INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Friday, November 30, 2012

TUTAKUKUMBUKA SHARO MILIONEA!

 
Majonzi na vilio vilitawala kwenye msiba wa msanii wa Bongo Fleva pamoja na Bongo Movie ndugu yetu Sharo Milonea uliotokea katika Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga kwa ajali mbaya ya gari, msanii huyo alipokuwa akielekea kwenda kumuona mama yake mzazi na kukutwa na mauti.

  Msanii wa Bongo movie Ray alikuwa ni mmoja wa waombolezaji walioshiriki kwenye msiba wa ndugu yetu Sharo Milionea.....
Majonzi na vilio vilitawala..

Rachel Saguda na Batuli kwenye majonzi makubwa sana poleni dada zangu. .


Odama akiwa kwenye majonzi...
Mwili wa Marehemu ukiwasili nyumbani kwao..

Watu walizimia sana kwa uchungu wa kumpoteza ndugu yetu..

The Greatest akiwa kwenye majonzi..

Roma mwanamuziki wa kizazi kipya

Mzee Majuto mwenye kanzu akiwa pamoja Waziri Mwanamuziki wa wa Band ya Njenje wana Kinyaunyau..

Mh; Nape Nnauye naye alikuwepo, tunakushukuru sana kwa kujitoa katika misiba yote miwili, Asante sana Muheshimiwa kwa moyo uliotuonyesha wasanii,,, wewe ni mfano wa kuigwa na viongozi wenzako..

Majuto akiongea machache juu ya marehemu.

Mwili wa Marehemu tayari kwa kwenda kuzikwa.

Mwili ukipelekwa sehemu rasmi iliyoandaliwa kwa kuzikwa marehemu Sharo Milionea.

Poleni sana wasanii wetu wa Tanzania kumpoteza ndugu yetu sisi tulimpenda ila Mungu kampenda zaidi

Mtunisy Msanii wa filamu mwenye shati jekundu wakimsindikiza Msanii mwenzake Sharo Milionea.

Friday, November 23, 2012

JE SHILOLE KAOLEWA?



Staa wa filamu za kibongo maarufu kama Bongo Movies ambaye pia anafanya poa kwenye upande wa muziki, si mwingine ni Zuwena Mohamed alias Shilole ameendelea kushoot video ya single yake kwa jina la “Dudu” aliyompa collabo mkali wa Q-Chillah.
Kwenye utengenezaji wa video hiyo Shilole ameweza kuigiza kama anaolewa {Bi. Harusi} huku mume wake kwenye video hiyo akiwa Mo Rocka.
Kwa wapenzi wa msanii Shilole tegemeeni kupaipata video hiyo soon kwenye Television yako kwani mzigo mzima umesimamiwa na Kampuni ya Kwetu Studio.

KAJALA KUANDAMWA NA MAGONJWA YA 'UNENE' GEREZANI

MSANII wa filamu Bongo ambaye yuko nyuma ya nondo Gereza la Segerea, Dar es Salaam kwa mashitaka ya kuuza nyumba iliyowekewa kizuizi na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Kajala Masanja anaweza kupata gonjwa la moyo kufuatia kunenepa sana akiwa gerezani humo.


Kajala Masanja wakati akipandishwa katika Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam Jumatatu wiki hii. Kajala aliyepandishwa katika Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam Jumatatu iliyopita, muonekano wake kwa sasa uliwashangaza watu katika mahakama hiyo baada ya kuonekana amenenepa sana kuliko alivyokuwa uraiani.
Baadhi ya watu walisikika wakihojiana wenyewe kwa wenyewe kama kuishi gerezani kwa muda mrefu kunasababisha mtu kunenepeana kama yeye.
“Hivi kumbe gerezani kunaweza kumnenepesha mtu jamani? Kajala shavu dodo,” alisema mwanamke mmoja ambaye mwenzake alikuwa kinyume naye.
Mwenzake: “Ila kunenepa kwa aina hii halafu unakaa kwa muda mrefu kuna hatari ya kupata magonjwa ya moyo. Unajua uraiani chakula kinachukuliwa na kazi za siku nzima, gerezani muda mwingi ni kukaa tu, inabidi afanye mazoezi ya kupungua.”


Kajala akionekana kanenepa kuliko alivyokuwa uraiani. Mwingine: “Dah! Hebu mcheki kwanza, yaani anazidi kuwa bomba kila kukicha, sasa hivi amekuwa shavu dodo kuliko hata alivyokuwa uraiani! Tusidanganyane jamani, piga ua kutakuwa na mtu anamtunza huyu hukohuko aliko si bure. ”
Hata hivyo, miongoni mwa waliodatishwa na muonekano wa Kajala ni msanii mwenzake, Mahsein Awadh ‘Dokta Cheni’ ambaye alimsogelea na kutaka kumkumbatia lakini alizuiliwa na askari waliokuwa wakimlinda.


...akiwa na sura ya tabasamu.
 
Source: Vituko Vya Mtaa

Thursday, November 22, 2012

FILAMU YA FAMILY WAR KUINGIA SOKONI 27 - 11 - 2012 (WIKI IJAYO)

J-Film 4 Life chini ya Mkurugenzi Jennifer Kyaka (Odama) sasa wanakuletea filamu mpya inayoitwa "Family War." kwahiyo wadau na wapenzi wa filamu msikose kuangalia filamu hii, kwani utaelimika, utaburudika, utafundishwa na kuadabishwa.
J-Film 4 Life baada ya kukuletea filamu ambazo naamini ulishaziangalia kama Chocolate na House Maid na nyingine nyingi ambazo ni gumzo jijini Dar es Salaam, sasa imeona ikuletee filamu hii mpya yenye viwango vya kimataifa. Kama unavyojua J-Film 4 Life ni kampuni ambayo inatoa filamu za viwango vya juu sana.

ROSE NDAUKA UFUNGUKA KUHUSU SKENDO YA KUWA TAPELI




Habari mpya kutoka kwa Rose Ndauka baada ya kupiga story na mwandishi wa habari hii ni kuhusu skendo za utapeli.....

Mrembo huyu amefunguka na kusema kwamba kumekuwa na madai mengi sana kwamba amekuwa akiitisha usahili kwa wasanii chipukizi na kuwachukulia fedha bila kuwashirikisha katika filamu zake.....

Ndauka alikanusha na kusema kwamba sio habari za kweli kwani anapoita usahili pale mtu anapofanya vizuri anamchukua na kama akifanya vibaya basi anamuelekeza ili siku nyingine atakapoitaji tena aweze kushiriki tena.

Hayo ndiyo maneno ya Rose Ndauka baada ya kuchonga nasi kuhusiana na tetesi ambazo zilikuwa zikizungumziwa kwamba anawachukia wasanii chipukizi wa filamu.

MAYA: 'TUNAIUNDA UPYA BONGO MOVIE'


Mayasa Mrisho ‘Maya’.

STAA wa movie za Kibongo anayeitumikia Kampuni ya filamu ya Kanumba The Great, Mayasa Mrisho ‘Maya’ amesema kuwa wapo katika mchakato wa kuipika upya klabu yao ya Bongo Movie.
Maya kama mmoja wa wanachama wa klabu hiyo, ameitonya Tollywood Newz kuwa kwa sasa wanatoa upya fomu za uanachama na amewataka wasanii kuzichangamkia.
“Wanaozihitaji fomu hizo wanaweza kuniona ili wajiunge, tuweze kufanya mchakato wa uchaguzi wa viongozi watakaoisimamia klabu yetu,” alisema Maya.


Share on facebookShare on twitterShare on print

PICHA MBALIMBALI ZA AUNTY EZEKIEL, MUMEWE NA WAGENI WAO, WAALIKWA LUNCH BAADA YA KUOLEWA


Maharusi Mr & Mrs Sunday Demonte wakiwa katika pose nyumbani kwa Salma Mgido mapema leo kwaajili ya chakula cha mchana
Aunty akiwa amepakata mtoto Seif wa da Katija Mashallah
 Kitu cha ndafu na madiko diko kibao
 Rahma Aunty Ezekiel na Mumewe Sunday wakikata ndafu huku waigizaji wenzake Aunty akiwemo, Ray, JB na Cloud walioenda harusini wakishuhudia tukio
 Ray akishuhudia kwa ukaribu tukio hilo
Bi Salma Mgido (mwenye pink) akiweka mambo sawa
 Mr & Mrs Demonte wakipata msosi
 Wageni waalikwa akiwemo mwenyekiti wa Jumuyia ya watanzania Dubai (mwenye kanzu ya blue) katika shughuli hiyo
 Cloud katika picha ya pamoja na Janja
Cloud na Janja wakibadilishana mawazo
 Ray katika pose na shabiki wake
 Le Familia Mashallah
 JB katika pose
 Katija, mumewe aka muarabu na mkewe na Ray katika pose

 Mumewe Katija, wanae na Sunita pia walikuwepo
Bi Salma mama wa shughuli......
 
 
Source:  Vituko vya Mtaa

SNURA -'NIKO TAYARI KUMUOMBA RADHI WEMA'.WEMA NAE AMGOMEA



 
BAADA ya kufikwa na msiba wa bibi yake mzaa mama hivi karibuni, staa wa filamu za Kibongo, Snura Mushi anajipanga kwenda kumuomba radhi staa mwenzake, Wema Sepetu baada ya kutokea kutokuelewana kati yao, .

Akizungumza na mwandishi wetu, Snura alisema kuwa anajisikia vibaya kuwa na maadui, hivyo msiba wa bibi yake umemfundisha kuwaomba radhi watu wote aliokosana nao siku za nyuma.

WENGINE TAYARI
“Tayari nimeshawafuata watu watatu na kuwaomba radhi na tumeshayamaliza ila amebaki mmoja tu ambaye ni Wema,” alisema Snura.
Snura amewataja watu aliowaomba radhi kuwa ni Mtangazaji wa zamani wa Runinga ya EATV, Lady Naa, mmiliki wa saluni pande za Mwananyamala Komakoma, Bonita na mshika kamera wa Chiddy Classic.
“Nashukuru wamenielewa na tumefungua ukurasa mpya wa maisha yetu na sasa si maadui tena,” aliongeza staa huyo.

BADO WEMA
Akimzungumzia Wema, Snura alisema kuwa yeye hana kinyongo tena na staa huyo na mambo ya zamani yameshapita, hivyo anataka kumuomba radhi pale alipomkosea ili kuisafisha nafsi yake.

WEMA AKIKATAA?
Snura alisema anaamini kuwa Wema atamuelewa na kama atakataa kumsikiliza, atamshukuru Mungu kwa kuwa lengo lake la kutoa dukuduku moyoni litakuwa limetimia.
Baada ya kumsikiliza Snura, mwandishi wetu alimpigia simu Wema na kumuuliza kama atakubali kuombwa radhi na Snura.

HUYU HAPA WEMA
“Kwa kweli siko tayari kuombwa radhi na Snura, kwa kuwa binafsi nikimchukia mtu huwa ninamchukia milele,” alisema Wema.
Kisha akaongeza:
“Mwanzoni si alijidai ananikomoa? Mwacheni aendelee kukomoa lakini sitamsikiliza kamwe.”



Wema na Snura enzi za ushosti wao. TUJIKUMBUSHE
Mastaa hao ambao walikuwa marafiki wakubwa waligombana Agosti mwaka huu na kufikia kujibizana kwenye vyombo vya habari.
Snura alitaka kutoa filamu ya Uozo wa Super Star ili kueleza mambo machafu ya Wema ambaye tayari ameshatengeneza filamu inayokwenda kwa jina la Super Star.
Kama vile haitoshi, Snura alihojiwa katika Runinga ya EATV kwenye kipindi cha Hot Mix na kusema kuwa alikuwa na siri nzito za Wema na kama akiziweka hadharani, staa huyo atashindwa kutembea mitaani.
Katika kujibu mapigo, Wema naye alimtaka Snura ajaribu kuweka hadharani mambo yake ili naye atoe yake.
Wema alisema alikuwa akiendesha maisha ya Snura kwa kumlipia pango na ada ya mwanawe na hata mapochi na nguo alizokuwa akizivaa staa huyo zilitokana na fedha zake.

Wednesday, November 7, 2012

BAADA YA FILAMU YA CHOCOLATE SASA NI ZAMU YA FAMILY WAR


J-Film 4 Life chini ya Mkurugenzi Jennifer Kyaka (Odama) sasa wanakuletea filamu mpya inayoitwa "Family War." Filamu hii itakuwa sokoni mwezi huu wa Novemba 2012 kwahiyo wadau na wapenzi wa filamu msikose kuangalia filamu hii, kwani utaelimika, utaburudika, utafundishwa na kuadabishwa.

J-Film 4 Life baada ya kukuletea filamu ambazo naamini ulishaziangalia kama Chocolate na House Maid na nyingine nyingi ambazo ni gumzo jijini Dar es Salaam, sasa imeona ikuletee filamu hii mpya yenye viwango vya kimataifa. Kama unavyojua J-Film 4 Life ni kampuni ambayo inatoa filamu za viwango vya juu sana.

 Odama akiwa kwenye setting ya camera....akisubiri kufanya mambo yake.
 Mambo yakiendelea kuiva
Odama akisubiria Action..............
 Watu wakiwa kazini...bizeeeeee
 Devie akifanya maajabu katika filamu ya Family War
 Grace Mapunda akifanya mambo yake kwenye scene ya hospitali
 Director Lamata (kulia) akitoa maelekezo kabla ya scene kuanza
 Recho Saguda akiwa on set kabla ya scene kuanza.
 Director Sajuki akitoa company kwa waigizaji wenzake kwenye scene za hospitali

 Hakuna kitu kizuri kama upendo. Sajuki na mke wake Wastara wanaonyesha upendo kwa vitendo.
 Umeona unywele....hayo ni mambo ya Family War
 Slim akiwa on set
 Cake haikuwa nyuma katika filamu hii
 Kazi imepamba moto hospitalini, yaani ni balaa tupu...
 Wakati mwingine usione fashion haya ni mambo ya Continuity...
 Pozi kwa pozi....
 Mlawa akitafakari script kabla ya scene kuanza
 Nikipitia script kabla ya scene kuanza

 Camera man Malik akiwajibika kazini...kuhakikisha kazi inaenda kama ilivyopangwa.


Tukipitia Script kabla ya scene kuanza

 Tukisubiria action kuanza tufanye vitu vyetu.

 Director akifuatilia scene kwa makini..

WADAU MSIKOSE KUNUNUA HII FILAMU.....ITAWAELIMISHA, ADIBISHA, KUFUNDISHA NA KUBURUDISHA.