INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Sunday, July 13, 2014

MAHOJIANO KATI YANGU NA MWANDISHI WA HABARI WA GLOBAL JUU YA UJAUZITO WANGU NA MAENDELEO YA J-FILM 4 LIFE



WIKI
iliyopita tuliyaanza makala haya kwa kujua baadhi ya hatua ambazo mwigizaji, Jenifer Kyaka ‘Odama’ amepitia katika maisha yake.

Jenifer Kyaka ‘Odama’
Tuliona alikotokea, vikundi ambavyo amepitia kabla ya kufanikiwa kufungua kampuni yake ya J Film 4 Life na kuanza kuzalisha sinema zake mwenyewe.
 Leo tunaendelea na hatua nyingine ambazo amepitia katika maisha yake likiwemo suala la mchumba wake wa kwanza walivyokutana:
Mwandishi: Wasomaji wanataka kujua ulikutana wapi na mchumba wako wa kwanza na ikiwezekana umtaje jina.

Odama: Mh! Hilo ni swali gumu lakini pia ni rahisi kwa sababu jibu lake ninalo. Ukweli ni kwamba boyfriend wangu wa kwanza tulikutana maeneo ya Posta jijini Dar lakini jina siwezi kumtaja na sipendi kumuongelea sana sababu ilishakuwa na sasa hivi kila mtu ana maisha yake.
Mwandishi: Siku hizi katika mitandao ya kijamii kuna timu zinazoanzishwa kwa lengo la kumsapoti msanii flani lakini huwa zinageuka kuwa sumu kwa kushambuliana, unazizungumziaje hizi?

Odama: Kwa upande wangu sioni kama kuna tatatizo kukiwa na Timu Odama lakini tatizo linakuja kama zitageuka na kuanza kumshambulia mtu kwa matusi, zikitumika vizuri zina manufaa makubwa.

Mwandishi: Kwenye maisha yako ulishawahi kusemwa vibaya, kutukanwa hadi ukamwaga machozi?

Odama: Aaa kwangu mimi haijawahi kunitokea na haitakaa itokee maana najiamini, siwezi kuyumbishwa na mtu nikalia bila sababu za msingi.

Mwandishi: Kwa nini sanaa ya Bongo inashindwa kupenya katika anga za kimataifa?

Odama: Tatizo ni mfumo wetu, kuanzia namna kazi zinavyoandaliwa hadi kusambazwa. Hakuna mtu wa kusimamia kwa nguvu zote ndiyo maana kila siku tunaendelea kunyonywa tu. Serikali ikilichukulia soko la filamu kama ajira, tunaweza kusonga mbele. Watuwekee utaratibu na sheria ambazo zitaleta fursa ya wasanii kuwa na mitaji mizuri na kuwekeza vifaa vikubwa vya kazi.

Mwandishi: Ulikuwa mjamzito, jamii haikujua hadi ulipokuja kujifungua, sababu hasa ilikuwa ni nini?

Odama: Watu wangu wa karibu walikuwa wanajua, lakini kwenye vyombo vya habari halikuweza kuwafikia kwa haraka labda ndiyo maana wanachi hawakujua lakini watu wote wanaonizunguka walikuwa wanajua. Hakuna sababu yoyote iliyonifanya niwe msiri lakini nahisi ilitokea tu watu wa habari wengi wao walikuwa hawajui kama mimi ni mjamzito.

Mwandishi: Au ulificha kwa sababu ulijifungua kabla ya kufunga ndoa?

Odama: Hapana bwana, mipango ya kuzaa ilikuwepo. Tulijipangia mimi na mwenzangu tukakubaliana tuzae na kisha ndoa itafuata hivyo siyo kwamba ilitokea bahati mbaya.

Mwandishi: Mashabiki wako wanataka kumjua huyo mzazi mwenzako anaitwa nani na pengine mnaishi naye au vipi?

Odama: Hilo ni swali gumu umeniletea. Watamjua muda utakapofika, wasijali, kila kitu kinakwenda na wakati.

Mwandishi: Wewe tunajua unaishi Kinondoni, je mnaishi pamoja na huyo baba mtoto au la!

Odama: Hilo nalo siwezi kulijibu bwana, uliza mengine kama kuhusu hii filamu yangu mpya ya Inside iliyotoka mwezi huu. Nimecheza vizuri kweli na marehemu Recho.
Mwandishi: Turudi kidogo katika kampuni yako, ina jumla ya wafanyakazi wangapi ambao wanategemea mshahara kutokana na mnachozalisha?

Odama: Kampuni yangu ina jumla ya watu kumi na tano ambao wote kwa pamoja tunategemea kile tunachokizalisha, tunalipana na maisha yanaendelea.
Mwandishi: Kipato mnachokipata kinawatosheleza wafanyakazi wote hao, pamoja na wewe mwenyewe kama mkurugenzi?

Odama: Yah! Kinatosha na ndiyo maana unaona tunaendelea mbele vinginevyo usingetuona tumefika idadi hiyo.

Mwandishi: Kama kampuni, mmeshazalisha filamu ngapi sokoni?

Odama: Filamu ni nyingi sana sidhani kama nitazikumbuka zote lakini kuna Un Broken Promise, Life to Life, All About Love, Loreen, Rude, House Made, Chocalate, Which Doctor, Pain Killer, Figo, Jicho Langu, Family War na nyingine nyingi tu.

Mwandishi: Mnatajwa sana katika masuala ya ushirikina ili mng’ae kisanii, kwa nini msimtegemee Mungu?
Usikose makala haya wiki ijayo kwenye gazeti hili hili.

No comments:

Post a Comment