Na IMELDA MTEMA/Uwazi
STAA wa filamu Bongo, Kajala Masanja kupitia kampuni yake ya Kay Intertainment, ameamua kuungana na mastaa kibao Bongo katika kutokomeza mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi ‘Albino’ yaliokithiri hivi sasa.
Kajala akiwa na wasanii wenzake.
Akichezesha taya na Uwazi, Kajala na timu yake nzima wameunda kitu kinachoitwa ‘Simama Nami’ ambapo tayari wameshatunga wimbo wa pamoja walioshirikiana na Mwasiti, Shilole, Linah, Keisha, Zamaradi, Kadjanito na wengine wengi. “Kwa kweli mauaji hayo yananiumiza kila kukicha, nilifikiria tutafanya nini hivyo nikaona bora tufanye hii kampeni ambayo naamini mimi na wenzangu tutafanikiwa. Kampeni hii si ya leo tu bali ni endelevu,” alisema Kajala.
No comments:
Post a Comment