Monalisa, Odama pamoja na Johari wakisubiria wateja.
Wasanii wa filamu wakiwemo Johari, Monalisa, Irene Uwoya, Odama, Richie pamoja na Jacob Stephan aka JB jana katika viwanja vya Biafra Kinondani jijini Dar es Salaam, wameendesha kampeni ya kuosha magari ili kuchangisha fedha itakayowasaidia waathirika wa ajali za barabarari waliolazwa kwenye wodi ya hospitali ya taifa yaMuhimbili.Akizungumza na Bongo5 kwenye banda la Jaffary Carwash ambapo shughuli hiyo ilipokuwa ikifanyika, JB alisema kama wasanii wana wajibu wa kufanya shughuli za kijamii ili kuisaidia.
Kajala Masanja akiosha gari
“Sisi kama wasanii tunaonyesha tunaweza kutumia nguvu zetu kuosha magari ili kupata pesa za kuwasaidia watu ambao wameathirika kwa ajali za gari. Kwahiyo hii ni sehemu ya wajibu wetu, tunawakaribisha watu waje waoshe magari yao,” alisema JB
JB akiwa na Irene Uwoya
Richie na Kajala wakiwa na mteja wao baada ya kuosha gari lake
Johari na Monalisa wakiosha gari
Richie akiosha gari
No comments:
Post a Comment