CREW
2015 Calendar
FILMS
FILMS 2
ADVERTS
INSIDE INAPATIKANA MADUKANI
FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015
JADA IPO SOKONI
Saturday, February 28, 2015
Friday, February 27, 2015
HOSPITALI YA MUHIMBILI NA CLOUDS MEDIA WAFANYA KAMPENI YA KUCHANGIA DAMU
Sehemu ya damu iliyokusanywa baada ya wananchi kuchangia.
Msanii, Kala Jeremiah akisisitiza watu kujitokeza katika kuchangia damu.…
Mtangazaji wa Kituo cha Redio cha EFM, Samira Kiango akichangia damu.
Wafanyakazi wa Clouds Media wakiwa kwenye kampeni ya uchangiaji damu.
Baadhi ya wataalamu wakitoa ushauri na huduma kabla ya kuchangia damu.
Baadhi ya wananchi wakiwa kwenye foleni.
WAKAZI wa jiji la Dar es Salaam, leo walijitokeza katika zoezi la kuchangia damu kwa ajili ya waathirika na wahitaji wa huduma hiyo.
Zoezi hilo lilifanyika katika Uwanja wa Karume, Ilala jijini Dar es Salaam kwa ushirikiano wa Clouds Media, Hospitali ya Muhimbili, Damu Salama na wadau wengine.
Msanii wa Muziki wa Hiphop, Kala Jeremiah amewahimiza wasanii na wananchi kujitokeza kuchangia damu ili kuokoa maisha ya Watanzania wengi wanaoaga dunia kwa kutokuwa na damu nyingi katika ajali na kwa kina mama wajawazito.
TIKO: NATAKA MTOTO WA PILI, WA KUNIPA MIMBA SINA
Na Hamida Hassan/Ijumaa
Staa wa filamu za Kibongo, Tiko Hassan amesema kuwa anatamani kupata mtoto wa pili kwa sababu mtoto wake wa kwanza amefikisha miaka 10, tatizo hana wa kuzaa naye.
Staa wa filamu za Kibongo, Tiko Hassan.
Akipiga stori na Ijumaa Tiko alisema yeye ni ‘mgonjwa’ wa watoto wachanga na anahisi sasa ni muda muafaka ila tatizo mwanaume aliyenaye hana mpango wa kupata mtoto. “Yaani acha tu, mpenzi niliyenaye naona kama hajajiandaa maana hata nikiongelea ishu ya kubeba mimba, naona ananipotezea lakini kiukweli nahitaji mtoto wa pili,” alisema Tiko

QUEEN SUZY HATIMAYE AJIFUNGUA
Na Waandishi Wetu/Ijumaa
MWANAMUZIKI wa Bendi ya FM Academia, Suzan Chubwa ‘Queen Suzy’ hivi karibuni amejifungua mtoto wa kike na ameeleza kuwa, amefarajika kwani alikaa muda mrefu tangu alipopata wa kwanza wa kiume.
Mtoto wa , Suzan Chubwa ‘Queen Suzy’ akiwa na babaake.
Mwanadada huyo alijaaliwa kupata mtoto huyo baada ya kuuficha ujauzito wake kwani alikuwa akikaa ndani tu mpaka alipojifungua.
Gazeti hili lilifanikiwa kuzungumza naye ambapo alikiri kujifungua katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na kusema amefurahi sana kupata mtoto wa kike kupitia mpenzi wake wa siku nyingi aitwaye G-Seven.
“Yaani nina furaha ya ajabu kwani ni bahati kwangu ‘kubalansi’, wa kwanza wa kiume, huyu wa kike, namshukuru sana Mungu,” alisema Queen Suzy.

CHID BENZ APATA MAJANGA TENA!
Na Shani Ramadhani/Ijumaa
HUKU kesi yake ya kukamatwa na madawa ya kulevya ikiwa bado inaendelea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar, msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Rashid Makwiro ‘Chid Benz’ amepata majanga tena baada ya juzikati kudaiwa kugonga daladala kwa nyuma wakati ‘akiovateki’ gari aina ya Scania maeneo ya Mabibo Sokoni jijini Dar.
Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Rashid Makwiro ‘Chid Benz’.
Chanzo kililitonya Ijumaa kuwa mara baada ya tukio hilo kutokea, Chid aligoma kulipa gharama za matengenezo ya gari hilo hali iliyozua mzozo mkubwa.
“Chid alikuwa mtata sana kukubali kosa, mzozo ukawa mkubwa, watu wakajaa lakini baadaye wakamalizana na kila mmoja akaendelea na safari zake,” kilidai chanzo hicho kilichoomba hifadhi ya jina lake. Baada ya kuzinyaka habari hizi, paparazi wetu alimtafuta Chid kwa njia ya simu yake ya mkononi, alipopatikana alidai alikuwa katika kikao cha familia hasingeweza kuongelea suala hilo.

MAIMARTHA AFUNGUKIA MAMBO YA CHUMBANI ZAIDI
Wiki hii kupitia safu hii tunaye Maimartha Jesse ‘Mai’ ambaye ni mtangazaji na mjasiriamali. Mwandishi wetu Hamida Hassan alimbana kwa maswali 10 mengi yakiwa yanahusu mambo ya chumbani zaidi, ungana naye…
Mtangazaji na mjasiriamali Maimartha Jesse ‘Mai’.
TQ: Ni chakula gani kizuri ambacho ukimpikia mumeo anasikia raha?
Mai: Mume wangu ni mpenzi sana wa wali samaki au ugali samaki, sambamba na vikorombwezo vingine.
TQ: Ukiwa sebuleni na mumeo mkiangalia vipindi mbalimbali vya televisheni ni mavazi gani unavaa na mapozi gani mnakaa?
Mai: Huwa tunakaa kwa heshima tu kwa sababu nina familia na wakati wote inakuwa karibu yetu.
TQ: Vipi uwapo chumbani na mumeo unapendelea kumtega kwa mavazi gani au nakshi zipi?
Mai: Kiukweli kule hakuna kuvaa nguo, ni cheni ya kiunoni, vikuku mguuni kwani tunakuwa wawili tu. Si unajua tena pale ndiyo eneo la kujidai na laazizi wangu?
TQ: Kwa mapenzi hayo mnayooneshana, siku ikitokea umemfumania mumeo na mwanamke mzuri kuliko wewe, utachukua uamuzi gani?
Mai: Siwezi kumuacha mume wangu kwa sababu jiji hili lina wanawake wabaya ambao wanajipeleka wao kwa wanaume. Nitakachokifanya ni kumvalisha mume wangu nguo kisha namrudisha nyumbani. Nikifika namuandalia juisi bariiidi. Baada ya hapo nitaenda kumalizana na mwizi wangu.
TQ: Utamfanya nini huyo mwizi wako?
Mai: Ukweli ajiandae kwa viwembe kwani nitahakikisha nimemchakaza sura yake, akitoka hapo akiona mume wa mtu atamuogopa kama ukoma.TQ: Inasemekana una hausigeli mkali sana, vipi siku mumeo uzalendo ukimshinda na ukawakuta kwenye kitanda mnacholala?
Mai: Hilo haliwezi kutokea. Unajua nimeshamsoma mume wangu na kugundua hawezi kujivunjia heshima yake kwa kutembea na mfanyakazi wetu, ila siku ikitokea ndiyo nitajua cha kufanya.
TQ: Kuna haka kaskendo ka’ mastaa wengi kujihusisha na usagaji? Wewe umeshawahi kushiriki kwa namna yoyote?
Mai: Huo ni uchafu, anayefanya hivyo maisha yamemshinda, hutasikia hata siku moja mimi nimefanya ujinga huo.
TQ: Inadaiwa wewe kwa kuchepuka ni noma na una kidumu chako (mwanaume wa pembeni), taarifa hizi zina ukweli wowote?
Mai: Heshima niliyonayo kwa kuitwa mke wa mtu siwezi kuitia doa, najiheshimu sana kuliko watu wanavyofikiria. Huwezi kuamini mimi nawashangaa sana wanaochepuka. TQ: Kabla ya ndoa umewahi kutoka na wanaume wangapi?
Mai: Kiukweli idadi ipo ila sipendi kuitaja kwa kuwa nahisi nitamkwaza mume wangu .
TQ: Kuna madai kuwa shepu uliyonayo Mchina anahusika sana, hebu funguka.
Mai: Hayo ni mambo yangu binafsi sipendi kuyaongelea bwana, kila mmoja ana maisha yake aliyoyachagua.

UCHAGUZI MKUU 2015 WASANII BONGO WANAUZUNGUMZIAJE?
Laurent Samatta
Habari ya mjini kwa sasa ni Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unaotarajiwa kufanyika Oktoba, 2015 ambapo Watanzania wote watatumia haki yao ya msingi ya kupiga kura, kuwachagua viongozi wanaowataka.
Showbiz Plus imewatafuta wasanii wa tasnia tofauti Bongo na kuwauliza mtazamo wao juu ya uchaguzi huo na hali ya upepo wa kisiasa Bongo ambapo wamefunguka kama ifuatavyo:
MRISHO MPOTO ‘MJOMBA’
Mkali huyu wa kughani na tungo za Kiswahili, yeye amefunguka:
“Kwanza kabisa uchaguzi umegawanyika sehemu mbili, kuna viongozi ambao wanahitaji madaraka na kuna wengine wanahitaji kufanya biashara.
“Vilevile hata wapiga kura nao wapo wanaojiandaa kufanya biashara kwa kujua kwamba wakimpigia kura kiongozi fulani, watanufaika na kitu fulani, tofauti na zamani ambapo utii na nidhamu kwa viongozi na wapiga kura ulikuwa mkubwa.“Sasa hivi hata wasanii nao wanafanya biashara kwa kutazama mgombea gani ana fedha ndiyo wanaenda kumfanyia kampeni, kwa hali hii tutegemee kuwa uchaguzi utakuwa wa kibiashara na si kutafuta kiongozi bora kwa taifa.”
EMMANUEL ELIBARIKI ‘NAY WA MITEGO’
Msanii huyu wa Bongo Fleva ameeleza mtazamo wake kuelekea uchaguzi mkuu:
“Uchaguzi wa mwaka huu unaweza kuwa mgumu sana kwa sababu watu wameelimika tofauti na zamani ambapo watu walikuwa wanafanya mambo bila kujielewa. Vijana na watu wengine wameelimika na kujua kiongozi gani anafaa na nani hafai.“Ule ujanja wa kusema baadhi ya vyama vitaiba kura nadhani hilo litakuwa gumu sana mwaka huu kwani kila mtu anapiga kura akiwa anajua haki zake za msingi.”
KHADIJA KOPA ‘MALKIA’
Malkia huyu wa mipasho, ambaye pia ana uelewa mkubwa kwenye mambo yanayohusu siasa alisema: “Kwa kweli mi naona mwaka huu utakuwa mzuri kwa upande wa wanawake kwa sababu katiba inayopendekezwa ikipitishwa kutakuwa na usawa katika kila nafasi ya uongozi kati ya wanaume na wanawake.
BABY MADAHA.
“Nawasihi wanawake kama wapo wanaoweza kuongoza nafasi mbalimbali wajitokeze kupigania nafasi hizo kuanzia urais, ubunge mpaka udiwani. Naamini tutaweza kufika mahali ambapo na sisi tutajivunia kuwa na viongozi wengi wanawake.”
KULWA KIKUMBA ‘DUDE’
Msanii huyu wa filamu alisema “Mtazamo wangu kwa kweli mi naona uchanguzi wa mwaka huu utakuwa mgumu kuliko changuzi zote zilizowahi kutokea ndani ya taifa hili, kwa sababu watu wengi wameamka na wanajua nini wanafanya.
“Lakini pia wananchi wanaanza kuwakataa baadhi ya vigogo wanaokuja mtaani kwa mbwembwe na baada ya kupata kile wanachokitaka wanakimbia na kujali maslahi yao binafsi, kwa hali hii baadhi ya vigogo wataanguka sana kwenye nafasi zao, tumeona kwenye Serikali za Mitaa mambo yalivyokuwa, tusubiri lakini uchanguzi utakuwa mgumu sana, vijana wengi walikuwa hawapigi kura lakini sasa wamejua maana halisi ya kura zao”.
AMINI MWINYIMKUU
Msanii huyu wa muziki wa Bongo Fleva naye alifunguka: “Uchaguzi wa mwaka huu mimi naona utakuwa mzuri kwa sababu kila chama kina mashabiki na wapenzi wake na kikubwa ambacho kinaonekana ni kwamba wananchi wengi wameelewa nini maana ya kupiga kura kwa lengo la kupata viongozi ambao wataleta maendeleo ndani ya taifa letu.”
EMmANUEL ELIBARIKI ‘NAY WA MITEGO’.
AMRI ATHUMANI ‘KING MAJUTO’
Mkali huyu wa komedi Bongo, naye alikuwa na mawazo yake: “Mwaka huu uchaguzi utakuwa wa raha na starehe maana tunahitaji kiongozi bora na kama inavyojulikana kwamba CCM ni chama kizuri hivyo kila kitu kitakuwa sawa na watu watafurahi, nadhani kila jambo halitakuwa gumu katika kufanikisha hili kuanzia ngazi ya urais, ubunge na hata udiwani.
BABY MADAHA
Mwanadada huyu anayefanya poa kwenye gemu la Bongo Fleva, alifunguka: “Naamini kuwa katika uchaguzi wa mwaka huu bado nafasi ya wanawake kwenye urais itakuwa ni ndogo lakini kwa upande wa nafasi za ubunge na udiwani wanaweza kufanya vizuri zaidi na watu wakashangaa kuona viti vingi vikichukuliwa na wanawake wenye kiu ya kuleta maendeleo ndani ya taifa letu. Mi naamini wanawake tunaweza.” EMMA-NUEL SIMWINGA ‘IZZO BUSINESS’
Mkali huyu wa Bongo Fleva kutoka Nyanda za Juu Kusini, mkoani Mbeya, naye amefungukia uchaguzi mkuu kwa kueleza kuwa anaamini uchaguzi wa mwaka huu utakuwa wa amani na utulivu.
“Kuhusu mambo mengine kama vurugu na machafuko, hivyo havina nafasi kabisa,” alisema.

Thursday, February 26, 2015
MAMA DIAMOND AREJEA KUTOKA INDIA, YUPO FITI
Mbongo-Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa na mama yake Sanura Kassim.
MUSA MATEJA/Amani
HAKUNA neno linaloweza kusemwa kwa mara nyingine zaidi ya Mungu ni mwema! Kauli hiyo inakuja kwa mara nyingine baada ya mama mzazi wa Mbongo-Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Sanura Kassim a.k.a Sandra kurejea nchini akiwa yupo fiti.
Habari rasmi kutoka chanzo cha kuaminika zinaeleza kwamba, mama mzazi wa Diamond amerejea nchini wikiendi iliyopita huku hali yake ikionekana kuimarika vizuri tofauti na mwanzo ambapo alirejeshwa nchini akiwa hoi kufuatia kushambuliwa na ugonjwa wa kupooza mkono na mguu.
“Kwa taarifa yenu mama Diamond amerudi yupo nyumbani kwake, Sinza-Mori (Dar).
“Cha msingi anamshukuru Mungu kurejea kwa afya yake ambapo kwa sasa yupo fiti, kaondokana na tatizo la kupooza, kwa sasa anaweza kutembea na kushika chochote kwenye mkono.
“Nimefurahi sana kumuona kwenye hali hiyo maana sasa hata unapoongea naye mwenyewe unajisikia faraja kwani ana amani moyoni mwake, ingawa bado anamalizia kutumia dozi na mara kadhaa dawa anazokunywa zinamfanya kupitiwa na usingizi sana, ila kwa hali yake sasa hakuna ubishi tena amepona na familia ina amani kwa jumla,” kilisema chanzo chetu kinachomtembelea mama Diamond nyumbani mara kwa mara. Jirani wa mama huyo ambaye hakupenda jina lake kuandikwa alisema kitendo cha mama Diamond kurejea akiwa na afya njema kimemfurahisha sana.

DADA WA AFANDE SELE AFIA GESTI
Dustan Shekidele, Morogoro
DADA wa msanii mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva, Seleman Msindi ‘Afande Sele’ Zaria Kambi (30) ambaye alikuwa ni mhudumu wa baa, amekutwa ameuawa kikatili katika Gesti ya Stavi (Gesti ya Marafiki) iliyopo Kichangani, mjini Morogoro.
Dada wa msanii mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva, Seleman Msindi ‘Afande Sele’ Zaria Kambi.
Tukio hilo la kinyama lilitokea usiku wa Jumapili iliyopita baada ya marehemu kuwa amekubaliana kulala pamoja na mteja aliyekuwa akimhudumia kinywaji, ambaye pia alikuwa amechukua chumba katika nyumba hiyo hiyo iliyokuwa na baa.
Kwa mujibu wa rafiki wa marehemu, ambaye pia alikuwa ni mhudumu wa gesti hiyo, Rehema Saleh, alisema mtu mmoja asiyefahamika, alifika kazini kwao na kupanga chumba namba 8A na baadaye alienda upande wa baa kunywa pombe akihudumiwa na Zaria.
“Mimi na Zaria (pichani) tunaishi jirani, sasa baada ya kumhudumia na yeye kununuliwa pombe, wakakubaliana walale pamoja, tunaishi jirani hivyo kila siku baa ikifungwa tunaongozana na jana tuliongozana njiani aliniambia amepata kichwa hivyo anakwenda nyumbani kuaga na baadaye arejee kwa bwa’nake huyo ambaye ni mara ya kwanza anaonana naye,” alisema Rehema na kuongeza.
“Cha ajabu saa 8 usiku napigiwa simu na mlinzi akidai Zaria amenyongwa na mteja wake, sikuwa na jinsi, kulipokucha nilifika hapa gesti na kukuta mwili wa marehemu ukiwa akitandani,” alisema na kuangua kilio.
Chumba cha Gest alichokutwa amekufa Zaria Kambi.
Mlinzi wa gesti hiyo, John Emmanuel akizungumzia tukio hilo, alisema majira ya saa 6 usiku Zaria aliingia katika chumba namba 8A na saa moja baadaye, akasikia kelele zikitoka chumbani humo, ambazo alihisi ni za kimapenzi.
“Sijakaa vizuri saa 8 usiku jamaa alitoka na begi lake akitaka nimfungulie aondoke huku mkononi akiwa na tiketi ya basi kuelekea Mbeya, nikamwambia kwanza twende chumbani kwake nikachunguze ndipo nimruhusu atoke, awali aligoma na mimi nikagoma kumfungulia geti, tukaganda kama dakika mbili akakubali kwenda chumbani tulipofika tukamkuta Zaria amekufa huku akiwa mtupu, nikamjulisha bosi Pascal Mafikiri ambaye aliita polisi wakamchukua mtuhumiwa na mwili wa Zaria,” alisema.
Mama mzazi wa marehemu, Mwajuma Hassani Kambi ambaye ni Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Mwande Kata ya Kichangani kwa tiketi ya Chadema alipokea taarifa za kifo cha mwanaye Jumapili usiku.
Alisema mwanaye ameacha mtoto anayeitwa Rashid lsmail Kaliembe ambaye anasumbuliwa na uvimbe tumboni na kwamba kila mwezi alikuwa akipelekwa Muhimbili kwa matibabu. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Leonard Paulo alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba mtuhumiwa, Erick Bruno, ambaye ni mkazi wa Manzese Tip Top Dar es Salaam, anashikiliwa. Marehemu huyo alizikwa Jumanne iliyopita mjini Morogoro.

Wednesday, February 25, 2015
THEA: NIMEEPUKA MAJUNGU!
Gladness Mallya/Mchanganyiko
MSANII mkongwe katika filamu Bongo, Salome Urassa ‘Thea’ amefunguka na kusema kwamba kwa sasa amebadili aina ya maisha yake kwa kuwaepuka marafiki wanafiki aliokuwa akikutana nao kwenye makundi ya majungu.
Msanii mkongwe katika filamu Bongo, Salome Urassa ‘Thea’.
Akipiga stori mbili tatu na gazeti hili hivi karibuni, Thea alisema siku hizi hata akienda location anafanya kile kilichompeleka na baada ya hapo anarudi nyumbani mapema ili kumuwahi mumewe. “Siku hizi nikienda location nafanya kilichonipeleka, nabadilisha nguo narudi nyumbani kwangu maana sipendi sana kukaa kwenye vikao yaani makundi maana ndiyo mwanzo wa manenomaneno na majungu hivyo nayaepuka, kwani hayanisaidii pia nimepunguza marafiki maana mimi ni mke wa mtu,” alisema Thea.

MONALISA, BANANA WAPATA AJALI KAZINI
HAMIDA HASSAN/Mchanganyiko
MASTAA wa filamu ya Daddy’s Wedding, Yvone Sheryl ‘Monalisa’, Banana Zoro, Sandra, Mama Abdul na wenzao hivi karibuni walipata ajali walipokuwa kwenye maandalizi ya filamu hiyo kwenye mbuga ya Saadani.
Staa wa filamu ya Daddy’s Wedding, Yvone Sheryl ‘Monalisa’.
Ajali hiyo ilitokea katika daraja moja dogo mbugani hapo ambapo walikusanyika kwa ajili ya kushuti mojawapo ya vipande vya filamu hiyo mpya, lakini likaporomoka na kuwafanya baadhi yao kuumia na wengine kupata mshtuko mkubwa.
Banana Zoro. “Aliyeumia zaidi ni Sandra lakini alipewa matibabu ya haraka na kuruhusiwa, ila tunamshukuru Mungu tulifanikiwa kumaliza salama na hatukudaiwa chochote,” alisema na kumtaja pia Jenerali Ulimwengu kuwa mmoja kati ya waigizaji walio ndani ya filamu hiyo.

WASTARA AZIMIA KISA MAPENZI
Waandishi wetu/Mchanganyiko
DIVA wa filamu nchini, Wastara Juma ambaye kwa sasa anaripotiwa kuwa katika mapenzi na mwigizaji mwenzake, Bond Bin Suleiman anadaiwa kupoteza fahamu mara tu baada ya kupewa taarifa kuwa mpenziwe huyo amepata mtoto wa nne kwa mwanamke mwingine, Risasi Mchanganyiko linakupa stori kamili.
DIVA wa filamu nchini, Wastara Juma akiwa hospitali baada ya kuzimia.
TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo makini, Wastara alipenyezewa ubuyu na mpenzi wa zamani wa Bond, Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’ na kuambiwa kwamba asijishebedue kwani Bond ana mwanamke mwingine ambaye amejifungua mtoto wa nne hivi karibuni.
“Tunakushangaa unavyojinadi kuwa Bond ni wako na kumpa zawadi ya keki ya bethidei wakati mwenzako amezaa na mwanamke mmoja baamedi hivi karibuni. Tena si kwamba mtoto huyo ni wa kwanza, ni wa nne,” kilisema chanzo hicho kikimnukuu Aunty.
ALIVYOZIMIA
Chanzo hicho kifunguka kuwa, baada ya kupewa taarifa hizo na Aunty Lulu, alizimia ghafla na kulazwa hospitali.“Wastara alizimia punde tu baada ya kupewa taarifa hizo, nasikia walimkimbiza hospitali, akapewa huduma nasikia kidogo sasa hajambo. Ishu ilikuwa mbaya, Aunty Lulu alimmchana laivu.”
Wastara Juma akiwa na Bond Bin Suleiman.
AUNTY LULU ANASEMAJE?
Risasi Mchanganyiko lilimtafuta Aunty Lulu ambaye hapo awali alikuwa akilalamikia penzi la kitumwa la kupigwa mara kwa mara na Bond na hata kufikia mahali na kushukuru Mungu kwa kutengana kwao na kumuuliza kama habari hizo zilikuwa na ukweli wowote.
“Ni kweli nilimwambia kila kitu Wastara na tulikuwa tumepanga kwenda kumuona mtoto aliyezaliwa ili kujua kama kweli ni wa Bond.“Mimi niliamua kufunguka baada ya Bond kunitukana na kunitolea maneno mazito, kwani nilichoka, kama amepata presha na kulazwa hilo mimi silijui,” alisema Aunty Lulu.
TUJIUNGE NA WASTARA
Kwa upande wake, Wastara naye alikiri kupoteza fahamu na kulazwa hospitalini, lakini akakataa mambo hayo kumtokea kwa sababu ya kusikia taarifa hizo, bali kutokana na kuzidiwa na malaria.
“Nimepata nafuu na nimeshatoka hospitali, nilikuwa nimepatwa na homa kali ya malaria, madaktari waliniambia nilikuwa na malaria 10, kwa muda wa wiki mbili nilikuwa naumwa, lakini nikazidiwa kidogo, hivi sasa niko sawa na hapa ndiyo nashuka uwanja wa ndege natokea Mwanza,” alisema.
AMEKWEPA VIUNZI?
Mwanahabari wetu alipombana zaidi Wastara kutaka kujua kuzimia kwake kama kulitokana na kupata habari za Bond kuwa na watoto wanne, alisema siyo kweli kwani asingeweza kushangazwa na jambo hilo hasa kwa vile Bond ni mwanaume lijali na pia ana maisha yake ambayo hayamhusu. “Mimi nina maisha yangu, yeye ana maisha yake, sasa jamani mimi nitapatwaje na presha kwa mambo hayo? Labda nikuambie tu kuwa hakuna lolote linaloendelea kati yangu na yeye zaidi ya masuala ya kikazi tu. Ninaomba uelewe hivyo kwa sababu huo ndiyo ukweli,” alisema.

Tuesday, February 24, 2015
IYOBO ASHIKWA NA KIGUGUMIZI KUHUSU MUME WA AUNT
Chande Abdallah/Uwazi
DANSA wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Mose Iyobo ambaye anatajwa kuwa mpenzi wa msanii wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel ameshikwa na kigugumizi kuhusu tuhuma za kumpachika mimba Aunt ambaye ni mke wa mtu.
Dansa wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Mose Iyobo akiwa na Aunt Ezekiel.
Mose alionesha kigugumizi hicho baada ya kutaitiwa na paparazi wetu akiulizwa anajisikiaje kumpachika mimba mke wa mtu na vipi kama mume wa Aunt anayedaiwa kufungwa huko Dubai ataachiwa huru na kurudi.“Aaahhaa.. Mhh..Hayoo ni ya Aunt mwenyewe mimi hayanihusu,” alisema Mose kisha kimya kirefu kikafuatia kabla ya kuikata simu yake.

Monday, February 23, 2015
MAMA WA MTOTO ALBINO ALIYEUAWA AMLIZA JB
Mwandishi wetu, mwanza/Ijumaa wikienda
Hali si shwari hata kidogo! Wikiendi iliyopita staa wa sinema za Kibongo, Jacob Steven ‘JB’ alijikuta akiangua kilio na kuungwa mkono na mastaa wenzake, Amri Athumani ‘Mzee Majuto’ na Single Mtambalike ‘Richie’ walipomtembelea wodini mama mzazi wa mtoto Albino, Yohana Bahati (1) aliyeuawa kikatili, Ester Thomas (30) ambaye naye alijeruhiwa vibaya kichwani, Ijumaa Wikienda linakuhabarisha.
Staa wa sinema za Kibongo, Jacob Steven ‘JB’ akiwa na Amri Athumani ‘Mzee Majuto’walipomtembelea wodini mama mzazi wa mtoto Albino, Yohana Bahati (1) aliyeuawa kikatili, Ester Thomas.
Tukio hilo la majonzi lilijiri kwenye Hospitali ya Bugando mkoani hapa ambapo wasanii hao walikwenda kumfariji mama wa mtoto huyo aliyetekwa mjini Geita hivi karibuni.
Walipofika wodini hapo, JB na wenzake walitoa yao ya moyoni kupinga vikali ukatili aliotendewa mama huyo na mwanaye huku wakitahadharisha juu ya laana inayoweza kuikumba jamii yetu kwa tukio hilo.
JB: Nampa pole sana mama Yohana. Hii ni aibu kubwa kwa taifa letu na jamii pana duniani.
Watu hawafanyi kazi kujipatia kipato halali. Mafisadi wanataka kujipatia fedha kupitia njia za kishetani za kuwaua wenzetu. Albino ni wenzetu na tunawapenda. Lazima wahalifu wakamatwe na wahukumiwe kunyongwa.
Mzee Majuto: Inasikitisha sana. Haivumiliki. Albino ni wenzetu na wana uwezo mkubwa wa kulisaidia taifa letu. Wahusila lazima wakamatwe na tuone wakichukuliwa hatua kali.
Richie: Natokwa na machozi. Hiki ni nini? Hatuwezi kufumbia macho jambo hili hasa sisi wenye nafasi kubwa ya kukemea vitendo hivi.
Single Mtambalike ‘Richie’ nae akimjulia hali mama huyo.
Mara baada ya mastaa hao kutoa la moyoni katika wodi aliyolazwa mama huyo, iligeuka kama msiba kwani kila aliyekuwepo alikuwa akiangua kilio kwa uchungu.
Tayari mtoto Bahati amezikwa baada ya mwili wake kupatikana ukiwa hauna baadhi ya viungo huku mama yake akiendelea na matibabu baada ya kufanyiwa oparesheni sehemu ya kichwani aliyojeruhiwa vibaya wakati akinyang’anywa mwanaye. KUTOKA KWA MHARIRI
Global Publishers tunaungana na dunia nzima kukemea vikali mauaji ya Albino ambayo rekodi inaonesha hutokea wakati wa uchaguzi mkuu hivyo tunavitaka vyombo husika kufanya kazi yake ili kuliondolea taifa aibu hii nzito.

Saturday, February 21, 2015
JB: RAIS KIKWETE TUTAKUFA MASKINI!
Laurent Samatta/Risasi
NGULI wa filamu za Kibongo, Jacob Steven ‘JB’, amesema kuwa pamoja na kuendelea kulia juu ya kuibiwa kazi zao, anamkumbusha Rais Jakaya Kikwete kutimiza ahadi yake aliyowahi kusema kwenye msiba wa nguli wa filamu, Steven Kanumba kuwa atawashungulikia wale wote wanaoiba kazi za wasanii na kutoa kopi.
Nguli wa filamu za Kibongo, Jacob Steven ‘JB’.
JB alitoa ombi kwa uchungu ambapo alifunguka kuwa pamoja na kuwepo kwa wasambazaji lakini bado wasanii wamekuwa wakilia kila siku hasa pale wanapopeleka filamu zao sokoni. “Rais wetu alitoa kauli kuwa anawashungulikia wale wote wanaohusika na wizi wa kazi zetu, lakini hadi leo bado hajatekeleza hilo, lakini hatuwezi kushindwa kusema kuwa tunaumia sana, tunaomba atusaidie,” alisema JB.

MISS DODOMA AOKOKA
Stori: Shani ramadhani
Aliyekuwa Miss Dodoma mwaka 2005, Eva Evans amemrudia Mungu kwa maana ya kuokoka kwa kile alichodai kutotimia kwa malengo aliyojiwekea.Akizungumza na mwanahabari wetu, Eva alisema tangu akiwa mdogo, alijiwekea kiapo kuwa endapo atashindwa kumpata mume mwema, basi atafanya kazi ya kumtumikia Mungu.
Aliyekuwa Miss Dodoma mwaka 2005, Eva Evans akiwa kanisani.
“Nakumbuka mapito yangu yote tangu nikiwa mdogo mpaka nikaingia kwenye masuala ya urembo nilijiwekea nadhiri ikifika muda mambo yangu hayajakamilika, itanibidi nimrudie Mungu wangu.
“Baada ya kupitia urembo nilichumbiwa, hapohapo nikaanza kuhudhuria mikutano mbalimbali ya neno la Mungu, siku moja Nabii akitoa neno, nilimsikia akisema kuna binti mmoja hapa anataka kuolewa apite mbele haraka sana, basi nikapita mbele na nilipofika pale alianza kuniombea na baadaye alianza kuniuliza maswali.
“Akaniambia mwanaume anayetaka kunioa hana sifa za kuwa mume bora na kama nabisha nimchunguze, basi nikamchunguza na kugundua kuwa hakuwa na sifa.“Basi nilivyojua tu nikaamua nisitishe mipango ya ndoa zikiwa zimesalia wiki mbili tu ili ndoa ifungwe, nashukuru Mungu nilieleweka, na kuanzia hapo nikaamua kuokoka kabisa, ninaomba sana Mwenyezi Mungu aniletee mume mwema,” alisema mrembo huyo. Eva alifunguka kuwa katika mashindano ya urembo kuna uchafu mwingi hivyo akawashauri wasichana walioko huko kumrudia Mungu.

JINI KABULA ALIA NA CD ZA ‘MAGAIDI’
Stori: Gladness mallya
MSANII wa filamu Bongo, Miriamu Jolwa ‘Jini Kabula’ amefunguka kwamba anateseka na viashirio vya vita hasa baada ya CD zilizosambazwa na watu wasiojulikana wanaosema ni magaidi kudai kuwepo kwa vita nchini.
Msanii wa filamu Bongo, Miriamu Jolwa ‘Jini Kabula’.
Akipiga stori na gazeti hili, Jini Kabula alisema amekuwa akikesha akimuomba Mungu ailinde nchi ya Tanzania na aiepushe na vita kwani tangu amezaliwa mpaka alipofikia amekuzwa na amani na anajivunia kuwa Mtanzania na anafurahi hivyo Watanzania wote wanatakiwa kudumu katika maombi ili damu isimwagike kama hao magaidi wasiotakia mema nchi wanavyoahidi. “Namuomba Mungu usiku na mchana vita isitokee maana tumezoea amani sasa ikitokea ukweli sijui tutafanyaje na tutakimbilia wapi hivyo ni jukumu la kila Mtanzania kumuomba Mungu atuepushe na janga hilo,” alisema Jini Kabula.

GLOBAL WALIVYOFANYA MAHOJIANO NA ODAMA KUJUA KUCHANGIA WANAUME
MAMBO yanazidi kunoga ndani ya safu hii ya Sindano 5 za moto, kutokana na maombi yenu, leo tumemleta kwenu mwigizaji Jeniffer Kyaka ‘Odama’, tiririka naye:
Staa katika tasnia ya filamu Bongo, Jeniffer Kyaka ‘Odama’.
Paparazi: Mambo vipi Odama! Tuanze moja kwa moja na swali la kwanza, hivi kwa sasa una mpenzi? Mbona hatumjui?
Odama: Mambo poa! Mpenzi ninaye, nampenda muda bado wa kumuanika.
Paparazi: Ulishawahi kuchangia bwana na mwanamke mwingine katika maisha yako?
Odama: Hapana, sina kumbukumbu hiyo.
Paparazi: Hadi leo hii unaweza kukumbuka idadi ya wanaume ambao umewahi kutoka nao kimapenzi?
Odama: Nakumbuka, kama mtu hukumbuki idadi basi lazima utakuwa una kichaa. Nakumbuka kwa sababu idadi ni ndogo, ila hapa sitataja idadi yao.
Paparazi: Hivi baba mtoto wako ni nani hasa au ndiye uliyenaye hadi sasa?
Odama: Hilo liweke kapuni kwa sasa, nitalizungumza ‘next time’.Paparazi: Inasemekana wewe ni miongoni mwa warembo ambao wanaoongoza kwa kutongozwa Bongo Movies, ni kweli?
Odama: Hiyo kawaida kwa mtoto wa kike, nadhani sipo peke yangu.

Friday, February 20, 2015
MSANII WA BONGO FLEVA MEZ B AFARIKI
MSANII wa muziki wa Bongo Fleva aliyekuwa akiwika na kundi la Chamber Squad, Moses Bushagama ‘Mez B’ amefariki dunia asubuhi ya leo majira ya saa 4:30 mjini Dodoma.
Mez B akiwa katika moja ya mahojiano yake na kituo cha TV.
Hii imekuwa ni pigo la pili kwa kundi la Chamber Squad kupoteza memba wake baada ya awali kumpoteza Albert Mangweha ‘Ngwear’.Katika makala haya yanauelezea undani wa Mez B mpaka kufikia umauti.
MEZ B NI NANI?
Mez B amekulia mjini Dodoma maeneo ya Area C. Akiwa anasoma katika Shule ya Sekondari ya Mazengo, Dodoma ndipo alipokutana na wenzake Noorah, Ngwear pamoja na Dark Master.
Kwa mara ya kwanza walipokutana shuleni hapo, walianzisha kundi la CFG yaani Chemba Fleva Guys lililokuwa likiundwa na Ngwear, Mez B pamoja na Nzeku.
Walipomaliza shule, wakaamua waendeleze kundi na kubadilisha jina na kujiita Chamber Squad.
Awali Chamber Squad ilianzishwa na Tino Mkale, Mgulu George na wengine kibao ambao hawakuwa na majina kabla ya kuliacha kundi hilo likimilikiwa na Ngwear, Noorah, Mez B na Dark Master.
Rehema Chalamila (picha ya chini) ambaye ni mmoja ya mastaa waliowahi kushirikisha na Mez B katika Wimbo wa Basi Kama Vipi.
AANZA KUNG’ARA
Mez B alianza kutambulika kama mwanamuziki wa R&B ambapo alitoka na Wimbo wa Fikiria na baadaye akawika na nyimbo kama Furaha Tele, Mama na Mwana, Nichukue pamoja na Mpenzi njoo aliyokuwa amemshirikisha Afande Sele.
Nyimbo nyingine zilizompa umaarufu ni pamoja na Kidela, Nimekubali, Shemeji, Basi Kama Vipi akiwa ameshirikiana na Ray C na Noorah.
Miongoni mwa wimbo uliopandisha kundi la Chamber Squad ni pamoja na Home Sweet Home ambao Mez B aliutendea haki kwa upande wa kiitikio.
Marehemu, Albert Mangweha 'Ngwair' enzi za uhai wake.
NGWEAR AFARIKI, MMOJA APUNGUA
Mei 28, 2013 Kundi la Chamber Squad lilipata pigo kwa kuondokea na memba wao, Albert Mangweha ‘Ngwear’ ambaye alifariki akiwa nchini Afrika Kusini alikokwenda kufanya shoo kwenye miji mbalimbali nchini humo ikiwemo Johannesburg na Cape Town.Alizikwa mkoani Morogoro, Juni 6, 2013 katika makaburi ya Kihonda.
Baada ya hapo kundi la Chamber Squad lilibakiwa na vichwa vitatu ambavyo ni Noorah, Mez B pamoja na Dark Master.
Memba mwenzao, Dark Master alishawahi kusema kuwa kundi hilo bado lipo na walikuwa njiani kuja na nyimbo mfululizo.
Mez B akiwa na majeraha baada ya kujerehuliwa na mtu asiyejulikana.
ASHAMBULIWA, ATAKA KUULIWA
Zikiwa zimepita wiki chache tangu Mez B ampoteze memba mwenzake, Ngwear alipata balaa la kushambuliwa na mtu asiyemfahamu akiwa sehemu ya burudani maeneo ya Sinza, jijini Dar.
Usiku huo Mez B alikuwa ameenda kutafuta chakula (Chips) na kushuhudia mtu mmoja akiamuliwa na mabaunsa achomwe visu.
Tukio hilo lilianzia pale Mez B alipofika eneo hilo ambalo alishangaa mtu mmoja akiitusi serikali pamoja na Mez B mwenyewe hali iliyozua tafrani.Kitendo cha Mez B kuondoka, baunsa mmoja alimfuata mtu aliyekuwa akitukana na kumuamuru amchome visu Mez B. Ujasiri ulimsaidia Mez B kwani alikuwa achomwe shindoni lakini alikwepa na kuchoma baadhi ya maeneo ya usoni.
Suala hilo alilipeleka mbele ya vyombo vya sheria ambapo bado kesi ilikuwa ikiendelea.
Picha aliyopiga Mez B na wasichana wawili katika Fukwe za Mikadi, jijini Dar.
AFUMWA AKIJIACHIA NA WASICHANA UFUKWENI
Septemba mwaka jana, Mez B alilingia katika msala wa kukutwa katika Fukwe za Mikadi, jijini Dar akiwa na wasichana ambao walionekana wakiwa watupu.
Moja ya magazeti pendwa, yalichapisha habari hiyo ambayo picha zilimuonyesha Mez B akiwakumbatia huku wasichana hao wakionekana watupu kama walivyozaliwa.
Wasichana hao waliotambulika kama Vicky na Rebecca walikuja kubainika kuwa siyo raia wa Tanzania na kudaiwa kuwa Mez B alikuwa akitengeneza video ya wimbo mpya na wasichana hao waliomba kupiga picha naye tu baada ya kumuona.
Marehemu, Mez B akiwa studio enzi za uhai wake.
AANZA KUUGUA
Februari mwaka huu, Mez B alianza kuugua na kulazwa katika hospitali moja mkoani Dodoma akiwa anasumbuliwa na maumivu ya kichwa na shingo hali iliyomfanya awe chini ya uangalizi wa madaktari.
Kauli yake ya mwisho baada ya kuugua ilikuwa ni kuomba msamaha kwa mashabiki kwa kuchelewa kuanza ‘projekti’ mpya kutokana na hali iliyokuwa ikimkabili.
“Bado nasumbuliwa na Pneunomia tangu mwezi wa 12 mwaka jana lakini kwa sasa naendelea vizuri na matibabu na nategemea kuruhusiwa muda wowote. Nikitoka nitaendelea na projekti yangu,” alisema Mez B.
AFARIKI DUNIA
Mez B amefariki dunia saa 4:30 asubuhi katika Hospitali ya Mwananchi mjini Dodoma ambapo alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa Homa ya Mapafu ambao kitaalamu unajulikana kama Pneunomia.
Taratibu juu ya mazishi bado hazijafanyika na tutaendelea kukujuza zaidi.
Uongozi na wafanyakazi wa Global Publishers unatoa pole kwa ndugu na wana familia wa Mez B kwa msiba uliotokea.Bwana ametoa na Bwana ametwaa, jina la Bwana lihimidiwe Amen.

TOP 10 YA WAIGIZAJI WA KIKE WENYE MVUTO AFRIKA!
Stori: Amran Kaima na Mtandao Tasnia ya filamu Afrika inakuwa kila siku kiasi kwamba zile ndoto za kufanya kama wenzetu wa Hollywood (Marekani) na Bollywood (India) huenda siku moja zikatimia.Kama ilivyo Hollywood na kwingine kwenye waigizaji wa kike wenye mvuto, wapo pia waigizaji wa kike Afrika ambao ni ‘visu’.Leo hii ikihitajika Top 10, kila mmoja atakuwa na yake lakini mtandao wa umefanya kazi ya kuorodhesha waigizaji 10 wa kike wenye mvuto kama ifuatavyo;
10. Elizabeth Michael ‘Lulu’
Binti huyu ana umri wa miaka 21 lakini ni mrembo na anayejiamini. Ni binti kutoka Tanzania mwenye kipaji cha kuigiza kiasi cha kuwa tishio kwa wakongwe. Ni kweli huwa anatumia ‘make up’ lakini hata akiwa hajatumia wala kuvaa ‘mawig’, bado anaonekana ni mwenye kuvutia.
9. Omotola Jalade Ekeinde
Ni mmoja wa mastaa wa kike nchini Nigeria mwenye mvuto wa aina yake. Kwa sasa ana umri wa miaka 37 na watoto wanne lakini bado anaonekana mrembo kiasi cha baadhi ya mashabiki wake kumuita Omosexy.Kutokana na kipaji alicho nacho, amejikuta akiwa na mashabiki wengi katika Bara la Africa na kwingineko duniani. Mbali na uigizaji pia ni mwanamitindo na mwananamuziki.
8. Chinyere Yvone Okoro
Huyu ni muigizaji anayetokea nchini Ghana. Katika orodha ya waigizaji wa kike waliomo nchini humo, mrembo huyu amebaki kuwa tishio na imemfanya kuingia katika orodha hii ya wasanii wa kike wakali Afrika.
7. Jackline Wolper
Huyu ni muigizaji kutoka Tanzania mwenye mvuto wa aina yake. Kwa mujibu wa maelezo yake, uzuri alionao unatokana na mfumo mzuri wa kula aliojiwekea. Anakula sana mbogamboga, matunda na maji mengi, hali inayomfanya autunze urembo alionao.
6. Genevieve Nnaji
Ana umri wa miaka 36, anatokea Nigeria. Mwanadada huyu anatajwa kuwa na mvuto wa aina yake kiasi cha kupata usumbufu kutoka kwa wanaume kibao.Ameigiza filamu nyingi na zote amezitendea haki kutokana na namna anavyouvaa uhusika.
5. Jackie Appiah Agyemang
Amezaliwa miaka 32 nchini Canada lakini amekulia nchini Ghana. Ni binti mrembo na mwenye kipaji ambaye aonekanapo kwenye televisheni, huthibitisha kwamba kuna kitu cha ziada alichojaaliwa na Mungu.
4. Nadia Buari
Huyu ni msanii kutoka Ghana aliyezaliwa miaka 30 iliyopita. Licha ya umri kusogea, hachuji kwa uzuri. Amecheza filamu nyingi na kadiri siku zinavyokwenda ndivyo anavyozidi kuwa tishio kwenye tasnia ya uigizaji.
3. Ini Edo
Hivi unaanzaanzaje kumuacha mrembo huyu pale unapotaja medemu wakali kwenye tasnia ya filamu Afrika? Naamini huwezi, labda uwe na chuki zako binafsi.Ana umri wa miaka 31 na ana uzuri wa asili unaomfanya atumike kwenye filamu nyingi za Nigeria.
2. Stephanie Okereke Linus
Huyu ni binti kutoka Nigeria ambaye wengi wanamtaja kuwa muigizaji mwenye mvuto kuliko wote Afrika. Ana miaka 33, aliwahi kushiriki mashindano ya urembo nchini Nigeria na kuibuka mshindi. Kuanzia hapo amekuwa gumzo kwa uzuri wake na amekuwa akitumika sana kwenye filamu nyingi.
1.Rita Dominic
Wafuatiliaji wa filamu za Nigeria watakuwa wanamjua vizuri binti huyu. Ana miaka 40 lakini bado anadai. Kila sehemu ya mwili wake ina muonekana wa kiurembo.
Angalia midomo yake, angalia macho na ngozi yake. Hakika ni kati ya waigizaji wa kike Afrika wenye mvuto wa aina yake.

Subscribe to:
Posts (Atom)