INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Friday, June 3, 2016

Rich Mavoko Asainishwa Rasmi Label Ya WCB

Msanii Diamond Platnumz, ameitambulisha rasmi label yake ya ‘WCB’ pamoja na kumsaini Rich Mavoko mbele ya waandishi wa habari.
Aidha, Diamond alimtambulisha dada yake, Queen Darleen kuwa mmoja kati ya wasanii wapya wa label hiyo.
Shughuli hiyo ilihudhuriwa na Katibu Mkuu wa Baraza la Sanaa Taifa, Godfrey Mngereza ambaye alizungumza na kumpongeza Diamond huku akiwataka wasanii wengine kushirikiana kwa namna hiyo.

Akiongea na waandishi wa habari katika hoteli ya Regency Park jijini Dar es salaam, Diamond amesema WCB imemsani Rich Mavoko ili kuleta chachu katika muziki.
“Nia ya kuwaita hapa ni kuonyesha kwamba wasanii tunaweza kushirikiana, tunaweza kufanya kitu kikubwa, ni muda wa kuonyesha sio ulimwengu wa vita kwa wasanii, watu wachukiane,” alisema Diamond. “Tukishirikiana wasanii kwa wasanii tutaonyesha mfano bora kwa jamii na hata mafanikio yataongezeka, kwa hiyo tuna Richard hapa na tunamshukuru sana, karibu kwenye familia,” alisema Diamond.
Kwa upande wa Rich Mavoko ameshukuru kusainiwa na WCB, huku akiwaahidi mashabiki wake mambo mazuri
“Mimi nizishukuru media zote ambazo zimefika kwenye shughuli hii maalum. Mimi nafikiri leo ni siku kubwa sana kwangu, kwa WCB pamoja na kwa tasnia ya muziki kwa ujumla. Lengo letu kubwa ni kuonyesha kwamba muziki wetu umefikia kwenye biashara kubwa sana, sisi tukionyesha umoja hata serikali itaweza kutusupport. Kwa hiyo sisi wasanii wenyewe kwa wenyewe tunabidi tuonyeshe undugu, pia serikali itaona sisi tupo serious kwenye kazi, kwa hiyo lengo la kuwa na Nasib WCB ni kufanya naye kazi, na naahidi kufanya kazi nzuri zaidi ili kufikisha muziki wetu sehemu fulani,” alisema Rich Mavoko.
Pia Katibu Mkuu wa Baraza la Sanaa Taifa (BASATA), Godfrey Mngereza ambaye alihudhuria shughuli hiyo, alimpongeza Diamond huku akiwataka na wasanii wengine kushirikiana ili kuleta chachu kwenye muziki.
“Ni vizuri sana tunapo waona wasanii watanzania wanawekeza katika industry ya muziki, kwa hatua hii inaondoa ile dhana kwamba wanaoweza kuwekeza kwenye muziki ni watu toka nje, kwa hiyo ni hatua kubwa sana, ni hatua ya msingi sana ambayo Diamond na team yake yote wameipiga katika kuonyesha dhahiri kwamba kila kitu kinawezekana,” alisema
Mavoko ambaye pia amechia wimbo uitwao ‘Story’, amesaini mkataba wa miaka 10.
Pia mmoja kati ya mameneja wa WCB, Sallam alisema mkataba huo haujamfunga Rick Mavoko kuondoka WCB, kama akihitaji kuondoka itabidi anunue mkataba huo ndipo aondeke.
Bongo5

No comments:

Post a Comment