INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Thursday, March 5, 2015

KIFO CHA KOMBA MINONG’ONO YAANZA

MWANDISHI WETU/Amani
WAKATI mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Mbinga-Magharibi (CCM), Kapteni John Damiano Komba (61) ukizikwa juzi kijijini Lituhi mkoani Ruvuma, minong’ono kuhusiana na marehemu imezungumzwa na baadhi ya waombolezaji, Amani limeinasa.


Mbunge wa Mbinga-Magharibi (CCM), Kapteni John Damiano Komba enzi za uhai wake.

Komba alifariki dunia alasiri ya Jumamosi iliyopita katika Hospitali ya TMJ jijini Dar es Salaam alikokimbizwa kwa ajili ya matibabu baada ya kuzidiwa na shinikizo la damu nyumbani kwake, Mbezi ya Tangi Bovu, Dar.

MINONG’ONO
Mwandishi wetu aliyekuwa akifuatilia mazishi hayo mwanzo mwisho, alianza kusikia minong’ono mbalimbali kwamba, marehemu alikuwa na wake wawili lakini watu wameshangaa kuona mke mmoja (mkubwa) pekee ndiye aliyepewa kipaumbele.“Jamani mimi nina maswali, pale Dar (Karimjee) mke wa marehemu ni Salome pekee ndiye anayepewa kipaumbele!

“Hata ndege ya kuja Songea, Salome ndiye aliyetajwa kwamba ataingia lakini si nasikia alikuwa na mke mwingine anaitwa Jane? Inakuaje huyu?” alisikika akisema mwombolezaji mmoja wakati msafara wa mwili wa marehemu Komba ukitoka Songea mjini kuelekea Lituhi.

Hata hivyo, mwombolezaji huyo hakupata majibu ya moja kwa moja huku baadhi ya watu wakimwambia akamuulize msemaji wa familia (Ndugu Mwakangale).

IDADI YA WATOTO
Kama hiyo haitoshi, mnong’ono mwingine uliibuliwa na waombolezaji wengine wakitilia shaka idadi ya watoto wa marehemu.Walisema kuwa, wasifu wa marehemu Komba uliposomwa katika Viwanja vya Karimjee, Posta jijini Dar, ulionesha ameacha watoto 11.

“Mimi jamani swali langu ni moja tu! Kwenye wasifu wa marehemu pale Karimjee, walisema ameacha watoto 11, lakini baadhi ya vyombo vya habari, Jumapili ikiwa ni siku moja baada ya kifo viliandika ameacha watoto 10.

“Sasa kumbukumbu yangu inaniambia kwamba, siku f’lani huko nyuma, niliwahi kumuona Komba akihojiwa na Salama Jabir kupitia Kipindi cha Mkasi (cha EATV), aliulizwa kuhusu watoto akasema anao 9 tu. Wanne ni wa mkewe Salome wengine akasema ni mambo ya ujana lakini hakutaja mama zao. Ukweli ni upi sasa?”

Hata hivyo, mwombolezaji aliyesema maneno hayo hakupata majibu ya uhakika, ila mtu mmoja aliyedai anaifahamu vema familia ya Komba alisema: “Mimi ninavyojua alikuwa na mke mwingine anaitwa Jane. Jane ana watoto wawili, Gerard ambaye alikuwa akionekana sana kwenye runinga akizungumzia kifo cha baba yake na Claudia, hao wengine sijui.”

MNONG’ONO WA MSONGO
Ukiachana na mambo ya familia, mnong’ono mwingine uliibuliwa ambapo kuna waombolezaji walikwenda mbali kwa kuamini kuwa, marehemu alifariki dunia kwa sababu ya msongo wa mawazo.
“Mwenzangu mimi nahisi itakuwa kaondoka kwa msongo wa mawazo, si unakumbuka alikuwa na tatizo la mkopo na benki? Ukiachana na hilo pia nasikia ile nyumba yake imeshapigwa mnada,” alisema muombolezaji huyo.

DAKTARI APIGILIA MSUMARI
Daktari mmoja aliyezungumza na Amani kwa sharti la kutotajwa jina lake gazetini, alisema ajuavyo yeye, Komba alifariki dunia kutokana na msongo wa mawazo.“Ni dhahiri kabisa, msongo wa mawazo ndiyo uliomuondoa Komba, inaonekana alikuwa na matatizo ambayo kuyatatua ilikuwa mzigo mkubwa kwake. Ile hali ndiyo ilimfikisha kwenye kupata presha na sukari kupanda. Ni hilo tu, angalieni sana, msiruhusu mawazo yatawale kichwani,” alisema daktari huyo.

MWENYEWE ALIKATAA
Kupitia Gazeti la Uwazi Mizengwe ya Uchaguzi la Februari 23, mwaka huu, Komba aliulizwa na mwanahabari wetu kuhusu kuwa na deni benki na tishio la mali zake kupigwa mnada ambapo alikanusha vikali akisema hadaiwi.

MSIKIE MWENYEWE
“Hakuna kitu kama hicho, aliyetoa taarifa hizo ni muongo, kama mkopo nilichukua muda mrefu sana na mpaka sasa sijaona watu wakija nyumbani kwangu kwa madai kwamba wanataka kupiga mnada nyumba yangu, siyo kweli, kama kuna anayenidai aje,” alisema Komba.

Gazeti hili lilifanya jitihada ya kuzungumza na msemaji wa familia ili kujua anazungumziaje minong’ono hiyo lakini hakupatikana kutokana na mikikimikiki ya mazishi, jitihada zinaendelea.

No comments:

Post a Comment