INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Tuesday, March 4, 2014

MH. JANUARI MAKAMBA AMPONGEZA MCHEKESHAJI MASANJA MKANDAMIZAJI KWA JUHUDI ZAKE ZA KUMTEMBELEA OFISINI KWAKE NA KUZUNGUMZA MASWALA YA WAIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI. HAYA ALIYASEMA KATIKA UZINDUZI WA ABLAMU YA MESS JACOB CHENGULA SIKU YA JUMAPILI o2.03.2014 UBUNGO PLAZA

Siku ya Jumapili  ilikuwa ni siku ya furaha na ndelemo katika ukumbi tulivu wa Ubungo Plaza katika kukamilisha kusudi la Mungu juu ya mwimbaji maarufu Tanzania Mess Jacob Chengula alipokuwa akizindua albamu yake ya "Mungu Habadiliki" Tamasha hili lilisindikizwa na waimbaji zaidi ya 20 waliovamia jukwaa na kuwaacha watu kupagawa na uwepo wa Mungu ulioachiliwa kwa njia ya uimbaji. Viti vilikuwa havikaliki na kuwaacha  ma-MC kuwa katika wakati mgumu sana wa kuwaomba watu wakae chini.


Mh. January Makamba wa pili kutoka kushoto
Kila mwimbaji aliimba kwa kiwango cha juu sana mpaka mgeni rasmi Mh Januari Makamba kuwaita baadhi ya waimbaji ili ashikane nao mkono kama ishara ya ku-appreciate kazi yao, mmojawapo alikuwa Edson Mwasabwite.
Baada ya uimbaji kufanyika, mgeni rasmi akiongozana na wachungaji na wazee wa kanisa kutoka katika kanisa la Mito ya Baraka kwa Askofu Mwakiborwa anakoabudu Mess Jacob Chengula walipanda jukwaani kwa lengo zima la kuiombea albamu ile na kuifungua rasmi.
Mgeni rasmi Januari Makamba alipomaliza kuizindua aliweza kuongea machache kuhusiana na waimbaji. Aliwapongeza waimbaji kwa ushirikiano wao waliuonyesha katika kumuunga mkono rafiki yao Mess Jacob Chengula. Alikipongeza Chama Cha Muziki Tanzania na viongozi wao kwa kazi nzuri wanayofanya kwa waimbaji wa nyimbo za Injili. Mh Januari Makamba aliwaalika viongozi wa Chama cha Muziki Tanzania na baadhi ya waimbaji kufika katika Bunge la Jamhuri ya Muungano ili waweze kutoa matatizo yao na changamoto wanazopata katika huduma yao ya uimbaji.
Mh. Januari Makamba aliweza kuwaonya waimbaji wa nyimbo za injili juu ya style za uchezaji ambazo hazina baraka kwa mwenyezi Mungu kuziacha na kucheza kama vile Mungu anavyotaka watu wake wamchezee. Pia aliwaonya wale waimbaji ambao wamebarikiwa na kuwa maarufu sana, waachane na tabia ya kujivuna na kujiona wao ni wao. Mbali na kuwaalika katika Bunge, pia aliwaomba waimbaji na viongozi kutosita kufika ofisini kwake muda wowote na hakuna mtu atakayeweza kuwazuia kumuona hata kama atakuwa na majukumu mengi, lakini katika masuala ya Mungu kwa kupitia waimbaji na viongozi wa nyimbo za injili yuko tayari kusimamisha kwa muda na kuwasikiliza.

Pia alimpongeza sana Mwingizaji na mchekeshaji Emmanuel Mgaya (Msanja Mkandamizaji) kwa juhudi zake za kumtembelea ofisini kwake na kuzunguza matatizo ya waimbaji wa nyimbo za injili Tanzania. Na hii imemfanya leo Mh. Januari Makamba kuwataka waimbaji kupanga siku ya kwenda Bungeni ili wakatoe matatizo yao kwa wakuu wa nchi.

Wimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania

MDOGO WAKE NA MH.JANUARI MAKAMBA AKITAMBULISHA WATU WALIONGOZANA NA KAKA YAKE MH.JANUARI MAKAMBA
 Mdogo wake na Mh. Januri Makamba
Mtoto wa Mh Januari Makamba akitambulishwa
Mh Januari Makamba akimwangalia mwanae wakati wa kutambulishwa
 Mtangaza wa Passion FM Bwana Sanga

KIPINDI CHA WAIMBAJI KUACHIA MASONGI YA BWANA MUNGU WETU
Silas Mbise
 Neema Gasper

KIPINDI CHA MESS JACOB CHENGULA KUINGIA UKUMBINI KWA MARA YA KWANZA

Mess Jacob Chengula akiongozana na Masanja Mkandamizaji wakiingia ukumbini
Watu wakimsindikiza Mess Jacob Chengula akielekea kwa Mgeni Rasmi Mh. Januari Makamba

Mh. Januari Makamba akisalimiana na baadhi ya waimbaji akiwemo Masanja Mkandamizaji, Bony Mwaitege na wengine wengi waliomsindikiza Mess Jacob Chengula katika High Table
Mess Jacob Chengula akisalimina na mdogo wake na Mh. Januari Makamba na kulia ni mwanae na mheshimiwa
Bony Mwaitege


Kulia ni Mess kabla ya kuzindua albamu yake akiwa katika pozi baada ya kumaliza zoezi la kuwasalimia wageni waalikwa waliokaa katika High Table ya Mh. Janauari Makamba
Hawa ni waimbaji wa nyimbo za Injili waliokaa High Table
 Mess Jacob Chengula akisalimiana na Mgeni Rasmi Mh. Januari Makamba
 Mess Jacob Chengula na Mh. Januari Makamba

 Masanja Mkandamizaji na Bony Mwaitege
Mh. Januari Makamba akicheza wakati Masanja Mkandamizaji akilianzisha songi lake la Watu wako Biszeee


KIPINDI CHA KUSOMA RISALA YA MESS JACOB CHENGULA
 John Shabani akisoma hotuba ya Mess jacob Chengula kwa mgeni Rasmi Januari Makamba

John Shabani

John Shabani akimkabidh mgeni rasmi Mh Januari Makamba hotuba ya Mess Jacob Chengula

Mh Januari Makamba aweka saini katika hotuba ya Mess Jacob Chengula
 Neema Gasper aliamua kutokelezea baada ya ku-perform
Neema Gasper
Tiketi zilizotumika katika uzinduzi huu. Kazi imefanywa na RumAfrica +255 715 851523

Picha zimepigwa na RumAfrica
+255 715 851523
Tembelea

MWIGIZAJI KUTOKA KENYA APATA TUZO LA OSCAR.














Lupita Nyong'o

Kama ilivyokuwa imetarajiwa na wengi mwigizaji mashuhuri kutoka Kenya Lupita Nyong'o amenyakuwa tuzo la Oscar la mwigizaji msaidizi wa kike kwa jukumu lake la kuelezea masaibu ya Patseh katika filamu ya utumwa ya ''12 Years A Slave.''

Baada ya kupokea tuzo hilo Lupita amesema " Haikwepi mawazo yangu kwamba hata dakika moja ya furaha katika maisha yangu ni shukran na maumivu makubwa kwa mtu mwingine.''
Kisha Lupita akaongeza kusema, " Na iwe ukumbusho kwangu na kila mtoto kwamba kokote unakotoka, ndoto zako ni halisi.''
Mwigizaji Jared Leto alinyakuwa tuzo la mwigizaji bora msaidizi wa kiume kwa jukumu lake la kuelezea maisha ya mwanamke aliye na jinsia mbili aliyekuwa na akiishi na virusi vya HIV katika filamu Dallas Buyers Club.
Alilazimika kupunguza uzani kwa kipindi kifupi ili kuigiza.
Sherehe ya kutolewa kwa tuzo hizo zimefanyika mjini Los Angeles nchini Marekani.

Monday, March 3, 2014

WEMA SEPETU AFANYA SHINDANO LA KUSAKA VIPAJI VYA KUIGIZA KWA WATOTO ENEO LA LEADERS JIJINI DAR LEO



Msanii wa Bongo Movie, Wema Sepetu na pia alikuwa ni jaji wa shindano la kusaka vipaji kwa watoto waliokuwa na umri kuanzia miaka minne(4) mpaka kumi na tano (15) akizungumza na mshiriki wa shindano hilo la kusaka vipaji kwa wanaojua kuigiza. Shindano hili limefanyika leo kwenye viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam na kuwapata watoto watatu waliokuwa wanaitajika.

Jaji Wema Sepetu akiwa na Jaji mwenzake Aunt Ezekiel walipokuwa wanawafanyia usahili watoto waliofika kwenye shindano la kusaka vipaji vya watoto wanaoweza kuigiza.

Msanii wa Bongo Movie, Wema Sepetu akicheza muziki na mmoja wa washiriki wa shindano la kusaka vipaji lililofanyika leo kwenye viwanja vya Leaders.


ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI

Director wa shindano la kusaka vipaji, Adam akizungumza jambo

Msanii wa Bongo movie na aliyekuwa Jaji, Wema Sepetu akizungumza na mtoto aliyekuwa anashiriki kwenye shindano la kusaka vipaji kwa watoto wenye miaka minne mpaka miaka 14.

Baadi ya washiriki waliofika wakiwa na wazazi wao kwenye shindano la kusaka vipaji vya watoto wanaojua kuigiza.

Mmoja wa watoto akiigiza kwa kulia mbele ya majaji (hawapo Pichani) katika shindano la kusaka vipaji vya kuigiza lililofanyika leo kwenye viwanja vya leaders Club.


Msanii wa bongo movie akiiigiza na mmoja wa washiriki wa shindano hilo la kusaka vipaji vya watoto kwani alileta hisia kali kwa kuigiza vizuri

Palikuwa hapatoshi kwenye Stage maana watoto walikuwa wanafanya ya kwao


Msanii wa Bongo Movie, Aunt Ezekiel akiigiza na mmoja wa watoto waliokuwa kwenye shindano la kusaka vipaji.


Nae Adam (Kushoto) akuwa mbali maana hata yeye aliamua kuigiza na mmoja wa washiriki waliofika kwenye shindano hili

Wema Sepetu akiigiza na mmoja wa washiriki wa shindano la kusaka vipaji vya kuigiza

Baadhi ya washiriki wakiwa na wazazi wao




Hawa ndio watoto waliofanikiwa kuingia nusu fainali

Hawa watoto watatu ndio waliofanikiwa kushinda shindano hili mbalo liikuwa linahitaji watoto watatu

Sunday, March 2, 2014

KWANINI UKOSE TAMASHA HILI SIKU YA LEO..MESS JACOB CHENGULA KUZINDUA ALBAMU YAKE YA MUNGU HABADILIKI UBUNGO PLAZA

Jumapili ya leo ni balaa katika ukumbi wa kujidai UBUNGO PLAZA. Watu wa Mungu kukusanyika pamoja kumtukuza Mungu ambapo Mess Jacob Chengula atakuwa anazindua albamu yake ya Mungu Habadiliki. Njoo uone kazi ya Mungu na utabarikiwa sana na uimbaji wa leo

MHUSIKA WA TAMASHA
 Mess Jacob Chengula wa Mungu Habadiliki

ALBAMU INAYOZINDULIWA
Albamu ya Mungu Habadiliki ya Mess Jacob Chengula

ENEO LA UZINDUZI NI UBUNGO PLAZA

Katika hotel ya Blue Pearl

MGENI RASMI WA TAMASHA HILI

Mgeni rasmi ni Naibu Waziri wa mawasiliano Tanzania Mh Januari Makamba

WAIMBAJI WATAKAIMBA SIKU YA LEO JUMAPILI UBUNGO PLAZA

Rose Muhando

Masanja Mkandamizaji

Atosha Kissava

Bony Mwaitege

Upendo Nkone

Silas Mbise

Neema Gasper

Edson Mwasabwite

Madamu Ruti

Faraja Ntaboba

Bahati Bukuku

Mwanamapinduzi

Stella Joel


Enock

Miriamu Lukindo

Joshua Makondeko

VIINGILIO
VIP



VITI VYA KAWAIDA


WATOTO


TANGAZO LIMETENGENEZWA NA RUMAFRICA



Tembelea
www.messchengula.blogspot.com
www.rumaafrica.blogspot.com

FULSA KWENU MASHABIKI WA WEMA SEPETU..!! TAZAMA ALICHOKITANGAZA HAPA..!!

Mlete mwanao mwenye kipaji cha kuigiza acheze na Wema Sepetu, Aunt Ezekiel na Hemed Suleyman kwenye Movie mpya ya FAMILY..


Saturday, March 1, 2014

ILE FILAMU MLIYOKUWA MKISUBIRI YA JICHO LANGU ITAKUWA SOKONI TAREHE 31.03.2014. JIPATIE NAKALA YAKO

Anza mwezi Aprili na burudani kupitia  filamu mpya ya JICHO LANGU kutoka katika kampuni ya J-Film 4 Life. Tarehe 31.03.2014 ikifika jisogeze taratibu katika duka lililo karibu nawe ujipatie nakala yako ya JICHO LANGU.Ndani ya filamu hii utajifunza mengi kupitia mwigizaji maarufu nchini Tanzania Jennifer Kyaka (ODAMA) na wasanii wenzake. Hakika JICHO LANGU itakufungua mambo mengi ambayo ulikuwa hujui na hujawahi kuyaona yakitokea katika jamii yetu.