Blogger maarufu hapa nchini Mange Kimambi ametoa ushauri ambao mwenyewe ameuita wa bure kwa mwanadada mwenye jina lake hapa mjini Wema Sepetu, na kumtaka asizae kwa kulazimishwa na maneno ya watu, bali asubiri mpaka akiolewa.
Mange ametoa ushauri huo kwenye ukurasa wake wa instagram baada ya seke seke lililomkuta mwanadada huyo la kushambuliwa na watu wakimtuhumu kuwa hana uwezo wa kuzaa, kabla na hata baada ya kuharibika kwa ujauzito aliokuwa nao siku za hivi karibuni.
Mange amedai pia Wema ni mdogo kiumri kuitwa mama, hivyo asikimbilie kuzaa kama muda bado.
“Hivi kwanini unakubali kuwa pressured na wajinga wa social media kuzaa when you are not ready? Mbali na familia yako ni mimi peke yangu ndo ninae jua umri wako Wema, Wema huna hata 26 years we mtoto, toka lini mtu mdogo hivyo akawa classified as tasa? Why unakubali kupewa pressure uzae ukiwa mdogo hivi? hata kuolewa hujaolewa??
Ameendelea kwa kumshauri …..”Achana nao mdogo wangu, acha waongeee midomo mali yao, ubiri uolewe ndo uzae, mwishowe uje kuzaa mtoto while you are not ready au uzae na mtu huna mpango wa kuishi nae kisa tu uwakomeshe hawa wajinga wa kwenye mitandao. Utajikomesha mwenyewe, Please dont succumb to the pressure, You are way too young”. Ameandika Mange kwenye ukurusa wake, maneno yaliyosindikizwa na picha ya Wema sepetu.
Pamoja na hayo Mange pia alimtaka Wema kuwa kwenye mahusiano na watu wasiojulikana kama yeye mwenyewe alivyo, kwani itamsaidia kumuongoza na kuepuka maneno ya watu pale atakapokuwa msiri wa maisha yake, na kuepuka mabalaa ya kudhalilishwa na kukashifiwa kwenye mitandao, iwapo hawatafikia mahusiano yake na Idris hayatafanikiwa.
“If not nakushauri tafuta mwanaume ambaye hayuko hata Instagram au social media ili akuongoze vizuri. Find a guy mwenye maisha tofauti kabisa na ya kwako. Mkaka flani meneja wa benki huyo ndo atakubadilisha completely but these guys wa kwenye mitandao kama wewe issue itakuwa pale pale”, aliandika Mange.
Ifahamike kwamba Mange Kimambi ndiye mtu aliyevumbua kipaji cha Wema, na kumshauri kuingia kwenye mashindano ya ulimbwende ya Miss Tanzania, ambapo aliibuka mshindi na kuiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya urembo ya dunio (Miss World).
Eatv.tv
No comments:
Post a Comment