INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Wednesday, May 28, 2014

MAPICHA:MWILI WA MSANII RECHO KUSAFIRISHWA KWAO SONGEA KWA MAZISHI

MASTAA wa Bongo Muvi wamemlilia msanii mwenzao, Rachel Haule 'Recho' aliyefariki jana saa mbili usiku katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar baada ya kujifungua ambapo mtoto wake alifariki muda mfupi na baadaye yeye akafariki.

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa Bongo Muvi, Steve ‘Nyerere’, mwili wa Rachel utasafirishwa kwenda kwao Songea kwa ajili ya maziko. Habari nyingine za msiba zitatolewa wakati wowote na mtandao huu mara tu zinapopatikana.

Mwenyekiti wa Bongo Muvi, Steve Nyerere akilia kwa uchungu.

Huzuni tele ikiwa imetawala wasanii waliokuwa viwanja ya Leaders.

Bi. Mwenda akilia kwa uchungu.

Mume wa Rachel aitwaye Saguda akiwa na majonzi.

Mwigizaji Johari akiwa na huzuni.

Cathy Rupia akiomboleza.

Steve akizungumza na wanachama wa Bongo Muvi, viwanja vya Leaders.

Bongo Muvi wakijadili cha kufanya.

Wasanii wakipanga utaratibu wa msiba wa mwenzao.

Wasanii wa Bongo Muvi wakiwa Muhimbili baada ya kupata habari za kifo cha mwenzao.


Tuesday, May 27, 2014

MWIGIZAJI WA FILAMU RACHEL HAULE AFARIKI DUNIA ASUBUHI YA LEO

Tunasikitika kwa wapenzi wa fiilamu Tanzania na Watanzania wote, leo hii hatunaye tena Rachel Haule. Mwenyekiti wa Filamu Tanzania ametoa taarifa za kifo cha Rachel Haule kwa kupitia chombo cha habari Clouds katika kipindi cha Clouds 360. Wasanii wanakutana Leaders kwa maandalizi ya msiba huu.

Marehemu Rachel Haule


Tuesday, May 20, 2014

ANGALIA PICHA MWILI WA ADAM KUAMBIANA UKITOLEWA MOCHWARI MUHIMBILI



Mwili wa Marehemu Adam Kuambiana ukiwa ndani ya gari la kubebea maiti baada ya kuchukuliwa moshwari Muhimbili, unapelekwa nyumbani kwake, Bunju, Dar ambako utalala huko kabla ya kuagwa Viwanja vya Leaders na kuzikwa Kinondoni, kesho.
Waombolezaji wakiwa wamelifungua gari la kubebea maiti ili kuweka jeneza lenye mwili wa Adamu Kuambiana leo mchana.

Waombolezaji wakilia kwa uchungu, mmoja akiwa amedondoka baada ya mwili wa Kuambiana kuwekwa kwenye gari la kubebea maiti nje ya moshwari Muhimbili Dar.

Msanii wa Filamu Bongo, Dude akihojiwa na Global TV On Line nje ya moshwari, Muhimbili.


Mmoja wa wasanii wa Bongo Muvi akihojiwa na Global TV on line.

Dude(kulia), Johari, (katikati) na msanii mwingine wakiwa nje ya mochwari, Muhimbili wakisubiri mwili wa marehemu Adam Kuambiana kutolewa na kusafirishwa kwenda Bunju, Dar leo mchana.

HIKI NDICHO KILICHOMUUA MSANII WA FILAMU ADAM KUMBIANA

Msemo huu umetimia juzi kufuatia kifo cha ghafla cha mwigizaji na mwongozaji wa filamu za Kibongo, Adam Philip Kuambiana (38) kilichotokea akiwa njiani kukimbizwa kwenye Hospitali ya Mama Ngoma, Mwenge jijini Dar es Salaam baada ya kuugua.


Mwili wa Adam Kuambiana ukipelekwa Hospitali ya Muhimbili. Kuambiana aliugua ghafla kwenye kambi ya kurekodi filamu na wasanii wenzake iliyopo katika Nyumba ya Kulala Wageni ya Silvarado iliyopo Sinza ya Kwaremmy, Dar.

NINI CHANZO CHA KIFO?
Akizungumza na Ijumaa Wikienda Jumamosi iliyopita nje ya Hospitali ya Mama Ngoma, msanii wa Bongo Fleva, Aboubakar Katwila ‘Q-Chillah’ alisema muda mchache kabla ya kufikwa na mauti, Kuambiana alimlalamikia maumivu ya tumbo ambapo Ijumaa iliyopita alisema hali yake si nzuri kwani alikuwa akiendesha damu tupu.



Mmoja wa wasanii aliyekuwa katika harakati za kushuti video na Adam Kuambiana akilia kwa uchungu.

Q-Chillah alisema: “Jana (Ijumaa) jioni Kuambiana na wasanii wenzake walikuwa baa wakinywa pombe hadi usiku mnene lakini bado aliendelea kulalamikia maumivu ya tumbo.
“Wenzake walimuuliza ni kwa nini alikuwa akiendelea kunywa pombe kama anaumwa? Akawaambia wamuache!
“Baada ya kumaliza kunywa kila mmoja alikwenda kulala chumbani kwake huku tukiahidiana kwamba itakapofika saa 3:00 asubuhi tuwe tayari kwa ajili ya kwenda ‘location’.
“Lakini ulipofika muda huo sisi tukiwa tayari kwa safari tulikwenda kugonga mlango wa chumba chake bila mafanikio.


Yobunesh Batuli akiwa na simanzi nzito. “Cha kushangaza, alisikika sauti yake kwa mbali. Kwa bahati nzuri mlango ulikuwa wazi, mmoja akaingia ndani na kumkuta ameanguka chooni na hajiwezi. Neno lake la mwisho alisema kwamba anajisikia kuishiwa nguvu na anaharisha damu.
“Kutokana na hali yake hiyo mbaya tulimbeba na kumlaza kitandani kisha tukatafuta gari na kumkimbiza Hospitali ya Mama Ngoma ambapo daktari alisema kwamba alishafariki dunia muda mrefu.”



Rais wa Bongo Muvi, Steve Nyerere (katikati) na Mtitu wakiwa katika hali ya majonzi.

VIDONDA VYA TUMBO VYATAJWA
Kwa mujibu wa watu wa karibu, Kuambiana kwa muda mrefu amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa vidonda vya tumbo (ulcers). Lakini pia inadaiwa alikuwa akisumbuliwa na kisukari (diabetes).

DAKTARI AELEZEA
Ijumaa Wikienda lilimtafuta daktari mmoja wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (aliomba jina kuhifadhiwa) ili azungumzie kuhusu vidonda vya tumbo, alisema:
“Kwa kawaida, mtu kuharisha damu kwa sababu ya vidonda vya tumbo inawezekana kabisa, hiyo kitaalam inaitwa heamatemesis. Inatokana na perforation ya tumbo yaani kidonda kuwa kikubwa.
“Kwa mtumiaji wa pombe ni kipindi anatakiwa kusimama au kuacha moja kwa moja. Kama hatajali afya yake anaweza kufa ghafla kwani uwezekano wa utumbo kukatika ghafla ni mkubwa.”

ALIJUA KIFO CHAKE
Q-Chilla ambaye ni miongoni wa wasanii wanaocheza filamu hiyo, aliendelea kusema kuwa siku chache kabla ya kifo, Kuambiana alimwambia filamu yake hiyo inayoitwa Jojo ndiyo ya mwisho, hatajishughulisha tena na sanaa na alikuwa na mpango wa kwenda China kupumzika kwa muda mrefu.



Ni simanzi na majonzi. “Nimeumia sana kwani hii filamu ndiyo ilikuwa apate fedha nyingi sana kwa sababu ni ya kwake mwenyewe na ni kali mno, amecheza vizuri akinishirikisha mimi.
“Lakini ndiyo hivyo tena imeishia katikati, sijui ni nani atakayeiendeleza maana mwenyewe katuachia majonzi yasiyoelezeka,”alisema Q-Chillah.

AMEMFUATA MDOGO WAKE
Habari zaidi zinasema kwamba, Kuambiana ameaga dunia hata arobaini ya mdogo wake wa damu, Patrick haijafika. Patrick alifariki dunia mwezi mmoja uliopita.

AKUTANA NA MHARIRI WA GLOBAL
Ijumaa saa 10:00 jioni maeneo ya Sinza Kwaremmy jirani na Silvarado, Kuambiana alikutana na Mhariri Kiongozi wa Magazeti Pendwa ya Global Publishers, Oscar Ndauka.
Mhariri huyo alimuuliza ni kwa nini hawaonani siku hizi, Kuambiana akajibu:
“Nipo Mr Ndauka, nipo bwana. Tutaonana lakini sina hakika sana.” Kuambiana alionekana mwenye afya njema na alimtania mhariri huyo kwa kumwambia: “Naona siku hizi Ndauka unazidi kunenepa tu, mi maisha yananipiga.”



Msanii Sandra akilia kwa uchungu.

STEVE NYERERE, BATULI WALIA SANA
Baada ya taarifa kuenea, wasanii mbalimbali wa filamu walikusanyika katika Hospitali ya Mama Ngoma ambapo Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ na Yobnesh Yusuf ‘Batuli’ walivunja rekodi ya kulia kufuatia kifo hicho.



WADAU WAZUNGUMZIA MTU KUANGUKA CHOONI
Wadau na mashabiki wa filamu waliokuwa eneo hilo walisikika wakisema kwamba wasanii wengi hawana tabia za kucheki afya zao, jambo ambalo linawagharimu kiasi cha kupoteza maisha.
Wengine walisikika wakisema kwamba watu wanaoanguka chooni mara nyingi huwa hawaponi, wakipona huwa wanapooza miili.



Mke wa marehemu Adam Kuambiana, Janeth Rithe ambaye ni Diwani wa Kata ya Kunduchi akifarijiwa.

“Unajua watu wengi wanakosea, pale mtu anapodondoka chooni wanamkimbiza hospitali badala ya kumtibu kienyeji, mtu akianguka chooni tu anatakiwa kupewa ndizi mbivu lakini akipelekwa hospitali lazima afe,” walisikika watu.

HISTORIA YAKE KWA UFUPI
Marehemu Kuambiana alizaliwa mwaka 1976, Ifunda mkoani Iringa. Kabila ni Mmakua wa mkoani Mtwara.
Marehemu Kuambiana anatarajiwa kuzikwa kesho kwenye Makaburi ya Kinondoni jijini Dar.
Mungu ailaze pema peponi roho yake. Amina.

MWILI WA ADAM KUAMBIANA WAHIFADHIWA MUHIMBILI, VILIO VYATAWAL




Mwili wa Marehemu Adam Kuambiana ukiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kuhifadhiwa leo mchana.



Rais wa Bongo Movies, Steve Nyerere akiwa analia nje ya chumba cha maiti Muhimbuli.





Wasanii wakilia kwa uchungu nje ya chumba cha maiti katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili mchana wa leo.

Wednesday, April 16, 2014

GRACE RWEGASHA MWENYE NDOTO ZA KUIGIZA KWA SASA AMETOA ALBAMU YAKE YA MY SAVIOUR GOD

Mwimbaji wa nyimbo za injili Tanzani mwenye ndoto kubwa za kuwa mwigizaji wa filamu Tanzania ambaye kwa sasa anamtumikia Mungu kwa njia ya uimbaji. Amesema anatamani sana kuigiza kwani ana kitu hiki ndani ya moyo wake kwa muda mrefu sana. Yupo tayari kufanya kazi na mtu yeyote yule ili atimize ndoto yake.

Grace akishirikiana na mdogo wake  Joshu Rwegasha wameamua sasa kumuimbia Mungu na kumtukuza ili Mungu mwenyewe ajitwalie utukufu. Waimbaji hawa ni ndugu (ni mtu na mdogo wake). Baada ya Bwana Joshu kuona ana kitu ndani yake cha kumtukuza Mungu aliamua kumjulisha dada yake Grace Christian Rwegasha kwamba anahisi kumuimbia Mungu na wakati umeshafika, Grace alikubaliana na wakaamua kuingi studio na kufanya albamu yao hii ya kwanza.

Grace Christian Rwegasha

Grace anasema kwake ni mara ya kwanza kufanya huduma ya uimbaji ni alipata wakati mgumu sana wa kuamua kuanza kuimba kwani alikuwa hajajipanga kwa kazi hii ya Bwana. Ila alisema hali ya kumuimba alikuwa nayo moyoni tangia muda mrefu sana lakini hakufikiria kwamba atakuja kuingia studio na kufanya kama alivyofanya siku ya leo. Garce alisema katika uimbaji wake anapata ugumu sana kuimba kwa kutumia lugha ya Kiswahili  ila anapoimba kwa lugha ya Kiingereza anajisikia huru zaidi na ukiangalia albamu yao nusu ni nyimbo za Kiswahili na nusu ni nyimbo za Kiingereza.

Grace Christian Rwegasha
Ukisikiliza nyimbo zao hakika utatambua ya kwamba waimbaji hawa wamekuja kufanya mapinduzi ya muziki wa Injili Tanzania, kuna vitu vya kipekee ambavyo huwezi kusikia kwa waimbaji wengine wanavyotumia katika huduma yao  ya uimbaji.

Grace Christian Rwegasha
Joshua (Joshu) ni kijana ambaye amekuwa mtundu sana katika eneo la muziki kwa muda mrefu sana, na sasa yuko Mwanza kimasomo katika chuo cha St. Agastine. Amekuwa akitamani sana muziki na ikafikia kipindi anatengeneza biti za muziki na kuimba. Kuna baadhi ya nyimbo alizoimba katika albamu hii ametengeneza biti yeye mwenyewe. Kwa sasa Joshu yuko Mwanza kimasomo na dada yake Grace yupo hapa Dar es Salaam.

Grace Christian Rwegasha
Waimbaji waliomba sana watu wawapokee kwani ndio wameanza kufanya kazi ya Mungu na pia waliwaomba watu wa media kuonyesha ushirikiano wao katika kupiga nyimbo zao na kufanya mahojiano ili watu waweze kujua ya kwamba kuna kitu kipya Mungu anatumia kwa kazi yake. Pia aliomba ushirikiano na watumishi wa Mungu katika huduma zao na matamsha yao kuwashirikisha

Rumafrica iko katika maandalizi ya kutengeneza DVD yao ya maohojiano ambayo utasikia katika Youtube, Facebook na katika blogu hii na blogu mbalimbali.

Grace na Joshu wamesema wako tayari kufanya kazi ya Mungu mahali popote na wakati wowote kwani wameojitambua ya kwamba wameitwa na Mungu kufanya kazi  ya Bwana.

Mbali na uimbaji, Rumafrica iliona kuna kitu ambacho watumishi hawa wanacho hasa katika kuhubiri na kutoa ushauri. Utakuja kujua haya utakaposikia mahojiano yetu.

Unaweza kuwasiliana na Grace kwa simu +255 788 443 346 au +255 654 407080

MUNGU AKUBARIKI

Thursday, April 3, 2014

FILAMU YA JICHO LANGU SASA IKO MADUKANI.

Ile siku tuliyokuwa tukisuribi sana sasa imefika, hatimaye filamu ya JICHO LANGU imetoka siku ya leo. Sasa unaweza kujisogeza taratibu madukani kujipatia nakala yako. Usisubiri wenzako waangalie ndipo usimuliwe, wewe unatakiwa kuwa wa kwanza kuwasimulia wenzanko juu ya kile utakachokiona katika filamu hii ambayo Watanzania wengi na wana Afrika Mashariki  wamekuwa wakiisubiri kwa hamu sana.

Kama ulikuwa hujui, filamu hii imetengenezwa na kampuni ya J-FILM 4 LIFE  kwa viwango vya kimataifa, hasa ukiangalia color, sound na wahusika waliocheza katika filamu hii. Ujumbe uliomo hakika unafaa kabisa katika jamii yetu inayotuzunguka. Utaweza kumuona Odama akifanya yake katika filamu pamoja na wasanii wengi maarufu ambao umewasikia. Usipange kuikosa filamu hii maana imefunika mbaya.

FAHAMU HISTORIA FUPI YA WASTARA SAJUKI TOKA ALIPO ANZA KUIGIZA MPAKA SASA


Wastara Sajuki si jina geni kwenye ulimwengu wa bongomovies. Ni mmoja wa wanadada wanofanya vizuri sana kwenye filamu nchini na wenye ushawishi mkubwa sana ndani ya tasnia hii. Ifuatayo ni historia fupi ya mwanadada huyu.

Early life
Wastara Juma Issa alizaliwa Septemba 27, mwaka 1983 huko mkoani Morogoro. Mwaka 1989 akajiunga na Shule ya Msingi Mvomelo ‘A’ na kufanikiwa kumaliza elimu yake ya msingi mwaka 1995. .Mwaka 1996 alijiunga na Sekondari ya Agricalture mkoani humo.

Career
Mwaka 1999 Wastara aliingia rasmi kwenye sanaa ya maigizo na filamu yake ya kwanza kucheza iliitwa Utaishia kunawa akiwa na gwiji wa vichekesho nchini King Majuto.

Mwaka 2004 mpaka 2006 alianza kuonekana kwenye mchezo wa Miale uliokua unarushwa na kituo cha television cha ITV

Akutana na Jennifer Mgendi

Wastara hakudumu sana kwenye kundi hilo, alikutana na kina Jenifa Mgendi ambaye pia walifanikiwa kuigiza naye filamu iliyowashirikisha baadhi ya wasanii wa kitambo akiwamo Dino na wengineo.

Mwaka 2007, Wastara alifanya usahili kwenye filamu ya mdau Ande John iliyofahamika kama Pelemende, akafaulu na kuigiza kwenye filamu hiyo kisha zikafuata filamu nyingine kama Penina kabla ya kutimkia nchini Kongo kufanya biashara.

Akutana na Sajuki

Aliporejea kutoka Kongo, Julai, 2007, Wastara aliitwa na mwigizaji Shija ambaye alimuomba aigize naye filamu baada ya kumuona kupitia kazi mbalimbali alizowahi kufanya hapo nyuma.

Huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa Wastara kukutana na Sajuki ambaye sasa ni mumewe wa ndoa kwani Shija alikuwa akifanya kazi zake za uigizaji kwa kupata msaada mkubwa kutoka kwa Sajuki.

Wastara alicheza filamu kadhaa akiwa na Shija pamoja na Sajuki hadi baadaye walipokuja kugundua kuwa matatizo ya uhusiano yaliyowakuta (Sajuki na Wastara) yanafanana kwani kila mmoja wao alitendwa na mpenzi wake ndipo walianzisha uhusiano wa kimapenzi.

“Eeeeh! Kazi na dawa, tuligundua kuwa matatizo yetu yanafanana. Taratibu tukaanza uhusiano ili kufarijiana,” anasema Wastara.

FILAMU WALIZOZALISHA

Wakiwa ndani ya umoja wao, Sajuki na Wastara, walifanikiwa kuporomosha filamu zaidi ya 20 ikiwemo Mboni yangu iliyopata umaharufu mkubwa

APATA AJALI

Wakati harakati za ndoa zikiwa zimepamba moto, mwaka 2009 Wastara alipata ajali ya pikipiki iliyosababisha akatwe mguu.

Wakati huo tayari alikuwa ameshachumbiwa na Sajuki.

Juni mwaka huo huo,

wasanii hao waliopitia changamoto kadhaa za maisha, walifunga ndoa na kuanza rasmi maisha ya mume na mke.

Baada ya hapo, kupitia kampuni yao ya Wa-Jey waliendelea kuzalisha filamu kama Briefcase, The Killers, Seven Days na nyinginezo.

Tarehe 2 mwezi wa kwanza (1) mwaka 2013 Wastara alimpoteza mume wake kipenzi Juma Kilowoko (sajuki) jambo lillilosababisha kupumzika sanaa kwa muda na badae alilejea kwenye tasnia na kutoa filamu ya Shaymaa amabayo ilipata umaharufu mkubwa

Nampaka sasa anaendelea kufanya filamu nchini Tanzania

Thursday, March 27, 2014

HII NDIYO FILAMU YA TANZANIA INAYOSUBIRIWA KWA HAMU KULIKO ZOTE

Filamu mpya ambayo inasubiriwa kwa hamu kubwa kwasasa ni JICHO LANGU toka kampuni ya J-Film 4 Life inayomilikiwa na Odama Jennifer Kyaka. Filamu hiyo inadaiwa ni moto wa kuotea mbali kiasi cha wamachinga kuisubiri kwa hamu kubwa. Odama, Salim Ahmed(Gabo), Thadeo Alexander na Grace Wapunda wameonyesha uwezo mkubwa humo ndani yenye funzo kubwa kwa jamii. JICHO LANGU itaingia sokoni rasmi tarehe 31 mwezi huu wa tatu. usikose kununua nakala yako halisi.

MUONEKANO MPYA WA LULU WAFANANISHWA NA MTUMISHI WA MUNGU

Actress mwenye jina kubwa Elizabeth Michael "Lulu" ameshangaza watu kadhaa wakiwemo mashabiki wake kutokana na muonekano wake mpya katika jarida la Vibe Magazine Tanzania ambalo litatoka muda si mrefu. Lulu anaonekana kama mtumishi wa Mungu wa dini ya kikristu katika picha hiyo huku ikiambatana na maneno" can you judge me".

BONGO MOVIE UNIT YATOA MSAADA KATIKA HOSPITALI YA MWANANYAMALA


Kundi la Bongo Movie Unit ambalo linaundwa na baadhi ya wasanii wa filamu Swahiliwood leo limetoa msaada wa vitu mbalimbali katika hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es salaam. Kundi hilo lilitoa msaada huo kwa ushirikiano wa kampuni ya Mabibo Beer(wauzaji wa vinywaji vya Windhoek na Climax) ambayo inadhamini maadhimisho ya miaka mitatu tangu kuundwa kwa kundi hilo ambalo kwasasa mwenyekiti wake ni Steve Nyerere.








Saturday, March 22, 2014