INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Friday, April 27, 2012

SHUKRANI ZA PEKEE ZIENDE KWA WOTE WANAOGUSWA NA TATIZO LA SAJUKI
Juzi jumatano nilirusha mahojiano niliyoyafanya na Wastara kuhusu ugonjwa wa msanii Sajuki ambae ni mumewe.Sajuki anasumbuliwa na uvimbe tumboni toka mwaka jana mwezi wa saba.Kupitia leo tena ya clouds fm wengi mlisikia na mkaguswa kuwa sehemu ya wale wanaochangia kumwezesha Sajuki kupata matibabu nchini India mwezi ujao.

Kabla sijaanza kampeni hii nilikutana na Wastara akanieleza hali waliyokuwa nayo.Nikaongea na mkuu wa vipindi clouds fm kwamba tufanye kitu tusiishie tu kutoa taarifa akakubali na ndio maana niliiweka hewani katika leo tena.Kwa mtu yoyote mwenye huruma na imani akimsikia huyu dada lazima alie.Hata juzi wakati nafanya kipindi nikiwa hapa Dodoma nilishindwa kujizuia kulia.Niliweka nadhiri moyoni mwangu na Mungu wangu kuwa kama ni yeye alitaka niwe Dina Marios basi sauti yangu na isikike na lengo la kupata pesa ya matibabu ya huyu kijana ipatikane.Na kweli baada ya kufanya tu kipindi kikaisha kuna mama amejitolea tiketi ya ndege ya kwenda na kurudi ya watu wawili.Watu mbalimbali wamejitokeza kuchangia na pia wengi wamejiunga nami katika kampeni hii akiwemo Shamim Mwasha wa 8020 blog,Joyce Kiria wa wanawake live na wengine wengi.

Pia shukrani za pekee zimwendee mbunge wa viti maalum vijana mheshimiwa Esta Bulaya ambae baada ya kuongea nae ameguswa na tunaenda katika ngazi ya juu zaidi kupata tunachokitaka.Kwa sasa tunajaribu kuipeleka kwa waziri wa vijana utamaduni sanaa na michezo Dr.Emmanuel Nchimbi.Kwa lolote endelea kusikiliza clouds fm the people station.

Bado unaweza kuchangia kwa Mpesa 0762189592 na kupitia Akiba commercial bank acount no 050000003047 Wastara Juma.

No comments:

Post a Comment