INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Tuesday, March 3, 2015

VIONGOZI, WASANII NA WANANCHI WALIVYOMUAGA KAPTENI KOMBA DAR


Wasanii wa filamu na muziki wa Bongo Fleva wakiimba wimbo maalum wa kumuaga marehemu Komba.
Baadhi ya wasanii walioimba wimbo maalum.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nauye (katikati) akiimba wimbo maalum na wasanii wa muziki wa dansi


Jeneza lenye mwili wa marehemu likiwa viwanja vya Karimajee.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DK. Jakaya Mrisho Kikwete, akiongoza maelfu ya Watanzania kuuaga mwili wa Kapteni John Komba, katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.


Rais Mstaafu wa awamu ya pili wa Tanzania Ali Hassani Mwinyi akipita kando ya jeneza lenye mwili wa John Komba.


Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa akitoa heshima za mwisho.


Spika wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda akiaga.


Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Eduard Lowassa, akipita kando ya jeneza.

Huyu ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulahman Kinana.


Aliyekuwa Katibu Mkuu wa zamani wa CCM. Yusuf Makamba akilia kwa uchungu wakati anakaribia jeneza.


Huyu ni mwanasiasa mkongwe Kingunge Ngombale-Mwiru.


Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Dk. Rejinard Mengi akiaga.

Waziri wa Utalii Razaro Nyalandu akiaga mwili wa marehemu John Komba.

Mkuu wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna wa Polisi, Selemani Kova, akipiga saluti wakati wa kuaga.


Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Fenella Mukangala, akitoa heshima zake za mwisho.


Huyu ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Benard Membe.


Mchungaji Getrud Rwakatale akitoa heshima za mwisho.

Mwenyekiti wa Chama cha TLP Augustine Mrema akipita kando ya jeneza.


Anna Tibaijuka akitoa heshima zake.


Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)akipita kumuaga marehemu Komba.

Huyu ni Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia.

Mbunge wa Urambo Magharibi, Prof. Juma Kapuya, akitoa heshima zake za mwisho.
Mbunge wa Kilosa, Mustapha Mkullo, akitoa heshima zake.

Huyu ni Mbunge wa Nzega, Hamis Kingwangala.

Sehemu ya umati wa waombolezaji.

Mwakilishi wa Kambi ya Upinzani, Joshua Nasari, wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)akiongea jambo.

Spika wa Bunge, Anna Makinda akitoa ujumbe katika msiba huo.

Rais Kikwete (katikati) akiwa na makamu wake Gharib Bilal (kushoto) na Spika Anna Makinda.


Rais Mstaafu Benjamin Mkapa (wa pili kulia) akiwa na mkewe Anna (wa tatu kulia) wakiwasili viwanja vya Karimjee.

Waziri mkuu aliyejiuzulu,Edward Lowassa (kulia)akisalimiana na Mkapa.


Spika wa Bunge, Anna Mkapa (kushoto) akiwa na Mkapa.

Mbunge wa Kinondoni Idd Azzan (kushoto) akiwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe.

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba (kulia) akiwa viwanja vya Karimjee.

Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba (kulia)akisalimiana na mwanasiasa mkongwe, Kingunge Ngombale.

Wake wa marehemu Komba, katikati ni mke mkubwa, Salome, na kulia ni mke mdogo.

Miongoni mwa wanafamilia wa marehemu Komba.

Mwili wa marehemu John Komba ukiingia Karimjee ili kuagwa na wananchi na viongozi leo jijini Dar.

KOMBA ALIAGIZA AZIKWE HIVI

Na Waandishi Wetu/Uwazi
KWELI kila kifo kina sauti yake! Siku tatu zimekatika tangu Mbunge wa Mbinga Magharibi (CCM), John Damian Mtokambali Komba kufariki dunia kwa matatizo ya presha na kisukari, jipya limebainishwa na Gazeti la Uwazi.

Mfano wa kaburi alilolitaka Kapteni Komba.

ILIKUWA MAKABURINI
Jipya hilo ni kuibuliwa kwa mahojiano yaliyowahi kufanywa kati ya marehemu na gazeti ndugu na hili, Amani la Mei 2, 2011 kwenye Makaburi ya Mwananyamala, Kinondoni jijini Dar es Salaam ambapo marehemu alisema akifa angependa azikwe kifahari.

ILICHOAGIZA
Katika mahojiano hayo yaliyofanyika kwenye mazishi ya msanii wa Kundi la Tanzania One Theatre (TOT), Fatuma Ally ‘Fatuma Dogodogo’, marehemu Komba alisema hatafurahi kule aendako endapo atazikwa kwenye kaburi lisilo na hadhi.

Alisema: “Ninaamini kaburi langu likijengwa katika muonekano mzuri itakuwa rahisi hata kwa watu watakaokuwa wanakuja kuniombea kuvutiwa kuliko kunifukia kawaida.“Kwa hiyo nasema siku mimi nikifa naomba kaburi langu lijengwe kwa marumaru na juu liwekewe kioo cha ‘kuslaidi’ ili hata mtu akitaka kuja kufanya ibada ya kuniombea, avute kioo kisha ashuke ngazi hadi kwenye jeneza langu, siyo kama hivi wanavyozikwa wengine.”

KWA MAANA HIYO BASI
Kwa kauli hiyo ya Komba, alimaanisha kaburi lake, licha ya kujengwa kwa marumaru kwa nje na kuwa na kioo cha kuslaidi juu, lakini alipenda kuwe na ngazi za kutoka juu hadi chini ambako kuna jeneza.
Kauli ya Komba iliendelea kumaanisha kwamba, alitaka jeneza lake lisifukiwe kwa juu na zege wala udongo ili iwe rahisi kwa mtu kufika chini kumwombea.

MTOTO WA MAREHEMU AISEMEA FAMILIA
Akizungumza na Uwazi baada ya kuulizwa kuhusu wosia huo wa baba yake, mtoto mmoja wa marehemu aliyesema si msemaji wa familia hiyo alisema kuwa, katika vikao vilivyokaa juzi Jumapili, familia iliamua kwamba itafanya lile linalowezekana katika kuuhifadhi mwili wa baba yake kwenye nyumba yake ya milele.

“Huo wosia unaosema wewe mwandishi sisi hatuujui ila mwili wa baba utahifadhiwa vizuri na kwa hadhi yake kama baba yetu na Mbunge wa Mbinga.
“Pia tutazingatia kuwa, baba alikuwa mtu wa watu achilia mbali wapiga kura wake. Kwa hiyo hatutamwangusha baba yetu katika kuuhifadhi mwili wake,” alisema mtoto huyo.

RATIBA YA MAZISHI
Mwili wa marehemu Komba ulitarajiwa kutolewa Hospitali ya Rufaa Lugalo, Dar na kulazwa nyumbani kwake, Mbezi Tangibovu, juzi ambapo ungelela hapo.Jana, mwili ulitarajiwa kupelekwa kuagwa katika Viwanja vya Karimjee, Dar na baadaye kusafirishwa kwenda Songea ambapo ungeagwa kwenye Uwanja wa Majimaji na baadaye kuelekea Kijiji cha Lituhi, Mbinga, Ruvuma kwa mazishi leo hii (kama watafika mapema).

Marehemu Komba alifariki dunia kwenye Hospitali ya TMJ, Dar baada ya kuzidiwa nyumbani kwake.
Mungu ailaze pema peponi roho ya marehemu. Amina. Habari: Haruni Sanchawa, Chande Abdallah, Denis Mtima na Shani Ramadhani.

SHAMSA: SIJAACHANA NA MUME WANGU

 Na IMELDA MTEMA/Uwazi
MSANII wa filamu anayetamba na Filamu ya Chausiku, Shamsa Ford amewafungukia watu wanaoeneza taarifa kuwa ameachana na mumewe, Dickson Matoke kwamba hakuna kitu kama hicho.

Msanii wa filamu anayetamba na Filamu ya Chausiku, Shamsa Ford.

Akizungumza na Uwazi, Shamsa alisema kuwa hajaachana na mumewe huyo na wote wanaosema hivyo watakuwa wanamtaka.“Bado nipo na mume wangu tena kajaa tele, nashangaa hao wanaosema kuwa tumeachana labda wanamtaka,” alisema Shamsa.

KAJALA KUTOKOMEZA MAUAJI YA ALBINO


Na IMELDA MTEMA/Uwazi

STAA wa filamu Bongo, Kajala Masanja kupitia kampuni yake ya Kay Intertainment, ameamua kuungana na mastaa kibao Bongo katika kutokomeza mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi ‘Albino’ yaliokithiri hivi sasa.


Kajala akiwa na wasanii wenzake.

Akichezesha taya na Uwazi, Kajala na timu yake nzima wameunda kitu kinachoitwa ‘Simama Nami’ ambapo tayari wameshatunga wimbo wa pamoja walioshirikiana na Mwasiti, Shilole, Linah, Keisha, Zamaradi, Kadjanito na wengine wengi. “Kwa kweli mauaji hayo yananiumiza kila kukicha, nilifikiria tutafanya nini hivyo nikaona bora tufanye hii kampeni ambayo naamini mimi na wenzangu tutafanikiwa. Kampeni hii si ya leo tu bali ni endelevu,” alisema Kajala.

Monday, March 2, 2015

ODAMA: SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA MSIBA WA MH. KPATENI JOHN KOMBA

Hakika nimepokea taarifa hizi kwa majonzi makubwa sana kwa kifo cha Mbunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Captain John Komba kilichotokea jioni ya tarehe 28/02/2015. Nimemfahamu Mh. John Komba kwa usanii wake wa uimbaji miaka ya 90 katika kazi zake za usanii. Mh. John Komba amekuwa nuru na kioo kwa wasanii wengine kwa tabia yake nzuri na ucheshi. Hakika sitaweza kumsahau Mh. KapteniJohn Komba kwa umakini katika kazi zake hasa pale alivyoweza kuongoza kwaya, bendi na pia katika uongozi wake kama Mbunge wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania.

Jeniffer Kyaka (Odama)

Mbali na kuwa msanii, pia Mh. Kapteni John Komba aliona haitoshi na ndio maana aliamua kugombea ubunge katika jimbo la Mbiga Magharibi na kushinda kwa kishindo kikubwa. Hii inaonyesha kuwa jamii ilimkubali kutokana na uchapakazi wake na umakini katika kazi zake. Hakika pengo la Marehemu Mh. Kapteni John Komba halitakuja kuzibika kamwe, ameacha majonzi kwa taifa letu la Tanzania.

Ninatoa pole kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Mh. Dr. Jakaya Kikwete, Familia ya Marehemu Mh. Kapteni John Komba, Spika wa Bunge wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Mh. Anne Makinda, wadau wa sanaa Tanzania na kila mtu aliyeguswa na msiba huu. Ninatumaini tutaendelea kuenzi mema yote aliyofanya Marehemu Mh. John Komba hasa kudumisha upendo na amani kwa watu wote. Mungu azidi kututia nguvu katika kipindi hiki cha majonzi na wanafamilia Mungu awape nguvu..Amen

DR. FADHIL EMILY: ACHA KUTESEKA NA MAGONJWA SUGU

Dr. Fadhil Emily wa The Fadhaget Sanitarium Clinic Mbezi Beach, anakupa pole sana kwa magonjwa yanayokutesa kwa muda mrefu, ulikuwa gizani usijue wapi unaweza kupata uponyaji wako. Onana nami niweze kukusaidia na tatizo lako. Chukua uamuzi wa kufika katika kituo chetu au tupigie simu hapo chini nasi tutakusikiliza na kukusaidia. Pole sana kwa kuteseka kwa muda mrefu.

KOLETHA: TUHONGWE KWA MALENGO!

Mayasa Mariwata/ijumaawikienda
MSANII wa sinema za Kibongo, Coletha Raymond ‘Koletha’ amewataka mastaa wa kike kuzitumia vizuri fedha wanazohongwa na vigogo kwa kuwekeza kwenye miradi ili ziwanufaishe.

Msanii wa sinema za Kibongo, Coletha Raymond ‘Koletha’.

Koletha alisema suala la wasanii wengi wa kike kuishi kwa kutegemea wanaume wakware lipo wazi kabisa, isipokuwa wengi wao wanajisahau kwa kuzitumia hovyo kwa starehe badala ya kuwekeza kwenye miradi. “Wasanii wengi wanategemea kuhongwa lakini wawe makini na hao wanaowahonga, kama ni gari wapewe kadi na chochote kile kiwe na uthibitisho ili mwisho wa siku wasiumbuke na kuchekwa lakini cha muhimu zaidi ni kuwekeza kwa maisha ya baadaye maana wengi wanaishia kujivunia nyumba za kifahari za kupanga wakati uwezo wa kujenga upo,” alisema Koletha.

MUME:SIKUBALI NDOA YANGU NA JACK IVUNJIKE!

Mwandishi Wetu/ijumaawikienda
MUME wa mwigizaji Jacqueline Pentezel ‘Jack Chuz’, Gadna Dibibi amefunguka kuwa kamwe hawezi kukubali ndoa yake ivunjike kirahisi, atapambana hadi dakika ya mwisho.Kauli hiyo ya Gadna ameitoa ikiwa ni siku chache tangu vyombo vya habari viripoti kuwa wawili hao waliooana mwaka 2013, wamemwagana na kila mtu anaishi kivyake.


Mwigizaji Jacqueline Pentezel ‘Jack Chuz’, akiwa na mumewe Gadna Dibibi.

“Sijampa talaka Jack hivyo bado ataendelea kuwa mke wangu halali, nitahakikisha hilo linabaki kuwa hivyo. Kama kupishana kauli, tulipishana na ni vitu vya kawaida lakini haiwezi kuwa ndiyo mwisho wa uhusiano wetu labda ningekuwa nimempa talaka,” alisema Gadna.Alipotafutwa Jack ili kusikia kauli yake kuhusu ishu hiyo, alisema: “Sitaki kuzungumzia hilo nipe muda kidogo.”

LADY NAA AANIKA SIRI YA KUMPENDA ZARI



Mtangazaji Lady Naa.

Hamida Hassan/ijumaawikienda
KUMBE! Aliyekuwa shemeji wa Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ wakati ikisemekana anatoka na mtoto wa mbunge, Najma, Mtangazaji Lady Naa ameanika siri juu ya ukaribu wake na mpenzi wa sasa wa Diamond, Zarinah Hassan ‘Zari’ kuwa usitafsiriwe kuwa ni usaliti kwani ndiye anayeshikilia usukani kwa sasa.

Lady Naa ameliambia Ijumaa Wikienda kuwa anampenda Zari na haoni sababu ya kumchukia wakati amekuta uhusiano wa mdogo wake (Najma) na Diamond umeshavunjika. “Namkubali Zari kwa sababu nyingi tu, kwanza amemkuta Diamond hana mwanamke kwani hata kwa Najma alikuwa ameshapita, pia ni mwanamke mwenye akili,” alisema Lady Naa.

YALIYOJIRI JIONI YA JANA MSIBANI KWA KAPTENI KOMBA



Mkurugenzi wa bendi ya African Stars, Asha Baraka, akisaini kitabu cha rambirambi.

Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Edward Lowassa, akisalimiana na Asha Baraka msibani hapo.

Msanii wa maigizo, muziki na mwanaharakati wa Chama Cha Mapinduzi, Ummy Wenceslaus ‘Dokii’, akisaini kitabuni.

(Habari/Picha: Chande Abdallah/GPL)

RAIS KIKWETE AFARIJI FAMILIA YA MAREHEMU KEPTENI JOHN KOMBA SIKU YA JANA



Rais Jakaya Mrisho kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo alipokwenda kutoa pole na kuifariji familia ya Mbunge wa Mbinga Magharibi na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Marehemu Kepteni John Komba aliyefariki dunia jana, nyumbani kwa marehemu Mbezi kwa Komba jijini Dar es salaam leo March 1, 2015.

Rais Jakaya Mrisho kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo alipokwenda yeye na Mama Salma Kikwete kutoa pole na kuifariji familia ya Mbunge wa Mbinga Magharibi na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Marehemu Kepteni John Komba aliyefariki dunia jana nyumbani kwa marehemu Mbezi kwa Komba jijini Dar es salaam leo March 1, 2015.

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo walipokwenda kutoa pole na kuifariji familia ya Mbunge wa Mbinga Magharibi na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Marehemu Kepteni John Komba aliyefariki dunia jana, nyumbani kwa marehemu Mbezi kwa Komba jijini Dar es salaam leo March 1, 2015.

Rais Jakaya Mrisho kikwete na mkewe Mama Salma kikwete wakimfariji familia ya Mbunge wa Mbinga Magharibi na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Marehemu Kepteni John Komba aliyefariki dunia jana, nyumbani kwa marehemu Mbezi kwa Komba jijini Dar es salaam leo March 1, 2015.
Fedrick Sumaye akimpa pole mfiwa mke wa Marehemu bi Salome John Komba.
Mbunge wa Jimbo wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari akiandika katika kitabu cha maombolezo.



Rais Jakaya Mrisho kikwete na mkewe Mama Salma kikwete wakiwafariji wasanii wa Tanzania One Theatre kufuatia kifo cha kiongozi wao, Mbunge wa Mbinga Magharibi na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Marehemu Kepteni John Komba aliyefariki dunia jana, nyumbani kwa marehemu Mbezi kwa Komba jijini Dar es salaam leo March 1, 2015.


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anna Makinda(kushoto)akimpa pole Hadija Kopa msanii wa Taarabu nyumbani kwa kapteni Komba.


Katibu uenezi wa Itikadi chama cha CCM Nape Nauye akiwapa mkono wa pole wasanii wa bendi ya (TOT) ya Marehemu Kapteni John Komba aliyokuwa akiimbia.

Dr. Jakaya Kikwete akiwa msibani kwa Marehemu John Komba-Mbezi Tangi bovu.


Waombolezaji wakiwa msibani.

(Habari/Picha: Dennis Mtima)