Mwanamuziki Dully Sykes akihojiwa na wanahabari (hawapo pichani) huko msibani Kawe Beach jijini Dar.
Dully akilia kwa simanzi wakati akipewa pole na waombolezaji waliofika msibani Mbezi Beach, Dar leo mchana.
Dully akipewa pole na baadhi ya waombolezaji waliofika msibani leo.
Ebby Sykes enzi za uhai wake.
MAZISHI ya mwanamuziki mkongwe nchini ambaye ni baba mzazi wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Dully Sykes, Ebby Sykes yatafanyika leo saa 10 jioni katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
Mzee Sykes alifariki dunia jana mchana akiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa vidonda miguuni vilivyopelekea kueneza sumu katika mwili wake na kumsababishia mauti.
Kwa mujibu wa Dully, Mzee Sykes alikuwa akisumbuliwa na vidonda hivyo vilivyoshindwa kupona kutokana na kuvuta sigara. Lakini mbali na hilo hakuwa na tatizo lingine lolote.
Mzee Sykes amefariki akiwa na umri wa miaka 62 alizaliwa Februari 24, 1952. MWENYEZI MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MZEE SYKES MAHALI PEMA PEPONI.
No comments:
Post a Comment