INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Friday, August 21, 2015

Wizi Wa Kazi Za Wasanii Utaendelea Nchini Kwa Kuwa Hakuna Sheria: Ernest Napoleon

MSHINDI wa tuzo ya East Afrika kupitia filamu yake ya ‘Going Bongo’, Ernest Napoleon, ameweka wazi kwamba haiwezekani kuzuia uharamia wa kazi za wasanii kwa kuwa hatuna sheria ya kufanya hivyo.
Napoleon alisema kuzuia uharamia wa kazi za wasanii kwa Tanzania itaendelea kuleta vilio kwa wasanii wake hadi mifumo itakaporekebishwa na sheria zikatungwa.

“Huo ndio ukweli wala tusidanganyane, hatuwezi kuzuia uharamia wa kazi za wasanii kwa kuwa hakuna sheria za kuzuia uharamia huo hivyo kila mtu anayeingiza fedha kwa wizi huo ataendelea kunufaika hadi sheria zitakapopatikana na mifumo ikabadilika,” alieleza Napoleon.
Napoleon ambaye anatarajia kuandaa filamu yake mpya atakayoichezea visiwani Zanzibar, aliongeza kwa kuwataka wasanii kuendelea kufanya kazi nzuri na kuhangaika kuzisambaza katika matamasha mbalimbali ili kujitangaza kwa ajili ya kutengeneza soko kubwa la filamu zao zijazo.
Mtanzania

No comments:

Post a Comment

There was an error in this gadget