Mtayarishaji na Muigizaji wa filamu Nice Mohamed ‘Mtunis’amesema kwamba filamu yake ya Who’s Bad itakuwa kazi yake ya kufungia
mwaka kwa kuzima kazi nyingine za filamu zilizoingia pamoja na filamu
hiyo ambayo inafanya vizuri sokoni baada ya kuingia mitaani hivi
karibuni.
“Kama ambavyo wengi wamenizoea ninapotoa kazi inakuwa ni bora na
lazima ikimbize sokoni, sinema yangu ya Who’s Bad itafunga mwaka kama
kazi bora nakuwa makini sana katika utengenezaji wa filamu na ndio
kilichofanyika katika filamu hiyo wasanii wamekamua sana na kuonyesho
uwezo wa hali ya juu,”anasema Nice.
Filamu hiyo imeshirikisha wasanii kama Patcho Mwamba na washiriki
wengine wanaofanya vizuri katika tasnia ya filamu, Mtunis amekuwa
akifanya vizuri katika tasnia ya filamu Bongo kazi alizofanya ni kama
Bar mead, Who’s Bad,Clinic Love na kusambazwa na kampuni ya Steps
Entertainment.