INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Friday, August 16, 2013

MKURUGENZI WA J-FILM 4 LIFE JENNIFER KYAKA (ODAMA) ATEMBELEA CHUO CHA FILAMU TANZANIA CHA TFTC FOUNDATION UBUNGO KWAAJILI YA AUDITION YA FILAMU YAKE MPYA YA "JICHO LANGU" SIKU YA LEO

Siku ya leo Mkurugenzi wa J-Film 4 Life akiongozana na Director wa J-Film 4 Life Lamata aliweza kutembelea chuo cha filamu Tanzania cha TFTC FOUNDATION kinachomilikiwa na mwigizaji maarufu sana  Tanzania Mkurugenzi Pastor Myamba.  Chuo hiki kipo Ubungo nyuma ya ofisi za NSSF au karibu sana na kituo cha mabasi yaendayo mikoani hapa jijini Dar es Salaam. Chuo hiki kimejikita sana katika kufundisha vijana na watu wazima wanaotamani sana kuigiza au kucheza filamu.

Lengo kubwa la kutembelea chuo hiki ilikuwa ni kuwatafuta watu watakaoweza kucheza katika filamu mpya ya  Jennifer Kyaka (Odama) inayoenda kwa jina la JICHO LANGU.  Wanachuo waliweza kuonyesha vipaji vyao mbele ya Mkurugenzi wa J-Film 4 Life, na waliweza kumpa wakati mgumu sana Mkurugenzi wa J-FIM 4 LIFE, Jennifer Kyaka (Odama) na Director wake Lamata kuchagua wale watakaoweza kucheza katika scene itakayochezwa maeneo ya  makaburi huko Sinza- Makaburini. Na kilichowastajabisha  sana wanachuo hao ni jinsi walivyoweza  kufanya mambo makubwa hata kuzidi baadhi ya waigizaji maarufu.

Mkurugenzi wa J-Film 4 Life, Jennifer Kyaka aliweza kutoa histora fupi ya maisha yake ya filamu na kuwatia moyo wale wote wanaotamani kujikita katika sanaa ya uigizaji ya kwamba wasikate tamaa bali wazidi kufanya kwa bidii na wasiangalie sana maslai kipindi waanza bali waangalie sana kazi ili waweze kufahamika katika jamii, na jamii ikishawafahamu na kuona mchango wao kuwa ni mzuri basi wataweza kuwatumia na kununua filamu zao.

Director wa J-Film 4 Life, Lamata aliwaomba sana wale wote watakaocheza katika scene hii ya makaburini waweze kuvaa uhusika kamili ili waweze kupeleka ujumbe kwa jamii. Director Lamata aliwasihi vijana hawa watamini kazi yao na wafanye kwa moyo wao wote na sio kwa kuiga watu wengine.


 Mkurugenzi wa J-Film 4 Life Jennifer Kyaka (Odama) kushoto na Director wake Lamata wakielekea chuoni huku wakongozwa na Mkurugenzi wa chuo hicho cha Filamu Tanzania TFTC, Pastor Myamba maeneo ya Ubungo jijimi Dar es Salaam
 Jennifer Kyaka na Pastor Myamba wakiongea kabla ya kuingia chuoni

Picha ya pamoja
 Mkurugenzi wa TFTC Foundation Pastor Myamba na Directo wa J-Film 4 Life, Lamata wakiwa katika picha ya PA1
 Mkurugenzi wa J-Film 4 Life Jennifer Kyaka (Odama) akiwa katika moja ya ofisi ya chuoni hapo


Mkurugenzi wa J-Film 4 Life Jennifer Kyaka (ODAMA) akiandika jina lake katika kitabu cha wageni
Director wa J-Film 4 Life  Lamata akiachia jina lake katika kitabu cha wageni

ULIFIKA MUDA WA KUONGEA NA WANACHUO
 Kutoka kulia ni Agness, Mkurugenzi wa chuo Pastor Myamba,  Mkurugenzi wa J-Film 4 Life Jennifer Kyaka (Odama) na Director wa J-Film 4 Life  Lamata

 
Pastor Myamba akimchekesha Jennifer Kyaka wakati wa utambulisho

 Wanachuo wakimsikiliza Mkurugenzi wa TFTC Foundation, Pastor Myamba akitambulisha wageni waliomtembelea


 Mkurugenzi wa TFTC Foundation, Pastor Myamba akiwakaribisha wageni wake waliweza kumtembelea katika chuo chake
 Mmoja wa viongozi wa chuo upande wa wanachuo
Mkurugenzi wa TFTC Foundation, Pastor Myamba akiongea jambo na Mkurugenzi wa J-Film 4 Life Jennifer Kyaka


Wanachuo wakiwa makini sana kumsikiliza Mkurugenzi wa J-Film 4 Life, Jennifer Kyaka

 Ulifika wakati wa wanachuo kuuliza maswali kwa wageni wao waliowatembelea
  Director wa J-Film 4 Life  Lamata akijaribu kueleza yale yaliyowafanya wafike chuoni hapo



ULIFIKA WAKATI WA KUONYESHA VIPAJI VYA UIMBAJI

Katika filamu ya JICHO LANGU kuna scene itahitaji watu watakaoweza kuimba kwa hisia kali sana, kwahiyo ulifika wakati wa kusikiliza sauti za watu na kuangalia sura zao kama zinaendana na kile wanachokiimba
Mkurugenzi wa J-Film 4 Life akisikiliza kwa makini sauti za waimbaji pamoja na kuangalia hisia zao katika nyuso zao

Director wa J-Film 4 Life akisikiliza kwa makini sauti za waimbaji na kuangalia jinsi wanavyoweza kuvaa uhusika

Ulikuwa wakatii mgumu sana kwa majaji kuchagua aliyebora zaidi, kwani wote walionekana kuimba kwa kiwango cha juu sana



ULIFIKA WAKATI WA KUANGALIA WALIWEZA KUFANYA VIZUR ZAIDI

Hawa walibahatika kuchaguliwa katika scene ya kuimba

 Mkurugenzi wa TFTC Foundation, Pastor Myamba akimuonyesha Mkurugenzi wa J-Film 4 Life Jennifer Kyaka (Odama) majina 50 ya watu wataoweza kucheza katika scene ya makaburi 

ULIFIKA WAKATI WA KUPIGA PICHA ZA PAMOJA KWAAAJILI YA KUMBUKUMBU



ULIFIKA WAKATI WA KUTEMBELEA OFISI INAYOHUSIKA NA EDITING
Mkurungenzi wa TFTC Foundation aliweza kuwakaribisha wageni wake waliomtembea katika ofisi yake nyingine inayojihusisha na ku-edit video, na huko waliweza kupiga picha za pamoja kwaajili ya kumbukumbu.
Mkurugenzi wa J-Film 4 Life, Jennifer Kyaka
Mkurugenzi wa J-Film 4 Life, Jeniifer Kyaka akiwa na Afisa Utawala Agness
Jennifer Kyaka akiwa na Editor wa TFTC Foundation

Katikati ni blogger wa blog ya ODAMA na pia ni mkurugenzi wa RUMAFRICA.
ANGALIA MATUKKIO MENGINE KWA KUBONYEZA "Read More" HAPO CHINI








1 comment: