INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Monday, October 7, 2013

UNAMKUMBUKA "KISOSI' ALIYEKUA AKIIGIZA UTEJA AKIWA NA KITALE?? AOLEWA HUKO TEMEKE..!!



Msanii wa maigizo nchini, Bahati Abilah ‘Kisosi’, ambaye mara nyingi anaigiza kama teja la kike wiki iliyopita alifunga ndoa na Muhaji Salim nyumbani kwao Temeke jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wasanii mbalimbali. Akizungumza na paparazi wa Ijumaa huku akiwa mwenye furaha, Kisosi alisema kuwa anamshukuru sana mumewe huyo kumuoa kwani ni wanaume wachache wanaoweza kuzikubali kazi za wapenzi wao hususan za kisanii na kufunganao ndoa. Kisosi aliongeza kuwa, kwa jinsi anavyoigiza kama teja la kike na baadhi ya watu kumchukulia hivyo ingekuwa vigumu kuolewa lakini baada ya mchumba wake kujua ilikuwa kazi kama zingine wamefunga ndoa.

“Unajua watu wengi sana wanajua mimi ni teja kweli la kike kitu ambacho si kweli, hivyo mwanaume anayekuona kupitia michezo yako na akakupenda kutoka moyoni kama ilivyotokea kwangu ndiye mwanaume wa kweli nitadumunaye,” alisema Kisosi.


No comments:

Post a Comment