INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Monday, June 30, 2014

MZEE MAJUTO AWAALIKA WAOMBOLEZAJI KWENYE MSIBA WAKE

NI Wikiendi nyingine ambayo mapaparazi wetu, Dustan Shekidele ‘Mkude Simba’ Musa Mateja ‘Toz’ na Richard Bukos Mpigapicha Mkuu walijiachia viwanja mbalimbali kuwinda yaliyokuwa yakijiri na kumjuza moja kwa moja mkuu wao, Oscar Ndauka aliyekuwa makao makuu ya gazeti hili yaliyopo Bamaga, Mwenge jijini Dar es Salaam.


Msanii mkongwe na mkali wa maigizo na vichekesho, mzee Majuto (mwenye suti nyeupe) akiwa kwenye picha ya pamoja na mastaa wengine waliotunukiwa tuzo pia.

Akiwa ofisini Mkuu anaangalia saa na kubaini kuwa ni mida ya vijana wake kuwa viwanja hivyo anaamua kumtwangia Musa Mateja aliyekuwa Serena Hoteli ambapo kulikuwa na hafla ya utoaji wa Tuzo za Watu.

Saa 2:52 usiku
Mateja: Haloo ... naam mkuu wangu, nakupata bila mikwaruzo.
Makao Makuu: Haya niambie ushafika Serena kwenye hiyo hafla?
Mateja: Mkuu wangu nimefika hapa muda si mrefu nilipitia nyumbani kwa Aunt Ezekiel kulikuwa na shughuli, Wema Sepetu na mastaa wengine wa kike walikuwa wakimtunza mwenzao beseni baada ya kujifungua salama.

Makao Makuu: Mambo yalikuwaje huko?
Mateja: Mkuu huko ilikuwa ni minyonga tu ya kufa mtu, yaani kama huna simile utapatwa na aibu ya mfadhaiko yaani jinsi Wema anavyonyonga kiuno mmh... Acheni Diamond adate wajameni.
Makao Makuu: Aaa Mateja acha hizo hebu nidokeze na kinachoendelea hapo Serena Hotel?
Mateja: Mkuu huku mambo yameshamiri, namuona Mkurugenzi wa Benchmark Production, Rita Paulsen anaingia ukumbini huku akijiburuza na magongo.

Makao Makuu: Magongo! Amepatwa na swaibu gani tena?
Mateja: Hata mi sijapata uhakika sema kuna jamaa kaninong’oneza kuwa eti naniliu wake kamnaniliu lakini ntakwambia vizuri kesho.

Makao Makuu: Nini kingine kinaendelea hapo?
Mateja: Mkuu Mzee Majuto amepewa tuzo na sasa amefurahi sana na anawaalika watu kwenye msiba wake, anaomba siku akifa watu waje kwa wingi kwenye mazishi yake.
Makao Makuu: Dah! Huyo mzee haishi vituko nani wengine wamepata tuzo?
Mateja: Wengine ni Elizabeth Michael ‘Lulu,’ Salama Jabir, Nasibu Abdul ‘Diamond,’ Salim Kikeke wa BBC Swahili na wengineo.

Makao Makuu: Sawa Mateja angalia matukio kumbuka kupiga picha nitakusaka baadaye.
Saa 5:12 usiku|

NJEMBA YADATISHWA NA VIUNO VYA BIBI BOMBA
Makao Makuu: (Mkuu anamtwangia Bukos)

Bukos: Yaa mkuu wangu, nakupata kijana wako niko kwenye Bar moja inaitwa Madoto huku Mburahati nilikuwa nafuatilia Shindano la Bibi Bomba si unajua leo ilikuwa ndiyo fainali?
Makao Makuu: Nini kinaendelea huko uswazi kwa wanaofuatilia fainali hiyo kwenye runinga?
Bukos : Mkuu kuna muda Five Stars Modern Taarab walikuwa wakirindimisha burudani huyu Bibi Bomba, Ruth Manfred a.k.a Weusi Hawana Kwele, alikata nyonga mpaka akaenda chini kuna mlevi mmoja huku akajifanya eti amezidiwa baada ya kudatishwa na nyonga za bibi huyo kajitapa eti ni lazima atafute namba yake.

Makao Makuu: Dah! Hivi ni wangapi wameingia fainali?
Bukos: Mkuu fainali ya leo waliingia wabibi watano, Mariam Ligaya ‘Mamaa wa Mji Kasoro Bahari’, Anastazia Chambo, Ruth Manfred ‘Weusi Hawana Kwele’, Sofia Shomari na Sulaiya Mohammed ‘Agwe Solowenyo’.

Makao Makuu: Vipi nani kachukua hizo milioni 13 walizotangaziwa?
Bukos: Mkuu mpaka hatua ya mwisho walibaki wawili, Mariam Ligaya wa Moro na Ruth Manfred na Ruth Manfred ndiye kaibuka mshindi hivyo anakabidhiwa milioni 10 na zile milioni 3 ataongezewa milioni 2 na kupewa kiwanja Kigamboni chenye thamani ya shilingi milioni 5.

Saa 6:57 usiku

MOSHI WA GANJA WATIBUA SHOO YA MIAKA 10 YA MKALI WA RHYMES MORO
Makao Makuu: (Mkuu anamtwangia Dustan Shekidele ‘Mkude Simba’) Halooo halooo Mkude Simba...
Shekidele: Nakupata Mkuu.

Makao Makuu: Haya niambie muda huu uko wapi?
Shekidele: Mkuu wangu niko katika Ukumbi wa Terminal Pub hapa Msamvu, Mkali wa Rhymes, Afande Sele na washirika wake wanapiga shoo ya kusherehekea miaka 10 ya kushikilia taji la mkali wa rhymes.
Makao Makuu: Ahaaa... vipi hali ikoje?

Shekidele: Mkuu mpaka mida hii, 20 Percent na Afande Sele mwenyewe wameshakamua tatizo alipotaka kupanda O-Ten ameshindwa kupiga shoo baada ya kuzidiwa na mambo fulani maana kwa muda mrefu nilikuwa nikimuona akipiga maji huku akila kuku moshi.
Makao Makuu: Nini kinaendelea sasa?

Shekidele: Mkuu onesho naona kama limevurugika maana mambo sasa ni vululuvululu, moshi umetawala ukumbini wengine wasiouzoea wanakohoa hovyo hata mimi hivi ninavyoongea nimeshindwa kuvumilia hali ya ndani niko nje ya ukumbi, yaani ukumbini watu macho mekundu kama wamemwagiwa unga wa pilipili.

Makao Makuu: Sawa Mkude Simba ukitoka hapo wapigie wenzako waambie mkapumzike.
Shekidele: Pouwa Mkuu.

No comments:

Post a Comment