudumia watu kwa namna ya ajabu,kuna kipindi watu walipandisha Mapepo kweli ikabidi nichukue jukumu lakuanza kuwaombea.Yani sasa sio filamu tena bali ilikuwa Uduma.Mwisho wa Nukuu".

Wiki ijayo ya Tarehe 27/7/2012 Pastor Myamba atakuja kuendeleza muendelezo wa Topic yetu ya (Nini faida ya Filamu za Kitanzania katika Maisha ya Mtu alie okoka.Je? Filamu hizi zinaweza badilisha maisha ya Mtu asie jua wokovu)


Pastor Myamba na Joyce Charz rafiki yako wa karibu akijishebeda na Myamba.

Usikose Rise$Shine ya Ijumaa itakapo fika Saa 9:00 asubuhi nitakapo kuwa na gwiji la Filam Emmanuel Myamba a.k.a Pastor Myamba atakapo funguka kwa undani.

KESI YA LULU KUPELEKWA MBELE NA MSAJILI MAHAKAMA KUU



Elizabeth Michael 'Lulu'

MSAJILI wa Wilaya wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam leo asubuhi Amiri Msumi ameahirisha kesi inayomkabili msanii wa maigizo nchini Elizabeth Michael maarufu kwa jina la Lulu anayetuhumiwa kumuua aliyekuwa msanii nyota wa filamu nchini Steven Charles Kanumba Aprili 7 mwaka huu .

Akiahirisha kesi hiyo jana Msajili huyo Msumi alisema kutokana na sababu za Jaji anayesikiliza kesi hii katika Mahakama Kuu Jaji Dk. Fauz Twaib kutokuwepo Mahakamani amelazimika kuahirisha kesi hiyo hadi Agosti 20.

"Kwakuwa Jaji Dk. Fauz Twaib ni mwalimu katika chuo cha Sheria hivyo yuko katika mitihani naahirisha kesi hii hadi tarehe hiyo niliyoitaja ambapo itakuwaja kwa kutajwa".

JAMES TEMU (UNCLE JIMMY), BAHATI BUKUKU, RULEA SANGA (BLOGER), DAVID ROBERT NA WENGINE KUJA NA FILAMU KALI YA KUMTUKUZA MUNGU WETU "DUNIA HAINA HURUMA"

Mwandishi: Rulea Sanga

Umefika wakati Mungu amezungumza na hawa watumishi wa Mungu kwa kuwapa maono ya kutengeneza filamu ya "Dunia Haina Huruma". Ujumbe huu unatoka katika nyimbo mpya ya mwimbaji maarufu Tanzania, Bahati Bukuku inayoitwa "Dunia haina Huruma" Nyimbo hii imekuwa gumzo jijini Dar es Salaam kutokana na ujumbe wake unaogusa maisha ya watu na kukuweka karibu sana na Mungu unapousikia. Kama hujawahi kuusikia, nakuomba ujitahidi kusikiliza Praise Power Radio na Wapo Radio utabarikiwa.

Mhusikaka mkuu wa filamu hii, Bahati Bukuku

Kutoka na wimbo huu, watumishi wa Mungu wameamua kukaa chini na kuuzambaza ujumbe huu kwa njia ya filamu. Kwahiyo utafaidika kuusikia kwa njia ya uimbaji na pia kwa njia ya maigizo.

Katika filamu hii kutakuwa na watumishi wa Mungu kama James Temu a.k.a Uncle Jimmy (ambaye ni mwigizaji wa filamu Tanzania na ni mtangazaji wa Praise Power Radio Tanzania, mbali na hapo ni blogger) , Rulea Sanga (ambaye ni blogger na ni graphic designer, na mwezi April 2012 alibahatika kuitwa na Nabii TB Joshua kutokana na kazii yake nzuri ya blogu), David Robert (huyu ni muimbaji wa nyimbo za injili Tanzania na ni mjasiliamali mkubwa sana Tanzania), Bahati Bukuku (Huyu ndiye mhusika mkuu wa filamu hii, ni mwimbaji wa nyombo za injili Tanzania na amekuwa baraka kwa wale waliosikia nyimbo zake), Riyama Ally (huyu ni mwigizaji wa filamu Tanzania, amefanya kazi nyingi katika uigizaji)

Wimbo wa Bahati Bukuku wa Dunia haina huruma unagusa sana mioyo ya watu, hasa wale walioko katika ndoa na wale wanaotaka kuingia katika ufalme wa ndoa. Kutokana na wimbo huo, mtumishi wa Mungu Bahati Bukuku akaamua kuja na wazo la kutengeneza filamu ambayo itaonyesha kila kitu alichokiimba katika wimbo huo.

Mshiriki mwingine wa filamu ya "Dunia haina Huruma", Blogger wa RUMA AFRIKA, Rulea Sanga. Hapa akiwa katika gari la Wise Men wa Nabii TB Joshua katika Synagogue ya THE SCOAN. Kumbuka mwezi Aprili 2012 aliitwa na Nabii TB Joshua kutokana na kazi yake nzuri ya blogu yake ya www.rumaafrica.blogspot.com

Kwa sasa kila kitu kuhusina na filamu hii kimeandaliwa, ila kilichobaki ni kumtafuta dada mrembo na mwenye kuvutia, kwani kuna sehemu inahitajika kwaajili ya dada ambaye ni mrembo sana. Kama wewe unajiona ni mrembo na uunajiamini na unaweza kuigiza tunaomba uwasiliane kwa namba hii +255 713-763939.


Kumbukeni haya yote yanafanyika kwaajili ya kumtangaza Kristo na kuonyesha kuwa hata sisi tuliokoka tunaweza kufanya vitu vikali na vizuri. Umefika wakati wa kupenda vilivyo vya Mungu na ku-support kazi ya Mungu. Support yako itatuwezesha kufanya vitu vikali. Mungu anatumia watu kufanikisha kile anachotaka kifanyike, na leo wewe utakuwa ni mmoja wa wale Mungu anapenda ushiriki katika ku-support kazi hii isonge mbele. Kama unamchango wako wowote tutashukuru sana kusikia na kupokea kwako, mchango unaweza ukawa na mawazo, fedha au vitu. Kama wewe ni mmiliki wa vyombo vya shooting unaweza ukajitokeza tukafanya kazi ya Mungu.

Kwa mujibu wa Bahati Bukuku, amesema filamu hii itakuwa ya utofauti na filamu za watu wengine kwani watu watakao shiriki filamu hii watapimwa uwezo wao wakufanya kazi napia watasafiri baadhi ya mikoa kukamilisha kusudio la filamu hii.
Wadau wa blogu hii endeleni kuitembelea, ili mfahamu kitu kinachoendelea.

Riyama Ally ni mtumishi wa Mungu na anacheza filamu za Kitanzania (Bongo Movie). Naye atashiriki katika filamu hii.

David Robert, ni mwimbaji wa nyimbo za injili Tanzania na mjasiliamali. Atashiriki
Uncle Jimmy , ni mwigizaji katika Bongo Movie na amecheza na waigizaji wakubwa Tanzania akiwaomo Ray, JB,O na wengine wengi. Katika filamu hii utaona kazi yake ya uigizaji katika muonekano mwingine.


NIKUPE KIONJO CHA TAMTHILIA

Bahati Bukuku alipigiwa simu na mwanamke mmoja ambaye alijitambuliha kuwa yeye ni mke mwenzake, alimpa taarifa mbaya akimwambia "Nenda kachukue mzoga wako Muhimbili" . Bahati Bukuku akiwa katika kutafuta marafiki zake kuulizia taarifa hizi ili kujua zaidi, aliamua kufika mochwari Muhimbili, na alipofika Muhimbili alikutana na taarifa mbaya za kuumiza moyo wake kutoka kwa wale waliokuwa hapo Muhimbili.
Bahati Bukuku aliingia chumba cha maututi na kuona mpenzi wake amepoteza fahamu na hawezi kumtazama. Nilijisemesha kuwa "Dunia haina huruma, haina fadhili, nani mwenye huruma anifariji, moyo unavuja damu kwa matatizo ninayopata."
Bahati Bukuku akamua kuwapigia ndugu wa mume wake Mbeya ili awaeleze yaliyomsibu, lakini cha kushangaza ni kwamba wote walimsusia. Akajaribu kuchukua card ya Bank ili kuangalia kama kuna pesa kidogo zimsaidie, lakina cha kusikitisha akaona ATM haizomi, hakuna pesa. Hakuchoka akaenda kwa daktari na kutaka kumuuzia gari aina ya Vogi, lakini daktari alikataa na kusema, "Haya magari yanakula mafuta sana kwahiyo sitoweza kuwa nalo". Akiangalia marafiki zake wanazidi kularua moyo wake kwa maneno makali.
Bahati Bukuku kila akimwaangalia mume wake anazidi kuchanganyikiwa na hawezi kuongea naye. Mashemeji zake hawataki kusaidia na kila akiomba msaada kutoka kwao, nao wanamwambia "Shemeji sisi tunaenda kuangalia mpira Ulaya" akiwaambia mawifi zake nao wanamwambia, "Wifi hatuwezi kukusaidia, tunaenda kucheza segere".
Bahati Bukuku akaamua kwenda tena kwa daktari kuomba asaidiwe. Na chanzo cha matatizo kikaanza hapo. Bahati akabidi azae mtoto na huyu daktari ili apate msaada, maana amehangaika sana bila ya kupata msaada, na mgonjwa hali yake ni mbaya sana.

Mzigo ukazidi kwa Bahati Bukuku, hali ikazidi kuwa mbaya sana, maana amefanya kosa la kufanya tendo la ndoa na daktari na kuzaa mtoto, na bado ndugu hawampendi.
Baada ya kupata nafuu kwa mgonjwa na kurusiwa nyumbani na kuendelea na maisha yake ya kwaida, Bahati Bukuku akamwambia kuwa nimezaa na daktari. Na hii nililifanya kutokana na kushindwa kupata msaada kutoka kwa ndugu na marafiki, wote walinikimbia, kwahiyo nikaamua kufanya hivyo kwa daktari ili nipate pesa ya kukusaidia upate matibabu.

Mume na Bahati Bukuku aliposikia habari hizo kuwa mke wake ana mtoto na daktari akachukua panga na kutaka kumuua.

Mume na Bahati aliondoka na baadae Bahati Bukuku akaitwa kijijini kwa mume wake. Alipofika kijijini akawasalimia, nao hawakuta kumjibu wala kumsikia. Kikao kikakaa kutaka kumhukumu, na wakamwambia Bahati Bukuku, "Kama unataka kuishi katika familia hii, mtoto auawe". Akamtazama mume wake na yeye akamtazama kwa hasira. Bahati aakjiuliza, amkimbile nani kwani ndugu, marafiki na mume wake hawamtaki.
Ndugu wakmuweka mtoto kati ili wampige mapanga, akatokea baba mmoja na kuwauliza, ambaye hana dhambi na awe wa kwanza kupiga panga huyu mtoto. Mume na Bahati Bukuku baada ya kusikia hilo aliomba msamaha kwa mke wake na kusema kuanzia leo hii ya dunia yameisha nataka kutengeneza na Mungu.

Bahati amegundua ya kuwa Mungu anaweza kujibu maombi na kusamehe. Hii ni stori fupi ya tamdhilia ambayo itakujia kwako, kuna mengi ambayo utayaona katika filamu hiyo, Utaona mazingira yatakyotumika, wahusika wanatavyokuwa serious kukuletea huu ujumbe.

Lakini nataka kukuuliza wewe mdau wangu, unafikiri Rulea Sanga, David Robert, Uncle Jimmy, Bahati Bukuku n, Riyama Ally anaweza kufaa katika kitengo kipi?

Kwa haraka haraka kuna wahusika wafuatao:

1. Mke wa yule mume mgonjwa
2. Mume ambaye ni mgonjwa
3. Dada aliyempigia simu mke wa yule mume
4. Marafiki /mashoga wa mke wa mume
5.Daktari
6. Ndugu wa mume
7. Watu waliokataa kumsaidia Bukuku akiwa na shida.
8. Ndugu aliyepigiwa simu na Bahati Bukuku
9. Wacheza segere
9. Ndugu waliomua kwenda Ulaya kuangalia mpira
10. Mtoto wa daktari ambaye aliambiwa akatwe mapanga
11. Mtu aliyewambia wasimkate mapanga
TUNAOMBA MAONI YAKO.

MOVIE MPYA YA BATMAN YAZUIA KASHESHE


Filamu mpya ya Batman inayoitwa The Dark Knight Rises imeanza kuonyeshwa jana.Filamu hiyo ambayo imecchezwa na Christian Bale imeanza kuonyeshwa nchini Marekani jana katika kumbi mbali mbali za sinema.Watu wengi waliojitekeza katika Theater ya 16 century Colorado wamekumbwa na maafa baada ya mtu asiefahamika ukingia na kupiga risasi hovyo.Watu zaidi ya 12 wamepoteza maisha akiwemo mtoto wa miaka 12,70 wamejeruhiwa pia yumo mtoto wa miezi mitatu.


Mtu huyo aliyetambuliwa kwa jina la James Holmes mwenye miaka 24.Aliingia ukumbini humo akiwa kavalia kama mmoja wa wahusika ambae amecheza kama adui katika filamu hiyo Tom Hardy aliyetumia jina la Bane.Anaonekana pichani.Alipoingia akatupa bomu la moshi na kisha kuanza kurusha risasi hovyo.





Wanafamilia mbali mbali wakifarijiana






Baba ambae mtoto wake wa miezi mitatu alipigwa risasi ya mgongoni akiwa hospital katika hali ya huzuni na kuchanganyikiwa.

Miongoni wa waliofariki yupo dada mtangazaji wa tv Jessica Ghawi.Muda wote akiwa katika jumba la sinema alikuwa akitweet namna anavyofurahia movie hiyo mpaka mauti yalipomkuta.

Tukio hilo limetokea jana usiku katika mji Colorado eneo linaitwa Aurora.Rais wa Marekani Barack Obama ametuma salamu zake za rambi rambi kwa wafiwa na kuwaomba wanachi wake kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu.Pia akawaomba kuwaombea wakazi wa eneo hilo waweze kupita katika wakati huo ambao umewaacha katika mshituko.

WEMA NA DIAMOND KUNASWA KIGOMA



Nasib Abdul Juma ‘Diamond



Wema Isaac Sepetu.Na Shakoor Jongo

STAA wa filamu Bongo, Wema Isaac Sepetu na kichwa kinachotingisha katika Bongo Fleva, Nasib Abdul Juma ‘Diamond’ wamenaswa wakiwa beneti mkoani Kigoma, Ijumaa lina data kamili.
Chanzo makini kilichopo mkoani humo, kimepenyeza habari hiyo kwa paparazi wetu kwa njia ya simu juzi, ambapo kilisema ukaribu wao uliamsha hisia kwamba huenda wawili hao wamerudiana.
“Wapo wote huku Kigoma, kwa Diamond ni sawa maana yupo na wasanii wenzake wa Kigoma All Stars, sasa Wema amekujaje? Kwanza siyo mwanamuziki, lakini pia siyo mtu wa Kigoma ni wa kutoka Tabora,” kilieleza chanzo hicho.
Baada ya kupata habari hiyo, Ijumaa lilimvutia waya Diamond zaidi ya mara tatu lakini simu iliita bila kupokelewa.
Wema alipopigiwa simu alipatikana na kufafanua ishu nzima ilivyo. Huyu hapa msikie: “Ni kweli nipo huku Kigoma lakini sipo na Diamond. Nimekuja kwa mwaliko wa Zitto Kabwe (Mbunge wa Kigoma Kaskazini).
“Mimi na Diamond ni marafiki tu, hatuwezi kuwa wapenzi tena, kila mtu na maisha yake. Kifupi nina mtu wangu ambaye tunapendana na kuheshimiana sana.”
Alipotakiwa kumtaja mpenzi wake mpya alisema: “Kwa sasa siwezi kumtaja, lakini siku si nyingi nitamuweka hadharani watu wamjue.”

NI KWELI MCHUNGAJI MTARAJIWA MASANJA MKANDAMIZAJI YUKO MSIKITINI?

Bado siamini kama hii picha ni mchungaji mtarajiwa Emmanuel Mgaya a.k.a Masanja Makandamizaji ambyae mbali na kuwa mchungaji mtarajiwa ni mwimbaji wa nyimbo za injili Tanzania. Hivi karibuni amezindua album yake ya "Hakuna Jipya" mkoani Iringa ambapo crew nzima ya Bongo Movie ilififika mkoani hapo kum-support.

Wewe uliyefanya kazi ya kum-edit na Photoshop ili Masanja aonekane yuko mskini, ujue sio fresh, unaharibu huduma ya rafiki yako.


Saturday, July 21, 2012

MSIBA WA MAMA MDOGO WA JENNIFER KYAKA (ODAMA) KUPELEKWA SHINYANGA

Mwigizaji wa filamu Tanzania, Jennifer Kyaka (Odama) anapenda kuwajulisha marafiki, ndugu na wadau wa blogu yake ya www.odama1.blogspot.com kuwa msiba wa mama yake mdogo aliyefariki Ijumaa 20 Julai 2012 katika hospitali ya Ocean Road utapelekwa Shinyanga na siku ya Jumapili itakuwa ni siku ya kuuaga mwili wa marehemu katika hospitali ya Ocean Road jijini Dar es Salaam kuanzia asubuhi, na baada ya hapo safari itaanza kuelekea Shinyanga. Mungu wangu na awabariki. Ameni

Jennifer Kyaka (Odama)

BONGO MOVIE-WEMA SEPETU AKIWA KATIKA CHARITY EVENT-ARUSHA WIKI ILIYOPITA

WEMA ALIWAULIZA WATOTO YEYE NI NANI.. ALL OF THEM WALISEMA WEWE WEMA SEPETU TUNAKUONAGA KATIKA MAGAZETI NA TV.. NAJIULIZA HAWA WATOTO WADOGO HIVI HAYO MAGAZETI WANAYAONAJE? NA WAPI... ILA HUYU PICHANI NDO ALIWAACHA WATU MIDOMO WAZI.. ALIWAAMBIE WENZIO.. MMEKOSEA HUYU ANAITWA WEMA "DIAMOND" WEMA ALITOA MACHO KAMA KAKABWA NA MFUPA.. ILIBIDI APIGE NAE PICHA.


ALIPOKELEWA NA ANGEL JUSTUS NA MISS ARUSHA 2012



GAUDENCIA... MWENYEWE ALIKUWA ANAJIITA DEREVA WA WEMA SEPETU... AKIWEKA MAMBO SAWA.




HAKA KATOTO KALIMPENDA SANA WEMA NA HAKAKUTAKA KUKAA NAE MBALI... WEMA U SHOULD ADOPT THIS KID.







MC WA SHUGHULI HII




SNURA ALIKUWEPO PIA.

RISALA FUPI KUTOKA KWA MLEZI WA KITUO HIKI CHA GOOD HOPE MBELE YA MGENI RASMI WEMA SEPETU

MAJIBU YA RISALA YALITOLEWA NA MGENI RASMI.. IKIWA NI KUSAIDIA KUHAKIKISHA HAWA WATOTO WANAPATA ELIMU, ALIWANUNULIA TV PAMOJA NA PESA TASLIMU ZA KIMAREKANI DOLA1000




ZILIKABIDHIWA KWA MLEZI WA WATOTO HAWA.

GAUDENSIA AKITOA SHUKURANI ZAKE KWA WEMA SEPETU NA TEAM YAKE KWA KUUNGANA NAO KWANI HUYU NDIO ALIKUWA MTU WA KWANZA KUFIKA KATIKA KITUO HIKI.

PENDO AMBAYE NDIE ALIYEANDAA SHUGHULI HII AKITOA MANENO YAKE MACHACHE








WATOTO WAKASEMA WEMA HUWEZI KUONDOKA HAPA ARUSHA BILA KUJUA KUCHEZA DISCO MALAPAA....

SAHAU CLUB ZENU ZA MJINI HAPA NI DISCO MALAPA KWA KWENDA MBELE.

CHANGAMKA.....

AISEE NATAMANI KUWAPA STORI YA HAWA WATOTO ILA DAAAAH...... THEY MADE MY DAY THAT DAY.

HASA HUYU... AM SURE WEMA HATAMSAHAU KATIKA MAISHA YAKE

TRULY LOVE ....... SIKUJUI HUNIJUI ILA TUNAPENDANA.

I SALUTE THESE LADIES........THEY ARE STRONG AND HARD WORKING.