INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Friday, February 20, 2015

MALICK: SIJAONA KAMA ROSE NDAUKA

Imelda Mtema/Ijumaa
MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, Malick Bandawe ambaye sasa anatamba na wimbo wake wa Tucheze amefunguka kwa mara ya kwanza kuwa tangu atengane na mzazi mwenziye, Rose Ndauka bado hajatokea wa kumtetemesha.

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Malick Bandawe.

Akizungumza na Ijumaa juzikati, Malick alisema kuwa huko nyuma alipomuona Rose alimtetemesha na kuamua kuingia mzimamzima mpaka kufikia hatua ya kupata naye mtoto lakini mpaka sasa hajatokea kama yeye.

Rose Ndauka. “Unajua mambo yanapotokea lazima kukubaliana nayo na huwezi kulazimisha. Tangu uhusiano wetu usambaratike, hajatokea kama Rose,” alisema Malick.

SANDRA: HATA NIKIMFUMANIA SIWEZI KUMUACHA MUME WANGU

Wiki hii kupitia ukurasa huu tunaye mwanadada anayefanya vizuri kwenye ulimwengu wa filamu anayefahamika sana kwa jina la Sandra lakini jina lake halisi ni Salama Salmini.Ni mama wa watoto wawili na anaishi na mume wake. Mwandishi Wetu Mayasa Mariwata hivi karibuni alimbana kwa maswali 10 na bila hiyana alitoa ushirikiano katika kuyajibu, shuka naye…


Mkongwe katika tasnia ya filamu Bongo,Salama Salmini 'Sandra'.

TQ: Ni kitu gani kilichokufanya udumu kwenye ndoa yako mpaka sasa jambo ambalo wasanii wengi linawashinda?Sandra: Unajua mwanamke mjinga anaivunja ndoa yake mwenyewe, mimi siyo mjinga hivyo nailinda kwa kadiri ninavyoweza. Uvumilivu, kupendana kwa dhati na kuheshimiana ndiyo siri kubwa.

TQ: Unapokuwa nyumbani kwako huwa unapendelea kuvaa mavazi ya aina gani, hususan ukiwa chumbani na mumeo?Sandra: Nikiwa nyumbani kwa kuwa naishi na wanangu huwa napenda kujifunga kanga na kuvaa madira lakini nikiwa chumbani, huko ni full kujiachia.

TQ: Inadaiwa wewe ni kati ya mastaa wasiopenda kufanya kazi za nyumbani na mara nyingi unamuachia majukumu hausigeli ikiwemo kumpikia mumeo, hili likoje?
Sandra: Sipendi kabisa mume wangu apikiwe chakula na hausigeli, mimi ni mwanamke ninayejua majukumu yangu, kwa hiyo hausigeli huwa ananisaidia tu.

TQ: Hivi siku ikitokea umemfumania mumeo utafanyaje?
Sandra: Kwa kweli naomba Mungu hilo lisitokee maana sijui maumivu nitakayoyapata, kwanza nitamsamehe sababu nampenda sana mume wangu.
TQ: Umeshawahi kuchepuka? Kuwa mkweli Sandra.

Sandra: Sijawahi kufanya hicho kitu wala sifikirii. Nifuate nini wakati kila kitu nakipata kwa mume wangu jamani? Sina tamaa za kijinga mimi.TQ: Hili la wasanii kuibiana mabwana halikutii hofu?
Sandra: Mimi sihofii hilo kabisa maana najiamini mno, kama mtu ni m****** malaya tu hata umchunge vipi akiwataka atatembea nao.

TQ: Ni sehemu gani ambayo inakupa mzuka zaidi kwenye jumba la mahaba?
Sandra: Ninapokuwa hayo maeneo kila kona ya mwili wangu huwa imejaa msisimko, ila napendelea zaidi ‘romance’.TQ: Siku za wikiendi unapendelea kufanya nini?
Sandra: Napenda kutoka na familia yangu kwenda ufukweni kuogelea na kubadilishana mawazo na mume wangu. TQ: Utapenda watoto wako warithi fani yako ya uigizaji?
Sandra: Sifikirii wanangu waje kuwa wasanii, kikubwa nawaombea mafanikio wawe watu bora zaidi kwenye taifa.TQ: Hivi baada ya kuolewa kwenda viwanja ndo’ basi?
Sandra: Naiheshimu sana ndoa yangu, sioni sababu ya kwenda kukesha klabu, huwa napenda kutulia chumbani na mume wangu na kutazama muvi.

Thursday, February 19, 2015

HATIMAYE FILAMU YA JADA IKO MADUKANI. FILAMU YA KWANZA KUTOKA J-FILM 4 LIFE KWA MWAKA 2015 KUWA SOKONI


SIMULIZI YA NATASHA - 6




ILIPOISHIA
Wiki iliyopita tuliishia pale nilipoeleza kwamba nilishangazwa na kitendo cha kuona wanawake wengi wanavaa nguo nyeusi nchini Angola…ENDELEA
NiLIambiwa waliokuwa wanavaa vile walifiwa na  waume zao vitani.
“Mungu wangu mbona wengi!” nilishtuka.Katika kundi la wanawake kumi, saba wote wamefiwa!
Kingine niliona vijana wengi wakiwa wamekatwa ama miguu ama mikono!  Kuuliza kisa eti ni vita! Kumbe vijana wakifika miaka 18 ni lazima kwenda vitani, baada ya miaka miwili anarudi kilema (siyo wote wanaorudi vilema).
Utawaonea huruma siku yao ya matibabu, makundi ya vijana kumi hadi ishirini kila baada ya muda utaona yanapita wote wamekatwa kiungo kimoja au viwili. Wenye bahati zao wanarudi salama na kumshukuru Mungu.
Mdogo wangu Tony aliingizwa shule inayoendeshwa na Wafaransa, Alliance Francaise ndiyo ilikuwa shule pekee inayofundisha Kiingereza. Kwa hapo haikuwa mbali na nyumbani, mimi nikapatiwa kazi ubalozini ya usafi ambayo niliifurahia sana, kazi ni kazi nitake kazi ya maana nimesoma?
Kazi yenyewe hiyo kwanza ilikuwa kama hisani toka kwa mheshimiwa Balozi, ama sivyo angeuchuna tu.
Cherrie akabaki nyumbani na mama akimfanyia fujo. Neno la kwanza la Kireno kujifunza likawa ni embaixada, nilihisia tu hata kabla sijauliza kuwa maana yake ni embassy kwa maana ya ubalozi, nikaambiwa sawa nimepatia.
Likaja la pili, bondia nikataka kujibu mimi siyo Mohamed Ally lakini ukiwa nchi ya watu usijifanye kimbelembele kujibu vitu maana kila eneo lina namna yake ya kuzungumza, mfano umetoka juani na kiu imekushika ukafika kwa Muangola anaweza akakuuliza akupe sumu?

Kibongo lazima utakataa hakuna mtu anayependa kufa siyo? Lakini kiukweli utashangaa sana ukiona wenzako wanapewa kinywaji na wewe mate yanakutoka kwa kunyimwa, kumbe sumu kwa Kireno ni juisi!
Meza ni meza. Kinyentu (nimeandika kwa Kiswahili) ni sh. mia tano wakati huku masela wanasema nyentu ni mia. Barida kule inatamkwa bariga maana yake tumbo. Fala si kwamba anakudharau ila maana yake sema! Huku kona ni kona kule ni neno lisiloweza kutamkika hadharani.
Shega kule maana yake inatosha, kuna maneno mengine yanafanana na Kiingereza hivyo unaweza kuhisi ni neno fulani ila hili la bondia ilibidi niwe mpole kuuliza maana yake ni nini? Kumbe Habari ya asubuhi! Upo hapo?
Kwa vile nilikuwa nikifanya kazi na pia kuna wafanyakazi wengine kama vile dereva Sumai, baba mtu mzima mwenye asili ya Kongo lakini kalowea Angola, nilifahamu Kireno haraka.
Kitu cha kuchekesha wananchi wa kule siyo wengi wanaofahamu Kiingereza ila usiwatete kwa Kiswahili, tulipoligundua hilo tukawa tunaogopa kuongea hata Kiswahili njiani maana ghafla anaibuka mtu akikusapoti unachoongea na kukwambia alikulia Morogoro au Dar, sasa ole wako uwe umemteta!
Kutokana na cheo cha baba, alikuwa akipokea vijana wageni waliojitosa kwenye kazi ya ubaharia.

FILAMU YA JADA IMETOKA LEO JIPATIE NAKALA YAKO SASA


MASTAA WAMCHANA DIAMOND

STORI: Mwandishi Wetu/Amani

IMEKULA kwake! Wasanii wa sinema na Bongo Fleva wamemchana vibaya staa wa muziki wa kizazi kipya, Nasibu Abdul ‘Diamond’ kwamba si mtokaji kwenye misiba ya wenzake.

Staa wa muziki wa kizazi kipya, Nasibu Abdul ‘Diamond’.

Wakizungumza na Amani kwenye maziko ya baba mzazi wa Mbongo Fleva, Abdul Sykes ‘Dully Sykes’, Ebby Sykes, Jumatatu iliyopita, wasanii hao walioomba majina yao yalindwe walisema kumbukumbu za vichwani mwao zinaonesha kuwa, Diamond amekuwa akichagua misiba ya kujitokeza hasa ile ambayo itampa ‘kavareji’ kwenye vyombo vya habari.

WASIKIE WENYEWE
“Mimi nakumbuka wakati wa kifo cha Kanumba (Steven), Diamond alitokea kwa sababu ulikuwa msiba mkubwa sana na kweli alipata kavareji ya kutosha kwenye media.

“Halafu akaonekana tena kwenye msiba wa baba yake Wema Sepetu, nadhani kwa vile alikuwa mtu wake Wema wakati huo asingeacha kwenda. Lakini baada ya hapo sikumbuki,” alisema msanii mmoja.
Msanii mwingine aliongeza: “Halafu Diamond na Dully ni washikaji, sasa jamaa tunasikia yuko Zenji tu hapo anakula bata na Zari (Zarina Hassan) lakini ameshindwa kuja Dar kumzika baba mzazi wa mshikaji wake.”

Akaongeza tena: “Kama sijasahau hata kwenye kifo cha mwanamuziki wa Bendi ya Msondo, marehemu Maalim Gurumo hakutokea japokuwa alikuwa amerudi nchini kutoka nje. Magazeti mliandika kwamba Wema alimzuia kwenda kuzika. Sasa ni vizuri kweli?”

WANAOTOA POLE KWENYE MITANDAO
Wakati wasanii hao wakimchana Diamond, wasanii wa filamu, Tamrina Poshi ‘Amanda’, Isabela Mpanda ‘Bela’ na Baby Madaha wao walisema wanakerwa na tabia ya baadhi ya wasanii kutohudhuria misiba ya wenzao na kuishia kutoa pole kwenye mitandao ya kijamii.

Wakizungumza na Amani, wasanii hao walisema imekuwa ni kawaida kwa wasanii kutohudhuria misibani bila kuwa na sababu na kuongeza kuwa tabia hiyo si nzuri kwa umoja wao.


AMANDA

AMANDA
“Mfano mzuri tunauona hapa leo, mwenzetu kafiwa na baba yake ukiangalia wasanii waliohudhuria wanahesabika lakini nimepata mshangao kwa sababu rafiki mkubwa wa Dully ni Diamond lakini hapa hajaonekana. Tunaona tu pole zinaishia kwenye mitandao. Mtu yupo Zanzibar tu hapo na anatupia picha akiwa na mpenzi.”

BELA NAYE
Kwa upande wake, Bela alisema alipata taarifa za msiba huo akiwa hospitali amelazwa lakini akaona ni vema ahudhurie mazishi kwa kuomba ruhusa kwa daktari pamoja na kuwa hali yake haikuwa nzuri.
“Nilikuwa nimelazwa na niliwekewa dripu kabisa baada ya kugundulika nina malaria tano, lakini nikaona siwezi kukosa kuhudhuria msiba kwa sababu marehemu mzee Sykes mbali ya kuwa baba yetu alikuwa mshikaji wetu sisi wasanii,” alisema Bela.


BABY MADAHA.

BABY MADAHA
“Jamani hili jambo lisikieni tu kwa watu, mimi sikuamini kwa sababu siku siyo nyingi Dully aliniambia baba yake anaumwa miguu na walikuwa kwenye mipango ya kumpeleka India akatibiwe, kumbe baadaye hali ilibadilika mpaka umauti ukamkuta, nimeumia sana.

“Wasanii tuache ‘u-snich’ (unafiki) kwa sababu wengi wetu wanaishia kuandika kwenye mitandao tu mi sidhani kama hiyo ni faraja, faraja ni kumfariji mwenzetu tena kwa ukaribu.”Diamond alipotafutwa kwa njia ya simu alisema: “Hata mimi nimeumia kwa kifo cha baba’ke Dully lakini si kwamba sijakwenda makusudi, nilikuwa na dharura.” Mzee Sykes (pichani) alifariki dunia, Jumapili ya Februari 15 katika Hospitali ya Muhimbili ambapo alikuwa akisumbuliwa na presha. Alizikwa Februari 16 katika Makaburi ya Kisutu, jijini Dar.

FAIZA: HAKUNA STAA MWENYE FIGA KAMA YANGU

Stori: Imelda Mtema/Amani
MZAZI mwenziye na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, Faiza Ally amesema kuwa hakuna staa yeyote hapa Bongo mwenye figa kama yake ya kuweza kuvaa ‘bikini’ na kujiachia kama yeye.


Mzazi mwenziye na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, Faiza Ally.

Akifunguka na Centre Spread, Faiza alisema kuwa wapo mastaa wengi wembamba lakini maumbo yao hayana mvuto hasa wakivaa bikini huku akitolea mfano wa Nancy Sumari na Jacqueline Patrick.


“Ukitaka kujua kama una umbo zuri tena la kimataifa wewe jaribu kuvaa bikini uone, ndiyo utajijua ni mrembo kiasi gani. Najitambua navutia kiasi gani nikivaa bikini,” alisema Faiza.

Wednesday, February 18, 2015

JADA KUTOKA KESHO 19.2015


HUYU NDIYE MNENGUAJI WA BENDI YA EXTRA BONGO ALIYEPIGWA NDOA VALENTINE DAY



Mnenguaji mkongwe wa Bendi ya Extra Bongo ‘Wazee wa Kizigo’ Otilia Boniface siku ya harusi yake.

MNENGUAJI mkongwe wa Bendi ya Extra Bongo ‘Wazee wa Kizigo’ Otilia Boniface siku ya Wapendanao ‘Valentine’s Day’ alipigwa pingu ya maisha na mchumba wake wa muda mrefu, Ally Kinde.

Ndoa hiyo iliyofungwa usiku nyumbani kwao Mbezi-Juu ilisindikizwa na ngoma pamoja na matarumbeta ambapo mitaa hiyo na ile ya Kinondoni nyumbani kwa bwana harusi ilisimamisha shughuli zote kwani wanawake waalikwa walijiachia kwa kukata mauno ya kufa mtu kihasara hasara.

Katika hali ya kushangaza, mwanaume mmoja aliyeonekana siyo riziki, aliwashtua watu baada ya kuonekana akikata mauno akiwa juu ya gari la Bwana harusi, jambo lililosababisha kutimuliwa na waalikwa.
Bwana harusi baada ya kufunga ndoa msikitini alikwenda kumpa mkono mkewe aliyekuwa ndani akimsubiri, huko alipokelewa kwa shangwe na wanawake waliokuwa wakibinuka isivyo kawaida.



Otilia mwenyewe alikuwa na furaha muda wote huku akisema anamshukuru Mungu kufunga ndoa kwani ni miaka mingi imepita tangu alipovishwa pete ya uchumba. “Dah, siamini maana nimetoka mbali sana na nilisubiri kwa muda mrefu sana siku hii na kweli imetimia, namshukuru Mungu kwa kweli maana ni kwa neema tu,” alisema.

Gazeti hili lilizungumza na Bwana harusi na kumuuliza kwa nini alichagua kufunga ndoa Siku ya Wapendanao;
“Nimeamua kufunga ndoa leo maana ndiyo bethidei yangu, nikaona ni vema nikamchukua na nimpendaye ili iwe siku ya historia zaidi.”

dondoo: Flora aseme ukweli, ujomba wa yeye na Gwajima umetoka wapi? Hilo tu ndiyo nataka alifafanue kwa undani maana wajomba...

“WOMEN MAKE IT HAPPEN” - EVENT



Siku Ya Wanawake Dunia huadhimishwa kila ifikapo Tarehe 8, mwezi wa tatu. Siku hii huadhimishwa kwa shughuli mbalimbali na kutambua mchango wa mwanamke katika maendeleo ya Jamii.

Mwaka huu kitaifa Siku hii itaadhimishwa mkoani Morogoro lakini kampuni ya TruMark ya mjini Dar es Salaam imeandaa warsha maalum katika maadhimisho hayo ambayo itafanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam Machi 7 mwaka huu.Kauli mbiu ya Siku hii ni Women Make It Happen’ ikiwa inamaanisha wanawake wanafanikisha.


TruMark imeamua kufanya tamasha hili, baada ya uzoefu tulioupata katika shughuli zetu za mafunzo ambazo tunatoa kwa watu mbalimbali, tulioana kuna changamoto mbalimbali ambazo wanawake wanazipata.

Hii likafanya tuone kuwa Siku Ya Wanawake ni jukwaa ambalo linaweza kukutanisha wanawake katika kada mbalimbali na kuzungumza mambo yao katika kujikwamua kiuchumi na kujifunza kwa wengine ambao walipitia changamoto hizo lakini leo hii wameweza kufika mbali baada ya kupambana.

TruMark imepata Baraka zote kutoka Wizara ya Wanawake Jinsia na Watoto katika kuandaa siku hii muhimu. Kwenye maadhimisho haya, kutakuwa na mada ambazo zitatolewa na wanawake kutoka katika kada tofauti, juu ya uongozi, biashara na uchumi, ujasiriamali.
Lakini pamoja na elimu ambayo itatolewa kutakuwepo na burudani pia kutoka kwa wasanii wanawake maarufu na chipukizi nchini ambao wataungana na wanawake wengine kusheherekea siku yao hii.

Wanawake wanakaribishwa kushiriki katika siku hii ili kuweza kupata elimu ambayo itawasaidia kwenye shughuli zao za kila siku. Kwa upande mwingine tunatoa wito kwa wadhamini kujitokeza ili kufanikisha siku hii kwani mama ndiye kiungo cha familia.

Na kama ijulikanavyo kuwa katika kila mwanaume mwenye mafaniko basi nyuma yake yuko mwanamke shupavu.

Trumark tunawakaribisha wadau na wahisani kutoa ufadhili. Mchango wowote utatambulika katika kufanikisha tamasha la wanawake litakalowawezesha walengwa ambao ni wanawake kufikia malengo yao kwa kutumia changamoto na kuzibadili kuwa fursa.

Asilimia 10 ya mapato yatakayopatikana kwenye tamasha hili yatakwenda kusaidia wasichana kupata mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kujitegemea kiuchumi. Wasichana hawa watatokana na shule tutakayoichagua.

Kuhusu TruMark hii ni kampuni inayojihusisha na utoaji mafunzo mbalimbali ya uongozi, biashara na ujasiriamali yenye lengo ya kuboresha ufanisi kwa matabaka mbalimbali katika jamii.
MWISHO.

Agnes Mgongo
Managing Director
TruMark
Human Potential Skills Development
Josam House Complex -Mikocheni
P.Box 12382- Dar es Salaam
Mobile: +255 754 095 017 / 658 095017
Email: amgongo@trumark.co.tz
Website: www.trumark.co.tz

WOLPER KANIPORA DEMU WANGU

Stori: Waandishi Wetu/Mchanganyiko
MSANII wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper amedaiwa kumchukua mpenzi wa msanii wa filamu ambaye pia ni mpigapicha, Farid Jamal ‘Farid Uwezo’ aliyejulikana kwa jina moja la Vivian.
Msanii wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper.

Chanzo cha habari kililiambia gazeti hili kuwa, tangu Wolper awe karibu na Vivi, Farid amekuwa akiumia sana kwani amekuwa akikosa muda wa kujiachia naye.

“Yaani Wolper kampora Farid Vivi wake, sasa hivi jamaa ameamua kumuacha maana anaona mambo hayaendi sawa.

“Watu wanajiuliza, Wolper anampa nini Vivi? Ni ushosti wa kawaida tu au kuna kingine. Maana mtu huwezi kumuacha mpenzi wako kisa msichana mwenzako,” kilidai chanzo hicho kilichoomba hifadhi ya jina lake.

Mpenzi wa ‘Farid Uwezo’,Vivian.

Baada ya kuzinyaka taarifa hizo, mwandishi wetu alimtafuta Farid na alipopatikana alisema ni kweli Vivi alikuwa mpenzi wake lakini Wolper kampora.

“Vivian alikuwa ni mpenzi wangu lakini baada ya kuwa na urafiki na Wolper alibadilika na kunikataa.

“Nilishindwa kujua sababu ya yeye kutotaka kuwa na mimi kwa kuwa Wolper ni msichana mwenzake. Inaniuma sana kwani nilikuwa nampenda sana, hata hivyo siwezi kumrudia kwani atakuwa ameshaharibika kitabia,” alisema Farid.


Msanii wa filamu Bongo, Farid Jamal ‘Farid Uwezo’.

Alipotafutwa Wolper kuzungumzia madai hayo alisema, anashangazwa na taarifa hizo na anachokijua yeye ni kwamba Vivian ni rafiki yake Farid ni mtu wake.

“Kwanza Farid ni mtu wangu wa karibu sana ambaye sidhani kama anaweza kusema maneno hayo. Pili Vivian ni rafiki yagu wa kawaida, mimi nadhani kuna maadui zangu wanataka kunichafua,” alisema Wolper.

CORETHA AJIVUNIA PUB, NYUMBA

Mayasa Mariwata/Risasi Mchanganyiko
MSANII nyota wa filamu, Coretha Raymond ‘Koletha’ amesema anajivunia mafanikio yake kimaisha, ikiwemo kumiliki pub na nyumba, licha kwamba haijamalizika kujengwa.
“Msanii nyota wa filamu, Coretha Raymond.

Sina budi kujivunia mafanikio niliyonayo kutokana na shughuli zangu za sanaa, naishi vizuri hapa mjini, kilichonifikisha hapa ni malengo tu, maana wengine wanaambulia patupu kwa kuendekeza starehe, licha ya hivyo pia nina duka la nguo linalonipatia kipato,” alisema msanii huyo.

Alisema katika kukabiliana na changamoto mbalimbali za kimaisha, alilazimika kuuza gari lake ili kuweka mambo yake sawa, lakini anamshukuru Mungu kwa vile mipango inakwenda kama alivyopanga.

PAM D KUTIMKIA NIGERIA!


Staa anayekimbiza na Wimbo wa Nimempta, Pam D akiwa katika pozi.

MSANII aliyefunga mwaka kwa shangwe kupitia goma la Nimempata, Pamela Daffa ‘Pam D’ yuko mbioni kutimkia nchini Nigeria, Showbiz linamchongo kamili.

Kwa mujibu wa Pam D, safari hiyo itafanyika ndani ya mwezi huu huku lengo kuu ni kwenda kufanya ngoma na msanii mkubwa mmojawapo nchini humo. “Ninafuraha kwani malengo yangu huenda yakatimia na kuwa msanii wa kike pekee kufanya kolabo na Wanaijeria. Kama mambo yakienda inavyotakiwa basi Watanzania wategemee kumsikia Pam D wa kimataifa,” alisema Pam D.

Tuesday, February 17, 2015

DUDE, ESTER WAWAPANDISHA MORI LA SABA

Imelda mtema/Uwazi
STAA aliyewahi kuvuma na kundi lake la Bongo Dar es Salaam, Kulwa Kikumba ‘Dude’ juzikati aliambatana na msanii mwenzake wa filamu, Ester Kihama katika Shule ya Msingi Mgulani kwa ajili ya kuwahamasisha wanafunzi wa darasa la saba kufaulu katika mitihani yao.


Staa aliyewahi kuvuma na kundi lake la Bongo Dar es Salaam, Kulwa Kikumba ‘Dude.

po waliwapandisha mizuka wanafunzi hao baada ya kuwapa zawadi washindi waliofaulu vizuri mitihani ya kila wiki na kuwaahidi kuwa kila wiki watakuwa wakitoa zawadi kwa washindi.


Msanii wa filamu Bongo, Ester Kihama.

Tunataka wanafunzi muwe mnasoma kwa bidii kwa kuwa hakuna kitu kizuri kama kusoma na kutimiza ndoto zenu. Tutakuwa tunakuja kila wiki kuwatembelea na kujua maendeleo yenu, pia kuhakikisha mwaka huu mnafaulu wote,” alisema Dude.

MAMA LORAA: BONGO MOVIES IMEKOSA BODI YA USHAURI

MLEZI wa Klabu ya Bongo Movies, Catherine Ambakisye ‘Mama Loraa’ amefunguka kuwa matatizo na mifarakano inayotokea ndani ya klabu hiyo ni kutokana na kukosa bodi ya ushauri.

Mlezi wa Klabu ya Bongo Movies, Catherine Ambakisye ‘Mama Loraa’.

Akilonga na Uwazi, Mama Loraa alisema wasanii mbalimbali ambao waliwahi kuiongoza klabu hiyo miaka ya nyuma ndiyo tatizo na kwamba Bongo Movies imekosa bodi inayotakiwa kushughulikia matatizo yanapotokea au kutoelewana kwa wasanii.

“Bongo Movies imekosa bodi ya ushauri. Nimeshawahi kuwashauri mara kadhaa wachague bodi ambayo itakuwa inadili na mambo ya klabu sambamba na kutoa ushauri hasa linapokuja suala la kusimamia pesa na ugomvi unapotokea,” alisema Mama Loraa.

MKE WA KITIME AZIKWA MAKABURI YA KINONDONI DAR


Marehemu Janeth Joan Kitime enzi za uhai wake.

Muonekano wa kaburi la marehemu Janeth Joan Kitime baada ya kuzikwa siku ya leo katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar.

Mwanamuziki mkongwe, John Kitime akiweka maua katika kaburi la mke wake.

Mzee Kitime na wanawe kulia wakiweka mchanga katika kaburi la marehemu.

Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho (kulia) akitoa pole.

Mzee Kitime akiteta jambo na msanii Dude.

Mmoja wa ndugu akijiandaa kuweka maua.
Kitime katikati akiwa na watoto wake wawili Ivan (kushoto) na Tina (kulia).
Wana familia wakiwa mbele ya kaburi la marehemu baada ya kuzika.



Wadau mbalimbali wakiwa kwenye msiba huo.

Monday, February 16, 2015

WEMA AMRUDISHA UJANA BI. MWENDA

STAA wa filamu za Kibongo, Wema Sepetu amemfanyia ‘sapraizi’ msanii mkongwe, Fatuma Makongoro ‘Bi. Mwenda’ kwa kumnunulia simu ya kisasa na kumfanya awe kama kijana.
Staa wa filamu za Kibongo, Wema Sepetu.

Wema alimfanyia sapraizi hiyo hivi karibuni kwa kummpeleka Bi.Mwenda katika maduka ya Mlimani City pasipo kumwambia wanakwenda kufanya nini na alipofika, akamnunulia simu hiyo yenye uwezo wa ‘internet’.Msanii mkongwe, Fatuma Makongoro ‘Bi. Mwenda’.

“Namshukuru sana Wema maana sikujua tunakwenda kufanya nini Mlimani City, nikashangaa ananikabidhi simu, nimefurahi na mimi kuwa kama vijana wa kisasa, kuingia WhatsApp na Instagram,” alisema Bi. Mwenda.

SIKILIZA CHANNEL TEN LEO KIPINDI CHA ACTION AND CUT JUU YA UJIO WA FILMU MPYA YA JADA


MAZISHI YA MZEE EBBY SYKES KUFANYIKA LEO MAKABURI YA KISUTU, DAR


Mwanamuziki Dully Sykes akihojiwa na wanahabari (hawapo pichani) huko msibani Kawe Beach jijini Dar.



Dully akilia kwa simanzi wakati akipewa pole na waombolezaji waliofika msibani Mbezi Beach, Dar leo mchana.





Dully akipewa pole na baadhi ya waombolezaji waliofika msibani leo.
Ebby Sykes enzi za uhai wake.

MAZISHI ya mwanamuziki mkongwe nchini ambaye ni baba mzazi wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Dully Sykes, Ebby Sykes yatafanyika leo saa 10 jioni katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.

Mzee Sykes alifariki dunia jana mchana akiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa vidonda miguuni vilivyopelekea kueneza sumu katika mwili wake na kumsababishia mauti.

Kwa mujibu wa Dully, Mzee Sykes alikuwa akisumbuliwa na vidonda hivyo vilivyoshindwa kupona kutokana na kuvuta sigara. Lakini mbali na hilo hakuwa na tatizo lingine lolote.

Mzee Sykes amefariki akiwa na umri wa miaka 62 alizaliwa Februari 24, 1952. MWENYEZI MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MZEE SYKES MAHALI PEMA PEPONI.

TANZANIA BLOGGERS NETWORK WAMFARIJI MZEE KITIME KWA KUFIWA‏


Mwenyekiti wa muda wa Chama cha Bloggers Tanzania (TBN), Joachim Mushi (kulia) akikabidhi ubani wa fedha shilingi 900,000 na kutoa pole kwa mwanamziki mkongwe, John Kitime (kushoto) ambaye amefiwa juzi na mkewe, tukio hilo lilifanyika jana Kimara eneo la Nguzo ya 800, jijini Dar es Salaam. Mzee Kitime ni mwanachama wa TBN.
Mwenyekiti wa muda wa Chama cha Bloggers Tanzania (TBN), Joachim Mushi (kulia) akitoa ujumbe wa pole kwa John Kitime na waombelezaji mara baada ya kukabidhi ubani wa fedha zilizotolewa na wanachama wa TBN jana eneo la Kimara Nguzo ya 800 jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wajumbe wa TBN walifika kumfariji Kitime ambaye pia ni mwanachama wa TBN.
Baadhi ya wajumbe wa TBN, wakiwa katika picha na mzee Kitime walipofika kumfariji na kutoa ubani wa TBN. Kutoka kushoto ni Sufian na Othman Michuzi pamoja na Mzee Kitime.
Kutoka kushoto ni mjumbe mshauri na Kiongozi wa TBN, Issa Michuzi, baadhi ya wanamuziki wa bandi ya Njenje, Mwenyekiti wa TBN, Mzee Kitime na mwanae akipata picha na baadhi ya waombolezaji marafii waliofika kumfariji.
Baadhi ya wanamuziki wa Njenje pamoja na wajumbe wa Chama cha Bloggers Tanzania (TBN) wakipata picha ya pamoja na mfiwa mwanamziki mkongwe, John Kitime walipofika msibani kumfariji jana Kimara eneo la Nguzo ya 800, jijini Dar es Salaam. Mzee Kitime ni mwanachama wa TBN.