INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Sunday, February 28, 2016

Diamond Afafanua Kuhusu Video Ya Make Me Sing

Baada kudaiwa Video yake mpya ‘Make Me Sing’ kufanana na ya Lil Wayne,’Make Me Sing’ Diamond amefunguka haya.
‘’Watu wanashindwa kuelewa kila kitu ambacho kinafanyika katika muziki sasa hivi kwenye videos kwenye kuimba na kila kitu,mashairi vilishafanyika,vilishaimbwa,kushutiwa kama vinafanyika ni marudio lakini kila mtu anarudia kwa namna yake anayoijua yeye kwa sababu ukisema nakupenda watu washaimba sana,lakini unafanyaje kwa namna yako wewe ili ilete utamu’’.

Sifahamu Kama Wema Alikuwa Na Mimba: Mirror

Msanii wa muziki wa bongo fleva Mirror, anayefanya kazi chini ya Wema Sepetu amesema hajui kama Wema alishawahi kuwa na mimba ila na yeye anasikia kwa watu na kwenye mitandao.
Msanii huyo ambaye anatamba na wimbo wake mpya Naogopa ambao ameimba na Baraka Da Prince ameyasema hayo alipokuwa akifanya mahojiano katika kipindi cha ENews kinachorushwa na EATV.

Shamsa Danga Ampongeza Magufuli .

MSANII wa filamu wa kike na mtangazaji wa televisheni Shamsa Danga amempongeza Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli baada ya kuangalia tasnia ya filamu na muziki kwa kuwaimiza mamlaka ya Mapato kukamata kazi ambazo hazina stempu za ushuru wa mapato hasa zile za kutoka nje.
“Nampongeza mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli kwa kutoa tamko kwa mamlaka ya Mapato TRA kuwabana wezi wa kazi zetu kwani hali imekuwa mbaya sana kwa filamu za kitanzania baada ya sinema kutoka nje kuuzwa bila kulipia ushuru na sisi kubanwa tulipe,”

Wednesday, February 24, 2016

Shilole Amsaka Mwalimu Wa Kiingereza Ili Kumnoa Aonane Na Nicki Minaj.

Msanii Shilole au Shishi Baby, anatafuta mwalimu wa kumnoa kwenye lugha ya kingereza, ikiwa ni maandalizi ya kuonana na msanii wa Marekani Nicki Minaj.
Kwenye ukurasa wake wa Instagram Shilole amendika tangazo akimtaka mtu ambaye ni mwalimu wa lugha hiyo kuwasiliana, ili aweze kuanza mafunzo hayo.

Linah Sanga Na Wizkid Wazua Jambo .

Imefichuka! Hatimaye ishu ya wanamuziki wa Bongo, Estelina Sanga ‘Linah’, kudaiwa kulala kitanda kimoja na msanii wa muziki kutoka Nigeria, Ayodeji Balogun ‘Wizkid’, imebumburuka.
Baada ya kuandamwa na skendo hiyo ya kutoka kimapenzi na Wizkid huku mashabiki wake waliyo wengi wakishindwa kuamini juu ya uhusiano huo, hatimaye sasa mambo yamevuja na kujidhihirisha kuwa kweli staa huyo alilala hotelini tena kitanda kimoja na Mnigeria huyo.

Wema Sepetu Achanganywa Na Mtoto Wa Kanye West Na Kim Kardashian

Siku moja baada ya mastar wakubwa Kim Kardashian na Kanye West kupost picha ya mtoto wao wa pili aitwaye ‘Saint West’ ameonesha kumchanganya sana bidada Wema Sepetu kwa kile alichokifanya kwenye mitandao yake ya kijamii.
Wema Sepetu jana amepost picha zaidi ya tatu Instgram za mtoto huyo huku akionesha ni jinsi gani ametokea kumpenda mtoto huyo na kudai ni mzuri sana, lakini haikuishia hapo Wema Sepetu aliamua kuweka picha hiyo kwenye Profile yake Instgram na kuweka picha hiyo kama Wall Paper na Screen save kwenye simu yake.

Shilole Hakuwa Mwanamke Mzuri Katika Maisha Yangu: Nuh Mziwanda

Nuh Mziwanda amedai kuwa Shilole hakuwa mwanamke aliyekuwa akimshauri mambo ya msingi.
Akiongea na Clouds FM, Nuh amedai kuwa ex wake huyo hakuwa hata kumshauri ajijenge kimaisha kwakuwa alipenda aendelee kuwa tegemezi.
“Nilikuwa naishi kwa mwanamke wangu (Shilole) alikuwa hataki ninunue hata feni, hajawahi kuniambia ninunue friji,kitanda niweke nyumbani kwa mama yangu vikae,ila wazazi wangu na ndugu zangu walikuwa wakinihimiza kuwa umri unaenda nifungue akili yangu nifikirie ninachopaswa kufanya, mapenzi yasiniendekeze,” alisema muimbaji huyo.

Maisha Yangu Yamekuwa Magumu Sanaa Navaa Ninja Ili Kupanda Daladala: Ray C

Mwanadada ambaye alifanya vizuri kwenyesekta ya muziki wa bongo fleva Ray C amefunguka na kusema kuwa maisha yake kwa sasa ni magumu.
Ray C alisema hayo kupitia kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa kupitia ting’a namba moja kwa vijana EATV, Ray C amedai kuwa kuna muda mwingine analazimika kuvaa hijabu kujificha ili aweze kupanda daladala na kuweza kufika hospital kwa ajili ya matibabu.

Saturday, February 20, 2016

Mange Kimambi Ampa Ushauri Wa Bure Wema Sepetu Baada Ya Mimba Kutoka.

Blogger maarufu hapa nchini Mange Kimambi ametoa ushauri ambao mwenyewe ameuita wa bure kwa mwanadada mwenye jina lake hapa mjini Wema Sepetu, na kumtaka asizae kwa kulazimishwa na maneno ya watu, bali asubiri mpaka akiolewa.

Ray Adai Kumuokoa Nay Wa Mitego Asipigwe.

STAA wa Bongo Movie, Vincent Kigosi ‘Ray’ kwa mara nyingine ameendelea kuteka ‘headlines’ baada ya kuibuka na kudai kuwa alishawahi kumuokoa staa wa Bongo Fleva, Nay wa Mitego asipigwe.
“Nilifanikiwa kumzuia kwasababu wasanii walikuwa wengi wakiongozwa na Wema Sepetu sasa nashangaa mwenzangu Nay ananisakama natumia pesa zote za mauzo ya filamu namalizia kwenye mkorogo,” alisema Nay.

Nipo Single Ila Nikipata Kijana Mwenye Malengo Sitasita Kuwa Nae: Johari

Msanii huyo ameyasema hayo alipokuwa akifanya mahojiano maalum na kipindi cha ENews kinachorushwa na kituo cha EATV.
‘Mimi kwa sasa nipo mwenyewe (Single) akitokea kijana mwenye malengo na mwenye dhamira ya kweli nipo tayari kuwa naye”Amesema Johari.

Mama Yangu Hapendi Nikae Mbali Nae: Ray

Msanii wa filamu Vincent Kigosi ‘Ray’ baada ya kuchanwa kwenye wimbo wa Nay wa Mitego ‘Shika Adabu Yako’ kuwa bado anaishi kwao, amejibu tuhuma hizo kwa kudai anaishi kwao mpaka sasa ili kuwa karibu na Mama yake.
Akizungumza katika kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM Ijumaa hii, Ray alisema yeye ni mtoto wa mwisho hivyo anahitaji kuwa karibu zaidi na Mama yake.

Muziki Unalipa Zaidi Kuliko Filamu: Snura

Mwanamuziki na muigizaji Snura Mushi amesema muziki unamlipa zaidi ndio maana hafikirii kwa kipindi hiki kuwaahidi mashabiki wake ujio wowote wa filamu. “Muziki unalipa kwa kuwa kila kitu kinamhusu msanii na meneja wake, lakini filamu ina mambo mengi kiasi cha kumfanya msanii kuwa na mambo mengi”.

Wednesday, February 17, 2016

Wema Sepetu Asikitika Kuharibikiwa Na Ujauzito.

"Ni kweli. Na imeniuma sana lakini nimefika kwenye hatua maishani mwangu naweza kusema Alhamdulillah for everything.

Alhamdulillah kwa wote wanaojua uchungu nilionao na wameonyesha moyo wa kibinadamu. Nawashukuru kwa upendo wenu, MNANIPA NGUVU.

Alhamdulillah kwa wote wanaojua uchungu nilionao na wamefurahia kwasababu zao binafsi. Nawashukuru kwa uwepo wenu, MNANIPA UJASIRI.

Alhamdulillah kwa siku ya kesho. Ilimradi nina pumzi, SITACHOKA KUJARIBU TENA.

Hata ukikosa, ukakosa, ukokosa eeeeeeh...sema ASANTE, KWELI YEYE NI MUNGU.

Alhamdulillah for EVERYTHING" ameandika Wema kwenye instagram

Producer Wa Mpango Mbaya Kwenda Nigeria Kuhudhuria Tuzo Za AMVCA 2016

MTAYARISHAJI na muongozaji wa filamu ambaye pia ni mwasisi wa Mtandao huu FC Staford Kihore anatarajia kutua nchini Nigeria kwa ajili ya kushuhudia utoaji wa tuzo za African Magic Views Choice Awards tuzo hizo ambazo zinatarajia kutolewa mwezi March 2016, akiongea na FC Kihore amesema kuwa anatarajia kutoa Lagos tarehe 2 March. 2016.

Mimi Ndiye Msanii Mkubwa Wa Filamu Nchini Ninayeuza Sana: Ray

MWIGIZAJI anayefanya vizuri zaidi sokoni katika soko la filamu nchini, Vicent Kigosi anasema kushuka kwa soko la filamu nchini na kukosa ushindani ambao ulikuwepo hapo awali.
Akifafanua zaidi  alisema tofauti na zamani filamu zilikuwa zikizungumziwa zaidi sababu ya ushindani wake mkubwa na marehemu Steven Kanumba.
ray32
Kigosi anasema kipindi hicho ya filamu kutoka kulikuwa na mambo mengi wakifanya ambayo hufanya watu waizungumzie kazi zao kutokana na ushindano wao.

Saturday, February 6, 2016

Aliyedaiwa Kumbaka Shilole Afunguka Mazito.

KATIKA maho-jiano na Mwandishi nguli wa burudani nchini wa Gazeti la Ijumaa, Erick Evarist, Februari 2012, msanii Zuwena Mohammed ‘Shilole’ alinukuliwa akieleza kisa hiki:
“Katika maisha yangu nimepitia mitihani mingi, mmoja wapo ni huu wa kulazimishwa kufanya mapenzi bila ridhaa yangu, kwa kifupi nilibakwa.”
Kwa kuwa kisa hiki cha kusikitisha kimesemwa sana na Shilole katika mahojiano yake mengi na vyombo mbalimbali vya habari, Gazeti la Ijumaa lililazimika kufunga safari mpaka wilayani Igunga mkoani Tabora ili kumtafuta anayetuhumiwa kumbaka ambapo lilifanikiwa kufanya naye mahojiano.

Masanja Mkandamizaji Kufungua Kituo Chake Cha TV Na Radio.

Mchekeshaji wa kundi la Orijino Komedi, Masanja Mkandamizaji ameweka wazi mpango wake wa kufungua kituo cha Radio na TV ambavyo atavisimamia yeye mwenyewe.
Akizungumza na 255 katika kipindi cha XXL cha Clouds Fm Alhamisi hii, Masanja alisema tayari ameshapata mafunzo ya uandishi wa habari ili kujifunza kuhusu kuendesha vituo hivyo.

Nisha Awa Balozi Wa New Hope Family Group.

MSANII wa Filamu hapa nchini, Salma Jabu ’Nisha’ amekuwa Balozi wa Kikundi cha New Hope Family Group chenye makazi yake Kigamboni Dar kinachojihusisha na masuala ya kutetea watoto waishio katika mazingira hatarishi.
Hafla ya kumtambulisha msanii huyo imefanyika leo katika Ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo) ambapo mwenyekiti wa taasisi hiyo, Omary Kombe, amesema lengo kubwa la kumteua Nisha kuwa balozi wao ni kutokana na mtazamo wao kuwa kupitia sanaa yake ya maigizo anaweza kuwa balozi mzuri kwani atatumia kipaji chake hicho katika kufikisha ujumbe kwenye jamii

Nimemchuna Ostaz Juma Kiasi Cha Kutosha: Johari

Mkongwe kwenye sinema za Kibongo, Blandina Chagula ‘Johari’ amevunja ukimya na kuweka bayana kuwa miaka kadhaa iliyopita aliwahi kumchuna sana Mkurugenzi wa Kampuni ya Watanashati Entertainment, Ostaz Juma Namusoma alipokuwa akimhitaji awe mchumba wake. Johari alifunguka hayo hivi karibuni baada ya mwanahabari wetu kumfungia safari hadi ofisini kwake Sinza-Mori, jijini Dar es Salaam na kumuuliza juu ya taarifa zilizokuwa kwenye makabrasha yetu kwamba mwigizaji huyo miaka kadhaa iliyopita, aliwahi kumchuna sana Ostaz Juma lakini habari hizo hazikuandikwa gazetini.

VJ Penny Apagawishwa Na Mimba Ya Wema Sepetu.

Mwanadada anayepiga dili la utangazaji kupitia Zouk TV ambaye aliwahi kuwa mpenzi wa Nasibu Abdul ‘Diamond’, Penniel Mungwilwa ‘Penny’ amefunguka kuwa mimba ya shosti wake, Wema Sepetu inampa ‘uchizi’ kwa kutamani kila kukicha na yeye anase ujauzito.

Thursday, February 4, 2016

Home Coming Na Going Bongo Ni Fundisho Kwa Watengeneza Filamu Tanzania: Rose Ndauka

Msanii wa filamu Rose Ndauka amesema kuwa filamu mpya ya Homecoming pamoja na Going Bongo ni filamu bora zaidi kuzinduliwa nchini mwaka 2016 ambapo amewataka wasanii wa Tanzania kuiga mfano.
Akizungumza na Bongo5 Jumatatu hii, Rose alisema kila msanii wa filamu aliyoangalia filamu hizo lazima alitoka na kitu.
“Mwaka umeanza kwa changamoto ya kazi, hivi karibuni kuna kazi zilizinduliwa Homecoming na Going Bongo, ni kazi kali sana,” alisema Rose.

Batuli Amshutumu Ray Kwa Kumtapeli, Ray Ajibu Mapigo.

Alianza Batuli kwa kuandika haya;
Haki Ya Mtu Haizami 
Swali: Movie Yako Nimecheza Mwaka Juzi Wiki Moja Kabla Ya Mwezi Mtukufu Wa Ramadhani, Makubaliano Yetu Ya Kazi Kimkataba Ni Siku 10 Tu Lkn Ulienda Kinyume Na Matokeo Yake Nilifanya Kazi Yako Mwezi Mzima Wa Ramadhan Je Ulikuwa Sawa!? Swali: Pamoja Na Usumbufu Wako Wote Nilifanya Kazi Sikufanya!? Kumbuka Nilikuwa Kwenye Swaumu
Swali: Toka Mwaka Juzi Mpaka Mwaka Jana Ni Mm Ndie Niliekuwa Nafuatilia Malipo Yng Ofisini Sio Chini Ya 20 Times Na Umekuwa Ukinikimbia Matokeo Yake Nikachoka Kuja, Simu Zng Umekuwa Ukizipokea Unapotaka Na Sms Unanijibu Unavyotaka Je Mkataba Wetu Ulisema Hivyo!? Swali : Naimani Ww Una Mkataba Upo Ofisini Kwako Upige Picha Tuone Kama Upo Unavyodai, Binafsi Kila Mtu Anajua Nyumba Yng Iliteketea Moto Hivyo Sina Kitu Na Ndio Maana Umekuwa Ukinitendea Unyama Huu Je Kuna Anaeweza Kukaa Kimya Zaidi Ya Mwaka Mmoja Na Hatimae Unaona Kazi Inatoka Wakati Hujalipwa!?
Swali : Ni Movie Ngapi Nilizofanya Kwenye Kampuni Yako Chini Ya Johari!? Ni Zaidi Ya 3 Je Nililalamika!? Kwanini Hii Ambayo Johari Hakuwepo Nikaingia Mkataba Na Ww Iweje Nilalamike!? Dhulma Itakufikisha Pabaya Sana, Tambua Nilifanya Kazi Yako Ktk Mazingira Magumu, Nilikuwa Kwenye Swaumu Baba Nilifuturu Mabarabarani Chipsi Na Vingine Visivyo Rasmi Yote Ni Ktk Kutimiza Kazi Yako, Nionyeshe Mkataba Unaosema Nilipwe Baada Ya Mwaka 1 Na Kuendelea Hakika Umeonyesha Ulivyo Na Roho Ya Dhulma Sijawahi Kulalamika Popote Kuhusu Unachonifanyia Kwa Sbb Nilijua Ipo Siku Utanilipa Changu Matokeo Yake Umeona Ujivishe Ujemedari Lakini Haitokisaidia Chochote, Kama Haki Yng Basi Itanifuata Hata Nikiwa Kaburini….Be Blessed….Allah Bariq
Ray akajibu kwa kuandika haya;.........

Nuh Mziwanda Amuangukia Shilole Ili Warudiane.

STAA wa Wimbo wa Msondo Ngoma, Naftari Mlawa ‘Nuh Mziwanda’, anasemekana amemwangukia kwa mara nyingine aliyekuwa mpenzi wake, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ kwa kumtaka warudiane.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, Mbongo Fleva huyo amekuwa katika wakati mgumu tangu alipoachana na Shilole hivyo kulazimika kumpigia simu na kumwandikia ujumbe wa maneno akimuomba amsamehe na warejeshe penzi lao kama ilivyokuwa zamani.

Zari Aogopa Kuishi Bongo.

Tumbuatumbua ya majipu ya Rais wa Awamu ya Tano, Dk. John Pombe Magufuli ‘JPM’ inadaiwa kumtisha mwandani wa Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kuja kuishi Bongo ikidaiwa kisa ni utajiri mkubwa alionao wenye shaka juu ya malipo ya ushuru na mapato.
Habari kutoka kwenye chanzo cha ndani cha familia ya Diamond, zimeeleza kuwa Zari alikuwa na mpango wa kuhamishia miradi na makazi yake rasmi Dar mwanzoni mwa mwaka 2016 lakini ndoto hiyo inaonekana kuyeyuka.

Riyama Ally Kufunga Ndoa .

Msanii wa filamu Riyama Ally, baada ya kuingia katika hatua ya Uchumba kimya kimya na mpenzi wake ambaye ni msanii chipukizi wa Bongo Fleva
leo Mysterio, amesema kuwa mpango wao wa kuhalalisha mahusiano yao umeanza kunukia, hasa baada ya msanii huyo kujihakikishia nafasi yake kwa kutoa posa.