INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Monday, June 30, 2014

MZEE MASINDE AKILEWESHWA KIMAPENZI NA MFANYAKAZI WAKE OFISNI..WANFANYAKAZI WAMZINGUA

Mzee Masinde anajikuta akiipagawisha na mapenzi ya mfanyakazi wake Taiya Odero (Suzy) ofisini kwake. Amwaga mapesa kibao na kumpa kile atakacho. Wafanyakazi wake wanamzingua, kazi hawapigi wanabaki amjungu na kusemana tu. Suzy anajikuta kutengwa na marafiki zake kama Davina, marehemu Rachel Haule na wengine wengi kutokana na majigambo aliyokuwa nayo na kushaua.

Nisikumalizie uhondo huu, jipatie nakala yako ya INSIDE 10.07.2014

Mzee Masinde

STEVE NYERERE ASIMIKWA UKAMANDA CCM TAWI LA BWAWANI

MWENYEKITI wa Bongo Movie Unity Steven Mangere ‘Steve Nyerere’ jana amesimikwa kama kamanda wa Tawi la Bwawani lilopo katika Kata ya Mwananyamala, hivyo msanii huyo kugeukia masuala ya siasa na kuahidi kuwapigani wasanii na wakazi wa eneo hilo.

Tukio hilo liloongozwa na Paul C. Makonda leo Mbunge wa Bunge maalum la Katiba, moja ya kazi aliyofanya kiongozi hiyo ni kufungua mashina ya wakereketwa (Wajasiliamali) na Kumsimika Kamanda wa Vijana wa Tawi la Bwawani Ndg. STEVEN MANGERE aka Steve Nyerere.

Katika kusherehesha sherehe hizo za Kumsimika kamanda huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bongo Movie Tanzania wasanii mbalimbali wa Bongo fleva na wasanii wa filamu walitoa burudani ya kufa mtu… Hakika sherehe zilifana kupita kiasi.

Baadhi ya wasanii na waigizaji wa filamu waliokuwepo hapo ni Jacob Stephen ‘JB’, Single Mtambalike ‘RICHIE RICHIE, Haji Adam ‘BABA HAJI’, Juma Chikoka ‘CHIKOKA’ Blandina Chagula ‘JOHARI’, KIM, Herieth, SANDRA, Jennifer Kyaka ‘ODAMA’,Rose Ndauka…MSAGASUMUkundi la MAKOMANDOO na wengineo kibao.

“Safari ya mafanikio ya mwaka 2014 tumeshaianza DSM,tutarudisha Majimbo,Kata na hata mitaa ukiwemo mtaa wa Bwawani ambao ulichukuliwa na wapinzani,”anasema Kamanda Steve Nyerere.

Sambamba na Mgeni Rasmi pia kulikuwepo na viongozi mbali mbali wa CCM na UVCCM, ambao ni Mjumbe wa Baraza kuu la UVCCM Taifa, William J. Malecela aka Le Mutuz Baharia,Mjumbe wa NEC Asha Baraka, Katibu wa UVCCM Mkoa DSM Kidando, Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi Mkoa wa DSM Komred Saady Khimji, Katibu wa UVCCM Wilaya ya Kinondoni, Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi Wilaya Kinondoni ndg Omar Omary Bomba, na viongozi mbalimbali wa Kata na Tawi, bila kumsahau Mwanamitindo Maarufu ndani na nje ya Tanzania Asia Idarous naye alikuwepo. PICHA KWA HISANI YA LE MUTUZ.


Steve Nyerere mwenyekiti wa Bongo Movie Unity.


Steve Nyerere akipitia katika matawi ya CCM

Steve Nyerere, Mike Sangu, Le Mutuz

Steve akisimikwa ukamanda na Mh. Paul Makonda

Bi. Mkubwa akifurahia kijana kuwa kamanda na kumtandika na gift ya likanga.



Steve Nyerere akivishwa ukamanda rasmi na Mh. Paul Makonda

Steve Nyerere tayari Kamanda kamili na ngao

TICO WA BONGO MUVI NDANI YA KENYA..ANATISHA

Filamu ya Sio Riziki inatayarishwa na mtayarishaji Sabby Angel inaaminika kuwa ndio itakuwa kazi ya kipekee kulingana na muunganiko uliopo kutoka Kenya na Tanzania, sinema hiyo inarekodiwa na kampuni ya Coastal Film Production ya Kenya.

“Ni kazi ambayo kwangu imekuwa chachu ya mafanikio kuweza kuongoza filamu inayoshirikisha wasanii mastaa wan chi mbili za Afrika Mashariki ni hatua kubwa kwangu, pia nipo na Director msaidizi wangu Hassan Feisal anaheshimika sana Kenya,”anasema Tico.

Mzigo huu wa hatari unawakutanisha mastaa wanaong’ara katika tasnia ya filamu Bongo kama Amri Athuman ‘King Majuto’, Hisani Muya ‘Tino’, Kulwa Kikumba ‘Dude’, Sabby Angel na wasanii wakali kutoka Kenya, tunausubiri mzigo kwa hamu .

Wasanii wa filamu wa Swahiliwood na wasanii wa Kenya

DIRECTOR anayekuja kwa kasi Swahiliwood Timoth Conrad ‘Tico’ yupo nchini Kenya na wasanii nyota wa Bongo wakirekodi filamu kali nay a kusisimua ya SIO RIZIKI akiongea na FC live kutoka Mombasa amesema kuwa wasanii nyota wa Kenya wanashiriki katika filamu hiyo.

Tico akiongoza filamu ya Sio Riziki kwa umakini


mpiga picha


Wasanii wakiwa katika picha ya pamoja
Mwanadada akiwa na Camera onset
Tico akiwa kazini
Tino na Dude wakiwa location
Tino akiwa katika moja ya scene
Tino akirekodi katika moja ya maduka

MZEE MAJUTO AWAALIKA WAOMBOLEZAJI KWENYE MSIBA WAKE

NI Wikiendi nyingine ambayo mapaparazi wetu, Dustan Shekidele ‘Mkude Simba’ Musa Mateja ‘Toz’ na Richard Bukos Mpigapicha Mkuu walijiachia viwanja mbalimbali kuwinda yaliyokuwa yakijiri na kumjuza moja kwa moja mkuu wao, Oscar Ndauka aliyekuwa makao makuu ya gazeti hili yaliyopo Bamaga, Mwenge jijini Dar es Salaam.


Msanii mkongwe na mkali wa maigizo na vichekesho, mzee Majuto (mwenye suti nyeupe) akiwa kwenye picha ya pamoja na mastaa wengine waliotunukiwa tuzo pia.

Akiwa ofisini Mkuu anaangalia saa na kubaini kuwa ni mida ya vijana wake kuwa viwanja hivyo anaamua kumtwangia Musa Mateja aliyekuwa Serena Hoteli ambapo kulikuwa na hafla ya utoaji wa Tuzo za Watu.

Saa 2:52 usiku
Mateja: Haloo ... naam mkuu wangu, nakupata bila mikwaruzo.
Makao Makuu: Haya niambie ushafika Serena kwenye hiyo hafla?
Mateja: Mkuu wangu nimefika hapa muda si mrefu nilipitia nyumbani kwa Aunt Ezekiel kulikuwa na shughuli, Wema Sepetu na mastaa wengine wa kike walikuwa wakimtunza mwenzao beseni baada ya kujifungua salama.

Makao Makuu: Mambo yalikuwaje huko?
Mateja: Mkuu huko ilikuwa ni minyonga tu ya kufa mtu, yaani kama huna simile utapatwa na aibu ya mfadhaiko yaani jinsi Wema anavyonyonga kiuno mmh... Acheni Diamond adate wajameni.
Makao Makuu: Aaa Mateja acha hizo hebu nidokeze na kinachoendelea hapo Serena Hotel?
Mateja: Mkuu huku mambo yameshamiri, namuona Mkurugenzi wa Benchmark Production, Rita Paulsen anaingia ukumbini huku akijiburuza na magongo.

Makao Makuu: Magongo! Amepatwa na swaibu gani tena?
Mateja: Hata mi sijapata uhakika sema kuna jamaa kaninong’oneza kuwa eti naniliu wake kamnaniliu lakini ntakwambia vizuri kesho.

Makao Makuu: Nini kingine kinaendelea hapo?
Mateja: Mkuu Mzee Majuto amepewa tuzo na sasa amefurahi sana na anawaalika watu kwenye msiba wake, anaomba siku akifa watu waje kwa wingi kwenye mazishi yake.
Makao Makuu: Dah! Huyo mzee haishi vituko nani wengine wamepata tuzo?
Mateja: Wengine ni Elizabeth Michael ‘Lulu,’ Salama Jabir, Nasibu Abdul ‘Diamond,’ Salim Kikeke wa BBC Swahili na wengineo.

Makao Makuu: Sawa Mateja angalia matukio kumbuka kupiga picha nitakusaka baadaye.
Saa 5:12 usiku|

NJEMBA YADATISHWA NA VIUNO VYA BIBI BOMBA
Makao Makuu: (Mkuu anamtwangia Bukos)

Bukos: Yaa mkuu wangu, nakupata kijana wako niko kwenye Bar moja inaitwa Madoto huku Mburahati nilikuwa nafuatilia Shindano la Bibi Bomba si unajua leo ilikuwa ndiyo fainali?
Makao Makuu: Nini kinaendelea huko uswazi kwa wanaofuatilia fainali hiyo kwenye runinga?
Bukos : Mkuu kuna muda Five Stars Modern Taarab walikuwa wakirindimisha burudani huyu Bibi Bomba, Ruth Manfred a.k.a Weusi Hawana Kwele, alikata nyonga mpaka akaenda chini kuna mlevi mmoja huku akajifanya eti amezidiwa baada ya kudatishwa na nyonga za bibi huyo kajitapa eti ni lazima atafute namba yake.

Makao Makuu: Dah! Hivi ni wangapi wameingia fainali?
Bukos: Mkuu fainali ya leo waliingia wabibi watano, Mariam Ligaya ‘Mamaa wa Mji Kasoro Bahari’, Anastazia Chambo, Ruth Manfred ‘Weusi Hawana Kwele’, Sofia Shomari na Sulaiya Mohammed ‘Agwe Solowenyo’.

Makao Makuu: Vipi nani kachukua hizo milioni 13 walizotangaziwa?
Bukos: Mkuu mpaka hatua ya mwisho walibaki wawili, Mariam Ligaya wa Moro na Ruth Manfred na Ruth Manfred ndiye kaibuka mshindi hivyo anakabidhiwa milioni 10 na zile milioni 3 ataongezewa milioni 2 na kupewa kiwanja Kigamboni chenye thamani ya shilingi milioni 5.

Saa 6:57 usiku

MOSHI WA GANJA WATIBUA SHOO YA MIAKA 10 YA MKALI WA RHYMES MORO
Makao Makuu: (Mkuu anamtwangia Dustan Shekidele ‘Mkude Simba’) Halooo halooo Mkude Simba...
Shekidele: Nakupata Mkuu.

Makao Makuu: Haya niambie muda huu uko wapi?
Shekidele: Mkuu wangu niko katika Ukumbi wa Terminal Pub hapa Msamvu, Mkali wa Rhymes, Afande Sele na washirika wake wanapiga shoo ya kusherehekea miaka 10 ya kushikilia taji la mkali wa rhymes.
Makao Makuu: Ahaaa... vipi hali ikoje?

Shekidele: Mkuu mpaka mida hii, 20 Percent na Afande Sele mwenyewe wameshakamua tatizo alipotaka kupanda O-Ten ameshindwa kupiga shoo baada ya kuzidiwa na mambo fulani maana kwa muda mrefu nilikuwa nikimuona akipiga maji huku akila kuku moshi.
Makao Makuu: Nini kinaendelea sasa?

Shekidele: Mkuu onesho naona kama limevurugika maana mambo sasa ni vululuvululu, moshi umetawala ukumbini wengine wasiouzoea wanakohoa hovyo hata mimi hivi ninavyoongea nimeshindwa kuvumilia hali ya ndani niko nje ya ukumbi, yaani ukumbini watu macho mekundu kama wamemwagiwa unga wa pilipili.

Makao Makuu: Sawa Mkude Simba ukitoka hapo wapigie wenzako waambie mkapumzike.
Shekidele: Pouwa Mkuu.

Sunday, June 29, 2014

SUZY AKIONYESHA MALAVIDAVI KWA BOSS WAKE NDANI YA FILAMU YA INSIDE


Kaa mkao wa kuvunjika mbavu na kujifunza mengi juu ya vituko vinavyofanyika maofisini. Jipatie nakala yako Julai.10.2014

ESHA BUHETI APANGUA TUHUMA ZA KUBEBWA ZIFF

BAADA ya mwanadafada Esha Buheti kutoka Bongo Movies kunyakua tuzo ya Mwigizaji Bora wa Kike katika Tuzo za Zanzibar Film Festival ‘Ziff’, iliibuka minong’ono kuwa hakustahili lakini mwenyewe ameibuka na kukanusha minong’ono hiyo.

Mkali wa filamu Bongo Esha Buheti
Akizungumza na paparazi wetu akiwa ameshikilia tuzo yake mkononi, Esha alisema hata yeye alikuwa surprised na tuzo hiyo lakini anaamini waandaaji wametumia vigezo vinavyostahili na ndiyo maana akashinda.
Akipangua minong’ono hiyo, Esha alisema kinachowasumbua watu wengi hususan wasanii wenzake ni majungu, hivyo hajali sana maana alijua na kamwe hawezi kutetereka.
“Wamekalia majungu na kutopendana, kiukweli mimi nilikuwa sifahamu kama nimeingia katika kinyang’anyiro hiki ambacho kimenifanya nipate tuzo, siku ya tukio saa tano usiku kuna shabiki wangu akanipigia simu na kunipa hongera nikamuuliza ya nini ndipo aliponijibu kuwa nimefanikiwa kuchukuwa tuzo ya Best Actress katika filamu ya Mimi na Mungu Wangu,” alisema Esha.

Esha Buheti akiwa kwenye pozi.
Mbali na ishu hiyo ya tuzo, Esha amezungumzia mambo mengi yaliyopita na yaliyopo kama ifuatavyo:
Risasi Jumamosi: Niliwahi kusikia kuwa una bifu na Jack Wolper unazungumziaje hili?
Esha Buheti: Ni kweli mimi na Wolper tulikuwa na bifu tena kubwa sana, bifu hilo lilisababishwa na ile kuvuja kwa meseji ambazo zilikuwa zikidaiwa ni za Kajala na CK ambaye alikuwa bwana wa Wema sasa baada ya meseji zile kuvuja, mimi si niliziweka Instagram na kisha kuandika kuwa kama ni kweli Kajala umefanya hivi unatakiwa kumuomba radhi Wema, dah! Wolper akaibuka na kunitolea maneno ya kashfa yenye kejeli, niliumia sana hapo ukawa mwanzo wa bifu letu.
Risasi Jumamosi: Baada ya hapo ikawaje?
Esha Buheti: Nami nikaanza kujibu mashambulizi ndipo Mwenyekiti wa Bongo Movie, Steve Nyerere (Steven Mengere)  alipoingilia kati swala lile na kusema kuwa Wolper amekosea, tukayamaliza.

Thursday, June 26, 2014

JAMANI...!!! FILAMU YA INSIDE YA JENNIFER KYAKA (ODAMA) KUWEPO MTAANI KUANIZI JUNI.07.2014

Sasa ile filamu iliyokuwa ikisubiliwa na Watanzania wengi ya INSIDE kutoka kwa Jennifer Kyaka (Odama) itakuwepo sokoni 10.07.2014. Filamu hii ambayo imechezwa katika  mazingira ya ofisini ikionyesha vituko vinavyofanyika maofisi na wafanyakazi na pia mabosi. Kama kawaida ya kampuni ya J-Film 4 Life ndio iliyohusika katika kutengeneza filamu hii ambayo ukiangalia utavutiwa na kujua mengi kuhusiana na vituko vya vinatokea  maofisini

Ndani ya filamu hii kuna vituko vya ajabu ukisingatia yumo Majuto, Beny, Dullah, marehemu Rachel Haule, Odama na wengine wengi kama unavyoona katika cover. Jipange mtu wangu kujipatia hii nakala ambayo mpya upate kuongeza siku zako za kuishi kwa kicheko.


Thursday, June 19, 2014

KANISA LA NCHI YA AHADI LAWAOMBEA WASANII WA BONGO MOVIE


VIFO mfululizo vya mastaa wa filamu za Kibongo vinaumiza, vinatisha na vinawanyima usingizi wasanii ambapo sasa wameamua kuitikia wito na kuingia kanisani kuombewa, Risasi Mchanganyiko lina mkoba wenye kila kitu.


...Maombi mazito yakifanyika kwa Dotnata kutoka kwa Mchungaji Mbeyela.

Wasanii waliotangulia mbele za haki kwa kufuatana ni Adam Kuambiana, Sheila Leo Haule ‘Recho’, George Otieno ‘Tyson’ na Said Ngamba ‘Mzee Small’.

Misiba hiyo imetokea ikiwa ni baada ya utabiri wa mtabiri maarufu Bongo, Maalim Hassan Hussein Yahya ambaye aliwatabiria vifo wasanii katika kipindi cha mwaka mmoja wa utabiri.


Mwakifwamba akiwa katika maombi

MASTAA KANISANI
Dawati la Risasi Mchanganyiko lilinasa habari kutoka katika chanzo chake, kilichoeleza kuwa Kanisa la Nchi ya Ahadi lilipanga kufanya maombi maalum, Jumapili ya Juni 15, mwaka huu kwa wasanii wa filamu Bongo kwa lengo la kuangamiza roho wa mauti anayekatisha ndoto zao.


Mchungaji Mbeyela akimwekea mkono Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania ‘TAFF’, Simon Mwakifwamba.

Pekupeku za gazeti hili zilionyesha kuwa, uongozi wa kanisa hilo ulisambaza ujumbe kwa wasanii mbalimbali wa filamu Bongo ukiwataka wafike kanisani hapo bila kukosa kwa ajili ya maombi.

“Wametoa tangazo hadi redioni, wamesisitiza wasanii waende kwa wingi ili wakaombewe. Wachungaji wa hilo kanisa wapo kwenye funga na maombi kwa ajili ya mambo mbalimbali yanayohusu nchi ikiwemo misiba ya wasanii wa filamu ambayo inatishia kiukweli,” kilisema chanzo hicho.

MAPAPARAZI KANISANI
Timu ya gazeti hili ikiambatana na wenzao wa Global TV walitinga kanisani hapo Jumapili iliyopita mishale ya saa tano asubuhi ambapo ilikuta kanisa likiwa limefurika waumini na baadhi ya wasanii wa filamu huku wengi wakiwa ni wale wanaochipukia.


...Simon Mwakifwamba na Illuminata Posh ‘Dotnatha’ wakiwa wamezama katika maombi mazito.

MWAKIFWAMBA, DOTNATHA WAWEKEWA MIKONO
Katika hali ya kushangaza sana, mastaa waliohudhuria walikuwa wawili tu; Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania ‘TAFF’, Simon Mwakifwamba na Illuminata Posh ‘Dotnatha’ ambao waliwekewa mikono na wachungaji waliokuwepo kwenye ibada hiyo.

Baadhi ya wachungaji waliowaombea mastaa hao ni Mchungaji Harris Kapiga na Mchungaji Mbeyela ambaye ni mume wa mwimbaji wa muziki wa Injili nchini, Upendo Nkone.

MCHUNGAJI ANENA
Mchungaji Kiongozi wa kanisa hilo, Harris Kapiga akizungumza na waandishi wetu baada ya ibada hiyo ya kuharibu roho wa mauti alisema, wasanii ni nembo ya taifa ndiyo maana wameona ni vyema kupambana na roho wa giza anayesababisha vifo miongoni mwao.


...Maombi ya nguvu yakiporomoshwa na mke wa Mchungaji kiongozi Harris Kapiga.

“Roho wa kifo ni kitu kamili. Anaishi katika ulimwengu wa giza, dawa yake ni maombi tu. Sisi kama kanisa tumeona ni vizuri kumlilia Mungu kwa ajili ya wasanii wetu, kwa maombi tuliyofanya, hakuna msanii mwingine atakayekufa katika kipindi hiki,” alisema Mchungaji Kapiga na kuongeza:

“Hatujali uchache wao, lakini tunaamini kuwa huko walipo watapokea uponyaji. Yaani hata kama kusingekuwepo na msanii yeyote, ibada ingeendelea kama kawaida. Kwa sasa nasema, wasanii wasiwe na wasiwasi juu ya roho wa mauti.”


Simon Mwakifwamba, Bahati Bukuku na Dotnata wakicheza wimbo wa Dunia Haina Huruma ulioimbwa na Bahati Bukuku.

MWAKIFWAMBA ANENA
Rais wa TAFF, Mwakifwamba alipoulizwa kuhusu uchache wa wasanii waliohudhuria ibadani hapo alisema: “Imani imekosekana kwa wasanii, maana kama wangekuwa nayo leo wengefurika hapa, lakini siwezi kuisemea nafsi ya mtu kwa maana kila mtu ana imani yake.
“Mimi nimefarijika sana na nina imani huyu pepo wa vifo anayetuandama hatakuwa na nafasi tena kwetu.”


Mchungaji Harris Kapiga akiongoza ibada ya maombezi Katika Kanisa la Nchi ya Ahadi, jijini Dar es Salaam.

DOTNATHA ACHARUKA
“Mimi nawashangaa wasanii wenzangu kwa kweli, hawana imani na mambo ya kiroho. Kiukweli ushirikika ni tatizo sana kwa wasanii. Leo kama wangekuja tukajumuika pamoja lingekuwa jambo zuri sana.

“Wasanii tupo kwenye hatari kubwa, lakini hii inatokana na wasanii wengi kujikita kwenye mambo ya kishirikina zaidi ya kumwabudu Mungu wa kweli. Nawashauri tumrudieni Mungu tutapona,” alisema Dotnatha.

Baadhi ya waumini wengine waliohudhuria katika ibada hiyo ya maombi.

TURUDI KWA MTABIRI
Hata hivyo, mnajimu maarufu nchini, Maalim Hassan Hussein Yahya hivi karibuni alisisitiza kuwa, vifo kwa wasanii nchini vitaendelea hadi mwaka wa kiutabiri utakapomalizika hapo Aprili, mwakani.

“Huu ni utabiri na kama nilivyosema, utabiri ni mambo ya mahesabu ya kinajimu. Hakuna kitakachobadilika, vifo kwa wasanii, tena siyo Tanzania pekee - duniani vitaendelea hadi mwezi Aprili mwakani,” alisisitiza Maalim Hassan.

MTABIRI MWINGINE
Baada ya kifo cha Mzee Small aliibuka mtabiri mwingine, aliyejitambulisha kuwa ni Nabii wa Kanisa la Ufufuo lililopo Buza, jijini Dar es Salaam, Yaspi Paul Bendera ambaye amekazia kuwa vifo kwa wasanii wa filamu za Kibongo vitaendelea.


...Mchungaji Harris Kapiga (kushoto) akiongoza maombi.

Akizungumza bila hofu, Nabii Bendera alisema: “Watakufa wasanii 20 ndani ya mwezi huu (Juni). Huu si utani, ni maono.”
Bendera aliwataka wasanii wafike kanisani kwake ili awaombee na kuwapaka mafuta matakatifu yatakayowakinga na vifo.


Mwakifwamba na Dotnana wakiwa wamezama katika neno.

TUJIKUMBUSHE
Katika misa ya kumuombea marehemu Tyson iliyofanyika hivi karibuni katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni, Dar, Mchungaji wa Kanisa la Huduma ya Inuka Uangaze, Buldozer Mwamposa aliwaombea wasanii wote akisema kuwa hakuna msanii atakayekufa tena.
Hata hivyo, licha ya kauli hiyo, siku chache baadaye mkongwe kwenye sanaa ya maigizo, marehemu Mzee Small alitangulia mbele za haki.


Mchungaji Mbeyela akizidi kuwaombea wasanii wa Bongo Muvi.

KUTOKA KWA MHARIRI
Sisi kama gazeti, hatuko upande wowote katika utabiri unaotangazwa na wanajimu na viongozi mbalimbali wa dini nchini lakini tupo pamoja na wafiwa katika kipindi hiki kigumu huku tukiamini kuwa kifo ni ahadi kutoka kwa Mungu.

Sunday, June 15, 2014

KWA HERI RAFIKI YANGU RACHEL (SHEILA) HAULE...MUNGU AKIPENDA TUTAONANA KWA MUNGU

Ninaumia sana Rachel, umeniacha mpweke, ulikuwa msaada wangu, mengi ulifanya katika maisha yangu, mambo mengine nilikuwa siyajui lakini rafiki yangu ulinifundisha na kunishauri na yamefanyika baraka kwangu na familia yangu. Rachel nakupenda sana, nimekosa mengi kutoka kwako na sijui lini nitaweza kupata ushauri wako na maneno yako ya faraja ambayo ulikuwa ukiniambia ninapopitia mapito fulani ya kimaisha.

Bye Rachel....!!!!!



SASA GEORGE TYSON AZIKWA KIJIJINI KWAO SIAYA,NCHINI KENYA BAADA YA KUKAA MUDA MREFU BILA KUZIKWA



Hapa ndipo mwili wa Marehemu George Tyson ulipozikwa mapema leo mchana katika kijiji cha Siaya,nchini Kenya.George Tyson ambaye alikuwa ni mmoja wa Waongozaji filamu mahiri hapa nchini Tanzania,alifarika kwa ajali ya gari wakati akitokea mkoani Dodoma kikazi akirejea jijini Dar.Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi.Amin.

Misa ya mwisho ya kumuombea marehemu George Tyson nyumbani kwao mapema leo mchana katika kijiji cha Siaya,nchini Kenya.

Ndugu na jamaa mbalimbali wakitoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa Marehemu George Tysombani kwako,katika kijiji cha Siaya nchini Kenya.

Baadhi ya Ndgu na Jamaa mbalimbali wakiwa kwenye maombolezo ya mwisho ya mazishi ya marehemu George Tyson mapema leo mchana,nyumbani kwao

Misa ya mwisho ya kumuombea marehemu George Tyson nyumbani kwao mapema leo mchana katika kijiji cha Siaya,nchini Kenya.

Mdau Felix akizungumza jambo na kuwashukuru Watanzania wote na wengineo walioshiriki kwa namna moja ama nyingine katika kuhakikisha mpendwa wao,ambaye Mwenyezi Mungu kampenda zaida anaenda kuishi kwenye nyumba yake ya milele.

Watoto wa marehemu George Tyson wakiwa katika picha ya pamoja.

Nyumba ya milele ya marehemu George Tyson kabla ya kulazwa.Picha kwa hisani kubwa ya Mdau William Mtitu kutoka kijiji cha Siaya,nchini Kenya.

Sunday, June 8, 2014

HISTORIA FUPI YA MAISHA YA MAREHEMU MZEE SMALL KABLA YA UMAUTI KUMFIKA LEO



Marehemu Said Ngamba ‘Mzee Small’

Katika historia fupi, Mzee Small alipata elimu ya msingi katika Shule ya Mingumbi huko Kilwa mkoani Pwani. Mbali na kuwa mkongwe, Mzee Small kila ulipobahatika kuzungumza naye alikuwa na kawaida ya kutamba kuwa yeye ndiye msanii wa kwanza kabisa Tanzania Bara kuchekesha runingani.Mzee Small alianza sanaa hiyo yapata miaka 31 iliyopita na alipata kufundishwa na mwigizaji Said Seif ‘Unono’ (ambaye pia kwa sasa ni marehemu).Mbali na kushiriki sanaa katika vikundi mbalimbali, Mzee Small wakati wa uhai wake ametumika katika vikundi vya mashirika kama vile Reli, NASACO na mengine mengi, ambayo kwa sasa hayajihusishi tena na shughuli hizo.Mzee Small alianza kujulikana sana katika fani ya uchekeshaji hasa pale alipoibuka na mchezo uliojulikana kama 50, 50, 100, na ule wa Mjini Shule uliomwelezea mwanamke wa kijijini aliyeolewa mjini.

Mbali na kutamba na michezo hiyo, Mzee Small alikuwa ni mcheshi na mwenye kupenda utani wakati wote, aliibuka na kichekesho kisemacho Nani Mwenye Haki, ambacho baadaye alikiboresha zaidi.

Baadaye aliibuka na kitu kingine kikali kilichokwenda kwa jina la Nani Kama Shule, huku akiwa amewashirikisha wakali wengine kama King Majuto, Kingwendu na wachekeshaji wengine wanaotamba kwa sasa Bongo.

Mzee Small alikuwa ndiye mmiliki wa kundi la sanaa linalojulikana kama Afro-Dance ambalo alilisajili mwaka 1994 kwenye Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) na kutoa ajira kwa vijana wa mitaani.

Pamoja na kuwa na uzoefu wa kisanaa, lakini mkongwe huyo hakuwahi kuwa na mpango wa kujiunga na kundi lingine, ila alichokuwa akifanya ni kurekodi na wasanii wengine alipokuwa akiitwa kwa makubaliano maalum.

Pia mkali huyo wa vichekesho enzi za uzima wake na uhai wake alikuwa akijishikiza katika duka moja Kariakoo la Home Shopping Centre kimatangazo.

Kutokana na vichekesho, Mzee Small huwa anatania kuwa sanaa ilimpa mke wa ndoa katika televisheni ambaye ni Bi Chau huku akianisha kuwa mkewe, Bi Fatuma huwa hana tatizo lolote na Bi Chau kwani anajua kinachoendelea kuwa ni kazi tu.


Mzee Small enzi za uhai wake akiwa na familia yake wakiwemo wajukuu

MATESO YA KIAFYA

Wakati akiendelea na harakati za kisanaa, mwaka juzi Mzee Small aliripotiwa kupatwa na ugonjwa wa kiharusi (stroke) alipokuwa kwenye shughuli za kisanaa Kanda Ziwa.

Ugonjwa huo ulimpa mateso makubwa huku akiwa hana msaada wowote. Wakati akiteseka na kiharusi alipata tatizo linguine kwenye ubongo huku akitakiwa kila mwezi kwenda kliniki kwa ajili ya ‘check- up.

Hakika kila nafsi itaonja mauti na leo Mzee Small ambaye mbali na kuiburudisha alikuwa akitoa mafunzo kwa jamii yetu kupitia kazi zake, leo ameonja mauti na Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema ampunzishe Mkali huyo wa vichekesho mahali pema.