MAMBO yanazidi kunoga ndani ya safu hii ya Sindano 5 za moto, kutokana na maombi yenu, leo tumemleta kwenu mwigizaji Jeniffer Kyaka ‘Odama’, tiririka naye:
Staa katika tasnia ya filamu Bongo, Jeniffer Kyaka ‘Odama’.
Paparazi: Mambo vipi Odama! Tuanze moja kwa moja na swali la kwanza, hivi kwa sasa una mpenzi? Mbona hatumjui?
Odama: Mambo poa! Mpenzi ninaye, nampenda muda bado wa kumuanika.
Paparazi: Ulishawahi kuchangia bwana na mwanamke mwingine katika maisha yako?
Odama: Hapana, sina kumbukumbu hiyo.
Paparazi: Hadi leo hii unaweza kukumbuka idadi ya wanaume ambao umewahi kutoka nao kimapenzi?
Odama: Nakumbuka, kama mtu hukumbuki idadi basi lazima utakuwa una kichaa. Nakumbuka kwa sababu idadi ni ndogo, ila hapa sitataja idadi yao.
Paparazi: Hivi baba mtoto wako ni nani hasa au ndiye uliyenaye hadi sasa?
Odama: Hilo liweke kapuni kwa sasa, nitalizungumza ‘next time’.Paparazi: Inasemekana wewe ni miongoni mwa warembo ambao wanaoongoza kwa kutongozwa Bongo Movies, ni kweli?
Odama: Hiyo kawaida kwa mtoto wa kike, nadhani sipo peke yangu.
No comments:
Post a Comment