INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Monday, February 9, 2015

JB AMRUDISHA REGINA KATIKA ULIMWENGU WA FILAMU


Filamu hii pamoja na kuchezwa siku nyingi bado watu wanaikumbuka sana.na wengine wanauliza yuko wapi Regima.Jerusalem itawaletea movie yake myingine ambayo alicheza na Marehemu Adam kuambiama mara baada ya kutoka filamu ya mvuvi chale.Asanteni kwa kupenda movie zetu”.
Hayo ndio maelezo ya JB ambae ndio mkurugenzi wa kampuni ya Jerusalem.

MSANII WA MAIGIZO 'MAMA MASHAKA' AFARIKI DUNIA


Mwajuma Abdallah ‘Mama Mashaka’ enzi wa uhai wake.

MSANII wa maigizo aliyewahi kuwika na kundi la Kaole Sanaa Group, Mwajuma Abdallah ‘Mama Mashaka’ amefariki dunia.
Mama Mashaka amefariki usiku wa kuamkia leo majira ya saa tano za usiku katika Hospitali ya Amana iliyopo Ilala, jijini, Dar.Kwa habari zaidi tutaendelea kukujuza hapa.



Waombolezaji wakiwa wenye nyuso za simanzi.


Bi Mwenda akiwa msibani leo

JADA...JADA...JADA...MUDA WAKE WA KUINGIA SOKONI UMEKARIBIA NI TAREHE 19.02.2015


REDDS MISS TANZANIA 2013, HAPPYNESS WATIMANYWA AFUNGUA CLUB YA KUJISOMEA WATOTO YA NKEMA


Redds Miss Tanzania 2013, Happness Watimanywa (wa pili kushoto), akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Club ya kujisomea watoto ya ijulikanayo kwa jina la Nkema Reading Club iliyopo Kinondoni Mtaa wa Kasana jirani na Kituo kinachojengwa kwa ajli ya Mabasi ya Mwendokasi nyuma ya Sheli ya Mwanamboka katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Club hiyo, Getrude Kilyabusebu.

Redds Miss Tanzania 2013, Happyness Watimanywa (kushoto), akiwafundisha kusoma watoto wakati wa hafla ya kufungua Club ya kujisomea watoto ya Nkema Reading Club iliyopo Kinondoni Dar es Salaam juzi ambapo alikuwa mgeni rasmi.

Redds Miss Tanzania 2013, Happyness Watimanywa akiwa katika picha ya pamoja na watoto na wazazi wao wakati wa hafla hiyo.

Mtoto Careen Elly akimlisha keki maalumu Redds Miss Tanzania, Happnes Watimanywa iliyoandaliwa kwa ufunguzi wa Club hiyo.

Watoto wakijisomea vitabu mbalimbali ndani ya Club hiyo. Kutoka kushoto ni Hope Njau, Careen Elly na Angel Mtango.

Mkurugenzi Mtendaji wa Club hiyo Getrude Kilyabusebu (katikati), akiwafundisha kusoma watoto hao.

Mmoja wa maofisa wa Club hiyo, Hilda Ngaja (kulia), akiwaelekeza jambo watoto hao.

Keki maalumu ya hafla hiyo ilivyokuwa ikionekana.

Mkurugenzi Mtendaji wa Club hiyo Getrude Kilyabusebu (katikati), akizungumza na wazazi watoto hao (hawapo pichani), wakati wa uzinduzi huo. Kushoto ni Mmoja wa maofisa wa Club hiyo, Rose Kelly na Redds Miss Tanzania 2013, Happyness Watimanywa.


Careen Elly (kulia), akimwelekeza mwenzake namna ya kuandika.
Redds Miss Tanzania 2013, Happyness Watimanywa akiwa katika picha ya pamoja na watoto wa Club hiyo pamoja na wazazi wao.

Dotto Mwaibale

WAZAZI wametakiwa kutowaacha watoto wao kucheza baada ya muda wa masomo badala yake wawapeleke kwenye vituo vya kujisomea ili kupata maarifa zaidi.

Mwito huo umetolewa na Redds Miss Tanzania 2014, Happyness Watimanywa wakati wa hafla ya kufungua Club ya watoto ya kujisomea ya Nkema Reading Club iliyopo Kinondoni Dar es Salaam juzi ambapo alikuwa mgeni rasmi.

"Tunawaomba wazazi kote nchini wajenge tabia ya kuwapeleka watoto kwenye club za namna hiyo badala ya kuwaacha wakicheza" alisema Watimanywa.

Mkurugenzi Mtendaji wa Club hiyo Getrude Kilyabusebu alisema ameamua kuanzisha clabu hiyo ili kutoa fursa kwa watoto kujifunza mambo mabalimbali ambayo hawayapati katika shule zao.

"Tunahitaji watoto wajifunze mambo ya utamaduni wetu badala ya kuiga utamaduni wa nchi za nje ndio maana tumeanzisha club hii ambayo itakuwa inawakutanisha watoto siku ya Jumamosi ambapo watakuwa na uwezo wa kusoma bila kushurutishwa" alisema Kilyabusebu.

Alisema watoto kushiriki katika club hiyo itawaongeza ujasiri na kujiamini katika masomo yao na hasa namna ya kujieleza mbele ya watu kwani hapa nchini kumekuwa na changamoto kubwa ya watoto na hata watu wazima kujieleza kwa ufasaha kwa lugha ya kiingereza na kiswahili mbele za watu tofauti na nchi zingine.

Mmoja wa wazaizi wa watoto hao Hellen Mwenda alisema club kama hiyo inawasaidia sana watoto kuwajengea uwezo wa kujiamini katika masomo yao kutokana na kuchanika na watoto wenzao.

Mwenda alisema pamoja na watoto kujifunza mambo mengine wakiwa shuleni kwao lakini kwa kuwapeleka katika club hizo wanapata vitabu ambavyo wanavikosa katika mashule yao.

Club hiyo ipo Kinondoni jirani na Vijana Social Hall ndani ya Ghorofa kilipo chuo cha Mweni Training College kwa maelekezo zaidi piga simu namba-0754-032589.

(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com

MALUMBANO YAZUKA KUHUSU MAZISHI YA KRISTINA BROWN AKIWA MAHUTUTI


Bobbi Kristina.
WAKATI binti wa mwanamuziki Bobby Brown aitwaye Bobbi Kristina akiwa 'ananusa' kifo, familia yake inajadili mipango ya mazishi yake, ambapo upande wa baba yake unajizatiti kupambana kutokana na vitendo ilivyofanyiwa wakati Whitney Houston (mama yake Bobbi) alipofariki.


Kwa mujibu wa tovuti ya TMZ, familia ya Brown haitaki tena hali hiyo itokee ambapo Brown aliondoka katika mazishi hayo baada ya waangalizi wa usalama kumkataza kukaa na Bobbi wakati wa misa ya kumwombea mama yake.
Bobby ananukuliwa akisema familia ya Houston ilikasirishwa na kitendo chake cha kuja na watu tisa wa familia yake kwenye mazishi hayo.
Habari zilizopo ni kwamba chumba alimolazwa Bobbi katika hospitali akiwa mahututi baada ya kukutwa akiwa ameanguka bafuni, kimewekewa kizuizi na familia ya Houston na kuna namba maalum ya kuingilia ndani ya chumba hicho.
Wanafamilia wengi wa upande wa Brown hawakupewa namba hiyo, jambo ambalo lilisababisha kutoelewana.
"Lolote likitokea kwa Bobbi Kristina, hatutakubali kufanyiwa vitendo kama vile sisi watoto wadogo," alisema mmoja wa wanafamilia ya Brown.

Saturday, February 7, 2015

AMANDA ATUA KATIKA KIPINDI CHA ME & YOU LOVE


Mtangazaji wa Kipindi cha Me & You Love, Shorvieny Mohamed kupitia Global TV Online akiwa katika pozi na mwigizaji mwenye figa ya aina yake Bongo Movie, Tamrina Posh 'Amanda' kabla ya kuanza mahojiano.


Tamrina Posh 'Amanda' akikwa katika pozi wakati wa mahojiano.…


Mtangazaji wa Kipindi cha Me & You Love, Shorvieny Mohamed kupitia Global TV Online akiwa katika pozi na mwigizaji mwenye figa ya aina yake Bongo Movie, Tamrina Posh 'Amanda' kabla ya kuanza mahojiano.


Tamrina Posh 'Amanda' akikwa katika pozi wakati wa mahojiano.




...Akiendelea kupozi

Patrick Buzohela akiwa katika pozi na Amanda.


Mpiga picha za video, Melkiadi Oreje (katikati), Shorvieny Mohamed (kushoto) wakipozi na Amanda.


...Amanda akiwa katika pozi na team ya Global TV online.

KIPINDI kipya kutoka Global TV Online cha Me & You Love kwa mara ya kwanza kitaanza kuonekana hewani kuanzia Alhamisi ya wiki ijayo. Kipindi hicho kinachotangazwa na Shorvieny Mohamed kitakuwa kikiwaunganisha mastaa, watu mashuhuri, wanasiasa na wengine wengi kuongelea uhusiano wa kimapenzi hasa kuelekea kipindi hiki cha Sikukuu ya Wapenda Nao 'Valentine Day'.

Friday, February 6, 2015

ZIMEBAKI SIKU CHACHE FILAMU YA JADA KUWA MITAANI


RAY C AAPA KUMSAIDIA DAZ BABA

Na Hamida Hassan
Staa wa muziki wa kizazi kipya, Rehema Chalamila ‘Ray C’ ameapa kumsaidia mwanamuziki mwenzake David Jacob ‘Daz Baba’ anayedaiwa kujihusisha na utumiaji wa madawa ya kulevya.
Chanzo chetu cha kuaminika kimeeleza kuwa, Ray C amekuwa akiumizwa na hali aliyonayo Daz Baba na amefanya kila awezavyo hadi kuongea naye ili aanze kutumia dozi ya Methadone ambayo wengi huipata katika Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar.

Staa wa muziki wa kizazi kipya, Rehema Chalamila ‘Ray C’.

“Ni kweli hali ya Daz Baba inasikitisha na Ray C huyuhuyu unayemjua kaongea naye na amemshawishi kuanza kutumia dozi,” kilidai chanzo hicho ambacho ni rafiki wa Ray C.
Baada ya kuzipata taarifa hizo, mwandishi wetu alimtafuta Ray C, alipopatikana alikiri kuanza mazungumzo na Daz ila akaomba asizungumzie walipofikia kwa sasa.

TASWIRA ZA VURUGU ZA MASHABIKI WAKATI WA MECHI YA NUSU FAINALI AFCON KATI YA GHANA NA EQUATORIAL GUINEA

MECHI ya pili ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) kati ya Ghana na wenyeji Equatorial Guinea kwenye uwanja wa Malabo jana usiku ilivurugika baada ya mchezo huo kusitishwa kwa zaidi ya dakika 30 kutokana na ghasia za mashabiki.

Mashabiki waliokuwa jukwaani waliwarushia chupa za maji wachezaji waliokuwa uwanjani huku polisi wa kuzuia ghasia sambamba na helikopta iliyokuwa ikiruka juu ya uwanja wakijaribu kuwatuliza mashabiki hao.

Vurugu uwanjani hapo zilikithiri katika kipindi cha pili cha mchezo kati ya Ghana na Equatorial Guinea.

Mpaka vurugu zinatokea uwanjani hapo, Ghana tayari ilikuwa kifua mbele kwa mabao 3-0 ambapo kwa matokeo hayo, Ghana imetinga fainali na itacheza dhidi ya Ivory Coast siku ya Jumapili.

Ushindi huo wa Ghana haukuwafurahisha mashabiki wa wenyeji, ambao walikuwa na matumaini makubwa kuona timu yao ikicheza fainali dhidi ya Ivory Coast.

Ghana ilianza kujipatia mabao yake kupitia kwa Jordan Ayew akifunga katika dakika ya 42 kwa njia ya penalti, Wakaso Mubarak dakika ya 45 na Andre Ayew akitupia la tatu katika dakika ya 75 ya mchezo.

Bao hilo la tatu ndilo lililozidisha fujo uwanjani hapo kwa mashabiki wa Equatorial Guinea kuwarushia chupa za maji wachezaji kiasi cha mpira huo kusimamishwa kwa muda mrefu.

Helkopta ya polisi ikijaribu kutuliza ghasia wakati wa mechi kati ya Ghana na wenyeji Equatorial Guinea jana.

Wachezaji wa Ghana wakitolewa uwanjani chini ya ulinzi mkali baada ya vurugu kutokea.…

Helkopta ya polisi ikijaribu kutuliza ghasia wakati wa mechi kati ya Ghana na wenyeji Equatorial Guinea jana.

Wachezaji wa Ghana wakitolewa uwanjani chini ya ulinzi mkali baada ya vurugu kutokea.

Polisi wakituliza ghasia za mashabiki kwenye Uwanja wa Malabo.

Polisi wakipambana na mashabiki.

Helkopta ikidumisha ulinzi uwanjani.
Chupa za maji zikirushwa uwanjani wakati wa vurugu.

RECHO WA THT ATAJA MALI ALIZOZIMILIKI KUPITIA MUZIKI


Muimbaji wa muziki kutoka THT, Recho ameweka wazi baadhi ya matunda aliyovuna kupitia muziki wake.

Akizungumza jana kwenye kipindi cha Sporah Show, Recho alisema anashukuru Mungu kazi anayofanya tayari imemwezesha kufanya mambo mengi ya muhimu.
“Nina kiwanja kwa kazi yangu mwenyewe, nina usafiri wangu kwa kazi yangu mwenyewe,” alisema. “Wala sijahongwa wala sijatumia pesa ya mtu yoyote ni kazi yangu mwenyew. Yaani nina vitu vingi, nina biashara yangu nafanya ndogo lakini ni ya kwangu mwenyewe na muziki ninaoufanya. Ukifanya muziki kama kazi utakulipa, ukiufanyia masihala basi.”

Wednesday, February 4, 2015

FILAMU YA JADA KUWEPO MITAANI MWEZI HUU WA FEBRUALI 2015

CHEKA ALIVYOHENYESHWA MAHAKAMANI

 Stori: Dustan Shekidele/Risasi Mchanganyiko

BONDIA bingwa wa dunia wa WBF uzani wa Kati, Francis Cheka ambaye juzi alihukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela kwa kosa la kumpiga mtu ngumi, alihenyeshwa kiasi cha kutosha kabla ya kupandishwa kwenye karandinga la Magereza lililompeleka kuanza maisha mapya katika gereza la Manispaa ya mkoa.

Awali, baada ya hukumu hiyo, Cheka alipelekwa katika chumba ambacho mahabusu hukaa kusubiri kuondoka na akiwa huko, alionekana akikabidhi baadhi ya vitu alivyokuwa navyo kwa ndugu na jamaa zake.…
 Bondia bingwa wa dunia wa WBF uzani wa Kati, Francis Cheka akiwa chini ya ulinzi mkali.

Wakati akiondolewa kwenda kupanda gari, Cheka alichukua simu yake na kuwapigia baadhi ya marafiki zake kuwajulisha juu ya msala huo, lakini Polisi hawakumruhusu kuendelea na jambo hilo, kwani walimnyang’anya na kumpeleka garini, ambako aliungana na mahabusu pamoja na wafungwa wengine.


Bondia Cheka akinyang'anywa simu asiendelee kuongea na marafiki zake.

Baadhi ya ndugu na jamaa wa Cheka waliokuwepo mahakamani hapo, waliangua kilio baada ya hukumu hiyo, akiwemo mkewe ambaye inasemekana kuwa ni mgonjwa. Mdogo wake naye aliangua kilio kikubwa kiasi cha kusaidiwa na meneja wa bondia huyo.
Cheka akichukuliwa na mahabusu wengine kwenye karandinga kwenda kuswekwa lupango.

Wakizungumzia hukumu hiyo, baadhi ya wakazi wa mjini hapa walisema Cheka aliichukulia kirahisi kesi hiyo na ndiyo maana amehukumiwa, kwani tokea kuanza kwake, hakuwahi kupeleka shahidi na hata siku ya hukumu, alishindwa kutoa utetezi wowote.

LULU AFANYA VIZURI CHUONI ANAKOSOMA

Stori: Chande Abdallah na Mayasa Mariwata/Risasi Mchanganyiko

Kichwa! Staa bei mbaya wa sinema za Kibongo aliyejizatiti katika masomo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ anadaiwa kuwafunika kimasomo wanafunzi wenzake katika Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) kilichopo Magogoni-Posta jijini Dar.
Staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ akipozi.

Akizungumza hivi karibuni chuoni hapo, mmoja wa wanafunzi wanaosoma na mwigizaji huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake alisema Lulu amekuwa akihudhuria vizuri darasani na kufanya vyema kwenye masomo yake mbalimbali zaidi ya wanafunzi wengi anaosoma nao.
“Lulu yupo vizuri sana kimasomo, anawapita hadi wanafunzi wengine. Mahudhurio yake ni mazuri na anafanya mitihani yake na kufaulu.

“Anavaa nguo zinazostahili na hapa chuoni kila mwanafunzi anampenda kwa sababu yupo ‘peace’ ile mbaya,” alisema mnyetishaji huyo na kusisitiza kuwa msanii huyo haishi kama supastaa.

MOTO WAUNGUZA GODORO, UKUTA KWA BELA

Stori: Waandishi wetu/Risasi Mchanganyiko
NYOTA wa filamu na muziki nchini, Isabela Mpanda ambaye ni maarufu kama Bela, hivi karibuni alijikuta katika majonzi baada ya kijana wake wa kiume kuwasha moto na kuunguza godoro na ukuta wa sehemu ya nyumba aliyopanga.
Godoro la Nyota wa filamu na muziki nchini, Isabela Mpanda likiwa limeteketea kwa moto.

Risasi Mchanganyiko lilimkuta msanii huyo akiwa amejiinamia nyumbani kwake muda mfupi baada ya majirani kumsaidia kuzima moto huo.
Ukuta wa nyumba aliyopanga Isabela Mpanda ukiwa umeungua kwa moto.

“Yaani sijui mtoto huyu kwa nini ananirudisha nyuma kwa sasa nina hali ngumu hivi afu ananiunguzia godoro, nitatoa wapi hela ya kununua lingine kwa sasa?” alisikika akilalamika msanii huyo na kuongeza kuwa licha ya kulazimika kununua godoro lingine, pia atatakiwa kutengeneza sehemu ya ukuta ulioungua.

DEMU AMLILIA ZITTO UKUMBINI

Stori: Waandishi Wetu/Risasi Mchanganyiko
HISIA! Mrembo mmoja ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja, ameshindwa kuzuia hisia zake na kuamua kumlilia hadharani Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Zuberi Kabwe.
Tukio hilo lilitokea katika ‘viwanja’ vya Escape One, Jumamosi iliyopita katika maadhimisho ya miaka kumi ya Nyumba ya Vipaji Tanzania (THT).
Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Zuberi Kabwe akiwa na wasanii wa THT jukwaani.

Awali, mrembo huyo huku akiwa na kinywaji chake mkononi, alionekana akielekea jukwaani baada ya kusikia msanii Ali Kiba anapanda stejini kupafomu.
“Weweee huu muda wa maangamizi sasa hivi jembe linakuja stejini ngoja nisogee nikampe kampani Mwana-Dare s salaam nampenda sana jamani Ali Kiba,” alisikika mrembo huyo huku sauti yake ikiashiria alikuwa na kilevi mwilini.

Wakati Kiba akiwa jukwaani, alimuita Zitto jukwaani ndipo mwanadada huyo alipomkimbilia mheshimiwa na kutaka kumkumbatia huku akilia na kusema katika wanasiasa ambao anawakubali, Zitto ni namba moja.
“Zitto… mheshimiwa…mbunge huwa nakukubali sana, dah leo nimepata bahati ya kuonana na wewe nataka tupige picha ya pamoja, mimi sijali watu watanijaji vipi ninachotaka hapa ni picha tu, nyie wapiga picha nipigeni basi maana nikiikosa leo ndiyo basi tena sijui nitamuona wapi,” alisikika dada huyo.
Mwanadada mrembo aking'ang'ania kupiga picha na Mh. Zitto Kabwe.

Kutokana na kuendelea kumg’ang’ania mbunge huyo, watu walibaki midomo wazi na kujiuliza kulikoni lakini bahati nzuri Zitto alifanikiwa kumkwepa mrembo huyo, akapanda jukwaani.
Wakati Zitto akiwa jukwaani na Ali Kiba sambamba na wasanii wengine walioimba wimbo wa Leka Dutigite, mrembo huyo alionekana chini ya jukwaa akitafuta namna ya kugusanisha mkono wake na mwanasiasa huyo kipenzi cha vijana lakini hadi dakika za mwisho, hakufanikiwa!