INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Tuesday, March 24, 2015

GWT JUMAPILI HII NDANI YA UKUMBI VICTORIA - VICTORIA PETROL STATION - DAR


LINAH AFANYA ‘BETHIDEI’ NDANI YA BOTI


Msanii wa Bongo Fleva, Linah akiwa amezungukwa na baadhi ya ndugu na jamaa zake wakati akikata keki iliyokuwa imeandaliwa kwa ajili ya sherehe ya kuzaliwa kwake iliyofanyika ndani ya boti.


Keki ya bethidei ikiwa mezani kabla ya kukatwa.


Linah akimlisha keki kaka’ake.


Mmoja wa waalikwa akilishwa keki.


Mwandishi wa magazeti ya Global Publishers LTD, Musa Mateja (kushoto), akilishwa keki na Linah.


Mmoja wa watangazaji wa Clouds TV, Jacob Mbuya (kushoto), akilishwa keki na Linah.


Linah (kulia), akilishwa kipande cha keki na mmoja wa marafiki zake.


Linah akiwa katika pozi na wasanii wenzake.


Mtangazaji wa Global TV Online, Shorvieny Mohamed akimfanyia mahojiano Linah kwenye sherehe hiyo.


Baadhi ya wasanii wa Bongo Fleva wakipata vinywaji kwa pamoja kwenye sherehe hiyo.



Msanii wa Hip Hop, Young Killer (kushoto), akiwa amepozi na msanii mwenzake Edo Boy ndani ya Ukumbi wa Paparazi uliopo ndani ya Hoteli ya Slipway.


Linah akipozi na marafiki zake.


Peter Msechu akikodoleana macho na Linah baada ya kukutana kwenye sherehe hiyo.


Msanii wa Bongo Fleva, Recho (kulia), akiwa katika pozi na marafiki zake kwenye sherehe hiyo.


Mwana FA (wa kwanza kushoto), akiwa katika pozi na Linah, pamoja na Andrew Kusaga.
Baadhi ya misosi iliyokuwa imeandaliwa kwenye sherehe hiyo ikiwa mezani.

STAA wa Bongo Fleva, Esterlina Sanga ‘Linah’, juzikati alifanya sherehe ya siku yake ya kuzaliwa (bethidei) ndani ya boti iliyokuwa ndani ya maji ya Bahari ya Hindi, jirani na eneo la Hoteli ya Slipway, Masaki jijini Dar es Salaam.

Wasanii kibao wa muziki wa kizazi kipya walihudhuria sherehe hiyo iliyofana vilivyo.

(HABARI/PICHA: MUSA MATEJA/GPL)

Monday, March 23, 2015

J-FILM 4 LIFE YAFANYA SHOOTING KATIKA TAMASHA LA MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI TANZANIA EVELYN KABWELILE KATIKA HOTELI YA REGENCY PARK MIKOCHENI DAR ES SALAAMA

Picha mnato na Rumafrica +255 715 851 523 www.rumaafrica.blogspot.com
Evelyn Kabwelile kwa uwezo wa Mungu aliweza kutimiza ndoto yake ya muda mrefu katika huduma yake ya uimbaji. Siku ya jana aliweza kuweka wakfu Audio CD yake inayoenda kwa jina la NJOO UONE katika hoteli ambayo kwa sasa anafanyia kazi ya Regency Park iliyoko kwa Nyerere Mikocheni jijini Dar es Salaam Tanzania siku ya Jumapili 22/03/2015. Uzinduzi huu uliongozana na waimbaji mbalimbali kama wanvyoonekana katika tangazo hapo chini.
Evelyn Kabwelile
Kikundi cha kusaidiana cha kusaidiana cha USHINDI kilweza kufika pale kikiwakilishwa na baadhi ya wajumbe kama vile Rulea Sanga, Tumaini Njole, Leah, Enoce, Sarah Mvungi na wengine wengi waliweza kufika. Eveln ni mmojawapo wa wanaushindi.

Watu wa kamera walikuwa ni crew ya J-FILM 4 LIFE ambayo iko chini ya mwigizaji wa filamu Tanzania, Jeniffer Kyaka (Odama). Unaweza kuwasiliana nao kwa simu hii +255 715 851 523
Evelyn Kabwelile kwa uwezo wa Mungu aliweza kutimiza ndoto yake ya muda mrefu katika huduma yake ya uimbaji. Siku ya jana aliweza kuweka wakfu Audio CD yake inayoenda kwa jina la NJOO UONE katika hoteli ambayo kwa sasa anafanyia kazi ya Regency Park iliyoko kwa Nyerere Mikocheni jijini Dar es Salaam Tanzania. Uzinduzi huu uliongozana na waimbaji mbalimbali kama wanvyoonekana katika tangazo hapo chini.
Kikundi cha kusaidiana cha kusaidiana cha USHINDI kilweza kufika pale kikiwakilishwa na baadhi ya wajumbe kama vile Rulea Sanga, Tumaini Njole, Leah, Enoce, Sarah Mvungi na wengine wengi waliweza kufika. Eveln ni mmojawapo wa wanaushindi.

Watu wa kamera walikuwa ni crew ya J-FILM 4 LIFE ambayo iko chini ya mwigizaji wa filamu Tanzania, Jeniffer Kyaka (Odama). Unaweza kuwasiliana nao kwa simu hii +255 715 851 523


 Kutoka kulia Mc. Sarah Mvungi, Evelyn, Mc. Masanja



 Kutoka kulia Mc. Sarah Mvungi, Evelyn, Mc. Masanja


 J-Film 4 Life Crew Abdul (kulia) na Farid


kutoka kulia ni Faraja Ntaboba (Mwanaushindi), Edson Mwasabwite,  Masanja
Rulea Sanga (mwanaushindi) wa tatu kutoka kulia



Mwanaushindi - Tumaini Njole
Rulea Sanga (kushoto) akifuatia Faraja Ntaboba na Masanja Mkandamizaji
Edson Mwasabwite akiimba wimbo wa Connection

Rulea Sanga (kulia)
Rulea Sanga (kulia)
Rulea Sanga (kulia)
Kutoka kulia mstari wa mbele Mc Sarah Mvungi, Tumaini Njole, Masanja, Edson Mwasabwite wakicheza wimbo wa Connection wa Edson Mwasabwite


KIPINDI CHA KUNUNUA AUDIO CD
 Kaka akitoa mchango wake kwa kununua CD (kushoto) akifuatia Mc. Masanja, mhusika Evelyn Kabwelile, Mc. Sarah Mvungi
 Evelyn Kabwelile (kushoto) na Mc. Sarah Mvungi
Wanaushindi - Kutoka kulia ni Leah Mwankundile na Tumaini Njole

ANGALIA MATUKIO MENGINE KWA KUBONYEZA
"Read More" HAPO CHINI KULIA CHINI KIDOGO

Thursday, March 19, 2015

DENTI MWENZAKE LULU ACHOMWA KISU, AFARIKI


WAANDISHI WETU, DAR
CHAMIWA Adamu (23), kijana ambaye ni mkazi wa Kilimahewa- Manzese jijini Dar, ameuawa kwa kuchomwa kisu cha shingo na mtu aliyetambulika kwa jina moja la Mpelu kisa kikidaiwa ni shilingi mia mbili tu!

Marehemu Chamiwa Adamu enzi za uhai wake.

Marehemu Chamiwa (pichani)alikuwa mwanafunzi mwenzake na staa wa filamu za Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ kwenye Chuo cha Magogoni, Dar.

Tukio la Chamiwa kuchomwa kisu lilijiri saa 11 jioni ya Machi 12, mwaka huu katika eneo lililofahamika kwa jina la Tishio, Manzese Midizini, Dar.

SIKU YA TUKIO
Akisimulia mkasa huo mwanzo mwisho, mmoja wa wanafamilia ambaye hakupenda kutaja jina alisema, siku ya tukio, Chamiwa alikuwa na wenzake (hakuwataja majina), kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Mpelu alitokea na kumwomba shilingi mia mbili.

“Marehemu alimwambia ana hela kubwa, kwa hiyo hana chenji, hivyo akamtaka amwache aende kutafuta chenji ili ampatie hiyo 200.“Ile anaondoka tu, Mpelu alimshika begani kwa nyuma, marehemu alipogeuka kumtazama, Mpelu akamchoma kisu sehemu ya shingoni. Palepale damu zikaanza kuchuruzika na marehemu akaanguka.
“Watu, akiwemo aliyemchoma kisu walimnyanyua marehemu na kumpakia kwenye gari iliyokuwepo pembeni ili kumpeleka Kituo cha Polisi Magomeni,” alisema mwanafamilia huyo.

KISU KILIVYOZAMA
Kwa mujibu wa mashuhuda, inadaiwa kuwa kisu alichochomwa Chamiwa, kilizama ndani ya mwili wake kwa umbali wa zaidi ya nchi mbili.


Simu ya marehemu.

MTUHUMIWA ATAKA KUTOROKA
Habari zinadai kwamba, wakiwa njiani kumpeleka marehemu kituo cha polisi, mtuhumiwa huyo alibaini Chamiwa alishafariki dunia, akaomba afunguliwe mlango wa gari ili ashuke (kwa maana ya kukimbia) lakini wasamaria wema hao walimkatalia kwa vile walishtukia kwamba kesi ingekuwa yao, hivyo wakaongeza ulinzi kwa mtuhumiwa mpaka kituo cha polisi.

WALIVYOSEMA MAJIRANI
Amani lilifanikiwa kufika nyumbani kwa marehemu na kuzungumza na baadhi ya majirani ambapo walisema Chamiwa alikuwa kijana mpole, mwenye kujituma na alikuwa hana shida kwa wenzake.“Tumeumia sana kusikia ameuawa kwa kuchomwa kisu. Tukimfikiria kijana wa watu alivyokuwa bado mdogo, maskini Chami! Amepoteza ndoto zake. Yeye ndiye aliyekuwa akishika nafasi ya baba mwenye nyumba kama mzee Adamu hayupo. Inauma! Ila tumuachie Mungu atamlipia,’’ alisema jirani mmoja.

SIMU YA MAREHEMU YAKUTWA NA DAMU
Amani lilifanikiwa kuiona simu aliyokuwa akiitumia marehemu enzi za uhai wake ikiwa imezimwa na kuchafukwa kwa damu iliyoganda.Mpaka juzi, mtuhumiwa huyo alikuwa bado anashikiliwa katika Kituo cha Polisi Magomeni huku uchunguzi ukiendelea.


Staa wa filamu za Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’.

CHUONI KWA MAREHEMU
Amani lilifika kwenye chuo alichokuwa akisoma marehemu Chamiwa ambapo liliambiwa alikuwa mwaka wa kwanza akichukua masomo ya Information of Technology (IT).Mkuu wa wanafunzi (Dean of Students) aliliambia Amani kwamba, taarifa za mwanafunzi huyo kuuawa kwa kisu zimewafikia na wanachosubiri ni ratiba ya mazishi ili washiriki pamoja na familia.

“Kusema kweli tumepokea taarifa hizo lakini tunachosubiri ni ratiba ya mazishi ili na sisi tuweze kushiriki,” alisema mkuu huyo bila kutaja jina lake.

Wakati Amani linaondoka chuoni hapo liliwapa pole wanafunzi wenzake marehemu hasa wale wa mchepuo sanjari na wake, lakini pia lilimtafuta Lulu kwa lengo la kumpa pole lakini ilidaiwa kwamba, alishaondoka kurudi nyumbani.

Marehemu Chamiwa alizikwa Machi 13, mwaka huu mkoani Morogoro.
Mungu ailaze pema peponi roho yake. Amina.