Muimbaji wa muziki kutoka THT, Recho ameweka wazi baadhi ya matunda aliyovuna kupitia muziki wake.
Akizungumza jana kwenye kipindi cha Sporah Show, Recho alisema anashukuru Mungu kazi anayofanya tayari imemwezesha kufanya mambo mengi ya muhimu.
“Nina kiwanja kwa kazi yangu mwenyewe, nina usafiri wangu kwa kazi yangu mwenyewe,” alisema. “Wala sijahongwa wala sijatumia pesa ya mtu yoyote ni kazi yangu mwenyew. Yaani nina vitu vingi, nina biashara yangu nafanya ndogo lakini ni ya kwangu mwenyewe na muziki ninaoufanya. Ukifanya muziki kama kazi utakulipa, ukiufanyia masihala basi.”
No comments:
Post a Comment