BAADA ya mwanadafada Esha Buheti kutoka Bongo Movies
kunyakua tuzo ya Mwigizaji Bora wa Kike katika Tuzo za Zanzibar Film
Festival ‘Ziff’, iliibuka minong’ono kuwa hakustahili lakini mwenyewe
ameibuka na kukanusha minong’ono hiyo.
Akizungumza na paparazi wetu akiwa ameshikilia tuzo yake mkononi,
Esha alisema hata yeye alikuwa surprised na tuzo hiyo lakini anaamini
waandaaji wametumia vigezo vinavyostahili na ndiyo maana akashinda.
Akipangua minong’ono hiyo, Esha alisema kinachowasumbua watu wengi
hususan wasanii wenzake ni majungu, hivyo hajali sana maana alijua na
kamwe hawezi kutetereka.
“Wamekalia majungu na kutopendana, kiukweli mimi nilikuwa sifahamu
kama nimeingia katika kinyang’anyiro hiki ambacho kimenifanya nipate
tuzo, siku ya tukio saa tano usiku kuna shabiki wangu akanipigia simu na
kunipa hongera nikamuuliza ya nini ndipo aliponijibu kuwa nimefanikiwa
kuchukuwa tuzo ya Best Actress katika filamu ya Mimi na Mungu Wangu,”
alisema Esha.
Mbali na ishu hiyo ya tuzo, Esha amezungumzia mambo mengi yaliyopita na yaliyopo kama ifuatavyo:
Risasi Jumamosi: Niliwahi kusikia kuwa una bifu na Jack Wolper unazungumziaje hili?
Risasi Jumamosi: Niliwahi kusikia kuwa una bifu na Jack Wolper unazungumziaje hili?
Esha Buheti: Ni kweli mimi na Wolper tulikuwa na bifu tena kubwa
sana, bifu hilo lilisababishwa na ile kuvuja kwa meseji ambazo zilikuwa
zikidaiwa ni za Kajala na CK ambaye alikuwa bwana wa Wema sasa baada ya
meseji zile kuvuja, mimi si niliziweka Instagram na kisha kuandika kuwa
kama ni kweli Kajala umefanya hivi unatakiwa kumuomba radhi Wema, dah!
Wolper akaibuka na kunitolea maneno ya kashfa yenye kejeli, niliumia
sana hapo ukawa mwanzo wa bifu letu.
Risasi Jumamosi: Baada ya hapo ikawaje?
Esha Buheti: Nami nikaanza kujibu mashambulizi ndipo Mwenyekiti wa Bongo Movie, Steve Nyerere (Steven Mengere) alipoingilia kati swala lile na kusema kuwa Wolper amekosea, tukayamaliza.
Esha Buheti: Nami nikaanza kujibu mashambulizi ndipo Mwenyekiti wa Bongo Movie, Steve Nyerere (Steven Mengere) alipoingilia kati swala lile na kusema kuwa Wolper amekosea, tukayamaliza.
No comments:
Post a Comment