INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Thursday, March 5, 2015

KIFO CHA MKE WA NOORAH CHAWALIZA WASANII

KIFO cha mke wa msanii wa Chamber Squard, Noorah aitwaye Anna Kingwalu aliyefariki dunia Jumanne ya wiki hii mkoani Morogoro, kimewaliza wasanii wengi katika tasnia ya muziki Bongo.


Msanii wa Chamber Squard, akiwa na marehemu mkewe Anna Kingwalu siku ya harusi yao.

Akizungumza na Centre Spread, kiongozi wa Kundi la Chamber Squard, Dark Master alisema kuwa kwa kipindi kifupi ndani ya mwaka huu kundi lao limepata pigo kubwa ambalo halitasahaulika katika maisha yao.

“Si wana Chamber pekee walioumizwa na msiba huu wa mwenzetu Noorah kumpoteza mkewe bali ni wasanii wote Bongo. Bado tupo katika kipindi hiki kigumu cha majonzi,” alisema Dark Master.

Februari 20, kundi la Chamber Squard liliondokewa na msanii mwenzao, Mez B na kufanya kundi hilo libakiwe na wasanii wawili ambao ni Dark Master na Noorah. Awali walimpoteza mwenzao Ngwear aliyefariki miaka miwili iliyopita nchini Afrika Kusini.

No comments:

Post a Comment