Wakitoka kwenye viwanja vya mnazi mmoja kuelekea Lumumba kuanza kazi.
Meya wa wilaya ya Ilala, Jerry Slaa akiwa kazini.
Wakiwa wanafagia.
Msanii mkongwe wa filamu, Mzee Kambi akisukuma toroli la takataka.
Kazi na dawa, wasanii wa filamu wakizungumza kidogo.
Mdogo wa Rose, Rachel Ndauka akimsapoti dada yake.
Mdau wa filamu Bongo anayewasaidia wasanii mambo mbalimbali, Mama Rolaa akiwa kazini.
Rose akionesha jiko la kisasa alilotoa kwa manispaa hiyo kwa ajili ya kuchomea takataka ambalo halina madhara kwa mazingira.
Rose Ndauka (katikati) akitoa shukurani kwa watu waliomsapoti.
Meya wa Ilala, Jerry Slaa (wa pili kushoto) akiwashukuru waliojitokeza kwenye kampeni hiyo, wa kwanza kulia ni mkurugenzi wa manispaa ya Ilala, Mwendahasara.
MSANII wa filamu za Kibongo, Rose Ndauka ameibuka na jipya ambapo leo amefanya kampeni ya kusafisha jiji aliyoipa jila la Ng’arisha Tanzania ambapo wadau mbalimbali wamejitokeza wakiwemo viongozi wa serikali na wasanii wenzake.
Kampeni hiyo imefanyika katika wilaya ya Ilala ambapo walianza kufagia kuanzia maeneo ya Lumumba mpaka Mnazi Mmoja.
No comments:
Post a Comment