BANTU FILM AWARDS Kilio cha muda mrefu cha wasanii wa Tanzania sasa kimefika kikomo baada ya wadau kujitokeza na kuanzisha tuzo ambazo zinaitwa Bantu Film Awards zinategemewa kufanyika mwezi ujao katikati tarehe na siku tutawajuliisha kupitia blog yako ya The Greatest, leo kulifanyika mkutano na waandishi wa habari katika hotel ya Serena kuzungumzia tuzo hizo, embu twende tuone mambo yalivyokuwa.....
Wasanii wa Bongo Movie wakiwa tayari kuanza mkutano na waandishi wa habari.
The Greatest, Richie na Jb wakimfuatilia mratibu wa tuzo za Bantu Film awards bwana Stewart akifafanua jinsi tuzo zitakavyokuwa
Irene Uwoya naye alikuwepo amesema kuwa amepania kuzoa tuzo za mwaka huu..
Tukiwa makini kufatilia kikao na mambo yatakavyokuwa.
Stewart ndiye Mratibu wa Bantu Film Awards
Stewart akiendelea kutoa ufafanuzi jinsi tuzo za Bantu zitakavyokuwa kwa waandishi wa habari
Safi sana kwa kweli wasanii wa Tanzania tumekuwa na faraja kubwa juu ya tuzo hizi za Bantu
Mambo yakiendelea........
Jb mwenyekiti wa Bongo Movie
The Greatest
Irene Uwoya
Single Mtambalike
Ulifika muda wa Jb kuongea yake machache kuhusu tuzo za Bantu, Kubwa alisisitiza kuwa umefika muda sasa ya wasanii kufanya kazi zenye ubora wa Kimataifa maana hiki ndicho kilkuwa kilio chetu cha muda mrefu sana maana hata wanafunzi wanapokuwa wanasoma lazima mwisho wa mwaka ukifika wanafanya mitihani kama kipimo cha mwaka mzima alichosoma na ndio maana leo nasi tumekuwa na kitu kama hiki cha kujipima kuwa ndani ya mwaka mzima umefanya kitu gani.
Hayo yalikuwa ni maneno ya Jb akiwawakilisha wasanii wa Tanzania nzima..
Waandishi wa habari wakifanya kazi zao kama kawaida yao
Mambo yakiendelea kupamba moto
Irene Uwoya naye akiongea yake machache
Single Mtambalike (Richie) naye akiongea mambo ya msingi yanayotakiwa kuzingatiwa katika tuzo hizo
Ulifika muda wa maswali na majibu toka kwa waandishi wa habari
Nikisikiliza swali toka kwa mwaandishi wa habari wa gazeti la Mwananchi...
Mratibu akilijibu swali ilo kwa ufasaha
Waandishi wa habari wakisiliza jibu kwa ufasaha
Maswali yakiendelea kuulizwa kikubwa waandishi walikuwa wanataka kujua ni vigezo vipi vitakavyotumika kuwachagua watakaokuwa bora kwa mwaka huu