MGOMBEA wa Chama cha Patriotic Front, Edga Lungu ameshinda uchaguzi wa urais nchini Zambia. Tume ya uchaguzi nchini humo imesema kuwa Lungu amepata asilimia 48 ya kura zilizopigwa.
Alikabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa mgombea wa upinzani Hakainde Hichilema. Wagombea wote wawili walikuwa wameahidi kuboresha mifumo ya elimu na kubuni nafasi za ajira. Uchaguzi huo uliandaliwa kufuatia kifo cha rais Michael Sata aliyefariki dunia mwezi Oktoba mwaka jana
Kwa
mara ya kuanza unagalia trailer ya filamu yangu ya JADA kwa kupitia
blogu yako pendwa ya Odama One. Ninawashukuru watu wote walioshirikiana
nami kumaliza zoezi la kushuti filamu yangu ya JADA ambayo ninauhakika
asilimia 100 ujumbe uliomo ndani ya filamu hii utaenda kubadilisha
maisha yako wewe. Jeniffer Kyaka (Odama)na mwane Jason
Filamu
yangu hii imetengezwa na kampuni yangu ya J-FILM 4 LIFE iliyopo
Kinondoni Biafra Dar es Salaam Tanzania. Katika filamu hii utaona
mabadiliko makubwa sana ya ubora (quality) katika picha, sauti, effects
na jinsi gani ujumbe ulivyomzito.
Siku ya tarehe 19.02.2015
filamu yangu itakuwa sokoni, kwahiyo unaombwa sana kama mdau wangu
kujipatia filamu hii na usikose kumjulisha na ndugu au jamaa yako wa
karibu juu ya ujio huu wa JADA.
Katika filamu hii utaweza kuona
jinsi gani mtoto anayeishi na mama wa kambo anavyokuwa mtukutu na kukosa
heshima ndani ya nyumba. Anashinda kumheshimu mama yake wa kambo
kutokana na kudekezwa kwa baba yake. Nisikumalizie uhondo wa filamu hii
ila kwa sasa angalia trailer hili na baaada hapo kajipatie filamu yako
sokoni
KIFO cha staa wa Nollwood, Muna Obiekwe kimezua gumzo kwa watu wengi nchini Nigeria na wengine ambao wanafuatilia tasnia ya filamu nchini Nigeria, sasa kuna mambo kadhaa ambayo yawezekana ulikuwa huyajui kuhusu staa huyo aliyefariki kutokana na matatizo ya figo.
Staa wa Nollwood, Muna Obiekwe enzi za uhai wake.
Alikuwa muoga wa waandishi wa habari Muna hakuwa tayari kujitokeza hadharani kuomba kuchangishiwa fedha kwa kuwa alikuwa muoga wa kuonekana kwa waandishi wa habari na alipenda maisha yake binafsi yasijulikane.
Muna alikuwa mlevi Inaelezwa kuwa alikuwa akinywa pombe sana licha ya kuwa daktari alimkataza kufanya hivyo. Alikuwa akijihudumia mwenyewe bila msaada wa watu wengine, lakini baadaye siku za mwisho za uhai wake alipata msaada mkubwa kutoka kwa Patience Ozokwor na Kanayo O.
Alimfuata Ibinabo Fiberesima Licha ya kuwa alikuwa mtu aaibu sana, siku za mwisho za uhai wake aliwasiliana na muigizaji wa kike wa Nollywood, Ibinabo Fiberesima lakini hakuwa na msaada kwa kuwa alifariki siku chache baadaye.
Muna alijua tatizo lake siku nyingi Alijua tatizo hilo siku nyingi lakini inaelezwa kuwa alijua atalitatua kimya kimya, aliyapuuzia maumivu aliyokuwa akiyasikia.
Muna alikuwa na mke na watoto wawili Wengi hawakujua lakini alikuwa ni baba wa familia na mwenye watoto wawili.
Kampuni
ya J-Film 4 Life ya mwanadada Jeniffer Kyaka (Odama) itaachia filamu
mpya ya JADA siku ya terehe 19.02.2015. Kama tunavyomjua mwigizaji
maarufu nchini Tanzania Odama ambaye kwa sasa ameamua kutoa filamu yake
ya JADA kama zawadi kwako mdau wa filamu Tanzania ili uweze kuburudika
na kujifunza mengi kutoka kwa mwigizaji huyu,
Katika
filamu hii utaweza kuona jinsi gani mtoto anayeishi na mama wa kambo
anavyoweza kuharibu ndoa ndani ya nyumba kwa vituko na udanganyifu. Mbali na hilo utaona mambo mengi sana ambayo yatakufanya wewe uweze kuwa na muonekano mpya kifikra na kimtazamo. Filamu hii itakubadilisha sana na kukuweka katika ulimwengu mwingine na uliouzoea. Hebu itazame sasa.
Pia unaweza kumuunga mkono na kuinua karama yake hii aliyopewa na mwenyezi
Mungu ya uigizaji kwa kununua filamu zake zilizopo
madukani kama zinavyooneka kwenye tangazo lililotengezwa na Rumafrica (+255 715 851523 www.rumaafrica.blogspot.com) hapo chini na hasa hii filamu mpya ya JADA.
ANGALIA PICHA ZA BEHIND THE SCENE ZA FILAMU YA JADA Picha zimepigwa na Rumafrica +255 715 851 523 | www.rumaafrica.blogspot.com
Rulea Sanga (kulia) na Wastara
ANGALIA MATUKIO MENGINE KWA KUBONYZA "READ MORE" HAPO CHINI KIDOGO