Siku ya jana Mkurugenzi wa J-Film 4 Life Jennifer Kyaka (Odama) alifanyiwa surprice na crew yake eneo la Magomeni akiwa anajiandaa kuanza shooting ya filamu yake mpya ya JICHO LANGU.
Odama akiwa njiani kuelekea Magomeni kwaajili ya shooting alijaribu kuwapigia simu baadhi crew yake waliokuwa katika NOAH iliyobeba vifaa vya shooting lakini hakuna mtu aliyeweza kupokea simu yake. Ulikuwa ni wakati mgumu sana kwake, kwani aliweza kujiuliza ni kwanini simu zake hazipokelewi? !!!! Alimuuliza blogger wake aliyekuwa naye katika gari lake juu ya kutopokelewa simu yake, naye blogger hakuwa na jibu sahihi...
Odama aliweza kufika katika eneo la kufanyia shooting (Magomeni) na alipofika mahali pale hakuweza kuwaona wenzake waliokuwa katika ili NOAH iliyobeba vifaa vya shooting. Odama aliweza kuwasubiria kwa muda mrefu sana bila ya mafanikio na alipokuwa akijaribu kuwapigia simu hakuna aliyeweza kupokea simu yake. Ulikiwa wakati mgumu sana kwake....!!!
Baada ya nusu sana crew yake ilifika katika eneo la tukio yaani Magomeni na baada ya kufika, Odama alionekana kushangazwa sana baada ya kuona gari lake (NOAH) lililokuwa limebeba vifaa vya shooting likiwa na watu walioshika mapulizo na watu wengine wakiwa busy sana wakihangaika huku na kule kwaajili ya kumfanyia surprice. CREW nzima ilitoka nje ya gari (yaani NOAH) huku ikimwimbia wimbo wa kumpongeza kumaliza mwaka na kuanza mwaka mpya wa kuzaliwa kwake. " Happy Birthday to you......!!!! Happy Birthday to you......!!!! "
Watu walijitokeza wengi sana mtaani wakiwa na furaha ya ajabu maana hawakutegemea kuona msanii mkubwa namna hii akifanya birthday yake kitaani...Ilikuwa ni siku ya furaha sana kwake.
Baada ya kumaliza shamrashara Odama na crew yake nzima waliweza kuendelea na zoezi la shooting. Na hivi ndivyo ilivyokuwa...!!!
Cake iliyoandaliwa na crew ya J-Film 4 Life kwaajili ya kumpongeza mkurugenzi wao Jennifer Kyaka kumaliza mwaka na kuanza mwaka mwingine.
Baadhi ya wanafunzi na majirani wakimwimbia Mkurugenzi wa J-Film 4 Life Jennifer Kyaka (Odama) katika siku yake ya kuzaliwa.
Mkurugenzi wa J-Film 4 Life akimega cake kwaajili ya kuwalisha majirani na watu wote waliokuwa katika eneo la l"location" hapo Magomeni
Mkurugenzi akionyesha sura ya furaha huku akistaajabu kilichomtokea eneo hilo la "location", kwani hakutegemea kabisa kufanyiwa surprice na crew yake. Hapa akionekana akiwalisha wanafunzi.
ULIFIKA WAKTI WA KULISHANA CAKE
ULIFIKA WAKTI WA KULISHANA CAKE
Neema ambaye amecheza katika filamu hii mpya ya Jicho Langu akilishwa cake. Amecheza kama mdogo wake na Odama
WENYEJI WA MAGOMENI WAKILISHWA CAKE
No comments:
Post a Comment