INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Monday, March 2, 2015

ODAMA: SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA MSIBA WA MH. KPATENI JOHN KOMBA

Hakika nimepokea taarifa hizi kwa majonzi makubwa sana kwa kifo cha Mbunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Captain John Komba kilichotokea jioni ya tarehe 28/02/2015. Nimemfahamu Mh. John Komba kwa usanii wake wa uimbaji miaka ya 90 katika kazi zake za usanii. Mh. John Komba amekuwa nuru na kioo kwa wasanii wengine kwa tabia yake nzuri na ucheshi. Hakika sitaweza kumsahau Mh. KapteniJohn Komba kwa umakini katika kazi zake hasa pale alivyoweza kuongoza kwaya, bendi na pia katika uongozi wake kama Mbunge wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania.

Jeniffer Kyaka (Odama)

Mbali na kuwa msanii, pia Mh. Kapteni John Komba aliona haitoshi na ndio maana aliamua kugombea ubunge katika jimbo la Mbiga Magharibi na kushinda kwa kishindo kikubwa. Hii inaonyesha kuwa jamii ilimkubali kutokana na uchapakazi wake na umakini katika kazi zake. Hakika pengo la Marehemu Mh. Kapteni John Komba halitakuja kuzibika kamwe, ameacha majonzi kwa taifa letu la Tanzania.

Ninatoa pole kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Mh. Dr. Jakaya Kikwete, Familia ya Marehemu Mh. Kapteni John Komba, Spika wa Bunge wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Mh. Anne Makinda, wadau wa sanaa Tanzania na kila mtu aliyeguswa na msiba huu. Ninatumaini tutaendelea kuenzi mema yote aliyofanya Marehemu Mh. John Komba hasa kudumisha upendo na amani kwa watu wote. Mungu azidi kututia nguvu katika kipindi hiki cha majonzi na wanafamilia Mungu awape nguvu..Amen

No comments:

Post a Comment