Mtoto wa wacheza filamu wawili nchini,Sajuki na Wastara ametimiza siku arobaini na kufanyiwa sherehe kubwa nyumbani kwao Tabata.Sherehe hiyo ilihudhuriwa na Wasanii wa Bongo Movie na watu wa kada tofauti na majirani zao.Hakika ilikuwa furaha tele kwa mama mtoto huyo Wastara na mumewe Sajuki kwani ukizingatia ni muda mrefu sajuki hali yake kiafya sio nzuri akiwa anasumbuliwa na maradhi ya uvimbe tumboni.Kubarikiwa kupata mtoto kwao ni furaha kubwa sana,vile vile kuona wasanii wenzao wa Bongo Movie wakija kwenye sherehe hiyo kwao ilikuwa ni furaha tosha.
Huyu ndio mtoto mwenyewe wa wasanii hao wawili
Akitolewa nje
Tukifuatilia maulidi
Nikiwa katika harakati za kumpokea mtoto
Kupa akiwa na Mzee Rupia,Mdau mkubwa wa Bongo Movie na Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Yanga
Mzee Rupia akiwa na Dinno
Tukifuatilia maulidi
Sajuki akimbeba mtoto wake
No comments:
Post a Comment