MASTAA ‘first class’ katika kiwanda cha filamu Bongo, Sylvia Shally
na Coletha Raymond ‘Koleta’ wanadaiwa kukopa mawigi dukani na kuingia
mitini.
Sakata hilo la aina yake limeibuliwa hivi karibuni ambapo
Flora Mwande maarufu kwa jina la ‘Gari Kubwa’ mkazi wa Mbagala, Dar
alisema anawadai kwa muda mrefu mastaa hao fedha za bidhaa mbalimbali
yakiwemo mawigi.
Gari Kubwa alisema kuwa yeye ndiye
anayewapendezesha mastaa hao kwa kuwakopesha nywele, pete, cheni na vitu
vingine vya kike vyenye mvuto lakini mwisho wanampiga chenga kulipa
fedha zake na kuingia mitini, jambo ambalo alidai limekuwa likimrudisha
nyuma kimaendeleo.
“Sylvia alikuja dukani kwangu, Sayansi,
Kijitonyama (Dar) Februari 17, 2011 akakopa nywele akisema yuko kwenye
maandalizi ya kwenda nchini Nigeria. Alichukua ‘lesi wigi’ lenye thamani
ya shilingi 150,000 lakini hajanilipa hadi leo. Mbaya zaidi hapokei
simu yangu, inaniuma sana,” alisema Gari Kubwa.
Aliongeza: “Siyo
huyo tu, Koleta naye alikuja kwangu Januari 5, 2011 na kukopa ‘lesi
wigi’ na pete, vyote vikiwa na thamani ya shilingi 170,000. Hajalipa,
nikimdai anasema eti simdai ina maana mimi sina akili timamu? Mimi mtu
mzima najua ninachokifanya bwana.
“Wito wangu kwao aisee walipe fedha zangu, nitafurahi sana.”
Mwandishi wa gazeti hili alifunga safari mpaka nyumbani kwa Koleta,
Makongo Juu, Dar na kusomewa mashitaka yake ambapo alifunguka:
“Katika maisha yangu naogopa sana dhuluma. Ni kweli Gari Kubwa ananidai
shilingi 100,000, tatizo anaongeza fedha kila kukicha, mara anadai
170,000, mara 150,000. Mimi najua ilibaki 100,000 nitamlipa nikipona, si
unajua kwa sasa naumwa?” alisema Koleta.
Akaongeza: “Halafu anakera
sana huyo mama, ukikopa kitu kwake lazima akutangaze, siku moja Uwoya
nilimuomba aniuzie cheni yake, nikawa nimesahau ATM kadi nyumbani,
nikashangaa ananiambia nisimfanye kama alivyofanya Sylvia kwa Gari
Kubwa, nikajua kumbe hata Sylvia anadaiwa.”
Paparazi wetu alimsaka
Sylvia kwa simu zake za mkononi bila mafanikio. Jumatatu ya Agosti 20,
2012 akatumiwa meseji lakini hakujibu.
Jumanne ya Agosti 21, saa 3:30, 3:45 na 4:11 asubuhi Sylvia alipigiwa simu lakini pia hakupatikana.
Posted by
VITUKO VYA MTAA
at
Thursday, August 23, 2012