INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Monday, February 2, 2015

MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI EDSON MWASABWITE ATUMBUIZA KATIKA UZINDUA WA FILAMU YA DINI YA PETER LUSE, MZEE MAGALI

Mwimbaji maarufu sana wa nyimbo za Injili Tanzania aliweza kushusha wingu la uwepo wa Mungu katika zoezi la kuzindua filamu ya dini ambapo WASANII wa filamu nchini, Peter Luse, Mzee Magali na Stanley Msungu walizindua filamu ya dini inayotambulika kwa jina la Behind The Pastors.
Peter Luse, Edson Masabwite na Mzee Magali wakicheza muziki.

Uzinduzi huo ulifanyika katika ukumbi wa Princess Hall, Sinza-Mapambano, jijini Dar, ambapo mtunzi wa filamu hiyo alisema madhumuni ya kuandaa filamu hiyo ni kubainisha changamoto wanazokutana nazo watumishi wa Mungu kama visa, ugomvi wa madhabahuni na ushirikina.

Baadhi ya watu waliohudhuria uzinduzi huo.

Mzee Magali akicheza muziki na mashabiki wake.

Bendi ya muziki wa injili kutoka katika kanisa la Nchi ya Ahadi ikitumbuiza.

Mtunzi wa filamu ya Behind The Pastors, Peter Luse akiongelea changamoto za filamu hiyo.

Stanley Msungu akizundua rasmi filamu kwa waalikwa.

PICHA:MAZISHI YA BABA YAO P QUARE NI SHEREHE KUBWA LAGOS


Acha kabisa! Mazishi ya baba wa mastaa wa muziki wa Nigeria, mapacha Peter na Paul Okoye wanaounda ‘Kruu’ ya P-Square, Moses Okoye aliyefariki dunia Novemba 24, 2014 yamekuwa kama sherehe, Ijumaa Wikienda limedodosa kilichojiri.



Mwili wa baba wa P-Square, marehemu Moses Okoye ukisindikizwa kwenye gari kwa tarumbeta.

Ishu hiyo ilijiri nyumbani kwa mastaa hao eneo la Ifitedunu, Jimbo la Anambra nchini humo Ijumaa iliyopita ikiwa ni siku 65 tangu mzee huyo alipofariki dunia baada ya kufanyiwa oparesheni ya goti alipodondoka kwenye ngazi nyumbani kwake maeneo hayo.

Wakina P-square wakiwa na wake zao katika msiba huo.

Tofauti na ilivyozoeleka kwamba kwenye msiba watu huwa wanalia na kuomboleza, mazishi hayo yaliyohudhuriwa na mastaa kibao nchini humo yalikuwa tofauti kwani watu walikuwa na nyuso za tabasamu huku wakiserebuka na matarumbeta juu.

Ulinzi mkali ukiimarishwa katika msiba huo.

Mbali na kuonekana kuwa kama sherehe, pia mazishi hayo yaliripotiwa kuwa ya gharama zaidi kuanzia jeneza lililobeba mwili wa baba yao, gari ‘spesho’ lililokuwa na jina la Dady badala ya namba za usajili na wahudhuriaji waliopiga sare nyeupe huku wakijifotoa picha wakicheka na kutupia kwenye mitandao ya kijamii.

Mwili wa baba wa P-Square ukiwa kwenye jeneza.

Pia kivutio kikubwa kilikuwa ni wake wa mastaa hao ambao walipewa ulinzi mkali uliowekwa katika mazishi hayo yaliyohudhuriwa kwa mualiko maalum.

Baba wa P-Square (aliyenyosha mikono) enzi za uhai wake.

Cha kushangaza, wakati mwili wa baba yao ukiwa mochwari, jamaa hao walidaiwa kuendelea na ratiba za kimuziki huku wakifanya shoo kama kawa jambo ambalo kwa Bongo haliwezekani.
Kwa sasa mastaa hao hawana mzazi hata mmoja baada ya mama yao naye kufariki dunia mwaka 2012.

MWIGIZAJI WA FILAMU TANZANIA APATA UBALOZI WA KAMPENI YA MEDO

MKALI wa sinema za Kibongo, Wastara Juma amepata shavu la kuwa balozi wa kampeni ya kumsomesha mtoto wa kike ijulikanayo kama Morogoro Education Development Organization (MEDO).Mkali wa sinema za Kibongo, Wastara Juma akisaini mkataba wa kuwa balozi wa kampeni ya MEDO.

Hafla fupi ya kusimikwa ubalozi huo na kusaini mkataba, ilifanyika hivi karibuni katika Ukumbi wa Hoteli ya Tamal, Mwenge jijini Dar ambapo baada ya kusaini, Wastara alianza kazi rasmi ya kuhamasisha watu kuchangia elimu ya mtoto wa kike huku akiongozwa na kauli mbiu ya kampeni hiyo isemayo ‘Sh. 500 yatosha kunipa elimu.’Wastara Juma akipiga picha ya pamoja na wadau wa kampeni hiyo.

Wastara alishukuru kupewa nafasi hiyo akieleza kuwa ni bahati kwake kwani wasanii wapo wengi.
“Ninawashukuru MEDO kwa kunipa nafasi hii, niwaahidi kuwa nitaitendea haki kuhakikisha nahamasisha uchangiaji wa fedha kwa ajili ya elimu ya watoto wa kike,” alisema Wastara.

Sunday, February 1, 2015

MOVI YA JADA ITAKUWA SOKONI



MIAKA 10 YA THT YASHEREHEKEWA KWA MBWEMBWE ZA KILA AINA

NYUMBA ya Vipaji Tanzania (Tanzania House of Talent - THT) jana ilifanya sherehe kubwa ya kutimiza miaka 10 tangu kuanzishwa kwake.

Sherehe hiyo iliyopambwa na shoo kali kutoka kwa wasanii wa THT na wasanii waalikwa, ilifanyika katika Viwanja vya Escape One jijini Dar, na kujaza umati wa mashabiki na wadau wa muziki ambao waliungana na THT katika kusheherekea siku hiyo.


Ben Pol na Jose Mara wakiwa katika picha ya pamoja.


Wadau mbalimbali wakitia saini zao kwenye bango la THT.
Kadja wa THT alikuwepo.

Mwasiti akiwa katika pozi.

Recho akiwa mbele ya kamera.

Mtangazaji wa Star TV, Sauda Mwilima akipozi.
Msanii wa THT, Ditto akipafomu baadhi ya nyimbo zake.
Msanii Peter Msechu akiongoza waimbaji.
Vumilia wa THT akikamua.

Mwasiti akikonga nyoyo za mashabiki kwa sauti yake nyororo.
Barnaba akitumbuiza na Vanessa Mdee.
Mrisho Mpoto ‘Mjomba’ akituma ujumbe wa burudani.
Zao la THT, Grace Matata, akinogesha sherehe hizo.
Msami ‘akiamshaamsha’.
Amin na Peter Msechu wakiwang’arisha nyota mashabiki wao.
Ndege Mnana, Lina, akiimba kwa hisia.
Mmoja wa wadhamini wa sherehe hizo akimkabidhi mwakilishi wa Ruge Mutahaba, zawadi ya picha ya miaka 10 ya THT.
Msanii Ally Kiba akiwapagawisha mashabiki.
Umati wa mashabiki ukifuatilia sherehe hizo.
Christian Bella akiimba kwa hisia za kufa mtu.

JUSTIN TIMBERLAKE ATHIBITISHA MKEWE KUWA MJAMZITO



BAADA ya kuwepo minong'ono ya hapa na pale kuwa mwigizaji Jessica Biel ana ujauzito wa mtoto wa kwanza wa mwanamuziki Justin Timberlake, huku mastaa hao wakikaa kimya, hatimaye staa Justin ameweka bayana kuwa mkewe huyo ni mjamzito.


Timberlake ameweka wazi hayo kwa kutupia picha katika mtandao wa Instagram jana ikiwa ni siku yake ya kuzaliwa akimbusu tumbo mkewe Jessica mwenye mimba na kuandika hivi:

'Namshukuru kila mtu aliyenitakia heri ya kuzaliwa! mwaka huu natarajia kupata zawadi kubwa mno. Nina hamu sana ya kumuona# Mvulana au msichana# Huwezi kujua# Na sisi hatujui pia# Wote tunasubiri kuona'…


BAADA ya kuwepo minong'ono ya hapa na pale kuwa mwigizaji Jessica Biel ana ujauzito wa mtoto wa kwanza wa mwanamuziki Justin Timberlake, huku mastaa hao wakikaa kimya, hatimaye staa Justin ameweka bayana kuwa mkewe huyo ni mjamzito.


Timberlake ameweka wazi hayo kwa kutupia picha katika mtandao wa Instagram jana ikiwa ni siku yake ya kuzaliwa akimbusu tumbo mkewe Jessica mwenye mimba na kuandika hivi:

'Namshukuru kila mtu aliyenitakia heri ya kuzaliwa! mwaka huu natarajia kupata zawadi kubwa mno. Nina hamu sana ya kumuona# Mvulana au msichana# Huwezi kujua# Na sisi hatujui pia# Wote tunasubiri kuona' aliandika Justin.

(Photo Credit: Instagram)

DIAMOND AMJIBU KWA VITENDO EX WA ZARI


Diamond akiwa kwenye baiskeli huku Zari akiwa kwenye BMW X6.


Baadhi ya post za King Lawrence Instagram akimkejeli Diamond.

STAA wa Bongo Fleva Nasibu Abdul ‘Diamond’, ameamua kumjibu kwa vitendo anayedai kuwa aliwahi kuwa mpenzi wa mwandani wake wa sasa, Zarinah Hassani ‘Zari’, King Lawrence ambaye amekuwa akimtupia maneno ya kumtusi na kejeli mitandaoni.

Diamond akipozi na mpenzi wake Zari.

King Lawrence ambaye ni binamu wa aliyekuwa mume wa Zari aliyezaa naye watoto watatu Ivan amekuwa akimnanga Diamond mitandaoni hasa Instagram kama mtu aliyefulia na hana fedha ambapo siku za nyuma aliwahi kuandika post akisema kuwa yuko tayari kumpatia kiasi cha Usd 40,000 sawa na zaidi ya shilingi milioni 71 Diamond aachane na Zari.

Katika kuonyesha kuchoshwa na tabia hizo za King Lawrence, Diamond ameamua kutupia picha yake akiwa amepanda baiskeli huku mpenzi wake Zari akiwa katika mkoko mkali aina ya BMW X6 akimaanisha kumkebehi mtu huyo kuonyesha kuwa hana kitu ila anaomba penzi kwa mtoto mkali aliye kwenye BMW.

DIAMOND, ZARI NDANI YA SONGEA


MFALME wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' tayari yupo katika Mji wa Songea mkoani Ruvuma akiwa na mpenzi wake Zarinah Hassan 'The Boss Lady' tayari kwa ajili ya shoo itakayosindikiza hafla ya Chama cha Mapinduzi (CCM) leo katika Uwanja wa Majimaji.

'AJIOA' BAADA YA KUKOSA MCHUMBA



Yasmin Eleby hakupata mchumba wa kumuoa mtu ambaye alitaka awe mume wake atakapofikisha miaka 40--kwa hivyo akafanya kitendo ambacho kimewashangaza wengi, aliamua kujioa mwenyewe.

Kwa mujibu wa mtandao wa MySanAntonio.com,Eleby aliahidi kwamba ikiwa hatapata mchumba wakati atakapokuwa ametimiza miaka 40, basi atafanya harusi ya mtu mmoja yaani atajioa ili kusherehekea miaka yake 40.

Duru zinasema kuwa mwanamke Eleby alifanya harusi yake mwenyewe katika makavazi ya Houston akiambatana na jamaa na familia yake na wageni wengine waalikwa.
Kwa sherehe hii, dadake Eleby ndiye aliendesha sherehe hio, kwani ni kinyume na sheria kwa mtu kujioa mwenyewe. Harusi ya kawaida ni kati ya watu wawili.

Katika picha za kanisani sherehe ilionekana kuwa ya kawaida bila ya mchumba.
Kulingana na John Guess Jr afisaa mkuu wa makavazi hayo, sherehe hiyo ilionekana kuwa bila tashwishi na kuonekana kama jambo la kawaida kwani makavazi hayo huwakumbatia watu wa jinsia mbali mbali kuendesha harusi zao hapo.

Aliposikia kwamba Eleby, ambaye anaishi na kufanya kazi ugenini alikuwa anapanga kujioa mwenyewe, aliharakisha kwenda katika eneo hilo kujionea mwenyewe.
"Eleby alipofikisha umri wa miaka 40 bila ya kupata mpenzi na mtu mwenye nia ya kumuoa, aliamua angejioa mwenyewe,''alisema Guess Jr ambaye anasema harusi hiyo imewashangaza wengi na kuwa gumzo katika mitandao ya kijamii.

Anasema anakubaliana na Eleby na mtazamo wake wa mapenzi kwamba mtu anaweza kujipenda na kujioa kwa kukosa wa kumuoa kwani cha muhimu ni mtu kujipenda kwanza kabla ya kupendwa.
"watu wengu huolewa bila ya kutafakari mara mbili kuhusu yule anayemuoa, '' Guess Jr alisema.
Anadhani kwamba pindi watu watakapomuona Eleby anavyojishughulikia mwenyewe, huenda akapata ushindani.
"ni mrembo, anafanya kazi kwa bidii na anasifika duniani na pia anaona uamuzi wake umewapa gumzo watu wengi. ''
Credit:bbcswahili.

HISTORIA YA MAISHA YA MH. JANUARI MAKAMBA TOKA ALIPOZALIWA MPAKA SASA



Nilizaliwa tarehe 28 Januari 1974 mjini Singida, kwa Bi. Josephine Joseph na Bwana Yusuf Makamba. Mwaka 1978, nilipelekwa kuishi kijijini kwa bibi mzaa mama Kyaka, Kagera wakati mama ameenda kuendelea na masomo ya uuguzi. Kijijini kwetu ilikuwa umbali mfupi kutoka Mutukula, mpakani mwa Tanzania na Uganda. Idi Amini alipovamia Tanzania mwaka huo, kitongoji chetu kinachoitwa Kituntu, sio Kituntu ya Karagwe unayoijua wewe Padre, karibu na Kyaka nacho kilipigwa mabomu. Mimi na bibi yangu tulikimbia makazi yetu na kuhamia kwenye kambi ya wakimbizi eneo linaloitwa Mwisa. Baba yangu wakati huo alikuwa mstari wa mbele kwenye vita dhidi ya Idi Amin. Tulikaa kambini kwa muda baadaye tukafanyiwa utaratibu wa kuondoka kwenda Biharamulo na mama akaja kutuchukua. Sina kumbukumbu kubwa sana ya kipindi hiki kwa kuwa nilikuwa bado mdogo ila nakumbuka mvua nyingi, milio ya ndege na mabomu.

Nimesoma shule nne za msingi katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu kutokana na wazazi kuhamishwa mara kwa mara katika utumishi wa umma. Lakini pia kuanzia darasa la tatu hadi la tano nilirudishwa tena kijijini, Kituntu Kyaka, kukaa na bibi. Maisha ya kijijini siwezi kuyasahau. Enzi hizo, miaka ya mwanzoni mwa 1980, maisha ya kijijini yalikuwa magumu sana, bidhaa muhimu kama sukari, sabuni, dawa za mswaki, chumvi, na nyinginezo, zilikuwa adimu. Kutoka kitongojini Kituntu hadi shuleni ilikuwa mwendo mrefu na baada ya shule nilikuwa na kazi ya kwenda kuchunga mbuzi wa bibi, na baada ya kuchunga mbuzi kila jioni saa moja ilikuwa ni kazi ya kuchota maji mtoni, na baada ya hapo ilikuwa ni kumsaidia bibi kuuza pombe ya lubisi usiku na Jumamosi ilikuwa ni kwenda shamba kupalilia migomba na mikahawa. Maisha yale yalinifundisha mambo mengi. Baada ya miaka mitatu, nilirudi kukaa na wazazi na kumalizia darasa la saba Shule ya Msingi Masiwani, Tanga Mjini.

Nilianza Sekondari katika shule ya Sekondari Handeni, Tanga. Nakumbuka wakati naanza pale shule ile ilikuwa bado inajengwa, sisi tulikuwa Form 1 wa pili na ilikuwa haina tofauti kabisa na shule ambazo sasa zinaitwa shule za Kata. Kwa kuwa hii ilikuwa shule ya kutwa, mzazi wangu alipohamishwa kikazi kutoka Handeni, nikahamia Shule ya Sekondari Galanos Tanga, ambayo ilikuwa shule ya Serikali ya boarding.

Nilikuwa mwanafunzi mzuri pale Galanos, na, nikiwa kidato cha tatu, nikachaguliwa kuwa Makamu wa Kiranja Mkuu. Nilikuwa nafanya vizuri darasani, nikachagua mchepuo wa sayansi nikiwa na combination ya Chemistry (Kemia), Biology (Baiolojia) na Agriculture (Kilimo) (CBA). Nilipata daraja la kwanza kwenye mtihani wa kanda wa mock wa kidato cha nne, nikiwa na uhakika wa kuendelea na A-Level katika Shule ya Sekondari Kibaha, shule pekee iliyokuwa inafundisha mchepuo wa CBA hapa nchini. Hata hivyo, nilifanyiwa hujuma kubwa kutokana na siasa zinazomhusu Mzee wangu na kufutiwa matokeo ya mtihani wa kidato cha nne.

Sikufa moyo, nilirudia mtihani kama mtahiniwa binafsi na kufaulu na kuweza kusoma A-Level katika Shule ya Sekondari Forest Hill Morogoro na nikapata Daraja la Pili kwenye mtihani wa Kidato cha Sita. Kabla ya kwenda Chuo Kikuu, niliamua kwenda kufanya kazi kwenye makambi ya wakimbizi kutoka Burundi yaliyokuwa wilaya ya Kasulu, Mkoani Kigoma. Niliipenda sana kazi ile ya kuhudumia wakimbizi na kuifanya kwa bidii kubwa. Nilipewa madaraka zaidi hadi kufikia nafasi ya Meneja wa Kambi Msaidizi wa Kambi ya Mtabila 2 iliyokuwa na wakimbizi zaidi la laki moja. Nilibahatika kuwa na wajibu na dhamana kubwa ya kuongoza kambi kubwa na wafanyakazi wengi nikiwa na umri mdogo tu wa miaka 21. Nilikuwa na wafanyakazi wengi, tena wengine watu wazima, waliokuwa wanaripoti kwangu. Nilikuwa na wajibu wa kuhakikisha kwamba wakimbizi laki moja wanapata viwanja vya kuishi, wanapata vifaa muhimu kama mahema, na wanapata chakula. Kazi ile ilibadilisha kabisa mtazamo wangu juu ya maisha. Baada ya kushuhudia adha wanayopata wanadamu wenzetu kutokana na vita hadi kukimbia makazi yao na nchi yao na kuja kukaa maporini kwenye nchi yetu, na baada ya kutafakari kuhusu udhalilishwaji na mateso yanayotokana na ukimbizi, niliamua kuachana na azma ya kusoma sayansi na uchumi na nikaamua kwamba maisha yangu nitayatoa katika kuchukua masomo kuhusu amani, na namna ya kutafuta amani ili nitoe mchango kwenye kuepusha vita na kupatikana kwa amani duniani. Hivyo, nilianza kutafuta vyuo duniani vinavyofundisha masuala ya amani. Nilipata chuo kimoja cha Wakatoliki Marekani, kinachoitwa St. John University. Lakini kilikuwa Chuo aghali kidogo, kwa hiyo nikaanza kusoma masomo ya awali kwenye Chuo kingine kidogo katika jiji la Boston kinachoitwa Quincy College na baadae nikajiunga na St. John University na kupata shahada ya kwanza ya sayansi ya masomo ya amani (Bachelor of Science in Peace Studies). Gharama za masomo zilikuwa kubwa na nilihangaika kufanya kazi mbalimbali, ikiwemo kazi za ulinzi na kuhudumia watu wenye magonjwa ya akili ili kulipia ada ya shule.

Baada ya kumaliza shahada ya kwanza, nilishinda tuzo ya kujiunga na taasisi ya Rais Mstaafu wa Marekani, Jimmy Carter, inayoitwa Carter Presidential Center iliyopo Atlanta hukohuko Marekani. Ilikuwa changamoto kubwa na fursa nzuri kwa sababu vijana wote waliojiunga pale walikuwa ni vijana mahiri sana na wenye uwezo mkubwa. Taasisi ile ilinipeleka nchini Sierra Leone kusimamia uchaguzi mkuu na kutekeleza mradi wa kufufua taasisi za haki zilizoporomoka baada ya vita. Nako pia nilijifunza mengi kuhusu ujenzi wa taifa.

Baada ya hapo nikaamua kuchukua shahada ya pili (Masters degree) kwenye Chuo Kikuu cha George Mason kilichoko Jimbo la Virginia, Marekani. Nilipata wakati mgumu kulipa ada, kiasi cha kukaribia kufukuzwa shule. Niliomba msaada kwa watu mbalimbali akiwemo Rais wa wakati ule Mhe. Benjamin William Mkapa. Bahati nzuri, alikubali kusaidia kwa sharti kwamba nije kutumia utaalamu wangu Serikalini nitakapomaliza masomo. Na ndivyo nilivyofanya. Baada ya masomo hayo, nikajiunga na Wizara ya Mambo ya Nje.

Mwaka 2005 nilifunga ndoa na mchumba wangu wa miaka minne, Ramona Urasa, na nimekuwa na familia yenye furaha sasa mwaka wa kumi. Pale Wizarani, nilipata fursa ya kufanya kazi na Waziri wa Mambo ya Nje wakati huo, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete. Nahisi alipenda kazi zangu na mara alipoamua kuwania nafasi ya Urais akanitaka nichukue likizo isiyo na malipo Serikalini ili niwe msaidizi wake kwenye kampeni zile. Siwezi kusahau maishani mwangu ile fursa kubwa kwani niliweza kuijua kwa kina nchi yangu na watu wake. Na kwa kuwa kampeni zinahusu ahadi za utatuzi wa kero za watu, nilipata fursa ya kujua kero za Watanzania kwenye kila wilaya ya nchi yetu.

Baada ya Rais Kikwete kushinda aliniteua kuwa Msaidizi wake Ikulu, nikiwa na jukumu la kumsaidia kuandika hotuba zake, pamoja na mambo mengine mengi ya uendeshaji wa shughuli zake za kila siku. Kazi ile ilikuwa ngumu kwa sababu inakulazimisha kujifunza na kujua karibu kila kitu ndani ya Serikali na duniani kwa ujumla, na kufanya utafiti karibu kila siku kwa sababu Rais anazungumza kila siku kuhusu mambo mbalimbali na kwa makundi mbalimbali. Pia kazi ile inakupa fursa ya kuhudhuria vikao vya Baraza la Mawaziri kama msikilizaji ambapo pia unajifunza mambo mengi ya uendeshaji wa Serikali, ikiwemo maamuzi muhimu ya kisera na kiutendaji yanavyofanywa. Ni nafasi ya heshima sana na sitamsahau Rais Kikwete kwa kunipa fursa ile.

Baba yangu alikuwa mwanasiasa karibu maisha yake yote lakini sikupata kuwaza kuingia kwenye siasa katika maisha yangu hadi nilipofanya kazi na Rais Kikwete. Baada ya kufanya kazi ile Ikulu kwa miaka mitano, nami nikahamasika na kuamua kushiriki katika uongozi wa umma. Niliamua kwenda kwetu Bumbuli kugombea nafasi ya Ubunge mwaka 2010, nikafanikiwa. Baada ya kuingia Bungeni nikapata nafasi ya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini. Kazi ile tuliifanya vizuri sana na wenzangu kwenye Kamati hasa katika kipindi kile kigumu cha mgao wa umeme na matatizo ya mafuta nchini.

Baada ya kitambo kidogo, nikateuliwa kwenye Sekretarieti ya Chama nikiwa kama Katibu wa NEC wa Siasa na Mambo ya Nje, na nikawa Mjumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM. Nilishika nafasi hizi katika kipindi kigumu sana kisiasa kwa Chama chetu na nilijifunza mambo mengi na kutoa mchango wangu kwenye kukijenga na kukiimarisha. Baada ya kitambo kingine, nikateuliwa kuwa Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia.

Kuhusu kubebwa na jina la mzazi, kama nilivyosema hapo awali, pamoja na kwamba mzazi wangu alikuwa kwenye siasa kwa muda mrefu, binafsi, ingawa nilipenda na nilishiriki kuwa kiongozi tangu shuleni, sikuwa na mawazo ya kuingia katika siasa. Nilipokuwa Sekondari nilipenda kuwa mwanasayansi wa kilimo.

Baada ya kuzunguka nchi nzima kwenye kampeni ya 2005 na baada ya kufanya kazi ya kumsaidia Rais Ikulu ndipo nilipobaini kwamba siasa, ukiiendesha vizuri na kwa manufaa ya watu, inayo nafasi ya kubadilisha maisha ya watu. Nilipofanya uamuzi wa kugombea Ubunge, sikutaka ushauri wa baba yangu kwa sababu nilikuwa na uhakika kwamba angenikatalia. Niliamua mwenyewe na nikaanza harakati na ndipo nikamwambia. Kwa hiyo, unaweza kuwa na mzazi mwanasiasa na bado ukaweza kuwa na uhuru wa kujiamulia mwenyewe unataka kufanya nini.

Ni kweli kwamba jina maarufu la mzazi aliye kwenye siasa linasaidia kwa maana tayari kuna watu ambao wanamheshimu na ambao wapo tayari kukusaidia. Lakini pia jina hilohilo linaweza kukuharibia kwa sababu pia unaweza kurithi maadui zake, ambao wanakuona wewe ni sehemu ya yeye hata kama una mawazo na mtizamo huru. Kwa hiyo, siasa yangu nimejitahidi kuifanya kama mimi binafsi. Mimi na baba yangu tuna staili tofauti za siasa na mimi nina namna yangu ya kufanya mambo ambayo inatofautiana na yake. Lakini pia kuna mambo mengi mazuri ambayo nimejifunza kutoka kwake ikiwemo haja ya kuwa na msimamo usioyumba katika unayoyaamini na haja ya kutokumuogopa mtu yoyote.

PICHA 2 ZA MAJABU:HUU NDIO MUONEKANO MPYA WA MSANII WA KENYA "NAZIZI "



Msanii Nazizi ameshangaza wengi kwa picha aliyoweka instagram saa tano zilizopita iliyoonyesha muonekano wake mpya na jinsi alivyopunguza mwili wake.

ZARI ATIA TIMU DAR NA KUTHIBITISHA KUWA DIAMOND NI MPENZI WAKE



Hii picha ni ya jana ijumaa ila haikueleweka kama walikuwa wametoka msikitini au ni mavazi ya swaggz ila ni katika mitoko yako ya weekend hii usije kushtuka utakapokutana na couple fulani ya ‘Ameizing’ ya TZ+UG, sababu Zari Tlale a.k.a The Boss Lady yupo ndani ya jiji la Dar au kama anavyopaita mrembo huyo D-City.


Kupitia Instagram mrembo huyo wa Uganda ambaye makazi yake yako Afrika Kusini amepost picha kadhaa akiwa na mpenzi wake Diamond Platnumz kwenye Gari aina ya BMW

Licha ya sasa kuwa Diamond na Zari wanajulikana kuwa nai wapenzi lakini wanapoulizwa juu ya Uhusiano wao wamekuwa wakikanusha na kusisitiza kuwa wanaproject ya pamoja.Lakini safari hii amethibitisha mwenyewe kwa kauli yake baada ya kumuita Girlfriend wa dancer wa Diamond 'wifi'