BAADA ya kufikwa na msiba wa bibi yake mzaa mama hivi karibuni, staa wa filamu za Kibongo, Snura Mushi anajipanga kwenda kumuomba radhi staa mwenzake, Wema Sepetu baada ya kutokea kutokuelewana kati yao, .
Akizungumza na mwandishi wetu, Snura alisema kuwa anajisikia vibaya kuwa na maadui, hivyo msiba wa bibi yake umemfundisha kuwaomba radhi watu wote aliokosana nao siku za nyuma.
Akizungumza na mwandishi wetu, Snura alisema kuwa anajisikia vibaya kuwa na maadui, hivyo msiba wa bibi yake umemfundisha kuwaomba radhi watu wote aliokosana nao siku za nyuma.
WENGINE TAYARI
“Tayari nimeshawafuata watu watatu na kuwaomba radhi na tumeshayamaliza ila amebaki mmoja tu ambaye ni Wema,” alisema Snura.
Snura amewataja watu aliowaomba radhi kuwa ni Mtangazaji wa zamani wa Runinga ya EATV, Lady Naa, mmiliki wa saluni pande za Mwananyamala Komakoma, Bonita na mshika kamera wa Chiddy Classic.
“Nashukuru wamenielewa na tumefungua ukurasa mpya wa maisha yetu na sasa si maadui tena,” aliongeza staa huyo.
BADO WEMA
Akimzungumzia Wema, Snura alisema kuwa yeye hana kinyongo tena na staa huyo na mambo ya zamani yameshapita, hivyo anataka kumuomba radhi pale alipomkosea ili kuisafisha nafsi yake.
WEMA AKIKATAA?
Snura alisema anaamini kuwa Wema atamuelewa na kama atakataa kumsikiliza, atamshukuru Mungu kwa kuwa lengo lake la kutoa dukuduku moyoni litakuwa limetimia.
Baada ya kumsikiliza Snura, mwandishi wetu alimpigia simu Wema na kumuuliza kama atakubali kuombwa radhi na Snura.
HUYU HAPA WEMA
“Kwa kweli siko tayari kuombwa radhi na Snura, kwa kuwa binafsi nikimchukia mtu huwa ninamchukia milele,” alisema Wema.
Kisha akaongeza:
“Mwanzoni si alijidai ananikomoa? Mwacheni aendelee kukomoa lakini sitamsikiliza kamwe.”
Wema na Snura enzi za ushosti wao. TUJIKUMBUSHE
Mastaa hao ambao walikuwa marafiki wakubwa waligombana Agosti mwaka huu na kufikia kujibizana kwenye vyombo vya habari.
Snura alitaka kutoa filamu ya Uozo wa Super Star ili kueleza mambo machafu ya Wema ambaye tayari ameshatengeneza filamu inayokwenda kwa jina la Super Star.
Kama vile haitoshi, Snura alihojiwa katika Runinga ya EATV kwenye kipindi cha Hot Mix na kusema kuwa alikuwa na siri nzito za Wema na kama akiziweka hadharani, staa huyo atashindwa kutembea mitaani.
Katika kujibu mapigo, Wema naye alimtaka Snura ajaribu kuweka hadharani mambo yake ili naye atoe yake.
Wema alisema alikuwa akiendesha maisha ya Snura kwa kumlipia pango na ada ya mwanawe na hata mapochi na nguo alizokuwa akizivaa staa huyo zilitokana na fedha zake.
No comments:
Post a Comment