INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Friday, June 3, 2016

Wema Alalama Kukosa Amani Sababu Ya Kuandamwa.

Msanii wa filamu na mjasiriamali Wema Sepetu amefunguka ya moyoni kutokana na namna mashabiki wake wa Instgram wanavyomchukulia na kumpa maneno ambayo muda mwingine yanamuumiza na kumkosesha amani na kumfanya ajione ni kama mkosaji mkubwa.

Wema Sepetu ameyasema hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram ha hayo yamekuja baada ya watu kuanza kusema maneno mbalimbali kwa kile alichofanya Wema Sepetu kupost picha ambayo ni promo ya kazi mpya ya msanii kutoka WCB. Baada ya kupost picha hiyo baadhi ya watu walianza kusema kuwa bidada huyo anatafuta kiki, wengine wakisema kuwa Wema Sepetu kwa Diamond Platnum apindui.
“Kitu ambacho nakiona kutoka Instagram, Watu wanapenda sana fujo fujo, Purukushani, mara huyu na huyu hawaongei, flani kamchukulia flani bwana, yule kafumaniwa. Hicho ndiyo mnachokiona kina kick. Ila mwisho wa siku ukija kuangalia , ni kweli maana dunia ya leo umbea unauza. Ila jamani ifike muda tukue mimi binafsi kuna vitu vinanichosha actually vimenichosha ifike muda kila mtu aangalie maisha yake na afanye kile kinachomridhisha nafsi yake. kwangu naangalia wat God has to say bout wat im doin… Imekuwa too much tokea nilivyopost uzalendo ikaonekana all sorts of Crazy, But u know wat, I dont care” aliandika Wema Sepetu
“Sasa basi, nitapost ninachotaka nyinyi endeleeni kujudge na kuleta conclusion zenu mnazojua… Iwe nataka attention, iwe natafuta kick, iwe nitokeje, iwe najipendekeza, iwe vyovyote It all comes down to me. Kuna msemo unasemaga tenda Wema uende zako… Dats how I roll. Na nimekuwa nikifanya hivyo siku zote. Sitegemei na wala sitaki mtu ninae msupport au kumuunga mkono na yeye afanye the same na wala sina haja na kupostiwa. Niwe sipindui au napindua It doesnt make A difference. Kwanza haya mambo ya kupinduana yameanzaga lini Mungu wangu. Ila instagram mna majungu sana. Mimi siwezi jamani mniachage basi sometimes, sina amani imekuwa kama nimeua” aliongeza Wema Sepetu
eatv.tv

No comments:

Post a Comment