ILIPOISHIA
Wiki iliyopita tuliishia pale nilipoeleza kwamba nilishangazwa na kitendo cha kuona wanawake wengi wanavaa nguo nyeusi nchini Angola…ENDELEA
NiLIambiwa waliokuwa wanavaa vile walifiwa na waume zao vitani.
“Mungu wangu mbona wengi!” nilishtuka.Katika kundi la wanawake kumi, saba wote wamefiwa!
Kingine niliona vijana wengi wakiwa wamekatwa ama miguu ama mikono! Kuuliza kisa eti ni vita! Kumbe vijana wakifika miaka 18 ni lazima kwenda vitani, baada ya miaka miwili anarudi kilema (siyo wote wanaorudi vilema).

Utawaonea huruma siku yao ya matibabu, makundi ya vijana kumi hadi
ishirini kila baada ya muda utaona yanapita wote wamekatwa kiungo kimoja
au viwili. Wenye bahati zao wanarudi salama na kumshukuru Mungu.
Mdogo wangu Tony aliingizwa shule inayoendeshwa na Wafaransa,
Alliance Francaise ndiyo ilikuwa shule pekee inayofundisha Kiingereza.
Kwa hapo haikuwa mbali na nyumbani, mimi nikapatiwa kazi ubalozini ya
usafi ambayo niliifurahia sana, kazi ni kazi nitake kazi ya maana
nimesoma?
Kazi yenyewe hiyo kwanza ilikuwa kama hisani toka kwa mheshimiwa Balozi, ama sivyo angeuchuna tu.
Cherrie akabaki nyumbani na mama akimfanyia fujo. Neno la kwanza la Kireno kujifunza likawa ni embaixada, nilihisia tu hata kabla sijauliza kuwa maana yake ni embassy kwa maana ya ubalozi, nikaambiwa sawa nimepatia.

Likaja la pili, bondia nikataka kujibu mimi siyo Mohamed Ally lakini
ukiwa nchi ya watu usijifanye kimbelembele kujibu vitu maana kila eneo
lina namna yake ya kuzungumza, mfano umetoka juani na kiu imekushika
ukafika kwa Muangola anaweza akakuuliza akupe sumu?
Kibongo lazima utakataa hakuna mtu anayependa kufa siyo? Lakini kiukweli utashangaa sana ukiona wenzako wanapewa kinywaji na wewe mate yanakutoka kwa kunyimwa, kumbe sumu kwa Kireno ni juisi!
Kibongo lazima utakataa hakuna mtu anayependa kufa siyo? Lakini kiukweli utashangaa sana ukiona wenzako wanapewa kinywaji na wewe mate yanakutoka kwa kunyimwa, kumbe sumu kwa Kireno ni juisi!
Meza ni meza. Kinyentu (nimeandika kwa Kiswahili) ni sh. mia tano
wakati huku masela wanasema nyentu ni mia. Barida kule inatamkwa bariga
maana yake tumbo. Fala si kwamba anakudharau ila maana yake sema! Huku
kona ni kona kule ni neno lisiloweza kutamkika hadharani.
Shega kule maana yake inatosha, kuna maneno mengine yanafanana na
Kiingereza hivyo unaweza kuhisi ni neno fulani ila hili la bondia
ilibidi niwe mpole kuuliza maana yake ni nini? Kumbe Habari ya asubuhi!
Upo hapo?
Kwa vile nilikuwa nikifanya kazi na pia kuna wafanyakazi wengine kama
vile dereva Sumai, baba mtu mzima mwenye asili ya Kongo lakini kalowea
Angola, nilifahamu Kireno haraka.
Kitu cha kuchekesha wananchi wa kule siyo wengi wanaofahamu
Kiingereza ila usiwatete kwa Kiswahili, tulipoligundua hilo tukawa
tunaogopa kuongea hata Kiswahili njiani maana ghafla anaibuka mtu
akikusapoti unachoongea na kukwambia alikulia Morogoro au Dar, sasa ole
wako uwe umemteta!
Kutokana na cheo cha baba, alikuwa akipokea vijana wageni waliojitosa kwenye kazi ya ubaharia.
Kutokana na cheo cha baba, alikuwa akipokea vijana wageni waliojitosa kwenye kazi ya ubaharia.
No comments:
Post a Comment