INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Friday, February 27, 2015

CHID BENZ APATA MAJANGA TENA!

Na Shani Ramadhani/Ijumaa
HUKU kesi yake ya kukamatwa na madawa ya kulevya ikiwa bado inaendelea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar, msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Rashid Makwiro ‘Chid Benz’ amepata majanga tena baada ya juzikati kudaiwa kugonga daladala kwa nyuma wakati ‘akiovateki’ gari aina ya Scania maeneo ya Mabibo Sokoni jijini Dar.

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Rashid Makwiro ‘Chid Benz’.

Chanzo kililitonya Ijumaa kuwa mara baada ya tukio hilo kutokea, Chid aligoma kulipa gharama za matengenezo ya gari hilo hali iliyozua mzozo mkubwa.

“Chid alikuwa mtata sana kukubali kosa, mzozo ukawa mkubwa, watu wakajaa lakini baadaye wakamalizana na kila mmoja akaendelea na safari zake,” kilidai chanzo hicho kilichoomba hifadhi ya jina lake. Baada ya kuzinyaka habari hizi, paparazi wetu alimtafuta Chid kwa njia ya simu yake ya mkononi, alipopatikana alidai alikuwa katika kikao cha familia hasingeweza kuongelea suala hilo.

No comments:

Post a Comment