INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Tuesday, September 30, 2014

MAZISHI YA KAKA YAKE NA CAMERAMAN WA KAPUNI YA J-FILM 4 LIFE BWANA MALICK SIKU YA JUMATATU 28.09.2014 MKOANI PWANI

Siku ya jana Cameraman wa J-Film 4 Life chini ya Mkurugenzi Jennifer Kyaka (Odama) Bwana Malick kwa masikitiko makubwa aliweza kushirikiana na ndugu na jamaa kumzika kaka yake aliyepata ajali kwa pikipiki na kupoteza uhai. Crew ya J-Film 4 Life iliweza kufika katika msiba huu mkubwa na kuungana na ndugu na marafiki kupumuzisha mwili wa marehemu mkoani Pwani.

Rumafrica iliungana na crew ya J-Film 4 Life katika safari ya mwisho ya kuaga mwili wa marehemu. Hakika tulisikitishwa sana na kifo cha kaka wa rafiki yaetu Malick na ndio maana hatukujizuia kuungana na wenzetu kwenda katika msiba huo mkubwa sana kwa Taifa la Tanzania.

Tukumbuke sote ndiko tunakuelekea, hakuna mwenye makazi ya kudumu hapa duniani
Kulia ni Bwana Malick akiwa na msanii wa Bongo Movie, mchekeshaji Kingwendu


Msanii wa Bongo Movi Kingwendu (kushoto) akiongea na mfiwa Malick mawili matatu..
 Mfiwa Malick
 Crew ya J-Film 4 Life- Kutoka kushoto ni Director Lamata, mzee wa boom Issa, msanii wa Bongo movie, Kupa, Make up Ashura, Light Abdul, cameraman Malick (mfiwa), mkurugenzi wa J-Film 4 Life Odama
 Crew ya J-Film 4 Life- Kutoka kushoto ni Director Lamata, still picture Rulea Sanga, msanii wa Bongo movie, Kupa, Make up Ashura, Light Abdul, cameraman Malick (mfiwa), mkurugenzi wa J-Film 4 Life Odama
 Wananchi wakielekea makaburini
 Mazishi yakiendelea. Msanii wa Bongo Movie Kupa (mwenye nyekundu) alikuwepo





 Issa (mbele) na Malick (nyuma)


Rulea Sanga wa pili kutoka kulia akitupia mchanga kaburini
 Kutoka kushoto ni Abdul, Malick na Rulea Sanga (waliovalia tshirts nyeusi)
 Rulea Sanga wa pili kutoka kushoto
 Rulea Sanga mwenye tshirts nyeusi akishirikiana na wakazi wa pwani wakati wa kuzika


 Odama
  Mkuugenzi Odama
 J-Film 4 Life Make Up, Ashura
  J-Film 4 Life Director Lamata
  J-Film 4 LifeCrew
  J-Film 4 Life
  J-Film 4 Life Crew
  J-Film 4 Life boss Odama


Odama and Malick

Monday, September 22, 2014

TAZAMA MASTAA WA BONGO WAKIOSHA MAGARI KUSAIDIA WAATHIRIKA WA AJALI!


Monalisa, Odama pamoja na Johari wakisubiria wateja.

Wasanii wa filamu wakiwemo Johari, Monalisa, Irene Uwoya, Odama, Richie pamoja na Jacob Stephan aka JB jana katika viwanja vya Biafra Kinondani jijini Dar es Salaam, wameendesha kampeni ya kuosha magari ili kuchangisha fedha itakayowasaidia waathirika wa ajali za barabarari waliolazwa kwenye wodi ya hospitali ya taifa yaMuhimbili.Akizungumza na Bongo5 kwenye banda la Jaffary Carwash ambapo shughuli hiyo ilipokuwa ikifanyika, JB alisema kama wasanii wana wajibu wa kufanya shughuli za kijamii ili kuisaidia.

Kajala Masanja akiosha gari

“Sisi kama wasanii tunaonyesha tunaweza kutumia nguvu zetu kuosha magari ili kupata pesa za kuwasaidia watu ambao wameathirika kwa ajali za gari. Kwahiyo hii ni sehemu ya wajibu wetu, tunawakaribisha watu waje waoshe magari yao,” alisema JB
JB akiwa na Irene Uwoya

Richie na Kajala wakiwa na mteja wao baada ya kuosha gari lake

Johari na Monalisa wakiosha gari

Richie akiosha gari

Saturday, September 20, 2014

ODAMA KUOSHA MAGARI BIAFRA LEO MCHANA


Jeniffer Kyaka (Odama)

Msanii wa Bongo Muvi anayeheshimika sana na jamii kwa kazi zake nzuri zinazofanywa na kampuni yake ya J-Film 4 Life dada Jennifer Kyaka (Odama) siku ya leo atakuwa akiosha magari yeye mwenyewe katika viwanja vya Biafra mchana wa leo. Ukitaka kumuona yeye na wasanii maarufu sana wa Bongo Muvi basi jisogeze pale Biafra uone mastaa hawa wakipiga kazi. Soma hilo tangazo


Friday, September 19, 2014

PICHA: ODAMA NDANI YA KITCHEN PARTY YA NDUGU YAKE NA DIRECTOR WA FILAMU TANZANIA LAMATA


Tunamshukuru Mungu siku hii ilikuwa ya kipekee sana kwa rafiki yangu Lamata katika Kitchen party ya ndugu yake. Tukiwa na baadhi ya wasanii wa Bongo Movie, tuliselebuka mpaka bhasiiii... tulimaza shughuli hii kwa amani na upendo...

Kutoka kulia ni Lamata, Kajala na Odama
 Jennifer Kyaka (Odama)
  Jennifer Kyaka (Odama)
  Jennifer Kyaka (Odama)
  Jennifer Kyaka (Odama)
  Jennifer Kyaka (Odama)
  Jennifer Kyaka (Odama)
  Jennifer Kyaka (Odama) na Kajala
 Jennifer Kyaka (Odama)

Saturday, September 13, 2014

STEVE NYERERE AJIUZULU URAIS BONGO MOVIE UNITY

 

Aliyekuwa Rais wa Klabu ya Bongo Movie Unity, Steve Nyerere. Rais wa Klabu ya Bongo Movie Unity, Steven Mengere 'Steve Nyerere' ametangaza kujiuzulu cheo hicho kupitia ukurasa wake wa instagram. Amedai kuna mpango mbaya dhidi yake hivyo akaona bora ajiengue pasipo kufafanua zaidi.

Wednesday, September 10, 2014

NAMSHUKURU MUNGU KWA KUNIWEZESHA KULIJENGA KABURI LA RAFIKI YANGU KIPENZI MAREHEM RACHEL HAULE

Asante MUNGU kwa kunipa kibali cha kuweza kusimamia kulijenga kaburi la rafiki angu kipenzi RACHEL HAULE mpaka hatua hii ilipofikia,,MUNGU aendelee kunisimamia mpaka hitimisho la ujenzi huu pia natoa shukrani kwa shemeji yangu wa ukweli kabisa @guda_boy tulieshirikiana katika jambo hili...MUNGU UMREHEMU NA UMWEKE MAHALI PEMA.


.

MIKOSI YAMKUMBA MSANII WA FILAMU TANZANIA, LUCY KOMBA KATIKA HARUSI YAKE

NDOA YA LUCY KOMBA MIKOSI JUU YA MIKOSI ndoa iliyokuwa ikisubiriwa kwa muda mrefu ya nyota wa filamu Bongo, Lucy Francis Komba na mzungu wake raia wa Denmark anayejulikana kwa jina moja la Janus hatimaye imefungwa na kutawaliwa na matukio yenye mikosi kibao.


Nyota wa filamu Bongo, Lucy Francis Komba na mzungu wake raia wa Denmark anayejulikana kwa jina moja la Janus wakiwa ni wenye furaha wakati wa harusi yao. Ndoa hiyo ilifungwa Jumamosi iliyopita kwenye Kanisa la Roman Katoliki Parokia ya Mtakatifu Benedict lililopo maeneo ya Kurasini- Bandari jijini Dar.

Baada ya zoezi hilo kumalizika, wawili hao na wapambe wao walikwenda katika Kisiwa cha Bongoyo, Dar kwa ajili kupiga picha za ukumbusho. Kisiwa hicho kipo Kilomita 2.5 kutoka Pwani ya Jiji la Dar.

Mdenmark Janus akimwelekeza jambo mke wake rasmi Lucy Francis Komba.

Hata hivyo, zoezi la kwenda kupiga picha kwenye kisiwa hicho liliingia mkosi kufuatia maharusi hao kupanda boti maeneo ya Slip Way, Oysterbay, Dar na kupigwa na mawimbi makubwa yaliyowafanya watumbukie baharini kabla ya kuokolewa na wapiga mbizi mahiri.

“Jamani sijui balaa gani hili? Yaani tumetumbukia baharini tukienda Bongoyo, viatu vimezama, nguo tulizovaa zimelowa, tukaletewa nyingine, simu yangu pia iliingia majini lakini tunamshukuru Mungu tuliokolewa na kuendelea na safari,”alisema Lucy alipoulizwa na gazeti hili.

Wapambe wakijipanga kutoa sapoti katika harusi hiyo.

Lucy alisema walifika salama kisiwani Bongoyo na kupiga picha mbalimbali za ukumbusho na baada ya kumaliza walianza safari ya kurejea mjini ili kwenda kula na watoto yatima wa Kituo cha New Life kilichopo Kigogo jijini Dar lakini wakapata mkosi wa pili.

Lucy alisema hajui ni nini, kwani alishangaa sana baada ya kutoka Bongoyo wakiwa maeneo ya Kinondoni kuna gari lililoonekana kuwafuatilia toka mbali, liliwafikia na kuligonga gari lililokuwa katika msafara wake waliokuwa wakichukua matukio kwa kamera ya video, wakashuka na kuanza kuwafanyia fujo kisha wakawapora kamera hiyo na kuondoka kwa kasi eneo hilo.

Wanaharusi Lucy Komba na mumewe Janus wakipozi kupata picha ya ukumbusho.

“Sijajua mpaka sasa wale watu ni akina nani na walikuwa na dhamira gani, sijui walitumwa? Nashindwa kuelewa maana walikuwa mabaunsa wawili na mwanamke mmoja,” alisema Lucy.
Mbali na misukosuko yote waliyopata siku hiyo, lakini maharusi hao walifanikiwa kufika katika Ukumbi wa Makumbusho uliopo Posta Mpya, Dar ambapo sherehe ya kifahari ilifanyika na kuhudhuriwa na marafiki wa bi harusi na viongozi kutoka serikalini.

Mbali na yote, shughuli hiyo ilikuwa na vituko mbalimbali ambavyo viliwakosha waalikwa, ikiwemo watu wa kareti kutoa salamu zao za kikomandoo, mtu wa mazingaombwe ya nyoka, wanenguaji kutoka Kampuni ya Bia ya Windhoek kutoa shoo ya nguvu na msanii mkongwe Bongo, Ummy Wenceslaus ‘Dokii’ kutumbuiza.

Maharusi wakiingia katika Ukumbi wa Makumbusho ulio Posta kwa ajili ya sherehe.

Bwana harusi naye alionesha mila ya kikwao kwa kulazwa chini na kuvuliwa viatu kisha kuvalishwa tena ikiwa ni ishara kwamba ameagana na ukapera.
Msanii huyo alipata zawadi kedekede kutoka kwa ndugu, jamaa na marafiki zake. Mama yake mzazi aliyekuwa Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi, Ilala, Marietta Minangi alimzawadia kiwanja kilichopo Bunju jijini Dar huku baba yake mdogo (jina halikupatikana) akimpa mbuzi na ng’ombe wawili wa maziwa.Kaka yake alimkabidhi shilingi milioni tisa taslimu ukumbini hapo na kamati ya sherehe ilimpa shilingi milioni tatu bila kumsahau Dokii ambaye alimzawadia matofali 500 na mifuko 10 ya simenti.
Kutokana na thamani kubwa aliyonayo mzazi wake kwa kumzaa na kumlea vyema, Lucy alimfanyia ‘sapraizi’ mama yake huyo kwa kumpa zawadi ya gari aina ya Toyota Prado ambalo alimkabidhi mahali hapo.
“Namshukuru sana mama yangu kwa malezi mazuri aliyonipa mpaka sasa nimeolewa, sioni cha kumlipa kwa thamani kubwa aliyonayo kwangu, ila nimeamua kumzawadia gari aina ya Prado, japo ana gari lakini nimemzawadia hili ikiwa kama upendo wangu kwake,”alisema Lucy ambaye siku si nyingi anataraji kuondoka nchini kwenda Denmark kwa mumewe.

MSHINDI WA TANZANIA MOVIE TALENTS (TMT) 2014, MWANAAFA MWINZAGO APOKELEWA KWA SHANGWE MKOANI KWAO MTWARA‏


Mara baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Mtwara, mshindi wa shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) 2014 Mwanaafa Mwinzago akitoa maneno ya shukrani kwa wakazi wa Mtwara waliojitokeza kuja kumpokea uwanja wa ndege wa Mtwara mapema jana. Vilevile alitoa shukrani zake zote kwa watanzania wote kwa kuweza kumpigia kura na kumfanya aibuke mshindi wa Milioni 50 za Tanzania katika fainali ya shindano la kusaka vipaji vya kuigiza lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents (TMT).

Wapenzi, mashabiki na wana Mtwara wakiwa nje ya uwanja wa ndege wa Mtwara wakisubiri kumpokea mshindi wa shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) 2014 Mwanaafa Mwinzago kwa ajili ya kumpongeza kwa kuibuka mshindi wa shilingi Milioni 50 za kitanzania katika fainali ya shindano la Tanzania Movie Talents (TMT)lililofanyika mwisho wa mwezi wa nane katika ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar Es Salaam.

Wakazi wa Mkoa wa Mtwara wakimpongeza mshindi wa TMT 2014 Mwanaafa Mwinzago ambaye amewasili Mkoani Mtwara ambapo ndio nyumbani kwao akitokea Dar Es Salaam mara baada ya Kuibuka mshindi na kujinyakulia kitita cha shilingi Milioni 50 za kitanzania.

Ndugu, jamaa na marafiki wa mshindi wa TMT 2014 Mwanaafa Mwinzago wakipiga picha ya pamoja mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mtwara akitokea Dar Es Salaam.
Shangwe na nderemo zilitawala katika viunga vya uwanja wa ndege wa Mtwara kabla na baada ya mshindi wa shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) 2014, Mwanaafa Mwinzago kutua katika uwanja wa ndege wa Mtwara akitokea Dar Es Salaam ambapo fainali ya shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) lilifanyika katika ukumbi wa Mlimani City.
Msafara wa kuelekea nyumbani kwa Mshindi wa TMT 2014 , Mwanaafa Mwinzago ukitoka katika uwanja wa ndege wa Mtwara.

Msafara ukielekea nyumbani kwa Mshindi wa TMT 2014 Mwanaafa Mwinzago,
Wazee kwa vijana wakimpongeza Mwanaafa Mwinzago wakati alipokuwa akipelekwa nyumbani kwao kwa Msafara wakati akitokea Uwanja wa Ndege
Vijana nao wakimpongeza mshindi wa TMT 2014 Mwanaafa Mwinzago

Wakazi wa Mtwara wakimpongeza Mshindi wa TMT 2014 Mwanaafa Mwinzago wakati alipokuwa akipita na masafara uliompokea uwanja wa ndege Mtwara na kumsindikiza hadi nyumbani kwao Magomeni Mkoani Mtwara mapema jana asubuhi
Wanafunzi wa shule ya msingi wakimpongeza Mwanaafa Mwinzago wakati alipokuwa akipita na msafara kutoka uwanja wa ndege wa Mtwara akielekea nyumbani kwaajili ya kujiandaa kwenda shule jana asubuhi wakati alipowasili kutokea Mkoani Dar Es Salaam.



Majirani, ndugu, marafiki na wakazi wa Mtwara wakimshangilia Mshindi wa TMT 2014 Mwanaafa Mwinzago wakati alipowasili nyumbani kwao eneo la Magomeni , Manispaa ya Mtwara Mikindani akitokea uwanja wa ndege wa Mtwara.

Saturday, September 6, 2014

MWIGIZAJI WA FILAMU TANZANIA AMUONYA MSHINDI WA MILIONI 50 WA TMT ASIBWETEK

MUIGIZAJI mwenye mvuto wa aina yake katika tasnia ya filamu Bongo, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’ amempa somo mshindi wa Shindano la Tanzania Move Talent ‘TMT,’ Mwanafaa Mwinzago kuwa asibweteke na ushindi aliopata bali azingatie masomo.

Muigizaji mwenye mvuto wa aina yake katika tasnia ya filamu Bongo, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’.

Akizungumza na Ijumaa juzikati, Lulu alisema ni kweli binti huyo ana kipaji na ilikuwa haki kushinda milioni 50 ila ajue bado ni mtoto na anatakiwa kukomalia elimu.

“Ustaa ni cheo kikubwa sana hasa katika jamii na kila mtu anakuangalia wewe, ili ujikontroo unatakiwa ujitambue na huwezi kujitambua kama huna elimu ya kutosha hivyo mimi namshauri aweke suala la masomo mbele kuliko ustaa alioupata,” alisema Lulu.

Mshindi wa Shindano la Tanzania Movie Talent ‘TMT,’ Mwanafaa Mwinzago.

Fainali za TMT zilifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita ndani ya Ukumbi wa Mlimani City ambapo Mwanafaa aliibuka kidedea.