Siku ya Jumapili ilikuwa ni siku ya furaha na ndelemo katika ukumbi tulivu wa Ubungo Plaza katika kukamilisha kusudi la Mungu juu ya mwimbaji maarufu Tanzania Mess Jacob Chengula alipokuwa akizindua albamu yake ya "Mungu Habadiliki" Tamasha hili lilisindikizwa na waimbaji zaidi ya 20 waliovamia jukwaa na kuwaacha watu kupagawa na uwepo wa Mungu ulioachiliwa kwa njia ya uimbaji. Viti vilikuwa havikaliki na kuwaacha ma-MC kuwa katika wakati mgumu sana wa kuwaomba watu wakae chini.
Mh. January Makamba wa pili kutoka kushoto
Kila mwimbaji aliimba kwa kiwango cha
juu sana mpaka mgeni rasmi Mh Januari Makamba kuwaita baadhi ya
waimbaji ili ashikane nao mkono kama ishara ya ku-appreciate kazi yao,
mmojawapo alikuwa Edson Mwasabwite.
Baada ya uimbaji kufanyika, mgeni
rasmi akiongozana na wachungaji na wazee wa kanisa kutoka katika kanisa
la Mito ya Baraka kwa Askofu Mwakiborwa anakoabudu Mess Jacob Chengula walipanda jukwaani kwa
lengo zima la kuiombea albamu ile na kuifungua rasmi.
Mgeni rasmi Januari Makamba
alipomaliza kuizindua aliweza kuongea machache kuhusiana na waimbaji.
Aliwapongeza waimbaji kwa ushirikiano wao waliuonyesha katika kumuunga
mkono rafiki yao Mess Jacob Chengula. Alikipongeza Chama Cha Muziki
Tanzania na viongozi wao kwa kazi nzuri wanayofanya kwa waimbaji wa
nyimbo za Injili. Mh Januari Makamba aliwaalika viongozi wa Chama cha
Muziki Tanzania na baadhi ya waimbaji kufika katika Bunge la Jamhuri ya
Muungano ili waweze kutoa matatizo yao na changamoto wanazopata katika
huduma yao ya uimbaji.
Mh. Januari Makamba aliweza kuwaonya
waimbaji wa nyimbo za injili juu ya style za uchezaji ambazo hazina
baraka kwa mwenyezi Mungu kuziacha na kucheza kama vile Mungu anavyotaka
watu wake wamchezee. Pia aliwaonya wale waimbaji ambao wamebarikiwa na
kuwa maarufu sana, waachane na tabia ya kujivuna na kujiona wao ni wao.
Mbali na kuwaalika katika Bunge, pia aliwaomba waimbaji na viongozi
kutosita kufika ofisini kwake muda wowote na hakuna mtu atakayeweza
kuwazuia kumuona hata kama atakuwa na majukumu mengi, lakini katika
masuala ya Mungu kwa kupitia waimbaji na viongozi wa nyimbo za injili
yuko tayari kusimamisha kwa muda na kuwasikiliza.
Pia alimpongeza sana Mwingizaji na mchekeshaji Emmanuel Mgaya (Msanja Mkandamizaji) kwa juhudi zake za kumtembelea ofisini kwake na kuzunguza matatizo ya waimbaji wa nyimbo za injili Tanzania. Na hii imemfanya leo Mh. Januari Makamba kuwataka waimbaji kupanga siku ya kwenda Bungeni ili wakatoe matatizo yao kwa wakuu wa nchi.
Pia alimpongeza sana Mwingizaji na mchekeshaji Emmanuel Mgaya (Msanja Mkandamizaji) kwa juhudi zake za kumtembelea ofisini kwake na kuzunguza matatizo ya waimbaji wa nyimbo za injili Tanzania. Na hii imemfanya leo Mh. Januari Makamba kuwataka waimbaji kupanga siku ya kwenda Bungeni ili wakatoe matatizo yao kwa wakuu wa nchi.
Wimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania
MDOGO WAKE NA MH.JANUARI MAKAMBA AKITAMBULISHA WATU WALIONGOZANA NA KAKA YAKE MH.JANUARI MAKAMBA
Mdogo wake na Mh. Januri Makamba
Mtoto wa Mh Januari Makamba akitambulishwa
Mh Januari Makamba akimwangalia mwanae wakati wa kutambulishwa
Mtangaza wa Passion FM Bwana Sanga
KIPINDI CHA WAIMBAJI KUACHIA MASONGI YA BWANA MUNGU WETU
KIPINDI CHA WAIMBAJI KUACHIA MASONGI YA BWANA MUNGU WETU
KIPINDI CHA KUSOMA RISALA YA MESS JACOB CHENGULA
John Shabani
John Shabani akimkabidh mgeni rasmi Mh Januari Makamba hotuba ya Mess Jacob Chengula
Mh Januari Makamba aweka saini katika hotuba ya Mess Jacob Chengula
Tiketi zilizotumika katika uzinduzi huu. Kazi imefanywa na RumAfrica +255 715 851523
Picha zimepigwa na RumAfrica
+255 715 851523
Tembelea
No comments:
Post a Comment