INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Friday, September 6, 2013

HUYU NDO TAPELI ALIE PONEA KIPIGO KIZITO KATIKA UZINDUZI WA FILAMU MPYA YA LULU "FOOLISH AGE"




Tapeli (katikati) akiwa anatolewa nje ya Ukumbi wa Mlimani City wakati wa uzinduzi wa Filamu ya Elizabeth Michael aka LULU mara baada ya kukamatwa akijaribu kutapeli katika moja ya Baa iliyokuwa ikitoa huduma kwa wakazi wa jiji waliofika kwaajili ya Kutazama uzinduzi wa Filamu ya Lulu mwishoni mwa wiki

Kijana ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja (katikati) akiwa amebebwa mzobemzobe na baadhi ya wafanyakazi wa Baa iliyokuwa ikitoa huduma ndani ya Ukumbi wa Mlimani city mara baada ya kukamatwa akitaka kufanya utapeli ndani ya baa hiyo iliyokuwa ikihudumia watu mbalimbali waliofika katika Ukumbi wa Mlimani City kwaajili ya Kushuhudia Uzinduzi wa Filamu ya Lulu iitwayo FOOLISH AGE uzinduzi uliofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City Mwishoni Mwa wiki

Baadhi ya Wafanyakazi na walinzi wakijaribu kumnusuru kijana huyo asipokee kichapo kutoka kwa wakazi wa jiji waliofika katika uzinduzi huo, huku mmoja wa wafanyakazi wa baa hiyo akitaka kupewa maelezo juu ya tukio zima ambalo kijana huyo alipokuwa akitaka kutapeli

Hapa sasa malezo yakiendelea huku akiwa kakamatwa haswa ili asiweze kuwachoropoka

Baadhi ya walinzi waliokuwepo katika uzinduzi huo wakiwa makini kuhakikisha amani inaendelea kuwepo na mtuhumiwa huyo anafikishwa kwenye ombo husika

No comments:

Post a Comment